Wednesday, November 16, 2016

IMAM NA FAMILIA YAKE WAMPOKEA YESU.


WAKIRI KUWA UISLAM NI DINI YA MASHETANI
IMAM KASEMA,, MAJINI NA MASHETANI NI YALE YALE.
IMAM ASEMA, KWENYE UKRISTO KUNA RAHA NA AMANI.
IMAM NA FAMILIA YAKE WAKIRI KUWA YESU NI MUNGU.

MPOKEE YESU SASA, USISUBIRI KESHO, UNAWEZA KUCHELEWA

MAMILIONI YA WAISLAM BARANI AFRIKA WANAMKIMBILIA YESU KRISTO ISIVYO KAWAIDA


“Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja” (Mathayo 24:14).
Ukisoma kurasa mbalimbali za kwenye mtandao juu ya kukua kwa dini ya Kiislamu, utakuta wengi wanasema kwamba Uislamu ni dini inayokua kwa kasi sana. Je, hilo ni kweli? Ni jambo gani linaloonyesha ukweli wa hoja hiyo?
Lakini tunao ushahidi wa Neno la Kristo kwamba siku za mwisho (yaani hizi tulizo nao), Injili itahubiriwa ulimwenguni kote. Pia, Mungu Yehova anaahidi kuwa hizi ni siku za kumwaga Roho wake kwa wanadamu wote. Hakika hizi ni nyakati za Injili ya Yesu Kristo kusonga mbele na kushinda na kubomoa kila upinzani na ukuta uliojengwa na adui ili kuwazuia wanadamu kumjua Mungu wa kweli na Mwokozi pekee, Yesu Kristo.
Uzuri ni kwamba, hili si jambo la mwanadamu. Hii ni kazi ya Mungu, Muumba mbingu na nchi Yeye mwenyewe. Ukristo si kama dini zingine ambazo zinajipigania zenyewe. Ukristo ni kazi ya Kristo mwenyewe! Kuipinga kazi hii ni kupingana naye. Na kuikataa kazi hii ni kumkataa Yeye mwenyewe. Mamilioni ya Waislamu wametambua sasa ni wapi uzima uliko.
Je, ndugu msomaji, umeshaingia kwenye safina ambayo ni Yesu Kristo? Usikubali kuachwa nje ya safina. Hakuna wokovu kwa mwingine awaye yote ila kwa Yesu Kristo peke yake!
Suala si dini. Suala ni maisha ya amani na furaha na mafanikio hapa duniani na kisha uzima wa milele mbinguni baada ya maisha haya. Dini hazitusaidii lolote kamwe – iwe ni Ukristo au dini nyingine!
Kama ingekuwa ni kuhesabu mafanikio ya dini katika historia nzima ya mwanadamu, basi dini zimefanikiwa sana kuleta mafarakano, chuki na uhasama baina ya wanadamu. Hakika hicho ndicho ambacho dini zimefanikiwa kufanya! Lakini Yesu – ah Yesu! Bwana wa amani! Bwana wa upendo! Bwana wa uzima na uzima tele! Yeye ni njia, ni kweli, ni uzima! Dini bila Yesu ni kupoteza kila kitu …!
Yafuatayo ni mahojiano kati ya mtangazaji Maher Abdallah wa kituo cha Al-Jazeera na Sheikh Ahmad Al Katani kuhusiana na suala la Waislamu milioni 6 kuingia kwenye Ukristo kila mwaka.
****************
Mtangazaji Maher:
Idadi ya Waislamu hivi sasa haizidi theluthi ya watu wa bara lote la Afrika. Hii inatilia maanani pia ukweli kwamba, sehemu kubwa ya Waislamu katika Afrika ni Waislamu wa Kiarabu. (Yaani ambao wanapatikana kaskazini mwa Afrika).
Ni wazi kuwa suala la uinjilisti na kuwageuza watu kuwa Wakristo kunakofanywa na Wakristo vimesaidia katika kugeuza hali hii ya mambo katika bara hili.
Katika kujadili mada hii, ninayo furaha kumkaribisha mtu ambaye ni mtaalamu wa suala hili la uinjilisti na kuwageuza watu kuwa Wakristo katika Afrika. Atalenga kwanza kuzungumzia zaidi suala la kuenea kwa Ukristo. Shekhe Ahmad Al Katani, rais wa Companions Lighthouse for Science in Libya, ambayo ni taasisi iliyojikita kwenye kusomesha maimamu na wahubiri wa Kiislamu.
Shekhe Ahmad:
Katika hali halisi, maneno haya (yaani ya Maher) hayasemi kikamilifu kile kinachotakiwa kusemwa. Kama tulivyosema mwanzoni, kila mtu anayo haki ya kuwakaribisha wengine kwenye dini yake; hiki ndicho kinachojulikana kama kuhubiri dini. Na kuhusu uenezaji wa Ukristo, hakuna mtu mwenye haki ya kuwatoa Waislamu nje ya dini yao, na umeuliza kuhusu rejea na rejea ziko nyingi sana.
Uislamu ulikuwa ni dini kuu ya Afrika na kulikuwa na lugha 30 za Kiafrika ambazo zilikuwa zikiandikwa kwa maandishi ya Kiarabu. Idadi ya Waislamu imepungua Afrika hadi milioni 316, ambapo nusu ya hao ni Waarabu wa Afrika Kaskazini. Kwa hiyo, katika eneo la Afrika ambalo tunalizungumzia, eneo lisilo la Waarabu, idadi ya Waislamu haizidi watu milioni 150. Tunapotambua kwamba Afrika ina watu bilioni moja, tunaona kwamba idadi ya Waislamu imepungua sana kutoka idadi iliyokuwapo mwanzoni mwa karne iliyopita.
Kwa upande mwingine, idadi ya Wakristo imeongezeka kutoka milioni moja mwaka 1902 hadi milioni 329, 882,000, au tuseme milioni 330 mwaka 2000.
Kila saa moja, Waislamu 667 wanaingia kwenye Ukristo. Kila siku moja, Waislamu 16,000 wanaingia kwenye Ukristo. Kila mwaka mmoja, Waislamu milioni 6 wanaingia kwenye Ukristo. Idadi hii ni kubwa sana.
Mwandishi Maher:
Hebu subiri kidogo. Unamaanisha ni Waislamu milioni 6 wanaingia kwenye Ukristo au wanaingia kwenye dini zingine?
Shekhe Ahmad:
Dini zingine haziwekwi kwenye kundi la kufanywa Wakristo; bali zinawekwa kwenye kundi la uinjilishaji. Dini nyingine katika Afrika ni upagani. Kwa hiyo ni Uislamu, Ukristo au upagani. Hakuna kitu kama kule Asia, kwa mfano, ambako kuna Ubudha au Uzoroasta. Kwa Afrika ni makundi haya matatu tu. Kwa hiyo, unapozungumzia kuhusu kuwafanya watu kuwa Wakristo, kunalenga dini nyingine pekee ya mbinguni, ambayo ni Uislamu.
*******************
Nini maana ya hali hii?
[Maelezo yangu mimi blogger]
Maandiko Matakatifu yako wazi kwamba: wa kwanza atakuwa wa mwisho (Mathayo 19:30). Ulaya na Marekani zilianza kuupokea Ukristo na kiwango kikubwa sana. Lakini hivi sasa wamemkataa Bwana Yesu na wanazidi kuzama zaidi na zaidi kwenye giza nene.
Afrika, ambayo ilikuwa katika giza nene la ibilisi la kutomjua Bwana huko nyuma, (kwa maana kwamba ilikuwa ya mwisho), katika nyakati hizi za mwisho, ndiyo inayokuwa ya kwanza. Nuru ya Injili inasambaa kama moto wa nyika. Na hili ni jambo linalotoka kwenye kiti cha enzi cha mbinguni kwenyewe kama nilivyosema hapo mwanzo.
Hata kama adui atajaribu kujiinua kwa kiasi gani, Neno la Bwana, kama kawaida yake, ni lazima litimie! Hata nukta moja haitaanguka hadi yote yatimie.
Ndugu msomaji, hebu jiulize mwenyewe, Ukristo haujawahi kushindana na mwanadamu ili kuwaingiza wanadamu kwa nguvu ndani yake. Haujawahi kushika panga wala bunduki ili kuwaingiza wanadamu kwenye imani hii! Sasa ni kitu gani kinachoufanya ukue kwa kasi namna hii? Mbona imani ya Kikristo ni imani ya upole, huruma, msamaha na maelewano lakini wakati huohuo inasonga mbele kwa kasi namna hii?
Bila shaka iko nguvu nyingine iliyo nyuma ya kundi hili. Nguvu hiyo ni Roho Mtakatifu, ambaye ni Mungu mwenyewe. Vita ya kanisa la Kristo siku zote imekuwa dhidi ya ulimwengu wa giza wa ibilisi. Na kwa sababu silaha zetu ni za kiroho (si za kimwili), hizo ni silaha za ushindi daima. Kanisa kamwe halishindani na wanadamu.
Bwana anatupenda sana wanadamu wake aliotuumba, ndiyo maana alikuja duniani na kuishi na kufa kwa ajili yetu. Mtu yeyote anayeshindana na Bwana hawezi kufika kokote. Tena ukichukulia kwamba mtu mwenyewe anashindana kwa silaha za kimwili dhidi ya silaha za kiroho!
Tafakari.
Jiulize.
Hoji mambo.
Chukua hatua.

ALLAH ANA-VAA NGUO KAMA VIUMBE


الكبرياء ردائي والعظمة إزاري
Allah ansema katika Hadithi hii Qudsi "Ukuu ndi vazi langu la juu na utukufu ndio vazi langu la chini".
Sasa kama Allah anavaa nguo inamana kuwa Allah ana mwili kama viumbe?
Msiba huu ni mkubwa sana ndugu wasomaji.
Katika Hadithi nyengine Qudsi, Allah anasema: "….Na mja wangu hajikurubishi kwangu kwa kitu nikipendacho zaidi kuliko yale niliomfaradhishia juu yake. Na mja huwa anaendelea kujikurubisha kwangu kwa nawafil (ibada zisizo za lazima) mpaka nampenda: "فإذا أحببته كنت سمعه الذي يسمع به، وبصره الذي يبصر به ويده التي يبطش بها ورجله) (التي يمشي بها" Basi nikimpenda nakuwa (Mimi ndio) sikio lake analosikia kwalo, na jicho lake analoonea na mkono wake anaoshikia na mguu wake anaoendea."
Hapo Allah kesha kiri kuwa yeye ana masikio, mikono na macho.
Ndugu wasomaji, teyari mmesha uelewa kuwa Allah ni kiumbe kama binadamu, kina Mwili, Mikono, Macho, Miguu na nyayo.
Mungu awabariki sana.
Katika Huduma yake,
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

ALLAH ANAKIRI KUWA YEYE ANA USO.


1) Allah anasema: "Popote mutapogeukia kuna Uso wa Mwenyezi Mungu". Sura 2, Aya 115.
Kwenye hiyo aya hapo juu, Allah amesha wajibu wanao bisha kuwa Allah hana uso. Je, kuwa na uso si sifa ya binadamu?
2) Allah anasema: "كل شيء هالك إلا وجهه" (Kila kitu kitaangamia isipokuwa Uso wake (Allah)." Sura 28 Aya 88.
Ndugu zanguni, Allah anaendelea kukiri kuwa yeye ana uso kama viumbe.
Ndugu wasomaji, teyari mmesha uelewa kuwa Allah ni kiumbe kama binadamu, kina Mwili, Mikono, Macho, Miguu na nyayo.
Mungu awabariki sana.
Katika Huduma yake,
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

ALLAH ANAKAA KWENYE KITI KAMA VIUMBE


Katika Sura 69:17 Surat al-Haaqqah tunasoma maneno haya:
“Na malaika watakuwa kandoni mwake na malaika wa namna nane watachukua kiti cha enzi cha Mola wako juu ya…”
Tena katika Sura 85:15 Syrat Buruj inamtaja Mungu wa Waislamu aitwaye Allah kuwa yeye ndiye mmiliki wa kiti cha enzi.
Swali ambalo napenda kuwauliza Waislamu wote Allah kumiliki kiti cha enzi. Je, kiti hicho anakifanyia nini? Huenda watu wakanishangaa. Nasema hivyo nikiwa na maana ya je, Allah naye anakaa katika kiti kama wakaavyo wanadamu? Je, ana miguu kama mwanadamu kama anakaa kama mwanadamu katika kiti cha enzi, basi haikosi hana tofauti na mwanadamu.
Angalia katika Sura ya 69: 44-45 Surat Al-haqqah twasoma.
“Na kama (mtume) angelizuia juu yetu baadhi ya maneno tu bila shaka tungalimshika kwa mkono wa kuume”.
Aya hii inaonesha kuwa Allah ana mkono wa kuume. Na kama Allah ana mkono wa kuume atakosaje mkono wa kushoto? Na kama Allah anasema atakosaje mdomo? Basi ondoeni dhana ya kwamba Allah hana mfano.
Ndugu wasomaji, teyari mmesha uelewa kuwa Allah ni kiumbe kama binadamu, kina Mwili, Mikono, Macho, Miguu na nyayo.
Mungu awabariki sana.
Katika Huduma yake,
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

ALLAH ANA MIKONO KAMA VIUMBE


وَمَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ {67}
“Na hawakumheshimu Mwenyezi Mungu heshima ipasayo, na siku ya Kiyama ardhi yote itakuwa mkononi mwake na mbingu zitakunjwa katika mkono wake wa kulia, …” (Az-Zumar; 39: 67)
“Mikono” Ya Mwenyezi Mungu Kama Ilivyosimuliwa Na Madhehebu Ya Makhalifa.
Wanazuoni wa madhehebu hiyo hapo juu wamesimulia ndani ya vitabu vyao kutoka kwa Abu Huraira ambaye amesimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama ifuatavyo:
“Adamu na Musa walikuwa na mazungumzo yafuatayo: Musa alisema: ‘Ewe Adamu! Mwenyezi Mungu alikuumba kwa mikono Yake Mwenyewe… Lakini uliwateremsha wanadamu kutoka kwenye bustani kwa sababu ya dhambi yako.’
Adamu akajibu: ‘Ewe Musa, Mwenyezi Mungu kwa hakika amekutukuza wewe, na akaandika Taurati kwa ajili yako kwa mikono Yake Mwenyewe.’”
Katika hadithi nyingine iliyosimuliwa kutoka kwa Abu Huraira, tunakuta:
“Mwenyezi Mungu huwa anashuka mpaka kwenye mbingu ya kwanza, na ananyoosha mikono Yake miwili na anasema…”
Halafu anaendelea kunukuu Ayah zifuatazo kwa ithibati ya madai yake:
وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنْفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ {64}
“Na Wayahudi walisema: Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba. Mikono yao ndio iliyofumba, na wamelaaniwa kwa sababuya yale waliyoyasema. Lakini mikono ya Mwenyezi Mungu iwazi, hutoa apen- davyo …” (Al-Maida; 5: 64)
فَسُبْحَانَ الَّذِي بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ {83}
“Basi ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo ufalme wa kila kitu, na kwake mtarejea.” (Yaasin; 36: 83)
قُلِ اللَّهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَنْ تَشَاءُ وَتَنْزِعُ الْمُلْكَ مِمَّنْ تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَنْ تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَنْ تَشَاءُ ۖ بِيَدِكَ الْخَيْرُ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ {26}
“Sema: Ewe Mola Mwenye kumiliki ufalme, humpa ufalme umtakaye, na humnyang’anya ufalme umtakaye. Na humtukuza yule umtakaye na kumdhalilisha umtakaye. Kheri yote imo mikononi mwako. Hakika wewe ni Mweza juu ya kila kitu.” (Aali Imraan; 3: 26)
Muhammad bin Muslim alimuuliza Imam Muhammad al-Baqir (a.s.) kuhusu Ayah ifuatayo:2
قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَنْ تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ ۖ {75}
“Akasema: Ewe Iblis, ni nini kimekuzuia kumtii yule niliyemuumba kwa mikono yangu?... (Swaad; 38: 75)
Ndugu wasomaji, teyari mmesha uelewa kuwa Allah ni kiumbe kama binadamu, kina Mwili, Mikono, Macho, Miguu na nyayo.
Mungu awabariki sana.
Katika Huduma yake,
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

ALLAH ANA MIGUU NA NYAYO KAMA VIUMBE


“Nyayo Za Mwenyezi Mungu” Na “Muundi Na Mguu” Wake!!”
Katika kitabu cha Tawhiid cha Ibn Khuzaimah, hadithi mbalimbali zinazohusiana na ‘mguu’ na ‘nyayo’ za Mwenyezi Mungu zimetajwa humo, aghalabu zikisimuliwa na Abu Huraira. Na zinaweza kupatikana vilevile katika Sahih Bukhari, Sahih Muslim, Sunan Tirmidhi, Musnad Ahmad Hanbal na Tafsiir za akina Tabari, Ibn Kathiir na Suyuti.
Abu Huraira anasimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.):
“Pepo na Jahannam zilikuwa na mzozo, kila kimoja kikijaribu kuonyesha ule ubora wake juu ya kingine.” Basi Jahannam ikazungumza: “Mimi nimependelewa kwa kuwepo kwa wale watu wenye kiburi na nguvu ndani yangu.” Pepo ikajibu: “Mimi sijui ni kwa nini hakuna mtu isipokuwa wale dhaifu na wanyenyekevu ndio walioingizwa ndani yangu!”
Hivyo Mwenyezi Mungu akaiambia Pepo:
“Wewe ndiye Msamaha Wangu, na kupitia kwako ninatoa msamaha kwa yeyote kati ya waja Wangu.”
Halafu Yeye akazungumza na Jahannam:
“Wewe ndio ghadhabu Yangu, na kupitia kwako wewe ninamuadhibu yeyote nitakaye kumuadhibu. Kila mmoja wenu atajaa.”
“Bali Jahannam haitajaa, hivyo Mwenyezi Mungu ataingiza mguu Wake ndani yake.”
Kisha Jahannam itagutia:
“Tosha! Inatosha!”
Ndugu wasomaji, teyari mmesha uelewa kuwa Allah ni kiumbe kama binadamu, kina Miguu na nyayo.
Mungu awabariki sana.
Katika Huduma yake,
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

UFARANSA YAFUNGA MISIKITI 2500 KWA KUHUSIKA NA UGAIDI


Ufaransa imefunga Misikiti 2500 yenye kufundisha chuki na kuchochea ugaidi.
Serikali ya Ufaransa imesema kuwa, hawata ruhusu chuki kufundishwa na Waislam wenye siasa kali. Hayo yalisemwa na Cazeneuve.
Tangazo hili lilitolewa baada ya Waziri Mkuu wa Ufaransa kuzuia misaada iliyo kuwa inaelekezwa kwenye hiyo Misikiti. Misaada hiyo ilikuwa inatoka nchi za Morocco, Algeria na Saudi Arabia.
Kwa habari kamili ingia hapa
.

UISLAM WAPIGWA MARUFUKU ANGOLA

Waziri wa Utamaduni, Rosa Cruz alisema kuwa, Uislam haujaruhusiwa na wala pewa ruhusa kishearia na Wizara ya Sheria na Haki za Binadamu nchini Angala.
Waziri Rosa alitwakumbusha wananchi wa Angola kuwa Wakristo ni Asilimia 95 nchini humo na nchi yao inautamaduni wa kikristo. Nukuu "We must remember that the country is made up to 95% Christian and has a rather Christian culture".
Hivyobasi, Serikali ya Angalo imeamua kuivunja Misikiti yote nchini humo ambayo ilijengwa kwa kuvunja Sheria za nchi. Misiki nchini humo ni haram na hairuhusiwi.
Kwa habari kamili na ya kina ingia hapa: http://ireport.cnn.com/docs/DOC-1063888

Jesus is good because He is God

 

TRENDING NOW