Tuesday, December 20, 2016

WAIMBA NA WASIKILIZA TAARABU WOTE KUINGIA JEHANNAM


“Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni maskhara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha” [Luqmaan: 6]. Na Ibn 'Abbaas (Radhiya Allaahu 'anhuma) pia amesema kuhusu Aayah: ((Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi)) "Ni nyimbo na maneno ya yanayofanana (ya upuuzi)" [Isnaad Sahiyh kutoka kwa Shaykh Al-Albaaniy].

WENYE KUIMBA/KUSIKILIZA MUZIKI WATAGEUZWA NYANI NA NGURUWE

Na akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Watakuweko watu katika Ummah wangu watakaojaribu kuhalilisha zinaa, uvaaji wa hariri, pombe na muziki. Baadhi ya watu watakuwa pembeni mwa mlima na mchungaji wao atawajia jioni na kuwaomba haja [fulani]. Watasema: "Rudi kesho". Allaah Atawaangamiza usiku, Atawaangushia milima kisha Atawabadilisha waliobakia wawe nyani na nguruwe na watabakia hivyo hadi siku ya Qiyaamah))[Al-Bukhaariy] 

Hadiyth hii inatuthibitishia kuwa madhambi yote hayo yako sawa sawa uharamu wake, kama vile zinaa na pombe ilivyo haramu, basi na muziki pia haramu sawa sawa. 

Sasa vipi Muislamu aone kuwa muziki sio maasi makubwa ya kujiepusha nayo? 

Imaam Abu Haniyfah amesema: "Kuimba (nyimbo, ngoma) ni katika madhambi makubwa ambayo inatakiwa Muislamu kujiepusha nayo haraka" Khofu zaidi imuingie Muislamu kuwa anaweza kupata adhabu ya kugeuzwa nyani au nguruwe kwa maasi haya kama tulivyoonywa katika Hadiyth ifuatayo: 

Na kasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Watu katika Ummah wangu watakunywa pombe wakiipa jina jengine lisilokuwa hilo, miziki itapigwa kwa ajili yao na watakuweko waimbaji wanawake. Allaah Atawadidimiza ardhini na Atawageuza wawe nyani na nguruwe)) [Ibn Maajah na Shaykh Al-Albaaniy ameipa daraja ya Sahiyh]

POLENI SANA WAISLAM MAANA ALLAH HAPENDI MUZIKI WA TAARAB WALA MUZIKI WA BONGO FLEVA

Shalom,

Dr. Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW