Friday, December 2, 2016

UNAKIFAHAMU KITI CHA HUKUMU CHA KRISTO?


Ndugu msomaji, kwanza kabisa ningependa tujifunze maana ya maneno haya machache.
Nini maana ya Hukumu?
Hukumu ni uamuzi wa mwisho kabisa unaotolewa na mahakama juu ya suala linalobishaniwa baina ya mlalamikaji na mlalamikiwa. Uamuzi huo ndio unaotoa kauli ya mwisho na kutamka ni nani
mwenye haki katika suala linalobishaniwa na ni nini wajibu wa yule aliyekosa ushindi.
Hakimu atakayekikalia kiti hiki ni Yesu Kristo . Yeyote leo anayemkana Yesu Kristo kuwa siyo mwana wa Mungu , atafahamu hapa kwamba hukumu yote iko chini yake ( Yohana 5:22 ; Matendo 10:38-41; 17:31; Warumi 2:16; 2Timotheo 4:1 ). Ni heri kufahamu mapema hivi leo kwamba Yesu ndiye hakimu na kuomba msamaha kwake, yeye yuko tayari kulehemu na kusamehe kabisa ( Isaya 55:6-7 ). Yesu atakapokikalia kiti cha enzi kikubwa cheupe atakuwa mwenye hasira, huruma itakuwa mbali naye kabisa ( Ezekieli 7:4; 8:18; Warumi 2:4-5 ).
Warumi 14:10-12 yasema, “Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.” Wakorintho wa Pili 5:10 yatuambia, “Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.” Kwa muktadha huu, ni wazi kuwa maandiko yote yanahusu Wakristo, sio wasio Wakristo. Kiti cha hukumu cha Kristo, kwa hivyo kinahuzisha Wakristo kutoa hesabu ya maisha yao kwa Kristo. Kiti cha hukumu cha Kristo hakitambui wokovu; hiyo ilithibitishwa na kusulubiwa kwa Yesu kwa niaba yetu (1Yohana 2:2) na imani yetu kwake (Yohana 3:16). Dhambi zetu zote zimesamehewa na hatutahukumiwa kwa sababu yao (Warumi 8:1). Hatustahili kuangalia katika kiti cha hukumu cha Kristo kuwa ni Mungu anazihukumu dhambi zetu, bali kuwa ni Mungu anatuzawadi kwa maisha yetu. Naam, vile Bibilia inasema, tutatoa hesabu sisi wenyewe. Sehemu ya hii ni kwa kweli ni kuzijibu baadhi ya dhambi zetu ambazo tulizitenda. Ingawa, hiyo haitakuwa jambo la kimsingi kuangazia kiti cha hukumu cha Kristo.
Katika kiti cha hukumu cha kristo, Wakristo watalipwa kulingana na vile walimtumikia Kristo kwa uaminifu (1 Wakorintho 9:4-27; 2 Timotheo 2:5). Baadhi ya vitu vingine tunaweza hukumiwa ni vile tulivyo tii jukumu kuu la kuihubiri injili (Mathayo 28:18-20), vile tulikuwa washindi kwa dhambi (Warumi 6:1-6), na vile tulizuia ndimi zetu (Yakobo 3:1-9). Bibilia inazungumzia Wakristo kupokea taji kwa mambo tofauti kulingana na vile walimtumikia Kristo kwa uaminifu (1 Wakorintho 9:4-27; 2 Timotheo 2:5). Taji tofauti zimeelezewa katika 2 Timotheo 2:5, 2 Timotheo 4:8, Yakobo 1:12, 1 Petero 5:4 na Ufunuo 2:10. Yakobo 1:12 ni muhtasari mzuri wa vile tunastahili kufikiria juu ya kiti cha hukumu cha Kristo: “Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.”
Watu watajitetea kwa kilio hapo na kusema “mimi nilifanya miujiza kwa jina lako”, “mimi nilitoa pepo kwa jina lako”, mimi nilishuhudia na kufuatilia n.k, na Yesu atasema sikuwajua ninyi; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu (Mathayo 7:22-23).
Kila mtu atatolewa hapo na kukamatwa kwa nguvu kisha atatupwa kwenye ZIWA LA MOTO. Ziwa la moto ni tofauti na kuzimu au Jehanum. Ziwa la moto kwa sasa halina mtu ndani yake. Wa kwanza kutupwa humo watakuwa Mnyama au mpinga Kristo na nabiii wa uongo (Ufunuo 19:20). Kisha atafuata Shetani (Ufunuo 20:10). Mateso ya ziwa la moto ni mazito zaidi kuliko Jehanum. Mauti au kifo ni Jehenum ya sasa, vyote pia vitatupwa katika ziwa la moto pamoja na wenye dhambi wote (Ufunuo 20:14-15, 21:8). Hapo itakuwa “kwaheri ya kutokuonana tena” kwa wenye dhambi na watakatifu.
Je, unataka kwenda kwenye ZIWA LA MOTO AU KWENDA MBINGUNI? Uchaguzi ni wako, ingawa mimi nakushauri umpokee Yesu Kristo, HAKIMU MKUU, ili upate uzima wa milele.
Shalom
Max Shimba Ministries

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW