Wednesday, May 3, 2017

ROHO MTAKATIFU NA KAZI ZAKE KWETU SOMO LA 2

Image may contain: bird, cloud and text
ROHO MTAKATIFU ROHO AWAFUFUAYE WATU WALIOKUFA KIROHO
Kurudi nyuma na kuacha wokovu kunaitwa pia kufa kiroho (Ufunuo 3:1;Waefeso 2:1). Kwa kila aliyerudi nyuma na kuacha wokovu, hii ni saa ya kuamka usingizini na kuanza upya (Warumi 13:11-12).
Lakini, je, inawezekana kuanza upya tena katika hali hii?
Ndiyo, kwa msaada wa Roho Mtakatifu. Hii ni kazi yake nyingine. Roho Mtakatifu ndiye aliyemfufua Yesu, alipokufa
 (Warumi 13:11).
Kwa jinsi hiyo hiyo, Roho Mtakatifu anaweza kutufufua kiroho na kutupa uhai tena wa kiroho (Waefeso 2:1,4-6). Mwambie Roho Mtakatifu kwamba unataka kufufuliwa kiroho, naye atafanya.
ROHO MTAKATIFU, ROHO AWATIAYE UZIMA WATU
Kabla ya kufa kiroho, hutangulia kuzimia kiroho. Shetani hutupeleka hatua kwa hatua, kama upepo katika tairi unavyotolewa kidogo kidogo kutokana na pancha ndogo.
Tukizimia kiroho, upendo wa kwanza unatoweka. Ingawa bado hatujafikia hali ya kufanya dhambi za uzinzi, uasherati, ulevi n.k kama mataifa, hata hivyo, mambo ya rohoni yanakuwa hayana mvuto kwetu kama mwanzo. Kuomba, kushuhudia, kuhudhuria ibada n.k, yanakuwa mzigo kwetu. Tunaanza kuvutwa zaidi na mambo ya dunia. Katika hali hii tunahitaji nguvu mpya, uzima mpya (Isaya 40:28-31). Anayefanya kazi hii pia ni Roho Mtakatifu, Roho wa uzima (Warumi 8:2). Pepo wa udhaifu wanatolewa kwa Roho wa Mungu (Mathayo12:28), na vivyo hivyo udhaifu wetu kiroho unatolewa na Roho wa Mungu.
Je umezimia kiroho, Mwambie Roho Mtakatifu akuzindue, naye atafanya.
ROHO MTAKATIFU ROHO ATUPAYE UTAKASO
Baada ya kuokolewa,tunahitaji pia kutakaswa.Bila utakaso, tutajikuta bado hatuna ushindi dhidi ya dhambi za ndani katika mawazo, na moyoni,ingawa tayari tuna ushindi dhidi ya dhambi za kutenda. Dhambi za ndani ,ni kama hasira, wivu ,chuki, masengenyo, kugombania ukubwa, kiburi, majivuno, kutokusamehe, kinyongo, kupenda udunia n.k.
Hivi vinaweza vikaonekana kwa watu waliookoka ambao hawajatakaswa: Mawazo yasiyo ya ki Mungu (Mathayo 16:21-23), kugombania ukubwa (Luka 22:24-26; Mathayo 20:20-22,25-28; Marko 9:30-37), hasira (Mathayo 20:24) wivu, fitina, ugomvi (Marko 9:38-39; Luka 9:49-50; 1Wakorintho 3:3-5), faraka na matengano (1Wakorintho1:10-13), umimi (Mathayo 28:6-13), kutokusamehe (Mathayo 18:21-35), chuki,kushindwa kuvumilia maudhi,kushtakiana wapendwa mahakamani (Luka 9:51-56; 1Wakorintho 6:1-8); Warumi 7:15 n.k . Mambo haya huondolewa kwa utakaso.
Ndiyo maana Yesu aliwaombea Utakaso wanafunzi wake waliokuwa tayari wameokoka (Yohana 17:14-19) Roho mtakatifu ndiye atupaye Utakaso (1Wakorintho 6:11; 1Petro1:2) Je, hujatakaswa, mwambie Roho Mtakatifu akutakase, yeye ni waminifu, atafanya (1Thesalonike 5:23-24)
ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUPAYE TUNDA LA ROHO
Katika Wagalatia 5:22-23, tunajifunza juu ya tunda la Roho. Katika lugha ya asili,yote katika mistari hii yanamaanisha kwamba Tunda la Roho ni moja tu,Upendo. Hata hivyo,upendo huo unadhihirishwa kwetu katika tabia na matendo kama furaha, amani, uvumilivu, utu wema,f adhili, imani, upole, na kiasi. Ni pale tu tunapokuwa na maisha yaliyojaa upendo, ndipo tunapokuwa tunatimiza mapenzi ya Mungu katika maisha yetu.
Pasipo upendo, tunakuwa shaba iliayo na upatu uvumao, tunakuwa si kitu. Lolote jingine tunalolifanya linakuwa halina faida (1Wakorintho 13:3). Hatuwi wanafunzi wa Yesu (Yohana 15:8) Sasa basi , ni muhimu kufahamu kwamba upendo ni tunda la Roho, tunalolipokea kutoka kwa Roho Mtakatifu.
Tukilipokea tunda hili, na kukua kila siku katika upendo (1Wathesalonike 3:12), Kama matunda yanavyokua, ndipo tunapokuwa wanafunzi wa Yesu kwelikweli.Tukiwa na tunda la Roho la upendo, tunakuwa na Furaha ya wokovu ambayo haiwezi kuondoka kwetu kwa sababu ya majaribu yoyote au kukosekana kwa lolote la kimwili (Yakobo1:2). Tutakuwa na amani ipitayo fahamu zote (Wafilipi 4:7) inayotuwezesha kuwa na amani na watu ambao tusingeweza kuwa na amani nao.
Tutakuwa na lengo la kutafuta amani na watu wote wakati wote (Waebrania 12:14) Tutakuwa na uvumilivu wa kipekee katika mateso, makwazo kutoka kwa watu n.k Tutakuwa na utu wema kwa watu wengine hata wale ambao hawajaokoka (Marko 10:17). Tutakuwa na fadhili yaani hali ya kutaka wakati wote watu wanaotuzunguka wawe na furaha.
Tutakuwa watu tuliojaa imani,tusiotetereka kirahisi.Tutakuwana upole yaani unyenyekevu (Mathayo 11:29; Wafilipi2:5-8) Na pili tutakuwa na kiasi (self-control)yaani uwezo wa kukataa kufanya lile ambalo Yesu hataki, kwa gharama yoyote.
Je, unataka kuwa na tunda la Roho katika maisha yako?Mwambie Roho Mtakatifu, naye atafanya.
USIKOSE SOMO LA 3: ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUSAIDIAYE KUOMBA
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW