Wednesday, April 27, 2016

JE, KUUA AU KUJIUA NI DHAMBI?


Ndugu msomaji,
Nimepata maswali kadhaa kwenye private messaging kuhusu kuua au kujiua.
Watu wanataka kufahamu kuwa, je, mtu akijiua atakwenda wapi?
KOSA LA KUUA AU KUJIUA
Kulingana na Biblia, kujiua si kigezo cha kukufanya uingie mbinguni bali ni kigezo cha kukuingiza Jehannam. Mtu asiyeokoka akijiua huwa amejipeleka moja kwa moja katika ziwa la moto. Mtu huyu atapelekwa huko kwa kukataa kwake wokovu kupitia Yesu, Biblia inasema kuwa USIUWE, Biblia inasema katika Yohana 10:10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.
Katika Yohana 10 aya 10 tumesoma kuwa Yesu amekuja ili wewe uwe na uzima.
Biblia inataja watu wanne waliojiua: Sauli (samueli wa kwanza 31:4), Ahithofeli (samueli wa pili 17:23), Zimri (wafalme wa kwanza 16:18), na Yuda (Mathayo 27:5). Kila mmoja wao alikuwa mwovu na mwenye dhambi. Biblia inachukulia kujiua sawa na kuua – na hivyo ndivyo ilivyo – kujiua mwenyewe. Mungu ndiye ni aamue lini na vipi mtu afe. Kuchukua jukumu hilo mkononi mwako kibiblia ni kufuru kwa Mungu.
KUUHESHIMU UHAI
Mungu alionaje kuuawa kwa Abeli?
Mungu anataka tuuheshimu uhai wetu wenyewe na wa wengine. Kwa mfano, katika siku za Adamu na Hawa, mwana wao Kaini alimkasirikia sana Abeli, ndugu yake mdogo. Mungu alimwonya Kaini kwamba hasira yake ingeweza kumfanya atende dhambi nzito. Kaini alipuuza onyo hilo. ‘Alimshambulia Abeli ndugu yake, akamuua.’ (Mwanzo 4:3-8) Mungu alimwadhibu Kaini kwa kumuua ndugu yake.—Mwanzo 4:9-11.
Katika Sheria ya Musa, Mungu alikaziaje maoni yanayofaa kuhusu uhai?
Maelfu ya miaka baadaye, Mungu aliwapa watu wa Israeli sheria zilizowasaidia kumtumikia kwa njia inayompendeza. Kwa sababu sheria hizo zilitolewa kupitia nabii Musa, nyakati nyingine zinaitwa Sheria ya Musa. Mojawapo ya sheria hizo inasema: “Usiue.” (Kumbukumbu la Torati 5:17) Hilo liliwaonyesha Waisraeli kwamba Mungu anathamini uhai wa wanadamu na kwamba wanadamu wanapaswa kuuthamini uhai wa wengine.
Je, Biblia inasemaje juu ya Mkristo akijiua?
Kwa kawaida watu hawapendi kufa, lakini watu fulani huhatarisha uhai wao ili kujifurahisha. Kwa mfano, watu wengi huvuta sigara, hutafuna miraa, au kutumia dawa za kulevya ili kujisisimua. Vitu hivyo huudhuru mwili na mara nyingi husababisha kifo. Mtu mwenye mazoea ya kutumia vitu hivyo hauoni uhai kuwa mtakatifu. Mazoea hayo ni machafu machoni pa Mungu. (Waroma 6:19; 12:1; 2 Wakorintho 7:1) Ili kumtumikia Mungu kwa njia inayompendeza, lazima tuache mazoea hayo. Ingawa huenda ikawa vigumu sana kuacha mazoea hayo, Yehova anaweza kutupa msaada tunaohitaji. Naye huthamini tunapojitahidi kuuona uhai wetu kuwa zawadi yenye thamani kutoka kwake.
Hii si kwamba kujiua ni dhambi ndogo machoni pa Mungu. Kulingana na Biblia kujiua ni kuua na kila mara ni kosa.
KUHESHIMU DAMU
Mungu ameonyeshaje kwamba kuna uhusiano kati ya uhai na damu?
Baada ya Kaini kumuua Abeli ndugu yake, Mungu alimwambia Kaini: “Damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika udongo.” (Mwanzo 4:10) Mungu alipotaja damu ya Abeli, alikuwa akizungumzia uhai wa Abeli. Kaini alikuwa amekomesha uhai wa Abeli, na sasa ilikuwa lazima Kaini aadhibiwe. Ilikuwa kana kwamba damu ya Abeli, au uhai wake, ulikuwa ukimlilia Mungu ili haki itekelezwe. Uhusiano kati ya uhai na damu ulionyeshwa tena baada ya Mafuriko ya siku ya Noa. Kabla ya Mafuriko hayo, wanadamu walikuwa wakila matunda, mboga, nafaka, na kokwa tu. Baada ya Mafuriko, Mungu alimwambia Noa na wanawe: “Kila mnyama anayetembea ambaye yuko hai anaweza kuwa chakula chenu. Kama nilivyowapa mimea ya majani, nawapeni hao wote.” Hata hivyo, Mungu alitoa amri hii: “Isipokuwa tu nyama pamoja na nafsi yake [au, uhai wake]—damu yake—msile.” (Mwanzo 1:29; 9:3, 4) Ni wazi kwamba Yehova anahusianisha uhai na damu ya kiumbe.
MAMBO AMBAYO BIBLIA INAFUNDISHA
Uhai ni zawadi kutoka kwa Mungu. —Zaburi 36:9; Ufunuo 4:11.
Ni kosa kutoa mimba kwa sababu uhai wa mtoto ambaye hajazaliwa ni wenye thamani machoni pa Mungu.—Kutoka 21:22, 23; Zaburi 127:3.
Tunaonyesha kwamba tunaheshimu uhai kwa kutouhatarisha na kutokula damu. —Kumbukumbu la Torati 5:17; Matendo 15:28, 29.
Wewe umemwamini Bwana Yesu Kristo? Angalia vile Yohana 3:36 inasema, una MAISHA YA MILELE! Sio “inawezekana” ama “natumaini hivyo” – LAKINI UNAO WOKOVU – UMEOKOKA!
Anayemwamini Mwana anao uzima wa milele; asiyemtii Mwana hatakuwa na uzima wa milele, bali ghadhabu ya Mungu hubaki juu yake." Yohana 3:36
Rafiki, kama umeomba maombi haya na umempokea Yesu Kristo – UMEOKOKA! Umefanya yale Mungu anasema ufanye – NA MUNGU HAWEZI KUSEMA UONGO! Katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu, ASIYEWEZA KUSEMA UONGO aliuahidi tangu milele. Tito 1:2
Tunapaswa kumshukuru Mungu sana kwa sababu ya kutupa zawadi ya uhai kwa upendo! Je, hilo halipaswi kutuchochea kuwaambia wengine kuhusu pendeleo la kupata uzima wa milele kwa msingi wa imani katika dhabihu ya Yesu? Ikiwa tunathamini uhai wa wanadamu wenzetu kama Mungu anavyouthamini, tutachochewa kuwahubiria kwa hamu na bidii. (Ezekieli 3:17-21) Tukitimiza jukumu hilo kwa bidii, tutaweza kusema kama mtume Paulo alivyosema: “Mimi ni safi kutokana na damu ya watu wote, kwa maana sikuepuka kuwaambia ninyi mashauri yote ya Mungu.” (Matendo 20:26, 27) Kuwahubiria watu kumhusu Mungu na makusudi yake ni njia bora ya kuonyesha kwamba tunathamini sana uhai na damu.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 27, 2016

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW