Monday, August 10, 2015

YESU NI MUNGU KUTOKANA NA QURAN (SEHEMU YA TANO)

1. Allah anasema kuwa Yesu ni Roho kutoka kwa Mungu.
2. Biblia inasema kuwa Mungu ni Roho.

Ndugu msomaji:

Allah katika Surat An Nisaai iliyoteremshwa Makka na kufanyiwa tarjuma na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani aya ya 171 inasema kuwa Yesu ni ROHO ILIYO TOKA KWA MUNGU. Hebu tusome kwanza hiyo aya hapa chini:


ALLAH ANASEMA KUWA YESU NI ROHO
Surat An Nisaai 171. Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi ISA MWANA WA MARYAM ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neo lake tu alilo mpelekea Maryamu, na NI ROHO ILIYO TOKA KWAKE. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha.

Allah anaendelea kusema kuwa Yesu ni ROHO KUTOKA KWAKE. Quran inakiri kuwa Roho ya Allah haikuumbwa na au tengenezwa bali ilikuwepo karne zote na Allah. Quran hiyo hiyo inakiri kuwa Yesu ni Roho ya Allah. Hivyo basi, tunaweza kukubaliana kuwa Roho hii ya Allah haina mwanzo " Allah's Spirit is eternal". (Yusuf Ali, The Holy Qur'an, p. 132) and  (Abdul-Haqq, Sharing Your Faith with a Muslim, p. 84).

Lakini katika Biblia iliyo kuja kabla ya Quran tunafundishwa kuwa Mungu ni ROHO: Soma


MUNGU NI ROHO
Yohana 4: 24 Mungu ni roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”

Biblia ambayo ndio Neno kamili la Mungu, inatuambia kuwa Mungu ni Roho. Quran nayo inasema kuwa Yesu ni Roho kutoka kwa Mungu, na wakati huohuo, Quran inakiri kuwa Roho ambaye ni Yesu alikuepo siku zote na Allah "The Spirit of God is Eternal".Yusuf Ali, The Holy Qur'an, p. 132

Ndugu Msomaji, hakuna ubishi tena kuhusu Uungu wa Yesu. Maana hata Quran sasa inakiri kuwa Yesu ni Roho kutoka kwa Mungu. Na tunapothibitisha hayo maneno kwa Kutumia Biblia kama tulivyo amrishwa na Allah katika Surat Yunus 94. Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka.

Leo naweza sema kuwa mimi sina shaka kuhusu kuwa Yesu ni Roho wa kutoka kwa Mungu na sina shaka kabisa kuwa huyo Roho ni Mungu: Yohana 4: 24 Mungu ni roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

Leo nimejibu hoja ya Waislam kuwa, Je, Yesu ni Mungu? Koran pamoja na Allah wanasema kuwa Yesu ni ROHO KUTOKA KWA MUNGU na Biblia inasema kuwa ROHO NI MUNGU.

Katika huduma yake,

Max Shimba
Copyright © Max Shimba Ministries 2015

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW