Saturday, March 26, 2016

NZI, MIKOJO, NA MATE YA MUHAMMAD NI DAWA KATIKA UISLAM


UTATA WA KUJITIBU KATIKA UISLAM
1. Eti Nzi ni dawa?
2. Eti Mate ya Muhammad ni Dawa?
3. Eti Kunywa Mikoja ni dawa!!!!
Jamani hii sayansi ya Kiislam ilitokea wapi?
MUHAMMAD ASEMA NZI NI DAWA
"Kama nzi ataangukia kwenye kinywaji cha yoyote kati yenu, itafaa kumchovya (kwenye kinywaji), kwani moja ya mbawa zake ina ugonjwa na linguine lina tiba (kiuasumu cha ugonjwa) (1). Maelezo chini ya ukurasa (1) yanasema "Tazama Hadithi na.673 juzuu ya 7 (kwa maelezo)" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 15 na.531 kabla ya uk. 335.
"Abu Huraira alisimulia: Nabii alisema, ‘Kama nzi wa nyumbani ataangukia kwenye kinywaji cha mmoja wenu, na amchovye nzi huyo (kwenye kinywaji), kwani moja ya mbawa zake ina ugonjwa na nyingine ina tiba ya ugonjwa huo." Bukharijuzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 16 na.537 uk.338.
Kwa taarifa, nzi aliyeshiba vizuri huenda haja kubwa kila baada ya dakika tano kwa mujibu wa
http://www.thebestcontrol.com/bugstop/control_flies.htm.
Abu Hureira ana kumbukumbu halisi: "Abu Huraira alisimulia: Nilimwambia Mtume wa Allah ‘Nimesikia simulizi (Hadithi) nyingi kutoka kwako lakini nimezisahau.’ Mtume wa Allah alisema, ‘Tandaza Rida (vazi) lako’ nilifanya kama alivyosema na kisha akaitembeza mikono yake kana kwamba anaijaza na kitu fulani (na kisha akaikunjua kwenye Rida langu) na kusema, ‘Chukua na jifunike shuka hili mwilini mwako.’ Nilifanya hivyo na baada ya hapo sijawahi kusahau kitu chochote." Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 3 sura ya 43 na.119 uk.89. Pia Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 sura ya 27 na.841 uk.538; Bukhari juzuu ya 9 sura ya 23 na.452 uk.332.
"Abu Huraira anasimulia: Mtume wa Allah alisema, ‘Ikiwa nzi ataangukia kwenye chombo cha yoyote kati yenu, mtu huyo na amchovye (kwenye hicho chombo) na kumtupa mbali, kwani kwenye bawa lake moja kuna ugonjwa na kwenye bawa linguine kuna uponyaji (1) (kiuasumu chake) yaani, tiba ya huo ugonjwa." Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 71 uk.58 na.673 uk.452-453.

Maelezo chini ya ukurasa (1) yanasema, "Kwa mujibu wa fani ya tiba sasa inafahamika sana kuwa nzi hubeba vijidudu vyenye kusababisha magonjwa (pathogens) kwenye baadhi ya sehemu zake kama ilivyosemwa na Nabii (karibu miaka 400 kabla wakati ambapo wanadamu walikuwa na ufahamu mdogo sana wa tiba ya kisasa). Kwa namna hiyo hiyo, Mungu aliumba viumbe na njia nyingine ambavyo vinaviua vijidudu hivi vinavyosababisha magonjwa k.m. kuvu la penisilini huua vijidudu kama Staphalococci na vinginevyo. Hivi karibuni majaribio yaliyofanywa chini ya usimamizi yameonyesha kuwa nzi hubeba vijidudu vyenye kusababisha magonjwa (pathogens) pamoja na viuasumu vya hivyo vijidudu. Kwa kawaida nzi anapogusa kimiminika kinachotumika kama chakula huathiri kimiminika kwa vijidudu vyake vinavyosababisha magonjwa, kwa hiyo ni lazima kumchovya ili kutoa pia kiuasumu cha vijidudu vyenye kusababisha magonjwa ili vipambane na vijidudu hivyo. Kuhusiana na somo hili, nilimwandikia pia rafiki yangu Dr. Muhammad M. El-SAMAHY mkuu wa Idara ya Hadithi ya Chuo Kikuu cha Al-Azhar Kairo (Misri) ambaye aliandika makala ya Hadithi hii na kuhusiana na fani ya tiba amesema kuwa wataalamu wa viumbe vidogo (mikrobiolojia) wamethibitisha kwamba kuna chembe chembe za chachu za longitudino zinazoishi kama vimelea ndani ya tumbo la nzi na chembe chembe hizi za chachu, ili kurudia mzunguko wao wa maisha huchomoza kupitia kwenye neli za kupumulia za nzi na endapo nzi atatumbukizwa tena kwenye kimiminika, chembe hizi hupasuka kwenye kimiminika na vitu vilivyomo ndani yake ni kiuasumu cha vijidudu vyenye kusababisha magonjwa ambavyo nzi huvibeba."

Kama angalizo, maelezo ya chini ya ukurasa yanamnukuu Daktari huyu kutoka kwenye idara ya Hadithi; hawakupata nukuu toka kwenye idara ya tiba au afya.
Bawa moja la nzi lina ugonjwa na bawa linguine lina tiba. Abu Dawud juzuu ya 3 na.3835 uk.1080.
Kama nzi ameangukia kwenye kinywaji, chovya bawa lake lingine kwenye kinywaji. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3504-3505 uk.38-39.
Muhammad na Maji Safi
Udhibiti wa afya kwa kuondoa maji machafu na takataka (Sanitation): Watu walipomuliza kuhusu kunywa maji ya kwenye kisima chenye nguo za hedhi, mbwa waliokufa, na vitu vyenye kunuka, Muhammad alisema kuwa maji ni safi kabisa na huwa hayachafuliwi na kitu chochote. Abu Dawud juzuu ya 1 sura ya 35 na.66-67 uk.16-17.
MUHAMMAD ASEMA KUNYWA MKOJO NI DAWA
Kutumia Mkojo wa Ngamia kama Tiba
Kwa mujibu wa Muhammad, watu waliteswa kwenye makaburi yao kwa sababu ya kujichafua na mkojo [wao wenyewe]. Bukhari juzuu ya1 kitabu cha 4 sura ya57 na.215 uk.141; Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 4 sura ya 57 na.217 uk.142.
Hata hivyo Muhammad aliwaamuru baadhi ya watu kumfuata mchungaji wake na kunywa maziwa na mikojo ya ngamia. Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 71 sura ya 6 na.589, 590 uk.398, 399 na juzuu ya 7 kitabu cha 71 sura ya 29 na.623 uk.418.
Muhammad pia alisema kuwa mkojo wa ngamia ni dawa nzuri. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 kitabu cha 31 na.3503 uk.38.
Baadhi ya Waislam waliambiwa kunywa mkojo wa ngamia, waliishia kuwa waasi na kumuua mchungaji. Muhammad aliamuru wakatwe miguu na mikono yao na macho yao yachomwe. Sunan Nasa’i juzuu ya 1 na.308-309 uk.255-256. Tazama pia Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 sura ya 152 na.261 uk.162.
Tongoo za Kidini Kama Tiba ya Kuumwa na Nge
Muhammad aliwafanyia tongoo watu wa Ansar kwa ajili ya kuondoa sumu iliyotokana na kuumwa na nge. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5442-5444, 5448 uk.1192, 1196.
Muhammad na Tiba Nyingine
Hakuna magonjwa yasiyokuwa na tiba kwa mujibu wa Sahih Muslim juzuu ya 3 uk.1199, 1200.
Allah ametengeneza dawa kwa kila ugonjwa isipokuwa uzee. Abu Dawud juzuu ya 3 na.3846 uk.1083.
Kitabu chote cha 31 kwenye Ibn-i-Majah (juzuu ya 5) kinahusu tiba. Kinasema kuwa kila ugonjwa isipokuwa uzee una tiba yake. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3436 uk.1.
Muhammad aliwaambia watu waliokuwa na maumivu kwenye miguu yao kujipaka hina. Abu Dawud juzuu ya 3 na.3849 uk.1084.
Collyrium (dawa ya kuoshea macho) hufanya macho yawe maangazu zaidi na kuzifanya nywele zikue. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 kitabu cha 31 na.3497 uk.35. Hata hivyo, collyrium inapaswa kutumiwa kwa kiasi cha namba witiri. Ibn-i-Majahjuzuu ya 5 kitabu cha 31 na.3498 uk.35-36; Abu Dawud juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.35 uk.8.
Kiuasumu cha sumu: "Mtu anayekula tende ‘Ajwa saba kila asubuhi, hatadhurika na simu au uchawi siku atakapoila." Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 65 sura ya 44 na.356 uk.260 na Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 72 sura ya 56 uk.451; Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 21 na.5080 uk.1129; juzuu ya 3 kitabu cha 21 na.5081 pia inaongeza uchawi.
"Aisha alinisimulia kuwa alimsikia Nabii akisema, ‘Kumini (cumin) nyeusi huponya magonjwa yote isipokuwa As-Sam.’ ‘Aisha alisema, ‘As-Sam ni nini?’ Nabii alimwambia, ‘Kifo.’" Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 71 sura ya 7 na.591 uk.400. Pia juzuu ya 7 kitabu cha 71 sura ya 7 na.592 uk.400 na Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 71 sura ya 10 na.596 uk.402.
Nigella Sativa huponya kila kitu isipokuwa kifo. Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 24 na.5489-5490; Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3447 uk.8; juzuu ya 5 na.3449 uk.9.
Tiba ya mshipa wa nyonga ni matako ya kondoo. Ibn-i-Majah juzuu 5 na.3463 uk.18-19.
Tiba ya uvimbe wa kwenye mapafu ni [mtishamba uitwao] ‘vita’ (wars), mshubiri wa India na mafuta ya mzeituni. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3467 uk.21.
Tazama www.MuslimHope.com/IslamAndScience.htm jinsi Muhammad alivyosema ni tiba ya kutupiwa kijicho.
Ushauri wa Muhammad Kuhusu Kuumika
Kuumika ni njia ya tiba ya kale inayohusisha kuweka kikombe chenye moto kwenye ngozi ya mgonjwa. Wakati kikombe na hewa ndani yake vinapoa, vinasababisha uwazi unaovuta damu nje.
Muhammad alisema kuwa njia ya kuumika ilikuwa ni tiba nzuri. Sahih Muslim juzuu ya 3 kitabu cha 24 na.5467 uk.1199; Sahih Muslim juzuu ya 2 kitabu cha 7 na.2740, 2741 uk.594; Ibn-i-Majah juzuu ya 5 kitabu cha 31 na.3476 uk.24; juzuu ya 5 kitabu cha 31 na.3478 uk.25.
Kuumika ni tiba nzuri zaidi. Abu Dawud juzuu ya 3 na.3848, 2850, 2851 uk.1084.
Muhammad alisema pia kuwa ikiwa watu watajiumika tarehe ya 17, 19 au 21 ya mwezi itakuwa ni tiba kwa kila ugonjwa. Abu Dawud juzuu ya 3 na.3852 uk.1084.
Abu Hind alimuumika Muhammad kwa mujibu wa Abu Dawud juzuu ya 2 na.2097 uk.562. Pia tazama Abu Dawud juzuu ya 3 sura ya 1464 na.3855 uk.1085; Ibn-i-Majah juzuu ya 3 na.2162-2163 uk.302-303; Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 29 sura ya 11 na.361, 362 uk.38-39; Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 71 sura ya 12-15 na.598-602 uk.403-405. Huu ulikuwa ni wakati alipokuwa anafunga. Ibn-i-Majah juzuu ya 4 na.3081 uk.330; Tirmidhi’s Shamaa-il sura ya 49 na.1, 2, 3, 4, 5, 6.
Hata malaika waliimwambia Muhammad aumikwe. Ibn-i-Majah juzuu ya 5 na.3477 uk.25 juzuu ya 5 na.3480-3481 uk.26.
Nategemea leo umejifunza kitu kuhusu Uislam ambao umejaa shaka na unategemea zaidi mambo ya dunia na sio kumtegemea Mungu aliye hai.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 26, 2016

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW