Saturday, August 8, 2015

YESU NI MUNGU KUTOKANA NA QURAN (SEHEMU YA PILI)


Ndugu msomaji,

Je Yesu anazo sifa za kipekee za Mungu kutokana na Quran? Hebu tuanze utafiti wetu kwa kusoma Quran na tujionee wenyewe kama kweli Yesu ni Mungu au la.

Moja ya sifa au adhama ya Mungu kutokana na Quran: ni Al-Warith, ikimaanisha MRITHI WA VYOTE. Hii sifa ya Al Warith ni moja ya Majina 99 ya Allah wa Quran.

Je, Yesu anayo hiyo sifa ya MRITHI WA VYOTE "Al Warith"? Haya tusome kwanza Quran na tuone kama Allah anayo hii sifa ya Al Warith.

Surat Maryam 40. Hebu jamani! Nawajue watu kuwa hakika Mwenyezi Mungu ndiye mrithi wa kuurithi ulimwengu wote na kila kiliomo ndani yake. Na hisabu yao wote ni juu ya Mwenyezi Mungu. 

Allah anasema kuwa yeye ni Mrithi wa vyote kwenye Quran iliyo andikwa miaka mia 632 AD baada ya Yesu. Ikimaanisha kuwa Yesu ndie aliye kuwa wa kwanza kukiri haya maneno kuwa yeye ni mrithi wa yote kutokana na ushahid wa Biblia iliyo tangulia kabla ya Quran.

Sasa tuangalie kama kweli Yesu anayo hii sifa ya MRITHI WA VYOTE ambayo ni adhama ya Mungu pekee kutokana na Koran iliyo andikwa miaka 632 baada ya Yesu.

Biblia takatifi inasema yafuatayo kuhusu Yesu Kristo:
Waebrania 1 aya 2 inasema: lakini katika siku hizi za mwisho
amesema nasi kwa njia ya Mwanawe, ambaye
amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, ambaye
kwa Yeye aliuumba ulimwengu. 

Katika aya hii tunasoma kuwa Yesu anaitwa “MRITHI WA VITU VYOTE” ambayo ni adhama/sifa ya Mwenyezi Mungu kama ilivyo shaidiwa na Koran Surah ya 19 na aya 40. Hivyo basi , Allah na Koran wamekiri kuwa Yesu ni Mungu kwasababu Biblia imetuthibitishia kuwa Yesu ni MRITHI WA VITU VYOTE miaka 632 kabla ya kuandikwa kwa Quran na uthibitisho huu upo kwenye kitabu cha Waebrania 1 aya ya 2.

Ndugu zanguni, huu ni ushahid tosha kuwa Yesu ni Mungu, maana leo tumejifunza kuwa Yesu alisema na kuitwa MRITHI WA VYOTE MIAKA 632 kabla ya Kuandikwa kwa Quran. Sasa kati ya Biblia iliyo kuja kabla ya Quran na Quran iliyo kuja baada ya Biblia, wewe utafuata kitabu kipi?  Watafiti wa mambo mbali mbali huwa wanatumia data za awali katika kuhakiki jambo. Na data tuliyo nayo kuhusu Mrithi wa vyote ambayo ni ya awali ipo kwenye Biblia na inasema kuwa MRITHI WA VYOTE NI YESU.

Hakuna ubishi hapa kuhusu URITHI WA VYOTE ambao ni wa Yesu, Maana yeye ndie Mwana wa Mungu na alithibitishwa kuwa Mrithi wa vitu vyote miaka 632 kabla ya Quran. 
Leo nimejibu hoja ya Waislam kuwa, Je, Yesu ni Mungu? Koran pamoja na Allah wanasema kuwa Yesu ni Mungu kwa kuwa Yesu anazo adhama zote na/au sifa zote za Mungu na moja ya sifa hizo ni AL-WARITH.

Katika huduma yake,

Max Shimba

Copyright © Max Shimba Ministries 2015

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW