Thursday, November 17, 2016

MAANA YA KANISA


Kwanza kabisa neno Kanisa linamaanisha "mkusanyiko wa waamini" kama ule wa Waisraeli chini ya Musa kwenye mlima Sinai walipopewa Amri za Mungu.
Neno hilohilo lilitumiwa na Wakristo wa kwanza kwa ajili yao wenyewe kusema wameshika nafasi ya Israeli kama taifa la Mungu hata wasipokuwa Wayahudi bali watu wa mataifa mengine.
Watu wengi siku hizi wanaelewa kanisa kumaanisha jengo. Huku si kuelewa kibibilia maan ya kanisa.
Neno “kanisa” maana ya asili yatoka kwa neno la Kiyunani ekklesia lili lo na maana ya “kusanyiko” au “walioitwa.” Maana ya asili ya “kanisa” sio ile ya jingo, bali ni watu. Ni kinaya kwamba unapowauliza watu ni kanisa gani wanashiriki, mara nyingi huwa wanajihushisha na jingo. Warumi 6:5, yasema, “…salimia kanisa linalokutana kwa nyumba.” Paulo anaashiria kanisa lilo katika nyumba yao- si jengo la kanisa bali mwili wa washiriki.
Wakristo walipoanza kujenga mahali pa ibada, pakaja kuitwa vilevile "kanisa" kwa sababu ndani yake lilikusanyika Kanisa hai.
Hivyo mara nyingi neno hilo linatumika kwa maana ya jengo, ambalo ni mfano mwingine uliotumiwa na Paulo kuhusu umoja wa Wakristo, ukiwa na Yesu kama jiwe kuu la msingi.
Majengo hayo ya ibada yanaweza kuwa na ubora tofauti hata upande wa sanaa; baadhi yake yanatembelewa na watalii na kuhifadhiwa kwa bidii kwa sababu hiyo.
Kwa namna ya pekee ni muhimu Kanisa kuu la kila jimbo (dayosisi), halafu Basilika na Patakatifu.
Jina hilo lilitumika kwa jumuia mama ya Yerusalemu, kwa kila mojawapo ya jumuia za Kikristo zilizotokana na umisionari wa wafuasi wa Yesu Kristo, na kwa umoja wao wa kimataifa uliotazamwa na Mtume Paulo kuwa Mwili wa Kristo, ukiwa na Yesu kama kichwa chake.
Kanisa ni mwili wa Kristo, ambapo ye ndie kichwa. Waefeso 1:22-23 yasema, “Akivitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.” Mwili wa Kristo umejengwa na wanaoamini katika Yesu Kristo toka siku ya Pentekosti (Matendo Ya Mitume 2) hadi Kristo arudi. Mwili wa Kristo uko na sehemu mbili:
1) Kanisa lote kwa ujumula ambalo ni wale wote wako na uhusiano na Kristo. “Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni Upendo” (1 Wakorintho 12:13). Aya hii inasema yeyote atakaye amini in sehemu ya mwili wa Kristo na ameupokea Roho wa Kristo ni ushaidi. Kanisa la jumla la Mungu ni wale wote ambao wamepokea wokovu kwa imani katika Yesu

2) Lile Kanisa ya nyumbani vile emeelezwa katia Wagalatia 1:1-2: “Paulo, mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu), na ndugu wote walio pamoja name, kwa makanisa ya Galatia.” Hapa tunaona kwamba katika mkoa (mji) wa Galatia kulikuwa na makanisa mengi chenye tunaita makanisa ya nyumbani. Kanisa la Kibaptisiti, Kilutheri, Katholiki na mengine, si kanisa, vile iilvyo katika kanisa la ujumla, bali haya ni makanisa ya nyumbani (Mshambani/Mjini), ule mwili wa nyumbania wa waumini. Kanisa la jumla linajumlisha wale wote ni wa Kristo na wamemwamini kwa wokovu. Washirika wa kanisa la jumla lazima watafute kuwa na ushirika na kujengana wakiwa katika lile kanisa la nyumbani.
Kwa ufupi, kanisa si jengo ama dini. Kulingana na Bibilia, kanisa ni mwili wa Kristo-wale wote wameweka imani yao kwa Yesu Kristo kwa wokovu (Youhana 3:16; 1 Wakorintho 12:13). Kanisa la nyumbani ni kusanyiko la Wakristo wa kanisa la jumla. Kanisa la nyumbani ni mahali ambapo washirika wa kanisa la jumla wanaweza kutumia nguz0 ya “mwili” ya 1 Wakorintho 12: himizana, funzaneni, na kujengana ninyi kwa ninyi katika hekima na neema ya Bwana Yesu Kristo.
KRISTO ALIPENDA KANISA
Kanisa ni kitu hai. Ni watu wote wanaozaliwa tena na wanaokuwa na Roho Mtakatifu mioyoni mwao.
Kanisa lina majina mengi mengine katika Agano Jipya. Tuangalie majina haya kwa kutusaidia kufahamu vizuri kama
kanisa ni nini.
1. Kanisa linaitwa “KUNDI” (Yoane 10:16). Kabila la Wayuda lilikuwa zizi. Kanisa ni kundi. Katika Yoane 10:16 Bwana Yesu alisema, “Na nina kondoo wengine, wasio wa zizi hili, sharti niwalete vile na watasikia sauti yangu; na watakuwa kundi moja, na mchungaji mmoja.” Hivi neno hili KUNDI linatukumbusha ya kwamba Wakristo wanakaa pamoja na wanachungwa na mapendo na Mchungaji Mwema, wakisikia sauti Yake na wakimfuata.
2. Kanisa linaitwa vilevile “SHAMBA LA MUNGU” (1 Wakorinto 3:9). Kanisa ni shamba la Mungu na ndani yake anataka kupata matunda kwa utukufu Wake. Hivi jina hili linatukumbusha maneno ya kuzaa matunda kwa Bwana.
3. Kanisa linaitwa vilevile “JENGO LA MUNGU” (1 Wakorinto 3:9). Neno hili linatuonyesha ya kwamba Mungu ana kazi ya kujenga. Anaongeza mawe hai kwa Kanisa Lake. Inafaa tutoe maisha yetu kwa kazi hii ya kujenga Kanisa Lake kwani Yeye Mwenyewe anaweka roho sana juu yake.
4. Linaitwa vilevile “HEKALU LA MUNGU” (1 Wakorinto 3:16). Jina hili linatukumbusha mara moja maneno ya kuabudu, na ya kwamba Mungu anaabudiwa tu na wale walio katika Kanisa Lake wakati wa sasa.
5. “MWILI WA KRISTO” (Waefeso 1:22,23). Kwa njia ya mwili wake mtu anaonyesha mafikili na makusudi yake. Hivi Kristo alichagua Kanisa kwa kujionyesha ndani yake kwa dunia leo. Wakati tunapofahamu neno hili, hatutafikili tena ya kwamba maneno ya Kanisa ni kitu kidogo, lakini tutajitoa kabisa kwa kusaidia mwili wa Kristo, ndilo Kanisa kwa njia yo yote tunayoweza.
KANISA LA MUNGU NI TAKATIFU
(1 Wakorinto 3:17).
Mungu anaita katikati ya mataifa watu kuwa watu Wake. Anawaweka mbali na dunia ya zambi na anataka watembee kwa utakatifu. Kwa njia ile tu Kanisa linaweza kuonyesha Mungu mtakatifu kwa dunia hii ya zambi.
KRISTO NI KICHWA CHA MWILI,
NDILO KANISA
Namna gani waamini wanaweza kuonyesha neno hili?
1. Kwa njia ya kukataa kuwa na mtu wa dunia kuongoza.
2. Tunaonyesha wazi ya kwamba Kristo ni Kichwa cha kanisa wakati tunapompa njia kutawala na kuongoza kazi zote za kanisa na kukata maneno yote. Labda watu wanaweza kuuliza, “Neno hili litawezekana namna gani? Namna gani Bwana aliye mbinguni ataweza kuongoza kanisa lililo hapa duniani?” Lakini tunajua kabisa ya kwamba watu wakimngojea na saburi kujua mapenzi Yake, atayafunua kwao.
Ndiyo, neno hili linaomba saburi na maombi. Ni nyepesi zaidi kuongoza maneno sisi wenyewe. Lakini tukumbuke ya kwamba tunaweza kutimiza utaratibu wa Agano Jipya kwa njia ya uwezo wa Roho Mtakatifu tu, na wale wasio tayari kumtegemea Yeye na kuomba na kumngojea na saburi hawataona namna gani Kichwa cha Kanisa, ndiye Kristo, anaongoza kanisa la pahali fulani hapa duniani.
3. Tusiseme na kinywa tu ya kwamba Kristo ni Kichwa cha Kanisa na halafu kubisha neno lenyewe na matendo yetu. Kuna wengine wanaosema na nguvu yote ya kwamba Kristo ni Kichwa cha Kanisa, lakini masemo yao ni bule
kwani wao wenyewe wanatawala kanisa na nguvu. Wanajifanyiza kuwa kama wafalme katika kanisa. Diotrefe alikuwa mtu wa namna hii (3 Yohana 9,10). Alitaka sana kuwa mtu wa kwanza. Alisema maneno mabaya juu ya watu
wa Mungu kama Yoane na alikataa kuwapokea. Alikataza hata watu wengine kuwapokea, na kama waliwapokea hata hivi, aliwafukuza toka kanisa. Neno namna hii linakana ya kwamba Kristo ni Kichwa cha Kanisa.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo
Shalom

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW