Pengine unaweza kujiuliza ni kitu gani ambacho kimenipelekea niseme jambo hilo wakati Waislamu wanaamini hivyo? Ni kwa sababu Wakristo wengi wamekuwa wakisilimishwa, kwa kuamimishwa kwamba, Yesu Kristo alikuwa muislamu! na vigezo ambavyo waislamu huvitumia kumnasibisha Yesu na Uislamu ni vingi, ila leo nitachambua viwili.
(1) Yesu kusema yeye ni mnyenyekevu.
(2) Yesu Kuingia kwenye Sinagogi
Hivyo ndo vigezo vikubwa kabisa ambavyo waislamu huvitumia, katika kumtangaza kwamba Yesu alikuwa muislamu yaani Kiarabu wanasema:- كان يسوع مسلم
(1) Nikianza na hoja yao ya kwanza, kwamba Yesu alikuwa Mnyenyekevu! nitanukuu andiko hilo walitumialo, nitaeleza hoja zao na majibu ya hoja, kwa mtu asiye mvivu wa kusoma, basi atapata kitu cha kujifuza kupitia somo hili:
Mathayo 11:29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
Hapo wanakuambia kwamba, Yesu amesema, mimi ni mnyenyekevu, hiyo ni lugha ya Kiswahili, ingekuwa ni Kiarabu angesema, "Ana'a Muslima" (انا مسلم) Kwani wanakuunganishia na moja wapo la andiko ndani ya Quran ambalo limetaja Kusilimu ni kunyenyekea.
Quran 2 Suratul Baqrah
ﺇِﺫْ ﻗَﺎﻝَ ﻟَﻪُ ﺭَﺑُّﻪُ
ﺃَﺳْﻠِﻢْ ﻗَﺎﻝَ ﺃَﺳْﻠَﻤْﺖُ ﻟِﺮَﺏِّ
ﺍﻟْﻌَﺎﻟَﻤِﻴﻦَ
131. (Kumbukeni) Mola
wake alipomwambia:
Nyenyekea! Akasema:
Nimenyenyekea kwa Mola wa
viumbe wote.
Hapo kwenye neno Nyenyekea, katika lugha ya kiarabu imesemwa, ﺃَﺳْﻠَﻤْﺖُ (Aslmatu) Kuonyesha kwamba Uislamu ni kunyenyekea, hivyo husemwa Yesu aliposema Mnyenyekevu, alisema Yesu ni muislamu, wakimaanisha kwamba, kila Mnyenyekevu ni muislamu, ukitaka kujua kwamba, ni wazugaji, walaghai na waongo wakubwa! Waulize kuhusu Mtu huyu.
2 Korintho 10:1 Basi, mimi Paulo mwenyewe nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo; mimi niliye mnyenyekevu nikiwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo ni mwenye ujasiri kwenu;
Waulizeni, "Ikiwa Mtu akiitwa Mnyenyekevu ni muislamu, Je! Paulo kusema yeye ni Mnyenyekevu, nae muislamu?" Utawasikia "Huyo ni kafiri mkubwa kabisa"
Hapo ndo unajiuliza Inakuwaje neno hilo moja, limfanye mwingine kuwa muislamu (Yesu) Na mwingine kuwa kafiri (Paulo) wakati wote ni wanyenyekevu? hapo ndo utagundua kuwa ni wababaishaji, Sasa ngoja nikupe darasa kuhusu Unyenyekevu wa Yesu, Je! ni sawa na Unyenyekevu unaokusudiwa na Waislamu yaani Uislamu? Nanukuu Biblia ya Kiarabu.
متس 11: 29 احملوا نيري عليكم و تعلموا مني لاني وديع و متواضع القلب فتجدوا راحة لنفوسكم
Hiyo ni Biblia ya kiarabu Mathayo 11:29 Ambapo Yesu, katika matamshi ya Kiarabu amesema.
وديع
(Wadiuun (Mpole)
و متواضع
Wamutawadhwiu (Na mnyenyekevu)
القلب
Al-qalbi (Wa Moyo)
Yesu Unyenyekevu wake umeitwa, Mutawadhwiu (متواضع)
Na siyo Muslimani (مسلم) Kama wanavyodai waislamu, hutumia ubabaishaji huo kwa kuwa wanajua kuwa, Wakristo wengi hawajui Lugha kiarabu, kwani katika Biblia ya Kiarabu, hakuna sehemu hata moja ambayo Yesu, amewahi kusema,
وديع و مسلم القلب
(Wadiuuni, Wamuslimul qalbi)
Kwa sababu neno Uislamu, limeanza kutajwa ndani ya Quran, baada ya Muhammad.
Unaposema Muislamu, Kiarabu huitwa, مسلم
Na pia Unyenyekevu pia ndani ya Quran umegawanyika, kuna unyenyekevu katika Swala, ambao huitwa ﺧَﺎﺷِﻌُﻮﻥَ (Khaashiuun)
Quran 23: Suratul Muumin
ﺑِﺴْﻢِ ﺍﻟﻠﻪِ ﺍﻟﺮَّﺣْﻤﻦِ
ﺍﻟﺮَّﺣِﻴﻢِ
Kwa jina la Mwenyeezi
Mungu, Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehemu.
ﻗَﺪْ ﺃَﻓْﻠَﺢَ
ﺍﻟْﻤُﺆْﻣِﻨُﻮﻥَ
1. Hakika wamefuzu
wenye kuamini.
ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﻫُﻢْ ﻓِﻲ
ﺻَﻠَﺎﺗِﻬِﻢْ ﺧَﺎﺷِﻌُﻮﻥَ
2. Ambao ni
wanyenyekevu katika swala
zao.
Kama ingelikuwa kila kunyenyekea ni Uislamu, basi ingesemwa mwamba.
ﻓِﻲ
ﺻَﻠَﺎﺗِﻬِﻢْ ﻣُﺴْﻠِﻤُﻮﻥَ
(Fii Swalaatihim Muslimuuna)
Bali imesemwa, fii swalaatihim Khaashiun yaani katika swala zao ni Wanyenyekevu
Hata Majambazi wawapo Chini ya Ulinzi wa Polisi, huwa wanyenyekevu, wenye kujisalimisha, sijawahi kuwasikia Waislamu wakisema, huo ni Uislamu, kwa sababu Wameyenyekea, Unyenyekevu, Kwa hivyo Yesu hajawahi kuwa muislamu, (مسلم)
(2) KUINGIA KWENYE SINAGOGI
Hoja hii ndo kubwa zaidi kwao, kuliko hata ile ya Unyenyekevu, kwa sababu hata muislamu asiyejua kiarabu, hutumia sinagogi kama fimbo kuonyesha kwamba Yesu ni Muislamu! Wakitumia.
Luka 4:16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.
Wakitoa andiko hilo, husema kwamba, Yesu aliingia kwenye Sinagogi, na kwa mujibu wa maelezo ya maneno magumu katika Biblia tafsiri ya mwaka 1952 Imesema, Sinagogi ni msikiti wa Wayahudi, kwa hivyo watakuuliza, "Wanaoingia msikitini ni watu wa dini gani? Ukijibu "Waislamu" Watakuuliza, "Yesu kuingia mle atakuwa nani?" Lazima utasema "Alikuwa muislamu" utaambiwa njoo msikitini uungane na Yesu. Wengine husilimia hapo,
Ila Waislamu hao hao waulize kuhusu mtu huyu.
Matendo 17:1 Wakiisha kupita kati ya Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalonike, ambapo palikuwa na sinagogi la Wayahudi.
2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu.
Waulize, Ikiwa Yesu ameingia kwenye Sinagogi, mnasema ni muislamu, Je! Paulo nae kuingia kwenye sinagogi kama ilivyokuwa Desturi yake, nae ni muislamu?
Utawasikia, "Aaah huyo Paulo ni kafiri mkubwa kabisa"
Hapo ndo unajiuliza, inakuwaje Yesu kuingia, kwenye sinagogi awe muislamu, halafu Paulo awe Kafiri, wakati wote desturi yao ni moja kuingia kwenye sinagogi? Hapo ndo utajua kuwa hao ni wababaishaji.
Sinagogi siyo msikiti kwa maana halisi:-
Wakati wa kutafsiri Biblia, wakati ule kiswahili kilikuwa bado hajikakua, wafasiri walikosa neno hasa la kuweka ili liwe na maana katika kiswahili, wakaona Waweke Msikiti wa Wayahudi, kwa sababu Mashariki ya kati, majengo yao ya ibada, yalikuwa katika mfanano, Muhammad alipoanzisha Ujenzi wa Misikiti, aliiga majengo ya masinagogi yalivyo, ndo maana wakaweka msikiti wa Wayahudi, na siyo Msikiti tu katika mfanano wa majengo, maana Masinagogi yalijengwa baada ya Waisraeli kitoka utumwani, yakitumika kama madarasa ya kufundishia Torati, na hata Ibada kwa sababu Hekalu lilikuwa moja, wasingewza kukusanyika wote
Ila kwa sasa, Lugha imepanuka! Ndiyo maana sasa huoni tena uwepo wa maneno magumu! Kufasiri Sinagogi ni msikiti wa Wayahudi kwa sababu lugha imekuwa pana, na hata ukisoma Biblia ya Kiarabu, Sinagogi, halijaitwa Masjid (مسجد) Ambapo katika Lugha ya kingereza, Mosque, bali Limeitwa hivi.
4: 16 و جاء الى الناصرة حيث كان قد تربى و دخل المجمع حسب عادته يوم السبت و قام ليقرا
Kumeandikwa
و دخل Wadakhara
المجمع
Ilal Maj'maa
Maj'maa مخمع Ndivyo Sinagogi linavyoitwa, Wakati Msikiti kiarabu huitwa, مسجد (Masjid)
Hata ukisoma katika Biblia ya kingereza, Sinagogi huitwa, Synagogue, na msikiti ni Mosque, Huwezi kwenda kusoma English Bible ukakuta sehemu ye yote imeandikwa, Synagogue ni Mosque, kwani hata Quran yenyewe inakiri wazi kuwa kuna tofauti baina ya sinagogi na Msikiti.
Quran 22: SUURATUL HAJJ
ﺍﻟَّﺬِﻳﻦَ ﺃُﺧْﺮِﺟُﻮﺍ ﻣِﻦ
ﺩِﻳَﺎﺭِﻫِﻢْ ﺑِﻐَﻴْﺮِ ﺣَﻖٍّ ﺇِﻟَّﺎ ﺃَﻥ
ﻳَﻘُﻮﻟُﻮﺍ ﺭَﺑُّﻨَﺎ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻭَﻟَﻮْﻟَﺎ
ﺩَﻓْﻊُ ﺍﻟﻠَّﻪِ ﺍﻟﻨَّﺎﺱَ ﺑَﻌْﻀَﻬُﻢ
ﺑِﺒَﻌْﺾٍ ﻟَّﻬُﺪِّﻣَﺖْ ﺻَﻮَﺍﻣِﻊُ
ﻭَﺑِﻴَﻊٌ ﻭَﺻَﻠَﻮَﺍﺕٌ
ﻭَﻣَﺴَﺎﺟِﺪُ ﻳُﺬْﻛَﺮُ ﻓِﻴﻬَﺎ
ﺍﺳْﻢُ ﺍﻟﻠَّﻪِ ﻛَﺜِﻴﺮﺍً
ﻭَﻟَﻴَﻨﺼُﺮَﻥَّ ﺍﻟﻠَّﻪُ ﻣَﻦ
ﻳَﻨﺼُﺮُﻩُ ﺇِﻥَّ ﺍﻟﻠَّﻪَ ﻟَﻘَﻮِﻱٌّ
ﻋَﺰِﻳﺰٌ
40. Ambao wametolewa
majumbani mwao pasipo haki
ila kwa sababu wanasema Mola
wetu ni Mwenyeezi Mungu. Na
kama Mwenyeezi Mungu
asingeliwakinga watu baadhi
yao kwa wengine, bila shaka
yangelivunjwa mahekalu na
makanisa, na masinagogi, na
misikiti ambamo jina la
Mwenyeezi Mungu hutajwa kwa
wingi. Na bila shaka Mwenyeezi
Mungu humsaidia yule
anayemsaidia Yeye. Hakika
Mwenyeezi Mungu ni Mwenye
nguvu Mtukufu.
Hapo Quran Imetaja kwa uwingi kila Jengo.
ﺻَﻮَﺍﻣِﻊُ
(1) Mahekalalu (Swawaamiu)
َﺑِﻴَﻊٌ
(2) Makanisani (biyaaun)
َﺻَﻠَﻮَﺍﺕٌ
(3) Masinagogi (Swalawaatun)
َﻣَﺴَﺎﺟِﺪُ
(4) Msikikiti (masaa jidu)
huo ni utofauti wa kuonyesha kwamba, Kuna tofauti kati ya sinagogi na msikiti, katika Somo hili sitafundisha Yesu alilitazamaje Sinagogi, lipo somo lake, ila tu nimeeleza utofauti wa Sinagogi na msikiti ambao unatumiwa na waislamu...
Hii sehemu ya kwanza sehemu ya Pili nitafafanua, Je! Yesu anaweza kuwa muislamu, kwa.
(1) Kuvaa Kanzu
(2) Kuwatawadha wanafunzi wake
(3) Kusema amani iwe kwenu.?
Imetayarishwa na Na Mtumishi Abel Suleiman Shiliwa.
Shalom,
Max Shimba Ministries Org
No comments:
Post a Comment