Monday, January 31, 2022

BIBLIA NI BORA KULIKO QURAN

 



Tofauti za Msingi katika ya Biblia na Quran:

Neno "Biblia" linatokana na na neon la Kilatini na la Kigiriki lenye maana ya "kitabu," jina linalofaa, tangu Biblia ni kitabu kwa watu wote, kwa wakati wote. Ni kitabu si kama vingine, ni ya hali yake yenyewe.

Vitabu sitini na sita tofauti vyaunda Biblia. Navyo ni pamoja na vitabu vya sheria, kama vile Mambo ya Walawi na Kumbukumbu; vitabu vya kihistoria, kama vile Ezra na Matendo; vitabu vya mashairi, kama vile Zaburi na Mhubiri; vitabu vya unabii, kama vile Isaya na Ufunuo; wasifu, kama vile Mathayo na Yohana; na nyaraka (barua rasmi kama vile Tito na Waebrania.

BIBLIA INA SURA 1,189 WAKATI QURAN INA SURA 114

B I B L I A:
Biblia ina Surah 1,189 ikiwa ni zaidi ya mara kumi ya Quran yenye Surah 114. Ndio maana Waislam wanaweza kukariri hizo sura chache na si miujiza bali ni jambo la kawaida tu.

Biblia imegawanywa katika sehemu mbili kuu: Agano la Kale na Agano Jipya. Kwa ufupi, Agano la Kale ni hadithi ya taifa, na Agano Jipya ni hadithi ya mwanadamu. Taifa ilikuwa njia ya Mungu ya kuleta Mwana-Adamu- Yesu Kristo ulimwenguni.

Agano la Kale inaeleza mwanzilishi na utunzaji wa taifa la Israeli. Mungu aliahidi kutumia Israeli kubariki dunia nzima (Mwanzo 12:2-3). Pindi tu baada ya Israeli ilianzishwa kama taifa, Mungu alianzisha familia ndani ya taifa hilo ambaye kupitia kwayo baraka zitapitia: jamaa ya Daudi (Zaburi 89:3-4). Kisha, kutoka ukoo wa Daudi ameahidi Mtu moja ambaye ataleta baraka ya ahadi (Isaya 11:1-10).

Agano la Jipya laeza kwa undani juu ya ujio wa mtu wa ahadi. Jina lake Yesu, na alitimiza unabii wa Agano la Kale kama Yeye aliishi maisha kamilifu, alikufa ili awe Mwokozi, na kufufuka kutoka wafu.

Q U R A N:
Quran 2:106
Aya yoyote TUNAYOIFUTA AU KUISAHAULIZA tunaleta iliyo bora kuliko hiyo au iliyo mfano wake. Hujui kuwa Mwenyezi Mungu anao uwezo juu ya kila kitu?

Kwanini Allah alikuwa anafuta aya zake? Je, tutawezaje iamini Quran iliyi futwa futwa?

Mwandishi maarufu wa Kiislamu-Caliph Uthman aliandika Quran na kuchoma aya ambazo hakupendezwa nazo! (Sahih Bukhari 6:61:510)

Hakuchoma tu aya za kuran bali Sura nzima ya kuran ilipotea na kusahaulika. (Sahih Muslim 5:2286)

Vile vile, aya zingine zilifutwa kwa maksudi. (Bukhari 6:61:527).
Mohammad aliwaagiza waislamu kujifunza uislamu kutoka kwa kuran ya Ubai na wala sio ambayo Zayd Ibn Thabit aliandika (ambayo ni ya kisasa) tazama (Bukhari 6:61:521).

Ibn Sad (Kitab al-Tabaqat al-Kabir vol.2 p.444 ) inasema kuwa maandiko ya kuran ya Zayd Ibn Thabit ni tofauti na ya Muhammad. Kwa hivyo waumini wamepotoshwa kwa kukariri kuran hiyo ya kisasa.

Jami At-Tirmidhi 3104 vile vile anasema kuran iliyopo sasa ni feki-ya Zayd Ibn Thabit.

Katika kufanya marekebisho mengi kwenye kuran watu walikuja na nakala tofautitofauti za kuran (Jami at-Tirmidhi 3104) hivyo kulikuwa na mtafaruku miongoni mwa wafuasi wa mohammad kwa sababu zilikuwa tofauti.

Kuran ya Ibn Masood ilikuwa na sura 111, ya Ubay ilikuwa na sura 116 na kuran ya Zayd (ambayo ndio inatumika sasa hivi) ina sura 114. Tazama (Ibn Daud , Kitab al-Masahif).

Hata zile zilizotajwa kuwa feki hazikuhifadhiwa kwa sababu mbuzi alikula sehemu ya aya zake (Sunan Ibn Majah 1934/1944).

Hivyo hamna aliyeandika kuran hadi baadhi ya waliokuwa wanakariri mafunzo ya Mohammad kufa na kulikuwa na hofu kuwa aya zilizosalia zingepotea kabisa (Bukhari z6:61:509).

Hivi ndivyo Zayd Ibn Thabit alipata kuandika kuran ambayo tunayo leo hii kutoka kwa shuhuda za wakariri waliobaki (kurasa chache tu kutokana na miaka 23 ya ufunuo).

BIBLIA INA AYA 31,102 WAKATI QURAN INA AYA 6,236 UKIONDOA NENO BISMILLAH

Biblia imeshehena aya takatifu ambazo ni zaidi ya mara 5 ya aya za Quran ambazo ndani yake kuna aya za watu na Mashetani.

BIBLIA INA MANENO 783,137 WAKATI QURAN INA MANENO 77,430

Waislam wanapodai kuwa eti wamekariri Quran ni kwasababu Quran ina maeno machache sana. Quran ni sawa na Asilimia 10 tu ya Biblia. Ikimaanisha kuwa, Muislamanatakiwa kukariri vitavu 10 zaidi ili aweze kukariri Biblia. Quran ni sawa na tamthilia, hadithi fupi na ndio maana Uislam unatumia Usaidizi wa Sahih Hadith za Muhammad. Kwenye Ukristo hatuna Hadithi za watu kama kwenye Uislam ila Biblia Pekee ndio Msingi wa Ukristo.

BIBLIA INA WAANDISHI 40 WANAO THIBITISHIKA NA IMEANDIKWA KWA MIKA MINGI WAKATI QURAN INA MWANDISHI MMOJA TU AMBAYE ANADAI ALIPOKEA UNABII BILA YA UTHIBITISHO WOWOTE ULE.

Biblia na Quran zinatofautiana katika mambo mengi, lakini napenda nizungumzie machache, ambayo naamini yanaweza kutusaidia kujibu swali hili kwamba: Kati ya Biblia na Quran, kitabu kipi kinastahili kuaminika?

KUHUSU BIBLIA
Zifuatazo ni sifa za Biblia:

Idadi ya waandishi
Biblia ni kitabu kilichoandikwa na waandishi takribani 40. Waandishi 30 waliandika Agano la Kale na waandishi 10 waliandika Agani Jipya.

Nyakati
Waandishi wa Biblia waliishi katika nyakati tofautitofauti.

Kwa muda gani?
Kuanzia wakati wa Musa hadi wakati wa akina Paulo na Yohana, ilichukua miaka zaidi ya 1500 kupata kila kitu ambacho ndicho kimekuja kuwa Biblia hii tunayoifahamu.

Aina ya waandishi
Biblia haikuandikwa na watu wa aina moja. Badala yake kulikuwa na aina mbalimbali za watu. Kulikuwa na wafalme, kwa mfano Sulemani hadi watu wa chini kabisa, kama vile akina Petro ambao walikuwa ni wavuvi waishio kijijini.

Lugha
Kwa asili, Biblia iliandikwa kwa lugha mbalimbali, yaani Kiebrania, Kiaramu na Kigiriki. Baadaye ndipo lugha hizi zikaja kutafsiriwa katika lugha karibu zote duniani hivi leo.

Mitindo ya uandishi
Biblia imeandikwa kwa mitindo mbalimbali ya uandishi. Kwa mfano:

Historia au masimulizi - Kutoka, Hesabu, Yoshua, Nyakati, n.k.
Sheria – Walawi na Kumbukumbu la Torati
Ushairi – Wimbo Ulio Bora na maombolezo
Unabii – Yeremia, Ezekieli, Habakuki, Yoeli, Malaki, Danieli, n.k.
Nyaraka au barua – Warumi, wakorintho, Waefeso, Yakobo, Petro, n.k.
Mafunuo – Ufunuo

Jinsi ujumbe ulivyokuja
Ujumbe wa Biblia ulikuja kwa njia mbalimbali ambazo ni za kawaida kabisa. Kwa mfano:

Mungu kuongea moja kwa moja na wanadamu. Mathalani aliongea na Adamu (Mwa. 2:16-17), Nuhu (Mwa. 6:13-21), Ibrahimu (Mwa. 12:1-3; 22:1-2) na Musa (Kut. 3:4; 4:16).
Kwa njia ya maono. Kwa mfano, alisema kwa njia ya maono na Ibrahimu (Mwa. 12:7; 15:1), Yakobo (Mwa. 46:2; 28:12-17), Isaya (Isaya 6:1-10), Ezekieli (Eze. 1:1-28; 10:1-22), n.k.
Kupitia historia ya kawaida ya maisha ya Waisraeli. Ndio maana historia hiyo imeandikwa na sisi tunajifunza kweli za kiroho kupitia maisha yao ya kimwili.

HII MAANA YAKE NI NINI?

Maana yake ni kuwa, kwa vile Biblia imeandikwa kwa muda mrefu sana, na watu wengi, na watu tofauti, ambao hawakujuana, walioishi nyakati tofauti, walioishi sehemu tofauti, waliokuwa na elimu na vyeo tofauti, basi tungetarajia kuwepo na mgongano, msigano, na tofauti kubwa kabisa katika ujumbe wake. Isingewezekana kabisa kibinadamu:

Kuwepo na ujumbe unaofanana kwa watu wote hao
Kuwepo na mtiririko safi unaoendana kimantiki na kukubaliana kabisa na majira na nyakati

Maana yake nyingine ni kwamba, ukweli huu unatoa ishara ya wazi kwamba Biblia imetoka kwenye chanzo kimoja tu. Wanadamu walioandika walikuwa wanatumiwa kama vyombo tu na huyo Mwandishi halisi ambaye ni Roho Mtakatifu. Ndiyo maana ujumbe wa watu wote unaendana na kukubaliana sawasawa licha ya tofauti zao kubwa namna hiyo.

KUHUSU QURAN

Quran ni kitabu ambacho, kama inavyoshuhudia Quran yenyewe, kilitokana na kushuka kwa aya kutoka kwa Allah. Aya hizi alipewa Muhammad, ambaye sasa kutoka kwake zilifika kwa wanadamu. Kwa hiyo, yafuatayo ni mambo kuhusiana na Quran pamoja na ujumbe wake:

Idadi ya waandishi
Quran imeandikwa na mwandishi mmoja tu. Kama alipokea kweli hicho anachosema au hakupokea ni vigumu kuthibitisha.

Nyakati
Kwa kuwa mwandishi ni mmoja, basi aliishi kwenye wakati mmoja tu alipokuwa hai.

Kwa muda gani?
Muhammad alipokea aya za Quran kwa muda wa miaka 23 tu.

Aina ya waandishi
Kwa vile ‘mwandishi’ wa Quran ni mmoja tu, hatuwezi kuongelea suala la aina za waandishi.

Lugha
Lugha iliyotumika kuandika ujumbe wa mwanzo wa Quran ni moja tu.

Mitindo ya uandishi
Kwa ujumla Quran ina aina moja tu ya uandishi, ambayo ni aina ya unabii.

Jinsi ujumbe ulivyokuja
Ujumbe wa Quran ulikuja kwa njia tofauti na ule wa Biblia.

Ubada bin Samit reported that when wahi descended upon Allah's Apostle (may peace be upon him), he felt a burden on that account and the colour of his face underwent a change. (Sahih Muslim, Vol. 4, p. 1248).

[Tafsiri: Ubada bin Samit alisema kwamba wakati wahyi alipomshukia Mtume wa Mwenyezi Mungu (amani iwe juu yake), alijisikia mzigo kutokana na hali hiyo na rangi ya uso wake ilibadilika. (Sahih Muslim, Vol. 4, 1248)]

Verily, al-Harith Ibn Hisham said: O Apostle of Allah! how does revelation dawn upon you? The Apostle of Allah, may Allah bless him, said: Sometimes it dawns upon me in the form of the ringing of a bell, and that is very hard on me; (ultimately) it ceases and I remember what is said. Sometimes the angel appears to me and speaks and I recollect what he says. Ayishah said: I witnessed the revelation dawning upon him on an extremely cold day; when it ceased, I noticed that his forehead was perspiring. (Ibn Sa'd, Kitab al-Tabaqat al-Kabir, Vol. 1, p. 228).

[Tafsiri: Hakika, al-Harith Ibn Hisham alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ufunuo huwa unakujaje kwako? Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ambariki, alisema: Wakati mwingine huja kwangu kama vile sauti ya kengele, na hii huwa ngumu sana kwangu; (hatimaye) unakoma na mimi ninakumbuka kile kilichosemwa. Wakati mwingine malaika hunitokea na anaongea na mimi nami hukumbuka yale aliyosema. Ayishah alisema: Nilishuhudia ufunuo ukimjia katika siku ambayo ilikuwa ya baridi kali sana; ulipomalizika, niliona kwamba uso wake unatoka jasho. (Ibn Sa'd, Kitab al-Tabaqat al-Kabir, Vol. 1, uk 228.)]

The Prophet added, "The angel caught me (forcefully) and pressed me so hard that I could not bear it any more. He then released me and again asked me to read and I replied, 'I do not know how to read.' Thereupon he caught me again and pressed me a second time till I could not bear it any more. He then released me and again asked me to read but again I replied, 'I do not know how to read?' Thereupon he caught me for the third time and pressed me, and then released me and said, 'Read in the name of your Lord, who has created (all that exists) has created man from a clot. Read! And your Lord is the Most Generous." Then Allah's Apostle returned with the Inspiration and with his heart beating severely. Then he went to Khadija bint Khuwailid and said, "Cover me! Cover me!" They covered him till his fear was over and after that he told her everything that had happened and said, "I fear that something may happen to me." Khadija replied, "Never! By Allah, Allah will never disgrace you. You keep good relations with your Kith and kin, help the poor and the destitute, serve your guests generously and assist the deserving calamity-afflicted ones." (Sahih Al-Bukhari, Volume 1, Book 1, Number 3).

[Tafsiri: Mtume aliongeza, "Malaika alinikaba (kwa nguvu) na kunikandamiza kwa nguvu sana kiasi kwamba sikuweza kustahimili zaidi. Kisha aliniachia na kwa mara nyingine akaniambia nisome, nami nikamjibu, 'Mimi sijui kusoma.' Hapo alinikaba tena (kwa nguvu) na kunikandamiza kwa nguvu sana kiasi kwamba sikuweza kustahimili zaidi. Aliniachia na kwa mara nyingine akaniambia nisome, nami nikamjibu, 'Mimi sijui kusoma.' Hapo alinikaba tena na kunikandamiza na kuniachia kisha akasema, “Soma kwa jina la Mola wako ambaye ameumba (vyote) Amemuumba mtu kwa bonge la damu. Soma! Na Mola wako ni mwingi wa ukarimu." Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu alirudi na wahyi huku moyo wake ukidunda kwa nguvu. Kisha akenda kwa Khadija binti Khuwailid na akasema, "Nifunike! Nifunike!" Nao wakamfunika mpaka hofu ilipomwishia na baada ya hapo akawasimulia kila kitu kilichomtokea na akasema, "Naogopa kwamba kuna kitu kinaweza kunitokea." Khadija alijibu, "Hapana! Kwa jina la Allah. Allah hawezi kukuaibisha. Una uhusiano mzuri na ndugu zako, unasaidia walio maskini na fukara, unawafanyia ukarimu wageni wako na kusaidia wenye misiba wanaostahili." (Sahih Al-Bukhari, Volume 1, Kitabu 1, Namba 3)]

………………………

Desturi za Kiislamu ziko kinyume na matumizi ya kengele kwani zinatajwa kuwa ni vyombo ya shetani. Desturi hizi hata zinasema kwamba malaika hawawezi kuwasaidia wale wanaobeba kengele. Ona mifano ifuatayo:

Abu Hurairah alisimulia kwamba Mtume (amani iwe juu yake) alisema: kengele ni ala ya muziki ya Shetani. (Sahih Muslim, Kitabu 024)

Imesimuliwa na Umar ibn al-Khattab: Ibn az-Zubayr alisema kwamba mteja wao mwanamke alimpeleka binti wa az-Zubayr kwa Umar ibn al-Khattab akiwa amevaa kengele miguuni mwake. Umar alizikata na kusema kwamba alikuwa amesikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (amani iwe juu yake) akisema: Kuna shetani katika kila kengele. (Sunan Abu Dawud, Kitabu 34)

Abu Hurairah alisema kwamba Mtume (amani iwe juu yake) alisema: Malaika huwa hawamsindikizi msafiri ambaye ana mbwa na kengele. (Sahih Muslim, Kitabu 024)

Imesimuliwa na Ummu Habibah: Mtume (amani iwe juu yake) alisema: Malaika huwa hawaongozani na watu wanaosafiri huku wana kengele. (Sunan Abu Dawud, Kitabu 14)

…………………………..

Swali linalokuja kwetu ni kwamba, mtume alipoulizwa ni vipi huwa anapokea wahyi (ufunuo), mojawapo ya njia alizozitaja ni kwamba, upo ufunuo ambao huja kwa sauti kama za kengele. Na hapa anasema kuwa kengele zinahusiana na shetani. Hapo inakuwaje?

Hitimisho
Rafiki uliyesoma makala haya, unapolinganisha vitabu hivi viwili (Biblia na Quran), unadhani ni kipi kinastahili kuaminiwa?

Siulizi kwamba unaamini kipi? Maana nadhani tayari unacho kile unachokiamini. Lakini swali langu ni kwamba, Kipi kinastahili kuaminiwa?











No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW