Wednesday, May 18, 2016

MASHOGA WA KIISLAMU WAMEFUNGA NDOA NCHINI UINGEREZA


Wanawake wawili raia wa Pakistan Waislamu wa jinsia moja wamefunga ndoa nchini Uingereza.
Rehana Kausar, miaka 34, na Sobia Kamar, miaka 29,wameweka historia pale walipofunga pingu za maisha katika sherehe iliyofanyika kwenye ofisi ya msajili, kisha haraka wakaomba hifadhi ya kisiasa baada ya kuwa wamefunga ndoa, wakidai kwamba maisha yao yatakuwa hatarini kama wakirejea kwenye nchi yao ya asili.
Wakishuhudiwa na wasimamizi wao na marafiki wawili, wanandoa hao walivalia mavazi meupe asilia ya ndoa pale walipofunga ndoa mjini Leeds, West Yorkshire.
Wawili hao, kutoka mikoa ya Lahore na Mirpur ya Pakistan, walisema walipokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa wapinzani nchini Pakistan - ambako mahusiano ya jinsia moja ni kinyume cha sheria na kuchukuliwa ni kusaliti Uislamu.
Na tangu habari za ndoa yao mapema mwezi huu kuzagaa, wanandoa hao walidai kupokea vitisho vya kuuawa hata kutoka nchini Uingereza
Kabla ya zoezi hilo, hata msajili aliwashauri wawili hao kufikiria kwa makini kuhusu uamuzi wao wa kufunga ndoa sababu ya mtazamo wa baadhi ya Waislamu kuhusu mahusiano ya jinsia moja.
Kausar alisema: "Nchi hii inatupatia uhuru wa kuamua na ni uamuzi binafsi mno ambao tumeuchukua.
"Halimuhusu mtu mwingine yeyote kwa hili tunalofanya katika maisha yetu binafsi.
"Tatizo lililopo Pakistan ni kwamba kila mmoja anaamini ni nyapara wa maisha ya watu wengine na anaweza kuamua vema kuhusu imani za watu wengine lakini huo si mtazamo sahihi na tupo katika taifa hili sababu ya makasisi wetu ambao wameteka nyara jamii yetu ambayo ni jamii vumilivu na inayoheshimu uhuru wa watu binafsi."
Kamar, alimwelezea mpenzi wake kama 'mwenza wa kiroho' na alisema wanawake hao wawili walizama kwenye mapenzi.
Sheria za Pakistan hazitambui ndoa za jinsia moja na hakuna sheria kukomesha ubaguzi.
Wanawake wote walikutana mjini Birmingham kama wanafunzi ndipo wakahamia nchini Pakistan kutoka Uingereza.
Baadaye walianza kuishi pamoja kama wapenzi huko South Yorkshire, ambako walikaa mwaka mmoja kabla ya kuamua kufunga ndoa.
Jamaa mmoja alisema: "Wapenzi hao hawakuwa na ndoa ya Kiislamu, inayofahamika kama 'nikah', kutokana na kushindwa kumpata Imamu wa kuendesha kile kinachoonekana kama ndoa yenye utata.
"Wamekuwa majasiri wakati wote kutokana na dini yetu kukataza mahusiano ya jinsia moja.
"Wanandoa hao wamekuwa wakitishiwa maisha kote hapa na Pakistan na hakuna namna yeyote wanayoweza kurejea kule."
Wanafunzi wengi wa Sharia - Sheria ya Kiislamu wanatazama mahusiano ya jinsia moja kama ni dhambi inayostahili adhabu kali.
Hakuna adhabu maalumu iliyotajwa lakini katika kesi nyingi za watu mashoga wanaopatikana na hatia huweza kuhukumiwa kifo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW