Thursday, May 4, 2017

ALLAH KAKIRI KWENYE QURAN KUWA YEYE SIO MUNGU


Naam, ngoja nimzike Allah leo kwa kutumia Quran yake dhaifu sana.
Waislam huwa wanaleta hii aya kupinga Uungu wa Yesu, au sio. Hebu tuisome aya kwanza.
Surat Al Maida 116. Na pale Mwenyezi Mungu atakapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Ati wewe uliwaambia watu: Nifanyeni mimi na mama yangu kuwa ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu? (Na Isa) atasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hainifalii mimi kusema ambayo si haki yangu. Ikiwa nilisema basi bila ya shaka umekwisha yajua. Wewe unayajua yaliyo ndani ya nafsi yangu, lakini mimi siyajui yaliyo katika nafsi yako. Hakika Wewe ndiye Mjuzi mkubwa wa yaliyo fichikana.
SASA NAANZA KUICHAMBUA AYA TARATIIIIB:
1. Allah anasema: NA PALE MWENYEZI MUNGU ATAKAPO SEMA;
Hivi kama kweli Quran ni maneno ya Allah, kwanini asisema na pale NITAKAPO SEMA? Lakini Allah anaonyesha kuwa yeye sie Mwenyezi Mungu. Maana Allah anamnukuu Mwenyezi Mungu.
2. Isa anajibu: WEWE UMETAKASIKA. Isa ATAMJIBU MWENYEZI MUNGU, na sio Allah. Maana Allah alikuwa anamnukuu Mwenyezi Mungu.
3. Wapi Wakristo wanasema kuwa Mama yake Yesu ni Mungu? HUU NI UONGO WA ALLAH. Hakuna aya hata moja kwenye Biblia inasema kuwa Maria mama ya Yesu ni Mungu.
HUU NI MSIBA MKUBWA SANA NA UNAWANYIMA WAISLAM WOTE USINGIZI. NAAM HABARI YA MUJINI NDIO HII. LEO ALLAH KAJISAHAU NA KUMNUKUU MWENYEZI MUNGU.
KUMBE ALLAH SIO MWENYEZI MUNGU.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

Wednesday, May 3, 2017

ROHO MTAKATIFU NA KAZI ZAKE KWETU SOMO LA 1

Image may contain: bird, cloud and text
ROHO MTAKATIFU, MTOA UTAKATIFU
Katika somo la kwanza katika mfululizo wa masomo haya yanayohusu Roho Mtakatifu, Tulijifunza kwamba Roho Mtakatifu, ni mtakatifu, hivyo anakuwepo na kudumu mahali palipo na utakatifu tu.Tukiwana maisha ya uchafu, yaani dhambi; humfanya Roho Mtakatifu akose makao kwetu,na hivyo hawezi kuwepo kwetu.Kama alikuwepo mwanzo kwetu,huondoka (1Samweli 16:14; Zaburi 51:4,10-11).
Sasa swali linakuja, tunawezaje kuwa watakatifu katika maisha yetu ili Roho Mtakatifu afanye makao kwetu?
Jibu ni kwamba, Roho Mtakatifu , ndiye huyohuyo anayetoa utakatifu tunaouhitaji. Sasa tunamwangalia Roho Mtakatifu kama Mtoa Utakatifu,kwa kutafakari kazi yake hiyo katika vipengere vitano:-
1. ROHO MTAKATIFU,ROHO ATUPAYE KUZALIWA MARA YA PILI
2. ROHO MTAKATIFU ROHO AWAFUFUAYE WATU WALIOKUFA KIROHO
3. ROHO MTAKATIFU, ROHO AWATIAYE UZIMA WATU WALIOZIMIA KIROHO
4. ROHO MTAKATIFU ROHO ATUPAYE UTAKASO
5. ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUPAYE TUNDA LA ROHO
1. ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUPAYE KUZALIWA MARA YA PILI.
Hatupaswi kamwe kudanganyika kwamba utakatifu siyo duniani ni mbinguni, tu, maandiko yanaeleza waziwazi kwamba watakatifu walioko duniani ndiyo anaopendezwa nao Mungu (Zaburi 16:3).
Hatupaswi pia kudanganyika kwamba tunaweza kufanya dhambi hapa duniani, halafu tukasalimika baada ya kufa, kutokana na misa ya wafu n.k (1Wakorintho 6:9-10; Waefeso 5:5-7; Wagalatia 6:7 ; Waebrania 9:27; IYohana 5:16; Kumbukumbu 10:17) la maana hapa ni kufahamu ni jinsi gani tunavyoweza kuwa na ushindi dhidi ya dhambi hapa duniani,na kuokoka kutupwa motoni, maana bila shaka tunatakiwa kuokoka tukiwa hapahapa duniani (Luka 19:8-10);Tito 3:3-4)
Tunawezaje kuwa na ushindi dhidi ya dhambi?
Ni kwa kuzaliwa mara ya pili, kwa Roho Mtakatifu (Yohana 3:3-10; Tito 3:3-5) Yesu Kristo, alijaribiwa sawasawa na sisi lakini hakutenda dhambi (Waebrania 4:14-15).
Ni nini siri ya ushindi wake huo?
Ni kwa sababu alizaliwa kwa Roho Mtakatifu, yaani alizaliwa tofauti na kawaida ya kimwili ya mume na mke. Sisi nasi tunapotubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha, tunapata rehema hii kwa imani tu (Mithali 28:13).
Tunazaliwa mara ya pili katika ulimwengu wa roho, na hivyo kuwa na uwezo wa kushinda dhambi kwa muujiza mkubwa. Katika hali ya kawaida ya jinsi tulivyozaliwa kimwili, kamwe hatuwezi kushinda dhambi. Ni mpaka tufanyike viumbe vipya kwa Roho Mtakatifu. Mwambie Roho Mtakatifu kwamba unataka kuzaliwa mara ya pili,naye atafanya.
USIKOSE SEHEMU YA PILI:
2. ROHO MTAKATIFU ROHO AWAFUFUAYE WATU WALIOKUFA KIROHO
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

MUNGU HANA DINI

Image may contain: text
Mungu Mtakatifu hana ushirika na dhambi. Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi. Mwanadamu hujaribu kumfikia Mungu kwa nija nyingi: DINI, matendo mema, sala, n.k., lakini hizi zote hazitoshi. Mwanadamu bado ni mwenye dhambi.
Dini ni jaribio la mwanadamu kuwa na uhusiano na Mungu. Imani ya kikristo ni uhusiano na Mungu kwa sababu yale ametufanyia kupitia kwa kusulubiwa kwa Yesu Kristo.
Sasa basi, ukisoma katia Taurat, au Zaburi au Injir hatusomi sehemu yeyote ile ambayo Mungu anasema kuwa watu waanzishe dini, bali tunasoma kuwa Mungu anawaambia watu wamfuate yeye. Ndio maana nasema Mungu hana dini.
Adam na Hawa hawakuwa na dini na hakuna ushahid katika Taurat na au Pentateuch kuwa Adam alikuwa na dini.
Musa Hakuwa na dini na hakuna ushahidi katika Taurat na au Pentateuch kuwa Musa au Abraham walikuwa na dini.
Daudi hakuwa na dini na hakuna ushahid katika Zaburi kuwa Daudi alifuata dini na au alikuwa na dini.
Hiyo hapo juu ni mifano michache tu ya kukufungua macho kuwa Mungu hana dini na wala hakuwaambia watu wawe na au waanzishe dini.
Kuna njia moja tu ya kushirikiana na Mungu . .
YESU KRISTO NI NJIA YA PEKEE YA KUONDOA DHAMBI.
Alikufa kwa ajili yetu ili tujue upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yetu. Yohana 14:6. Yesu ndie Njia.......
ALIKUFA ILI ATULETE KWA MUNGU
Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu.1 Petro 3:18
YESU YU HAI
Kristo alikufa kwa ojili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alitufuka siku ya tatu, kama yanenavyojil maandiko.1 Wakorintho 15:3,4
YESU NDIYE NJIA YA PEKEE
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.Yohana 14:6
Mwanadamu peke yake hawezi kushirikiana na Mungu. Mungu alimtuma Yesu afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu na tena awe daraja kati yetu na Mungu ili atulete kwa Mungu.
INAKUPASA KUMPOKEA YESU AWE MWOKOZI NA MTAWALA WAKO. Ndipo utajua upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yako.
UNAMPOKEA KRISTO KWA IMANI
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.Yohana 1:12
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.Waefeso 2:8,9
INAKUPASA KUMKARIBISHA YESU, MAISHANI MWAKO
Tazama, nasimama milangoni, nabisha, mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake . . .
UNAWEZA KUMPOKEA KRISTO SASA
Mungu anaufahamu moyo wako. Yafuatayo katika sala hii yanaweza kukusaidia kumpokea Kristo ukiomba kwa moyo wa kweli.
Bwana Yesu Kristo, ninakuhitaji, mimi ni mwenye dhambi. Nimekubali kwamba nimejitawala maisha yangu mwenyewe, na kutengana nawe. Asante kwa kifo chako msalabani kwa ajili ya dhambi zangu na kwa kunisamehe zote. Sasa nageuka na kutubu. Bwana, nakuomba uingie ndani ya maisha yangu na kunitawala kabisa. Badili maisha yangu yawe kama upendavyo wewe. Amin.
KWA KUWA SASA UMEMPOKEA YESU
Tangu ulipompokea Kristo mabadiliko mengi yametokea.
Yesu ameingia katika maisha yako. (Ufunuo 3:20)
Umesamehewa dhambi zako. (Wakolosai 1:14)
Umefanyika kuwa mwana wa Mungu. (Yohana 1:12)
Utazidi kujua makusudi ya Mungu kwa maisha yako. (2 Wakorintho 5:14,15,17)
JINSI YA KUKUA KIROHO
Kama mtoto mchanga unahitaji kukua
Utaendelea vizuri katika maisha ya kiroho ukiyafuata mashauri yafuatayo kila siku:
Zungumza na Mungu kwa maombi (Yohana 15:7)
Soma Neno la Mungu (Matendo 17:11)
Uwe mwaminifu kwa Mungu (Yohana 14:21)
Mshuhudie Kristo kwa matendo yako na maneno yako (Mathayo 4:19 na Yohana 15:8)
Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako (1 Petro 5:7)
Umruhusu Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-18 na Matendo 1:8)
NI MUHIMU KWA WAKRISTO KUSHIRIKIANA
Biblia inatuambia kukusanyika pamoja (Waebrania 10:25)
Ebu, tutumie mfano wa moto. Kuni nyingi zikirundikwa pamoja zinawaka vizuri sana, lakini ukiuondoa ukuni mmoja na kuuweka peke yake utapoa. Vile vile wewe haifai kuishi maisha ya kikristo peke yako.
Ukishirikiana na watu wengine ambao wamempokea Yesu kuwa Mwokozi wao utazidi kuwa na moto wa imani.
Uhudhurie kanisa ambapo watu wanaiamini Biblia kuwa ni kweli na Yesu anatukuzwa.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

UKRISTO SIO DINI BALI NI IMANI YENYE USHIRIKA NA MWENYEZI MUNGU






Ndugu msomaji,
Mara nyingi katika mihadhara ya Waislam, kumekuwa na maneno ya kusengenya Ukristo, eti, Uislam ndio dini ya Allah na Ukristo sio dini. Maneno hayo yamekuwa yakiwaumiza sana Wakristo, hasa pale wanapoambiwa walete aya kutoka Biblia inayo sema kuwa Ukristo ni Dini.
Ndugu zanguni, leo ningependa kujibu hii shutuma dhaifu na isiyo na msingi ya kuusingizia Ukristo na kumsingizia Mwenyezi Mungu kuwa anayo dini.
ASILI YA NENO UKRISTO NI NINI?
Neno Ukristo ni tegemezi ya kutoka kwa Jina "KRISTO". Hivyobasi, Mkristo ni mfuasi wa Kristo. Ni kama unavyoweza sema Mtanzania anatoka Tanzania na/au neno Mtanzania ni tegemezi kutoka Tanzania au Utanzania litakoka kwenye muungano wa U na Tanzania.
Lengo la Mkristo ni kutafuta ushirika wa karibu na Mungu. Ushirika huo unawezeshwa na kazi aliyoifanya Yesu pamoja na huduma ndani ya maisha ya Mkristo ya Roho Mtakatifu.
Mungu Mtakatifu hana ushirika na dhambi na wala hana dini. Kati yake na mwanadamu kuna ufa mkubwa wa dhambi. Mwanadamu hujaribu kumfikia Mungu kwa nija nyingi: DINI, matendo mema, sala, n.k., lakini hizi zote hazitoshi. Mwanadamu bado ni mwenye dhambi.
MAANA YA UKRISTO NI NINI?
Ukristo ni imani maalum kulinganisha na nyinginezo, Kwa sababu inasimamia zaidi ushirika na Mungu kuliko matendo ya kidini. Kinyume na kushikilia orodha ya masharti ya fanya haya na usifanye yale, Lengo la mkristo ni kutafuta ushirika wa karibu na Mungu Baba.
Wakristo huamini ya kuwa Biblia ni Neno la Mungu na mafundisho yake ndiyo mamlaka ya mwisho (Timotheo wa pili 3:16, Petro wa pili 1: 20-21). Wakristo huamini juu ya Mungu mmoja akaaye katika utatu, Baba na Mwana (Yesu kristo), na Roho Mtakatifu.
Wakristo huamini ya kuwa Biblia ni Neno la Mungu na mafundisho yake ndiyo mamlaka ya mwisho (Timotheo wa pili 3:16, Petro wa pili 1: 20-21). Wakristo huamini juu ya Mungu mmoja akaaye katika utatu, Baba na Mwana (Yesu kristo), na Roho Mtakatifu.
NINI MAANA YA DINI:
Dini ni jaribio la mwanadamu mwenye dhambi kuwa na uhusiano na Mungu Mtakatifu. Imani ya kikristo ni uhusiano na Mungu kwa sababu yale ametufanyia kupitia kwa kusulubiwa kwa Yesu Kristo.
UKRISTO SIO DINI BALI NI IMANI MAALUM INAYO SIMAMIA ZAIDI NA KUSHIRIKIANA NA MUNGU KULIKO MATENDO YA KIDINI AMBAYO HAYATO KUFIKISHA MBINGUNI.
Kuna njia moja tu ya kushirikiana na Mungu .
YESU KRISTO NI NJIA YA PEKEE YA KUONDOA DHAMBI.
Alikufa kwa ajili yetu ili tujue upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yetu.
IMANI YA KWELI NI IPI?
Imani ya kweli sio ile ya kuangazia sheria bali ya kanuni. Imani ya kweli ni uhusiano na Mungu. Mambo mawili ambayo dini zote zashikilia ni kwamba mwanadamu kwa njia moja au nyingine ametengwa kutoka kwa Mungu na anahitaji kupatanishwa Naye. Dini za uongo zatafuta kuzuluhisha shida hii kwa kutunza sheria au kanuni. Imani ya kweli yazuluhisha tatizo kwa kutambua kwamba ni Mungu pekee anaweza kurekebisha utengano, na amekwisha fanya. Imani ya kweli yatambua yafuatayo:
• Wote tumetenda dhambi na kwa hivyo tumetenganishwa na Mungu (Warumi 3:23).
• Kama hautarekebishwa, adhabu ya haki ya dhambi ni mauti na utengano na Mungu wa milele baada ya kufa (Warumi 6:23).
• Mungu alikuja kwetu kupitia Kristo Yesu na akafa kwa ajili yetu, akachukua adhabu ambayo tulistahili, na akafufuka kutoka kwa wafu ili adhihirishe kuwa kifo chake kulikuwa dhabihu iliyotosha (Warumi 5:8; 1Wakorintho 15:3-4; 2Wakorintho 5:21)
• Kama tutampokea Yesu kama mwokozi wetu, kuamini kifo chake kama fidia kamili ya dhambi zetu, tumesamehewa, tumeokolewa, kombolewa, patanishwa na kufanywa wenye haki na Mungu (Yohana 3:16; Warumi 10:9-10; Waefeso 2:8-9).
Kwa hivyo, huku dini nyingine zikitaka waumini wao watende mambo Fulani Fulani au wasitende mambo Fulani Ukristo ni juu ya kuwa na ushirika na Mungu.
Hivyo Basi, Ukristo ni Ufuasi wa Kristo ambaye ni Mungu. Yesu Kristo ni Mungu.
Max Shimba Ministries
Copyright © Max Shimba Ministries 2015
www.maxshimbaministries.org

KISA CHA MAMA MSAMARIA.

Image may contain: cloud, night and text
Kulikuwa na mama mmoja msamaria, mama huyu alikuwa akiishi eneo la baridi kali..siku moja alipokuwa akiota moto ndani katika nyumba yake ya vioo ndipo akaona ndege kwa nje’,ndege huyu alikuwa katika hali ya kuelekea kufa kutokana na baridi ingawa hatimaye ndege huyo alitimiza hatua ya kwanza ya furaha ya mama huyo kwa kutua kwenye mti mkubwa ulioota nje ya dirisha dogo la nyumba yake, na ndipo mama huyu akachukua mti mwingine mrefu anaoutumia kuchochea moto ndani na kuupitisha kwenye dirisha hilo ili ukaungane na ule wa nje na kutengeneza daraja na hatimaye kumwezesha ndege huyo kupita na kuingia ndani ili kujinusuru’…lakini ndege huyo alipoona mti huo ukichomoza toka kwenye dirisha hilo alihofu kwa kufikiri kuwa huenda ni mtu anayetaka kumpiga ili hatimaye kumfanya kitoweo na kwasababu hiyo ndege huyo aliruka na kutokomea kwenye baridi zaidi na hatimaye akafa huko’
Tamko la mama msamaria, alibaki kusema:- Laiti kama ningelikuwa na uwezo wa kujimithilisha’ nikawa mfano wa yule ndege’ ningelimsogelea na kumwambia’ ndege wenzangu eeeeh twende mule ndani tujinusuru na baridi!!!!!!
Kisa hicho kinaweka mkazo na kutoa mwangaza juu umuhimu wa tendo hilo la Bwana Yesu kuvaa umbile la kibinadamu katika harakati za kumfikia na kumwokoa mwanadamu, ambapo tunaona jinsi ambavyo haikuwa rahisi kwa mama msamaria kufanikisha dhamili yake ya kumwokoa yule ndege kwa njia ya kutumia mti ambao kimsingi kwa ndege huyo ulikuwa ni kitisho.
Kumbuka kuwa endapo Bwana Yesu angelikuja katika halihalisi ya utumkufu wake wa Kimungu wanadamu wangelihofu na kuangamia kama ambavyo tunaweza kuliona hilo katika mifano kadhaa ya matukio katika Biblia, soma historia hii ya kipindi cha wana wa Israel kwa utulivu:-
Kutoka 19:11-12
wawe tayari kwa siku ya tatu; maana siku ya tatu Bwana atashuka katika mlima wa Sinai machoni pa watu hawa wote17 Musa akawatoa hao watu katika kituo, akawaleta ili waonane na Mungu; wakasimama pande za chini za kile kilima. 18 Mlima wa Sinai wote pia ukatoa moshi, kwa sababu Bwana alishuka katika moto; na ule moshi wake ukapanda juu kama moshi wa tanuu, mlima wote ukatetemeka sana.19 Na hapo sauti ya baragumu ilipozidi kulia sana, Musa akanena, naye Mungu akamwitikia kwa sauti.20 Bwana akaushukia mlima, juu ya kilele cha mlima; Bwana akamwita Musa aende hata kilele cha mlima; Musa akapanda juu. 21 Ndipo Bwana akamwambia Musa, Shuka chini, uwaonye watu wasije wakapasua njia waje kwa Bwana kutazama,kisha wengi miongoni mwao wakaangamia.
Katika andiko hilo tunaona historia hiyo ya kile kilichowapata wana wa Israel ambao kimsingi walitoa madai ya kutaka kuonana na Mungu, na katika tukio hilo la kushuka kwa Mwenyezi Mungu ili kujifunua kwao wa Israel wengi walikufa kutokana na Mungu huyo kuja katika hali ambayo hawakuweza kuikabili.
Swali! Je’ Mungu aje katika hali gani ili mwadamu aweze kuikabili?
- Aje katika hali ya ng’ombe!
- Au aje katika hali ya simba! Au hali gani?
Biblia inataja namna Mungu alivyojidhihirisha kwa Kristo katika hali ambayo mwanadamu aliweza kuikabili.
1Timotheo 3:16
Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Hivyo maandiko hayo ya Biblia yantaja njia hiyo ambayo Mungu aliitumia kujidhihirisha kwa wanadamu yaani kwa kutwaa mwili wa kibinadamu ingawa haki yake ilijulikana katika ulimwengu wa roho.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

ROHO MTAKATIFU NA KAZI ZAKE KWETU SOMO LA 2

Image may contain: bird, cloud and text
ROHO MTAKATIFU ROHO AWAFUFUAYE WATU WALIOKUFA KIROHO
Kurudi nyuma na kuacha wokovu kunaitwa pia kufa kiroho (Ufunuo 3:1;Waefeso 2:1). Kwa kila aliyerudi nyuma na kuacha wokovu, hii ni saa ya kuamka usingizini na kuanza upya (Warumi 13:11-12).
Lakini, je, inawezekana kuanza upya tena katika hali hii?
Ndiyo, kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Hii ni kazi yake nyingine. Roho Mtakatifu ndiye aliyemfufua Yesu, alipokufa
 (Warumi 13:11).
Kwa jinsi hiyo hiyo, Roho Mtakatifu anaweza kutufufua kiroho na kutupa uhai tena wa kiroho (Waefeso 2:1,4-6). Mwambie Roho Mtakatifu kwamba unataka kufufuliwa kiroho, naye atafanya.
ROHO MTAKATIFU, ROHO AWATIAYE UZIMA WATU
Kabla ya kufa kiroho, hutangulia kuzimia kiroho. Shetani hutupeleka hatua kwa hatua, kama upepo katika tairi unavyotolewa kidogo kidogo kutokana na pancha ndogo.
Tukizimia kiroho, upendo wa kwanza unatoweka. Ingawa bado hatujafikia hali ya kufanya dhambi za uzinzi, uasherati, ulevi n.k kama mataifa, hata hivyo, mambo ya rohoni yanakuwa hayana mvuto kwetu kama mwanzo. Kuomba, kushuhudia, kuhudhuria ibada n.k, yanakuwa mzigo kwetu. Tunaanza kuvutwa zaidi na mambo ya dunia. Katika hali hii tunahitaji nguvu mpya, uzima mpya (Isaya 40:28-31). Anayefanya kazi hii pia ni Roho Mtakatifu, Roho wa uzima (Warumi 8:2). Pepo wa udhaifu wanatolewa kwa Roho wa Mungu (Mathayo12:28), na vivyo hivyo udhaifu wetu kiroho unatolewa na Roho wa Mungu.
Je umezimia kiroho, Mwambie Roho Mtakatifu akuzindue, naye atafanya.
ROHO MTAKATIFU ROHO ATUPAYE UTAKASO
Baada ya kuokolewa,tunahitaji pia kutakaswa.Bila utakaso, tutajikuta bado hatuna ushindi dhidi ya dhambi za ndani katika mawazo, na moyoni,ingawa tayari tuna ushindi dhidi ya dhambi za kutenda. Dhambi za ndani ,ni kama hasira, wivu ,chuki, masengenyo, kugombania ukubwa, kiburi, majivuno, kutokusamehe, kinyongo, kupenda udunia n.k.
Hivi vinaweza vikaonekana kwa watu waliookoka ambao hawajatakaswa: Mawazo yasiyo ya ki Mungu (Mathayo 16:21-23), kugombania ukubwa (Luka 22:24-26; Mathayo 20:20-22,25-28; Marko 9:30-37), hasira (Mathayo 20:24) wivu, fitina, ugomvi (Marko 9:38-39; Luka 9:49-50; 1Wakorintho 3:3-5), faraka na matengano (1Wakorintho1:10-13), umimi (Mathayo 28:6-13), kutokusamehe (Mathayo 18:21-35), chuki,kushindwa kuvumilia maudhi,kushtakiana wapendwa mahakamani (Luka 9:51-56; 1Wakorintho 6:1-8); Warumi 7:15 n.k . Mambo haya huondolewa kwa utakaso.
Ndiyo maana Yesu aliwaombea Utakaso wanafunzi wake waliokuwa tayari wameokoka (Yohana 17:14-19) Roho mtakatifu ndiye atupaye Utakaso (1Wakorintho 6:11; 1Petro1:2) Je, hujatakaswa, mwambie Roho Mtakatifu akutakase, yeye ni waminifu, atafanya (1Thesalonike 5:23-24)
ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUPAYE TUNDA LA ROHO
Katika Wagalatia 5:22-23, tunajifunza juu ya tunda la Roho. Katika lugha ya asili,yote katika mistari hii yanamaanisha kwamba Tunda la Roho ni moja tu,Upendo. Hata hivyo,upendo huo unadhihirishwa kwetu katika tabia na matendo kama furaha, amani, uvumilivu, utu wema,f adhili, imani, upole, na kiasi. Ni pale tu tunapokuwa na maisha yaliyojaa upendo, ndipo tunapokuwa tunatimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yetu.
Pasipo upendo, tunakuwa shaba iliayo na upatu uvumao, tunakuwa si kitu. Lolote jingine tunalolifanya linakuwa halina faida (1Wakorintho 13:3). Hatuwi wanafunzi wa Yesu (Yohana 15:8) Sasa basi , ni muhimu kufahamu kwamba upendo ni tunda la Roho, tunalolipokea kutoka kwa Roho Mtakatifu.
Tukilipokea tunda hili, na kukua kila siku katika upendo (1Wathesalonike 3:12), Kama matunda yanavyokua, ndipo tunapokuwa wanafunzi wa Yesu kwelikweli.Tukiwa na tunda la Roho la upendo, tunakuwa na Furaha ya wokovu ambayo haiwezi kuondoka kwetu kwa sababu ya majaribu yoyote au kukosekana kwa lolote la kimwili (Yakobo1:2). Tutakuwa na amani ipitayo fahamu zote (Wafilipi 4:7) inayotuwezesha kuwa na amani na watu ambao tusingeweza kuwa na amani nao.
Tutakuwa na lengo la kutafuta amani na watu wote wakati wote (Waebrania 12:14) Tutakuwa na uvumilivu wa kipekee katika mateso, makwazo kutoka kwa watu n.k Tutakuwa na utu wema kwa watu wengine hata wale ambao hawajaokoka (Marko 10:17). Tutakuwa na fadhili yaani hali ya kutaka wakati wote watu wanaotuzunguka wawe na furaha.
Tutakuwa watu tuliojaa imani,tusiotetereka kirahisi.Tutakuwana upole yaani unyenyekevu (Mathayo 11:29; Wafilipi2:5-8) Na pili tutakuwa na kiasi (self-control)yaani uwezo wa kukataa kufanya lile ambalo Yesu hataki, kwa gharama yoyote.
Je, unataka kuwa na tunda la Roho katika maisha yako?Mwambie Roho Mtakatifu, naye atafanya.
USIKOSE SOMO LA 3: ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUSAIDIAYE KUOMBA
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

MUHAMMAD ALIMKUFURU ROHO MTAKATIFU NA KUTENDA DHAMBI ISIYOSEMEHEKA

Image may contain: text
Leo nitawajibu Waislam wote duniani kwa kutumia Biblia Takatifu kuwa Muhammad alimkufuru Roho Mtakatifu ambaye alihaidiwa na Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wetu.
Bwana Yesu amesema kwamba: "...Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho Mtakatifu hawatasamehewa." - (Mathayo 12:31)
Je! Nini maana ya KUMKUFURU Roho Mtakatifu?
Tukianza na neno KUFURU, maana yake ni: Kusema maneno yakumtukana Roho Mtakatifu ambaye ni Mungu au kufanya matendo yanayomtukana Roho Mtakatifu. Tukiendelea kusoma Mathayo 12:32 tunaona Bwana Yesu anasema kwamba:
"Naye mtu ye yote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao." (Mathayo 12:32)
Dhambi ya kumkana Roho Mtakatifu, ni dhambi ambayo haiwezi kusamehewa.
Kufuru dhidi ya Roho Mtakatifu haitasamehewa kwa wanadamu, Mathayo 12:31–32 (Marko. 3:29; Luka 12:10).
MUHAMMAD AMEMTUKANAJE ROHO MTAKATIFU?
"Kwa maana HAO WALIOKWISHA KUPEWA NURU, na KUKIONJA KIPAWA CHA MBINGUNI, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, HAIWEZEKANI KUWAFANYA UPYA TENA HATA WAKITUBU; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na KUFEDHEHESHA kwa DHAHIRI." (Waebrania 6:4-6)
Tumeona hapo Biblia Takatifu imesema kuwa: "...wakaanguka baada ya hayo, HAIWEZEKANI KUWAFANYA UPYA TENA HATA WAKITUBU..." (Ebrania 6:6) ni kwa sababu wamefanya "...KUFEDHEHESHA kwa DHAHIRI." Wamezitukana kazi za Roho Mtakatifu ambaye ni Mungu kwa makusudi; dhambi hiyo ndiyo Yesu anasema kamwe haitasamehewa. Biblia Takatifu inazidi kusema kwamba:
"Maana, kama TUKIFANYA DHAMBI KUSUDI baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, HAITABAKI TENA DHABIHU KWA AJILI YA DHAMBI; bali kunakuitazama hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao. Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma... Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano ALIYOTAKASWA KWAYO kuwa ni kitu ovyo, na KUMFANYIA JEHURI Roho wa neema?" (Waebrania 10:26-29)
UTHIBITISHO WA KWANZA:
Yohana 1 aya ya 32 inasema: Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake "YESU".
Wote tunafahamu kuwa Muhammad hakuwa Mtakatifu na vile vile hakuwa anapaa kama ndege na alikuja miaka 600 baada ya Kristo, hivyo basi, ni dhahiri kuwa Roho Mtakatifu sio Muhammad ambaye alikuja miaka 600 baadae. Yohana hakuwai mwona Muhammad.
Waislam wanaposema kuwa Roho Mtakatifu ni Muhammad au Jibril, huko ni KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU ambaye ni Mungu.
UTHIBITISHO WA PILI:
Yohana 1:33, [ Yohana Mbatizaji anaendelea kusema] "Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu."
Yohana anaweka kiuwazi zaidi aya hiyo hapo juu kuwa Yesu ndie atakaye kuwa anabatiza kwa Roho Mtakatifu.
Kwa kifupi Yesu atamtuma ROHO ambaye ni Mwenye Nguvu ya Mungu na ni Mungu.
Je, Muhammad ni huyo Roho?
HAPANA KABISA, kwasababu Yesu aliwabatiza Wanafunzi wake na zaidi ya hapo, wafuasi wake walibatizwa kwa Roho Mtakatifu katika siku ya Pentekoste. Mda mchache baada ya Yesu kupaa kwenda kwa Baba yake Mbinguni, hivyo basi, na narudia tena, hii ilifanyika Miaka mia sita 600 kabla ya Muhammad kuzaliwa. Wanafunzi wa Yesu hawakubatizwa kwa kupitia Muhammad wala Waislam hawabatizi au batizwa.
Hivyo basi, Waislam kwa kumdhihaki Roho Mtakatifu ni KUFURU, na kumfanya Muhammad kuendelea na dhambi ya KUKUFURU ROHO MTAKATIFU.
UTHIBITISHO WA TATU:
Yohana 3 aya ya 5 inasema: Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.
Nauhakika hakuna Muislam duniani pote anayeweza kusema kuwa Muhammad anazaa, maana katika ya hapo juu Yesu anasema Mtu lazima azaliwe kwa Roho, JE, MUHAMMAD ALIZAA/ANAZAA?
Je, Waislam wanazaliwa kwa Maji na Roho? Naam teyari wamesha kufuru Roho Mtakatifu.
UTHIBITISHO WA NNE:
Yohona 3 aya ya 6 inasema: Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
Hapa Muhammad anatupwa nje mara moja kwasababu ya haya maneno ambayo Yesu ameyasema, kwasababu
#1 Muhammad alikuwa binadamu, mbaya zaidi hivi sasa amekufa -marehemu.
#2 Kwasababu tena, Roho inazaa kwa kutumia Nguvu ya Mungu, ambaye ni Roho Mtakatifu. Huku kuzaliwa kwa Roho kulianza miaka 600 kabla ya Muhammad kuzaliwa.
UTHIBITISHO WA TANO:
Yohana 3 aya ya 8 inasema: Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.
HAKUNA HATA MMOJA WETU ALIYE ZALIWA KUPITIA MUHAMMAD. Hivyo basi Muhammad anashindwa tena kuwa Roho ya Kweli na kuendelea kumkufuru Roho Mtakatifu.
UTHIBITISHO WA SITA:
Yohana 3 aya ya 34 inasema: Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.
Je, Muhamamd alikuwa hana kipimo?
Hapo tena Muhammad kashindwa maana alikuwa amepimiwa maneno tu na Allah wake. Muhammad alikiri kuwa yeye hajui Mungu atamfanya nini baada ya kifo, pale alipo ulizwa na watu, je, nini kitatokea baada ya kifo. Muhammad hakuwa "omniscient".
UTHIBITISHO WA SABA:
Yohana 4 aya ya 24 inasema: Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Mungu sio Muhammad, asante Mungu, kwa kuweka huu ukweli kuwa Roho Mtakatifu ni Mungu. Kumbe hata Jibril sio Roho Mtakatifu.
UTHIBITISHO WA NANE:
Yohana 6 aya ya 63 inasema: Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Muhammad hawezi kutoa uzima wa milele, ni kitu ambacho Mungu peke yake anaweza kukupa. Ndio maana tunajua kuwa Yesu ni Mungu, kwasababu, Yesu anatoa uzima wa Milele kwa wale wote wamwaminio.
UTHIBITISHO WA TISA:
Yohana 7 aya ya 39 inasema: Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.
Je, Muhammad atapewa kwa kila mtu ambaye anamwamini Yesu?
HAPANA KABISA, Quran inasema kuwa Ukimwanini Mwamad/
Allah basi umemwamini Allah. Hivyo Muhammad hawezi kuwa Roho ya Kweli, maana tunao Mwamini Yesu tumepewa Roho Mtakatifu na sio Muhammad ambaye amesha kufa.
UTHIBITISHO WA KUMI:
Yohana 14 aya ya 16,17, na 18 inasema: 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.
Hizi aya zinapendwa sana na Waislam na wanapenda kuzitumia kama ushahidi wao.
Je, Muhammad aliishi na Mitume wa Yesu katika karne/Century ya kwanza?
HAPANA KABISA TENA KABISA. Muhammad hakuwepo wakati wa karne/Century ya kwanza pale Wafuasi wa Yesu walipo pewa huyo Roho Mtakatifu. Yesu alisema kwa Wanafunzi wake kuwa hata waacha YATIMA, Je, iweje Muhammad aliye kuja miaka 600 baadae awe na Wanafunzi wa Yesu katika karne/Century ya Kwanza?
UTHIBITISHO WA KUMI NA MOJA:
Yohana 14 aya ya 26. Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
Hii aya Waislam hawaipendi kabisaa, kwasababu Yesu anasema KIUWAZI KABISA KUWA, ni nani huyu WAKILI wetu, NI WATATU KATIKA MUUNGANO MTAKATIFU. Huyu Roho Mtakatifu ana adhama zote za Baba na Mwana, HIVYO BASI, Muhammad tena ameshindwa vibaya sana hapa. Muhammad alikuwa Mtenda dhambi, huku Yesu hakuwai tenda dhambi hata moja.
UTHIBITISHO WA KUMI NA MBILI:
Yohana 15 aya ya 26 inasema: Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.
Kwa mara nyingine tena, hii ndio raha ya kufundisha katika context yake. Tumesoma katika aya hapo juu kuwa Yesu alisema nani ni Msaidizi wetu, na kwa undani zaidi, HAPA KWENYE HII AYA YA 26 Yesu anasema kuwa huyo Msaidizi ni Roho Mtakatifu.
Je, Muhammad aliishi wakati wa Mitume wa Yesu na kuwa msaidizi wao, HAPANA KABISA, inafahamika kuwa Muhammad alikuja miaka 600 baadae.
UTHIBITISHO WA KUMI NA TATU:
Yohana 16 aya ya 13 inasema: Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Muhammad tena ameshindwa hapa, maana hakunena na wala hakuwai sikia kutoka kwa Mungu, Yehova, bali kwa Jibril ambaye anadai kuwa alitumwa na Allah. Zaidi ya hapo, Muhammad hakutoa utabiri wa mambo yatakayo kuja. MUHAMMAD AMESHINDWA TENA KWA MARA YA KUMI NA TATU.
UTHIBITISHO WA KUMI NA NNE:
Yohana 16 aya ya 15 inasema: Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.
Yesu anasema kuwa yote ya Baba ni yangu, je, binadamu wa kawaida anaweza kudai kuwa kila kitu cha Mungu Baba ni chake?
Hakika Yesu ni Mungu. ZAIDI YA HAPO, Yesu anasema kuwa huyo Roho Mtakatifu atatufundisha kuhusu YEYE/Yesu, wakati inafahamika kuwa Muhammad hakuwai fundisha kuhusu Yesu na wala Muhammad hakuwai sema kuwa Yesu ana Baba. Kumbe basi Roho Mtakatifu hawezi kuwa Jibril au Muislam bali ni Mungu mwenye adhama zote za Baba na Mwana.
UTHIBITISHO WA KUMI NA TANO:
YESU ANAWAPA ROHO MTAKATIFU WANAFUNZI WAKE
Yohana 20 aya ya 21 na 22 inasema: 21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. 22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.
AYA HAPO JUU IPO WAZI kabisa kuwa YESU ALIWAPA ROHO MTAKATIFU WANAFUNZI WAKE NA HAKUWAPA MUHAMMAD AMBAYE alikuwa bado HAJAZALIWA.
Hivyo basi, leo nimetoa USHAHIDI ZAIDI YA KUMI NA TAKO KUTOKA INJILI YOAHANA kuwa Muhammad ALIMKUFURU Roho Mtakatifu kwa kujifanye yeye ni Roho ya Kweli.
Katika huduma yake,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

JE, WEWE NI RAFIKI WA MUNGU KAMA ALIVYO KUWA IBRAHIMU?


Wengi wetu wanaweza kushangaa, kama kweli binadamu anaweza kuwa rafiki wa Mungu. Biblia inathibitisha kuwa, wewe unaye soma hii makala unaweza kuwa rafiki wa Mungu.
Isaya 41:8. “Nawe, Israeli, mtumishi wangu; Yakobo, niliyekuchagua; mzao wa Ibrahimu, rafiki yangu (Mungu)”
Yakobo 2:23.”Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu”
Sasa tusome kidogo habari ya Ibrahimu:
Uru ulikuwa mjia ambao watu walikaa baada ya Gharika. Pakawa mji wa maana wenye nyumba nzuri. Lakini watu wa huko waliabudu miungu ya uongo. Ndivyo walivyofanya hata katika Babeli. Watu wa Uru na Babeli hawakuwa kama Nuhu na Shemu mwanawe, waliozidi kumtumikia Mungu.
Mwishowe, ilipopita miaka 350 tangu gharika, Nuhu mwaminifu akafa. Ilipopita miaka miwili mtu unayemwona katika picha hii alizaliwa. Alikuwa mtu wa pekee sana kwa Mungu. Jina lake ni Ibrahimu. Alikaa pamoja na jamaa yake katika mji huo wa Uru.
Kabla ya kuitwa Ibrahimu, jina lake lilikuwa Abram, laikini Mungu alimpa jina la Ibrahimu lenye maana ya Baba wa Mataifa mengi.
Vinyo hivyo, Serai jina la awali la Sara lilibadilishwa na Mungu. Maana ya jina jipya la Sara ni Mama wa mataifa mengi.
Siku moja Mungu alimwambia Ibrahimu (Abrahamu): ‘Ondoka Uru, wewe na ukoo wako, uende kwenye nchi ambayo nitakuonyesha.’
Je! Ibrahimu alimtii Mungu na kuacha starehe zote za Uru? Ndiyo. Ibrahimu alijulikana kuwa rafiki ya Mungu kwa sababu alimtii Mungu sikuzote.
Wengine wa jamaa ya Ibrahimu walimfuata alipoondoka Uru. Tera baba yake alimfuata. Hata Lutu mpwa wake. Na pia Sara mke wa Ibrahimu. Halafu wote wakafika Harani, na huko Tera akafa. Walikuwa mbali sana na Uru.
Muda kidogo Ibrahimu na jamaa yake wakaondoka Harani kuja Kanaani. Mungu akasema: “Hii ndiyo nchi nitakayowapa watoto wako.’ Ibrahimu alikaa Kanaani katika hema.
Mungu alianza kumsaidia Ibrahimu hata akawa na kondoo na wanyama wengine wengi na mamia ya watumishi. Lakini yeye pamoja na Sara hawakuwa na watoto wowote.
Ibrahimu alipokuwa mwenye miaka 99, Mungu alimwahidi hivi: ‘Utakuwa baba ya mataifa mengi.’ Lakini watoto wangezaliwa namna gani, maana Ibrahimu na Sara ni wazee mno?
Je, ninawezaje kuwa rafiki wa Mungu?
Yohana 15:14. “Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo”.
Kwa hiyo katika mstari huo hapo juu tunaona jinsi Yesu Kristo anavyokiri kuwa kuna watu wanaoweza kuwa rafiki wa Mungu. Lakini ipo gharama katika kuwa rafiki wa Mungu, gharama hiyo ni kutenda kila Mungu analokuamuru kulitenda pasipo kuchagua.
Hii ndio faida ya kuwa Mkristo, unakuwa rafiki wa Mungu na mtoto wa Mungu, tofauti na imani au dini zingine ambazo Mungu kwao ni kama adui yao.
Usikose somo la: Mungu anajaribu imani ya Ibrahimu.
Mwanzo 11:27-32; 12:1-7; 17:1-8, 15-17; 18:9-19.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

UTATA MKUMBWA NDANI YA KORAN Nini kitaingia PEPONI: Roho/Nafsi au Mwili au zote mbili?




Somo letu la leo ni la swali kwa Allah ambaye ameshindwa kujieleza, kuwa ni kipi kinaingia Peponi kati ya Roho/Nafsi au Mwili?

Koran inadai kuwa, baada ya ufufuo, ni mwili (baada ya kuungana na roho?) Ambayo inaingia peponi. Haya madai yamewekewa mkazo katika Koran. Angalia mistari ifuatayo 13:05, 17:98-99, 20:55, 34:7, 75:3-4.

Hata hivyo mistari ya 27-30 kwenye Sura 89 ipinga aya zilizo pita kwa kusema kuwa ni nafsi (Nafs) tu ambayo inaingia Peponi!

Quran 17:99. Kwani hawakuona ya kwamba Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi ni Mwenye kuweza kuumba mfano wao? Na Yeye amewawekea muda usio na shaka yoyote. Lakini madhaalimu hawataki ila ukafiri. 

Quran 75:3. Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?  4. Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake! 

Aya hizo hapo juu, zinadai kuwa Nafsi na Mwili vitaungana na kuingia Peponi, hayo ni maneno ya Allah kama alivyo yashusha kupitia Quran yake. Lakini Allah huyohuyo anabadilika na kusema kuwa Nafsi ndio itaingia Peponi. Hebu soma aya zifuatazo.

Quran 89 27. Ewe nafsi iliyo tua! 28. Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha. 

Katika aya hapo juu, Allah anaiamuru Nafsi irejee kwake. Sasa ni ipi kati ya Nafsi na Mwili vitaingia Peponi? Utata huu ni Msiba Mkubwa kwa Allah ambaye hafamu nini kati ya Nafsi na Mwili vitaingia Peponi.

Quran 31:28. Hakukuwa kuumbwa kwenu, wala kufufuliwa kwenu ila ni kama nafsi moja tu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kuona. 

Allah anaendelea kusema kuwa ni Nafsi ndio itaingia Peponi. Aya hizi zinapingana na maneno yake ya kwanza kuwa ni Nafsi pamoja na Mwili vinaingia Peponi. Hivi Allah ni kweli aliumba Binadamu? Mbona hafahamu nini kati ya Nafsi na Mwili itaingia Peponi?

Katika Uislamu, neema ya peponi haikamiliki bila raha ya pamoja ya Mwili na akili, maana Allah katoa ahadi ya wake 72 kwa wale wote watakao ingia Peponi. Vinginevyo, mtu atawezaje kunywa Zanzabil (76:17), na kuifurahia hicho kinywaji (76:13), kufurahia wanawali (55:56) na kunywa asali na maziwa (47:16-17) bila ya kuwa na Mwili?

Yousuf Ali (Nakala 6128 kwa aya 89:27-30) pia anasema kwamba ni roho ambayo inaingia mbinguni, na si mwili ambao utaharibika (Maoni yake ni kupingana na aya 75:3-4 zinavyo sema!). Soma aya 31:28 pia. Inasema kuundwa kwa mtu au ufufuo ni katika nafsi.

Ndugu wasomaji, Allah anaendelea kutoa utata katika uumbaji wake. Allah kwa mara nyingine tena ameshindwa kuufahamisha umma wake kuwa, ni nini kati ya Nafsir na Mwili vitaingia Peponi.

Koran si kitabu cha Mungu bali ni maneno ya Muham-mad ambayo alindika ili kukuza maono yake ya kisiasa. Kama Allah ni mungu, basi ifahamike leo kuwa Allah si Mungu aliye umba Mbingu na Nchi. Si Mungu aliye muumba Adamu na Hawa, bali ni Mpinga Mungu.

Katika huduma Yake.

Max Shimba

Copyright © Max Shimba Ministries 2013

Sunday, April 30, 2017

SABABU KUMI (10) KWANINI NAMPENDA YESU



1. YESU NI MCHUNGAJI MWEMA
Yohana 10: 10Mwivi huja ili aibe, kuua na kuangamiza. Mimi imekuja ili wapate uzima kisha wawe nao tele. 11‘‘Mimi ndimi Mchungaji Mwema. Mchungaji Mwema huutoa uhai Wake kwa ajili ya kondoo.
Yesu ninae mpenda ni mwenye Mikono Wazi na yupo tayari kutupokea sote. Sote tumefanya makosa, lakini habari njema ya Ukombozi ni kuhusu Upendo wa Mungu kwetu sisi ambao tunaupata kutoka na kupitia Yesu Kristo ambaye ni Bwana na Mwokozi wa Maisha yangu. Karibu kwa Mchungaji Mwema ambaye ni Yesu Kristo aliye kufa Msalabani kwa ajili ya dhambi zako.

2. YESU ALIKUJA KUWASAIDIA WALIO LEMEWA NA MIZIGO AU MATATIZO YAO
Matayo 11: 28 “Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. 29 Jifungeni nira yangu, mjifunze kutoka kwangu, kwa maana mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata raha nafsini mwenu. 30 Kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.’’
Ukristo sio kuhusu kufanya sheria bali ni kupokea jibu ambalo Yesu alisha kujibu pale Msalabani. Hii ndio Raha ya kuwa na Yesu. Yesu alisha maliza matatizo yako yote pale Msalabani, alisha maliza au ponya Magonjwa yako yote. Ndio Maana Yesu anasema kwako kuwa, NJOONI NINYI NYOTE MLIO LEMEWA NA MIZIGO. Kitu ambacho unatakiwa kufanya ni kuja kwa Yesu, halafu yeye atakupa Majibu yako yote. Sasa njoo kwa Yesu na upokee majibu ya matatizo yako.

3. YESU AMEKUSAMEHE -UPENDO WA MUNGU
Zaburi 103: 2 Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, wala usisahau wema wake, 3 akusamehe dhambi zako zote na kuponya magonjwa yako yote, Kumfahamu Yesu ni kujua kuwa Yesu alisha maliza kazi zote pale Msalabani, ikiwa pamoja na kukusamehe dhambi zako zote. Sasa basi, najua unasema kuwa labda ulifanya vitu vibaya hapo nyuma na unashindwa elewa kivipi Yesu atakusamehe dhambi zako. Ndugu msomaji, Yesu hajali nini umefanya hapo nyuma, Yesu anacho taka kutoka kwako ni kuwa, umkabidhi matatizo yako yoke na yeye alisha maliza kazi pale Msalabani. Sasa basi, mwambie Yesu kuwa wewe ni mwenye dhambi na omba msamaha na amini kuwa amesha kusikia na kukujibu/samehe. Yesu ni Mungu na Mungu wetu ni Upendo.

4. YESU NI UHURU
Warumi 8: 1. Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu ya adhabu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu, wale ambao hawaenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho. 2 Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti. 3 Kwa maana kile ambacho sheria haikuwa na uwezo wa kufanya, kwa vile ilivyokuwa dhaifu katika mwili, Mungu kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe kwa mfano wa mwanadamu mwenye mwili ulio wa dhambi na kwa ajili ya dhambi, Yeye aliihukumu dhambi katika mwili, 4ili kwamba haki ipatikanayo kwa sheria itimizwe ndani yetu sisi, ambao hatuenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho.
Kuna Uhuru Mkubwa sana unapo kuwa ndani ya Yesu Kristo. Unapo mkabidhi Yesu maisha yako na kuwamchia yeye ayaendesha, basi unakuwa huru kabisa. Yesu ni Mungu, na yeye anampango mzuri sana kwa maisha yako. Hivyo basi, nakusihi uache kuwa mungu wa maisha yako na Mkabidhi Yesu maisha yako ili akuonyeshe nini cha kufanya. Anza maisha ya Kiroho na Yesu ambaye ndie muumba wako. (2 Wakorintho 5:19) Dhambi haina mamlaka juu yangu kwa sababu mimi sasa naishi chini ya neema. (Warumi 6:14) Neema ni msingi wangu na ukombozi katika Kristo. Neema ya Mungu sio leseni ya dhambi, ni nafasi ya kufanikiwa.

5. YESU NI HAKI YANGU
Warumi 5: 1 Kwa hiyo, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa imani, tuna amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
Wokovu ni zawadi ya haki. (Warumi 5:17) Katika Ufalme wa Mungu, hakuna kufanya kazi ili kupata haki yako, bali haki yako ni zawaidi kutoka kwa Mungu. Dini zingine zinafundisha kuwa, wewe ufanye kazi na Mungu ndio nakupa haki yako, Katika UKRISTO, tunapokea zawadi ya Wokovu. Hivyo basi, elewa kuwa Yesu alisha kulipia kwa kupitia damu ya Msalaba.
Nakukaribisha kwa Yesu aliye hai ambaye ni Mungu na amekupa haki ya kuwa Mwana wa Mungu kwa kupitia damu yake.

6. YESU NI FURAHA YANGU
"Mambo haya mimi nimesema nanyi ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu ikamilike." (Yohana 15:11)
Furaha ni kitu kinacho toka ndani yako. Yesu anakaa ndani yako ndio maana YESU NI FURAHA YANGU. Maana yeye ndio mwanzo wa furaha na yeye ndie anayetupa furaha ndani ya maisha yetu.
Yesu anayeishi ndani yangu na yeye ndie anayetoa furaha, Yeye ni mwanga wa maisha yangu.. Yesu ndio anayenijua mimi ni bora, ananipenda zaidi. Yeye alitoa maisha yake kwa ajili yangu maisha yangu. Furaha ya Bwana ni nguvu zangu. (Nehemia 8: 9) Yesu ni yule ambaye ananipenda nani faraja kwangu. Nafurahi kwa furaha isiyo na kifani na kamili ya utukufu. (1 Petro 1: 8)

7. YESU NI UFUFUO
"Mimi ndiye ufufuo na uzima. Anayeniamini mimi hata kama anakufa, ataishi." (Yohana 11:25)
Yesu ndie anatoa maisha mapya na ya milele. Yeye ni ufufuo na uzima. Kwahiyo hauhitaji kutafuta wapi ulipo ufufuo na wapi ulipo uzima, "YESU YEYE NDIE UFUFUO NA YEYE NDIE UZIMA" na anaishi ndani yako. Anatoa ushindi katika maisha na maisha katika kifo. Hakuna haja ya kuishi kwa hofu, na hakuna haja ya kuogopa kifo.Yesu anasema, "Kwa sababu mimi ni hai, nanyi pia mtakuwa hai." (Yohana 14:19) Pia anatangaza, "Mimi nimeushinda ulimwengu." (Yohana 16:13)
Karibu kwa Yesu ambaye ni Ufufuo na Uzima.

8. YESU NDIE ANAYE DHIHIRISHA YOTE

"... Mimi najua yule niliyemwamini .." (2 Wakorintho, 1:12)
Maisha ya Mkristo au Kikristo sio maisha ya kukata tamaa. Ni maisha ya ushindi katika Yesu aliye hai. Tunajua Mungu kwa njia ya Neno lake. Kwa Neno lake anaongea na moyo wetu. Kwa Neno lake uwaangazia mioyo yetu. Neno lake huponya moyo wako. Kama unataka kujua Mungu ni nani, basi mwangalie Yesu. Kama unataka kujua Yesu ni nani, basi jifunze Neno lake. Neno inaonyesha Mungu ni nani na nini Mungu amefanya kwa ajili yetu. Neno pia linaonyesha sisi ni nani katika Kristo.

9. YESU NDIE ANAE NIONGOZA KATIKA KUFANYA MAAMUZI MUHIMU KATIKA MAISHA YANGU
"Kwa nini, kuna faida ya mtu, kama yeye kuupata ulimwengu wote na kuyapoteza maisha yake." (Marko 8:36)
Jambo la muhimu zaidi tunaweza kufanya katika maisha haya ni kujiandaa kwa ajili ya maisha yajayo. Barabara inayoongoza kwenye uzima ni nyembamba. Ni nyembamba, lakini ina faida. (1 Timotheo 3: 8) Yesu ni mlango. Sisi hutembea kwa njia ya Yesu ndani ya ukamilifu wa Mungu. Hivyo basi, Yesu ndie Njia itupelekayo kwenye uzima wa milele.
Ndugu msomaji, kama huna uhakikisho wa maisha baada ya kifo, nakushauri umpokee Yesu, hakika utapata uzima wa milele.

10.YESU NI DAKTARI WANGU
"4Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake, juu ya mti, ili kwamba,tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tupate kuishi katika haki. Kwa kupigwa kwake, ninyi mmeponywa. " (1 Petro 2:24)
Yesu alichukua udhaifu wangu. Yesu alichukua magonjwa yangu. Kwa kupigwa kwake mimi nikapona. Uponyaji wa Mungu ni kitu rahisi na rahisi kuamini, na uponyaji wa Mungu ni kitu rahisi na rahisi kupata. Roho Mtakatifu aliyemfufua Kristo kutoka wafu nI HUYO HUYO ANAYE FANYA MIUJIZA YOTE KWAKO. Nanyi ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, Yeye aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataihuisha pia miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya Roho Wake akaaye ndani yenu. (Warumi 8:11) Mungu alimtuma Neno lake kuniponya. (Zaburi 107: 20) Neno lake ni uzima na afya kwa mwili wangu wote. (Mithali 4: 20-22) Neno la Mungu kunilinda kutokana na maambukizi ya dunia hii.
Karibu kwa Yesu Kristo ambaye ni Daktari wa Madaktari.
Mungu awabariki sana,
Max Shimba Ministries Org.

BREAKING VIDEO: IDF pounding Hezbollah training compounds

  BREAKING VIDEO: IDF pounding Hezbollah training compounds. The targets included a Radwan Force training facility used for weapons drills ...

TRENDING NOW