Friday, August 14, 2015

MA-IMAMU, MASHEHE NA USTAADH HAWAKUTAJWA KWENYE QURAN

Ndugu msomaji,

Tukisema kuwa Uislam ni bandia, ndugu zetu wanakuja na madai kuwa tunasema uongo na maneno mengi yasio na hata ushahid wa aya.

Leo ningependa kuwauliza Waislam. 

1. Wapi katika Quran Allah kasema Uislam uwe na Ma-Imamu, Mashehe na Maustaadhi?
2. Tupeni sifa za Imamu kwa kutumia aya za Quran.
3. Tupeni sifa za Mashehe kwa kutumia aya za Quran.
4. Tupeni sifa za Ustaadh kwa kutumia aya za Quran.

Ningependa ndugu Waislam watupe aya moja kwa moja. Mimi leo hii sina muda wa ngonjera zisizo na aya. Watuletee aya. Mimi nataka kusilimu.

Waislam wanasema eti hii aya kwenye Surat Al Baqara inazungumzia Imam: 124. Na Mola wake Mlezi alipo mjaribu Ibrahim kwa kumpa amri fulani, naye akazitimiza, akamwambia: Hakika Mimi nitakufanya uwe mwongozi wa watu. Akasema: Je, na katika vizazi vyangu pia? Akasema: Ahadi yangu haitawafikia wenye kudhulumu. Link: http://www.quranitukufu.net/002.html

Hapo kwenye hiyo aya hakuna cha Imamu wala Shehe zaidi ya Allah kudai anampa uongozi Ibrahimu. 

Mkishindwa kutuletea aya kutoka Quran zinaso sema kuwa muwe na hao viongozi wenu wa dini, basi ifahamike kuwa Uislam ni dini ya bandia na kujitungia wenyewe.

Lakini tunapo soma Biblia iliyo kamilika tunapewa aya kuhusu viongozi wa Kanisa. Ngoja niweka aya chache ili kusaidia mada:



SIFA ZA WAANGALIZI WA KANISA

Bwana alikuwa wazi sana katika neno lake kuhusu jinsi Yeye anataka kanisa lake duniani kwa lipangwe na kusimamiwa. Kwanza, Kristo ni kichwa cha kanisa na mamlaka yake makuu (Waefeso 1:22; 4:15, Wakolosai 1:18). Pili, kanisa lenyewe linafaa kujitawala, liko huru kutoka mamlaka yoyote ya nje au udhibiti, na haki ya kujitawala na uhuru kutokana na kuingiliwa na uongozi wowote wa watu binafsi au mashirika (Tito 1:5). Tatu, kanisa linastahili kutawaliwa na viongozi wa kiroho likiwa na ofisi mbili kuu - wazee na mashemasi.

MA-ASKOFU NA WACHUNGAJI
1 Timotheo 3: 1 Hili ni neno kweli, kwamba mtu akitamani
kazi ya askofu, atamani kazi nzuri. 2Basi, imempasa askofu awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi,
anayejitawala, anayeheshimika, mkarimu, ajuaye kufundisha. 3Asiwe mlevi, wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda  fedha. 4Lazima aweze kuisimamia nyumba yake mwenyewe vizuri na kuhakikisha kwamba  watoto wake wanamtii na kuwa na heshima kwa kila njia. 5(Kwa maana kama mtu hajui jinsi ya kusimamia nyumba yake mwenyewe atawezaje  kuliangalia kanisa la Mungu?) 6Asiwe mtu aliyeongoka karibuni asije akajivuna na kuangukia kwenye hukumu ile ile ya Shetani.
7Inampasa pia awe na sifa njema kwa watu walio nje, ili asije akalaumiwa na kuanguka kwenye mtego wa ibilisi.

MASHEMASI
Sifa Za Mashemasi 8Vivyo hivyo, mashemasi nao wawe watu
wanaostahili heshima, wasiwe wenye kauli mbili au wenye kujifurahisha kwa mvinyo, wala wanaotamani faida isiyo halali. 9Inawapasa kushikamana sana na ile siri ya imani kwa
dhamiri safi. 10Ni lazima wapimwe kwanza, kisha kama hakuna neno dhidi yao, basi na waruhusiwe kuhudumu kama mashemasi.
11Vivyo hivyo wake zao wawe wanawake wanaostahili heshima, wasiozungumza maneno ya kuwadhuru wengine, bali wawe na kiasi na waaminifu katika kila jambo. 12Shemasi awe mume wa mke mmoja na inampasa aweze kusimamia watoto wake na
watu wa nyumbani mwake vema. 13Wale ambao wamehudumu vema katika huduma ya ushemasi hujipatia msimamo bora na ujasiri mkubwa katika imani yao ndani ya Kristo Yesu.

USHAHID ZAIDI: Tito (1:1-4), Tito (1:5—3:11) na Tito (2:11-15)

Ndugu msomaji, nimethibitisha kwa aya kuwa Wakristo wao hawajajitungia vitu bali kuna aya zinazo ongoza jinsi ya kupata hawa viongozi, lakini kwenye Quran na Uislam, hatuoni aya yeyote ile inasema kuwa Waislam wawe na Maimam au Shehe au Ustaadhi na wawe watu wa aina gani. 

Mimi leo ningependa Waislamu watuambie, kwanini wana Imamu, Shehe Ustaadh kwenye dini yao/ Hakika Uislam ni dini iliyo jaa shaka na MSIBA mkubwa sana kwa Muhammad.


Nawakaribisha Waislam waje kwenye Ukristo na wokovu wa kweli.

Mungu awabariki sana,

Max Shimba Ministries

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW