Kundi la mashoga nchini Canada limetangaza mpango wa kufungua umoja na kujenga msikiti katika mji wa Halifax ulioko mashariki ya nchi hiyo jimbo la Nova Scotia ambapo jamii ya mashoga, waliobadili jinsia na maimamu wanawake wataruhusiwa.
Kwa mujibu wa Syed Adnan Hussein mwanachama wa 'mambo ya kipuuzi' alisema wanampango wa kufungua msikiti huo kwa kuwa wamekuwa wakitengwa na kubaguliwa.
Aidha ameongeza kuwa msikiti huo utaruhusu maimamu wa kike katika ibada ya swala. Pamoja na kwamba hakuna takwimu sahihi ya mashoga katika Nova Scotia, Hussien amedai ni muhimu kupata sehemu ya ibada kwa ajili ya watu wa aina yao.
Mwanazuoni wa kiislamu aliyeko huko Halifax profesa Jamal Badawi anayefundisha chuo kikuu cha Saint Mary amesema kwanza kwa kufanya hivyo ni kupingana na mafundisho ya uislamu.
Amesema uislamu umeharamisha ndoa za jinsia moja, ushoga na kubadilisha jinsia. "Qurani imesema wazi ushoga haukubaliki, hivyo hawatengwi wala hawabaguliwi wanaambiwa mnachofanya ni haramu acheni", alisema profesa Badawi.
Aidha aliongeza kuwa, "Kila mtu ana haki ya kukubaliana au kutokubaliana na mawazo ya mtu yeyote. Lakini ubaguzi umekatazwa katika uislamu, kwamba sisi sote tunapaswa kuwa dhidi ya ushoga".
"Misikiti yote, kila mtu anakaribisha kufanya ibada bila kujali rangi wala jinsia", alisema Imam Ibrahim Alshanti.
Novemba mwaka jana, mashoga nchini Ufaransa katika mji wa Paris walifungua msikiti unaoruhusu wanawake kuingia bila ya hijabu.
No comments:
Post a Comment