
Kwanza kabisa neno Kanisa linamaanisha "mkusanyiko wa waamini" kama ule wa Waisraeli chini ya Musa kwenye mlima Sinai walipopewa Amri za Mungu.
Neno hilohilo lilitumiwa na Wakristo wa kwanza kwa ajili yao wenyewe kusema wameshika nafasi ya Israeli kama taifa la Mungu hata wasipokuwa Wayahudi bali watu wa mataifa mengine.
Watu wengi siku hizi wanaelewa kanisa kumaanisha jengo. Huku si kuelewa kibibilia maan ya kanisa.
Neno “kanisa” maana ya asili yatoka kwa neno la Kiyunani ekklesia lili lo na maana ya “kusanyiko” au “walioitwa.” Maana ya asili ya “kanisa” sio ile ya jingo, bali ni watu. Ni kinaya kwamba unapowauliza watu ni kanisa gani wanashiriki, mara nyingi huwa wanajihushisha na jingo. Warumi 6:5, yasema, “…salimia kanisa linalokutana kwa nyumba.” Paulo anaashiria kanisa lilo katika nyumba yao- si jengo la kanisa bali mwili wa washiriki.
Wakristo walipoanza kujenga mahali pa ibada, pakaja kuitwa vilevile "kanisa" kwa sababu ndani yake lilikusanyika Kanisa hai.
Hivyo mara nyingi neno hilo linatumika kwa maana ya jengo, ambalo ni mfano mwingine uliotumiwa na Paulo kuhusu umoja wa Wakristo, ukiwa na Yesu kama jiwe kuu la msingi.
Majengo hayo ya ibada yanaweza kuwa na ubora tofauti hata upande wa sanaa; baadhi yake yanatembelewa na watalii na kuhifadhiwa kwa bidii kwa sababu hiyo.
Kwa namna ya pekee ni muhimu Kanisa kuu la kila jimbo (dayosisi), halafu Basilika na Patakatifu.
Jina hilo lilitumika kwa jumuia mama ya Yerusalemu, kwa kila mojawapo ya jumuia za Kikristo zilizotokana na umisionari wa wafuasi wa Yesu Kristo, na kwa umoja wao wa kimataifa uliotazamwa na Mtume Paulo kuwa Mwili wa Kristo, ukiwa na Yesu kama kichwa chake.
Kanisa ni mwili wa Kristo, ambapo ye ndie kichwa. Waefeso 1:22-23 yasema, “Akivitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.” Mwili wa Kristo umejengwa na wanaoamini katika Yesu Kristo toka siku ya Pentekosti (Matendo Ya Mitume 2) hadi Kristo arudi. Mwili wa Kristo uko na sehemu mbili:
1) Kanisa lote kwa ujumula ambalo ni wale wote wako na uhusiano na Kristo. “Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni Upendo” (1 Wakorintho 12:13). Aya hii inasema yeyote atakaye amini in sehemu ya mwili wa Kristo na ameupokea Roho wa Kristo ni ushaidi. Kanisa la jumla la Mungu ni wale wote ambao wamepokea wokovu kwa imani katika Yesu










