Sunday, December 4, 2016

JINSI WACHAWI WANAVYOCHUKUA NYOTA YAKO


ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA


UTANGULIZI:

Huu ni mwendelezo wa somo la Nyota na Maisha mtu aliyonayo. Mathayo 2:1; Kama tulivyoona tangu mwanzo kuwa nyota ni kipawa, uweza, hatma au hali ya mtu ya baadaye. Tukaona nyota ya Yesu ilionekana kabla Yesu hajazaliwa na mamajusi wa mashariki walimwona kama Mfalme.


MAANA YA NYOTA:

Kama tulivyooa sehemu ya kwanza kuwa nyota ni kiashiria cha rohoni, kinachoonesha mtu atakuwa nani baadaye, mafanikio ya mtu au hatma ya mtu. Viashiria hivi ndivyo vinavyoitwa nyota.


NYOTA KATIKA BIBLIA:

Hesabu 24:14-17 Baraki alikuwa mfalme, na alipoona kuwa wanaisrael wanakuja ili kushambulia ufalme wake, akamtafuta Balaam amtabirie. Hayo ni maneno ya Balaamu aliyoona, Hivyo Balaamu alipoangalia taifa la Israel akaona nyota, kimsingi nyota ya mtu inaonyesha jinsi mtu atakavyokuwa baadaye. Hivyo balaamu aliweza kumuona Yesu tangu mwanzo na ndio maana mamajusi wa mashariki nao pia walimwona Yesu kama nyota.


Nyota yaweza kuonyesha kusudi la maisha ya mtu, na ndio maana ingawa Suleimani alizaliwa na mke wa Huria ambaye Daudi alimuua mumewe ili ampate lakini kwasababu nyota ya kujenga hekalu ilikuwa juu yake (yaani Suleimani), Mungu alimchagua kujenga Hekalu. Daudi alikuwa na watoto wengine wengi, lakini aliyechaguliwa kujenga ni Suleimani kwasababu ndio mwenye nyota ya kujenga yaani tangu anazaliwa


Isaya 47:8-12; Hapa biblia inataja neno “wajuao Falaki”, hii ni elimu inayohusu mambo ya nyota ambayo wachawi husoma. Katika Mathayo 2:1- Biblia inataja mamajusi, wao ni wasomaji wa nyota ambao waliiona nyota ya Yesu kabla ya Yesu hajazaliwa. Nyota ya Yesu iliwafanya mamajusi kumfuata kutoka mbali, na wakati huohuo Herode alifadhaika. Kumbe nyota ya mtu ikionekana watu wanaweza kuifuata na kukuletea unalohitaji. Watu wengi wapo katika vifungo mbalimbali kwasababu nyota zao zimefunikwa.


MAMBO 15 AMBAYO UTAYAONA KAMA NYOTA YA MTU HAIPO:

·        Umahiri na utendaji kazi wa mtu hauonekani; kama mtu hana nyota ule umahiri wa wake na utendaji kazi hauwezi kuonekana. Hata ajitahidi kufanya kazi kwa bidii umahiri hawezi kuonekana.


·        Hawezi kuwa mbunifu katika maisha; nyota huleta ubunifu sasa kama haipo basi ubunifu wa mtu hautaonekana. Mtu huyo atakuwa anashindwa kubuni kitu cha kufanya ili kupata mafanikipo katika maisha.


·        Hawezi kufanya kazi zake kwa ufanisi; nyota huleta ufanisi katika kazi, mtu akikosa nyota basi ule ufanisi wake hauwezi kuonekana, mtu huyo atakosa ufanisi katika kazi zake.


·        Hukosa mvuto; nyota huleta mvuto hivyo mtu nyota yake haipo, anakuwa anakosa mvuto hata wa watu kuomuona tena.


·        Hukosa kibali; nyota humfanya mtu awe na kibali hivyo mtu anapochukua nyota, kimsingi anakuwa amechukua kibali chako.


·        Huwezi kusikilizwa katika jamii; kwasababu nyota huleta kusikilizwa, mtu akichukuliwa nyota hawezi kusikilizwa katika jamii.


·        Hawezi kuthubutu;


·        Anakosa uthubutu wa kutenda;


·        Anakosa ujasiri wa kusema; mtu akikosa nyota anakosa ujasiri wa kusema.


·        Anakosa uthubutu wa kutoa maamuzi magumu; mafanikio ya mtu ni matokeo ya maamuzi magumu aliyowahi kuyafanya.


·        Anakosa ujasiri wa kudai unachojua ni kweli;


·        Huwezi kutumia hata kile ulichonacho; ndio maana ya lile andiko utajenga nyumba na mtu mwingine atalala ndani yake”.


·        Anakuwa na matatizo;


·        Anakuwa na hofu ya kutenda mapenzi ya Mungu; nyota ikichukuliwa mtu aweza kuwa na hofu ya yajayo, yaliyopo au yaliyopita.


·        Kukosa uaminifu kwenye mambo ya Mungu.


Kwahiyo wachawi au waganga wanapochukua nyota yako kimsingi, mambo hayo yanakuwa hayapo kwenye maisha yako.


JINSI WACHAWI WANAVYOCHUKUA NYOTA NA MATUMIZI YAKE:

Utajiuliza ni wakina nani wenye uwezo wa kuiona nyota; biblia inathibitisha kuwa waganga na wachawi wana uwezo wa kuiona nyota na kuifuata. Na kama nyota haina ulinzi wa Mungu waganga wanaweza kuichukua nyota. Kuna watu wanadhania kuwa uchawi haupo na kutokujali uwepo wake, lakini uchawi upo kwasababu biblia imetaja kuwa uchawi upo.


Wanachuaje; kwasababu wachawi wanaweza kuiona nyota ya mtu na kuifuata, hivyo wakigundua kuwa nyota ni nzuri wanaweza kuichukua na kumuuzia mtu mwingine; na ndio maana mtu anaweza kuzaliwa nyota ya uongozi, ujasiri, upendeleo, ubunifu au kupata kibali mbele za watu, alafu ikachukuliwa na kupewa mtu mwingine. Na ndio maana kuna watu ni matajiri kwasababu ya nyota za watu; na wakati huohuo mtu Yule ambaye nyota yake oimechukuliwa anaanza kuwa na matatizo; kile kibali au upendeleo aliokuwa nao awali hawezi kuwa nao tena.


Mtu aliyechukuliwa nyota; anakuwa na mafanikio mwanzoni lakini ghafla yanabadilika baada ya kuchukuliwa nyota. Kimsingi; Mungu akikupa kutu huwa kinadumu lakini kama maisha ya mtu yanaashiriwa na nyota pale nyota inapochukuliwa mtu huyo upendeleo wake unaanza kuondoka. Rudisha nyota yako kwa Jina la Yesu.


Maombi ya kuamuru aliyechukua Nyota yako arudishe:

Baba katika Jina la Yesu leo nimetambua kuwa nina nyota, nayo yaweza kuchuliwa na kunitia katika matatizo; hivyo ninaamuru ila aliyechukua nyota yangu arudishe katika Jina la Yesu. NInapokonya nyota yangu iliyochukuliwa katika Jina la Yesu, naamuru mahali popote ilipowekwa na kutumika ninaamuru irudi kuanzia sasa katika Jina la Yesu.


Ninaamuru umahiri wangu, ufanisi, uwezo wangu wa kutenda na uwezo wa kuthubutu ninaurudisha katika Jina la Yesu. Ninaamuru kibali, afya, ujasiri na mvuto wangu urudi katika Jina la Yesu; nataka nyota yangu katika Jina la Yesu.

UFUFUO NA UZIMA {THE GLORY OF CHRIST (T) CHURCH}
DAR ES SALAAM.

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW