Wednesday, May 3, 2017

ROHO MTAKATIFU NA KAZI ZAKE KWETU SOMO LA 1

Image may contain: bird, cloud and text
ROHO MTAKATIFU, MTOA UTAKATIFU
Katika somo la kwanza katika mfululizo wa masomo haya yanayohusu Roho Mtakatifu, Tulijifunza kwamba Roho Mtakatifu, ni mtakatifu, hivyo anakuwepo na kudumu mahali palipo na utakatifu tu.Tukiwana maisha ya uchafu, yaani dhambi; humfanya Roho Mtakatifu akose makao kwetu,na hivyo hawezi kuwepo kwetu.Kama alikuwepo mwanzo kwetu,huondoka (1Samweli 16:14; Zaburi 51:4,10-11).
Sasa swali linakuja, tunawezaje kuwa watakatifu katika maisha yetu ili Roho Mtakatifu afanye makao kwetu?
Jibu ni kwamba, Roho Mtakatifu , ndiye huyohuyo anayetoa utakatifu tunaouhitaji. Sasa tunamwangalia Roho Mtakatifu kama Mtoa Utakatifu,kwa kutafakari kazi yake hiyo katika vipengere vitano:-
1. ROHO MTAKATIFU,ROHO ATUPAYE KUZALIWA MARA YA PILI
2. ROHO MTAKATIFU ROHO AWAFUFUAYE WATU WALIOKUFA KIROHO
3. ROHO MTAKATIFU, ROHO AWATIAYE UZIMA WATU WALIOZIMIA KIROHO
4. ROHO MTAKATIFU ROHO ATUPAYE UTAKASO
5. ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUPAYE TUNDA LA ROHO
1. ROHO MTAKATIFU, ROHO ATUPAYE KUZALIWA MARA YA PILI.
Hatupaswi kamwe kudanganyika kwamba utakatifu siyo duniani ni mbinguni, tu, maandiko yanaeleza waziwazi kwamba watakatifu walioko duniani ndiyo anaopendezwa nao Mungu (Zaburi 16:3).
Hatupaswi pia kudanganyika kwamba tunaweza kufanya dhambi hapa duniani, halafu tukasalimika baada ya kufa, kutokana na misa ya wafu n.k (1Wakorintho 6:9-10; Waefeso 5:5-7; Wagalatia 6:7 ; Waebrania 9:27; IYohana 5:16; Kumbukumbu 10:17) la maana hapa ni kufahamu ni jinsi gani tunavyoweza kuwa na ushindi dhidi ya dhambi hapa duniani,na kuokoka kutupwa motoni, maana bila shaka tunatakiwa kuokoka tukiwa hapahapa duniani (Luka 19:8-10);Tito 3:3-4)
Tunawezaje kuwa na ushindi dhidi ya dhambi?
Ni kwa kuzaliwa mara ya pili, kwa Roho Mtakatifu (Yohana 3:3-10; Tito 3:3-5) Yesu Kristo, alijaribiwa sawasawa na sisi lakini hakutenda dhambi (Waebrania 4:14-15).
Ni nini siri ya ushindi wake huo?
Ni kwa sababu alizaliwa kwa Roho Mtakatifu, yaani alizaliwa tofauti na kawaida ya kimwili ya mume na mke. Sisi nasi tunapotubu dhambi zetu kwa kumaanisha kuziacha, tunapata rehema hii kwa imani tu (Mithali 28:13).
Tunazaliwa mara ya pili katika ulimwengu wa roho, na hivyo kuwa na uwezo wa kushinda dhambi kwa muujiza mkubwa. Katika hali ya kawaida ya jinsi tulivyozaliwa kimwili, kamwe hatuwezi kushinda dhambi. Ni mpaka tufanyike viumbe vipya kwa Roho Mtakatifu. Mwambie Roho Mtakatifu kwamba unataka kuzaliwa mara ya pili,naye atafanya.
USIKOSE SEHEMU YA PILI:
2. ROHO MTAKATIFU ROHO AWAFUFUAYE WATU WALIOKUFA KIROHO
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW