Tuesday, August 1, 2017

MUNGU AMEFANANA NA NINI?

Image may contain: text


Habari njema ni kwamba kuna mengi dhahiri juu ya Mungu! Wenye kukagua maelezo haya watatambua ya kwamba ni muhimu kwanza kusoma maelezo yote kwa jumla kabla kusoma vifungu husika vya biblia kwa ufafanuzi zaidi. Vifungu vya kukariri vya bibilia ni muhimu maana bila mamlaka kutoka kwa biblia maneno haya yangekuwa hayana tofauti na maoni ya kawaida ya wanadamu ambayo kila mara huwa na upungufu katika kumuelewa mungu (Ayubu 42:7). Kusema ya kwamba tunahitajika kujua mungu ni mfano wa nini ni jambo la hatari. Kuna hatari ya kutusukuma katika kukimbilia kuiabudu miungu ya uongo kinyume cha mapenzi yake (Kutoka 20:3-5).
Kile tu Mungu ametaka kifahamike juu ya yeye mwenyewe ndicho kinaweza kufahamika. Kitu kimoja ambacho Mungu amejitambulisha nacho ni “nuru”, kumaanisha ya kuwa yeye ni mwenye kujieleza mwenyewe juu ya hali zake (Isaya 60:19, Yakobo 1:17). Ukweli wa kwamba Mungu ametupatia ufahamu juu ya yeye mwenyewe usipuuzwe isije mmoja wetu akakosa kuingia kwenye pumziko lake (Waebrania 4:1). Uumbaji, biblia na Neno lililofanyika mwili (Yesu kristo) ni msaada kwetu katika kufahamu Mungu yu hali gani.
Natuanze kwa kufahamu ya kuwa Mungu ni muumba wetu na sisi ni sehemu ya uumbaji wake (Mwanzo 1:1, Zaburi 24:1). Mungu alisema kuwa mwanadamu ameumbwa kwa mfano wake. Mwanadamu yu juu ya viumbe vyote na alipatiwa mamlaka juu ya viumbe vyote (Mwanzo 1:26-28). Uumbaji umeathiriwa na “anguko” lakini baado umehifadhi baadhi ya kazi zake Mungu (Mwanzo 3:17-18; Warumi 1:19-20). Kwa kutafakari ukuu wa uumbaji na mapana yake uzuri wake na mpangilio, tunaweza kupata hisia za utisho wa Mungu.
Kusoma juu ya majina tofauti tofauti ya Mungu kunaweza kutusaidia katika kutambua jinsi Mungu alivyo. Majina yenyewe ni kama yafuatayo:
Elohim – Mwenye nguvu, mtakatifu (Mwanzo 1:1)
Adonai – Bwana, ikiashiria uhusiano wa mtumishi na bwana wake (Kutoka 4: 10, 13)
El Elyon – Aliyetukuka, mwenye nguvu kupita wote (Mwanzo 14:20)
El Roi – Mwenye nguvu kupita wote na aonaye (Mwanzo 16:13)
El Shaddai – Mwenyezi Mungu (Mwanzo 17: 1)
El Olam – Mungu wa milele (Isaya 40:28)
Yahweh – BWANA “NDIMI”, yenye maana ya Mungu wa milele adumuye kwa uwezo wake mwenyewe (Kutoka 3:13, 14).
Tunaendelea kutasmini hali za Mungu. Mungu ni wa milele, kumaanisha hakuwa na mwanzo na kuweko kwake hakutakoma. Hafi na hamaliziki (Kumbukumbu la torati 33:27, Zaburi 90:2; Timotheo wa kwanza 1:17). Mungu hanyamazishwi na habadiliki na ina maana ya kwamba ni wa kutegemea na kuaminiwa (Malaki 3:6; Hesabu 23:19; Zaburi 102: 26, 27). Mungu hafananishwi na yeyote wala chochote katika uweza wake, matendo na jinsi alivyo mtimilifu (Samueli wa pili 7: 22; Zaburi 86:8; Isaya40:25; Mathayo 5: 48). Mungu hachunguziki, haeleweki kwa kina, amepita uwezo wetu wa kiutafiti (Isaya 40:28; Zaburi 145: 3; Warumi 11: 33, 34).
Mungu ni wa haki, wala hapendelei mtu (Kumbukumbu la torati 32:4; Zaburi 18:30). Mungu ni muweza yote. Ana nguvu na anatenda kila kinachompendeza bila kutoka nje ya hali zake timilifu (Ufunuo wa Yohana 19:6; Yeremia 32:17, 27). Mungu yu kila pahali (Zaburi 139:7 -13; Yeremia 23:23). Mungu ni mwenye kufahamu yote. Anajua yaliyokuwepo, yaliyopo na yatakayokuwepo pamoja nay ale tuyawazayo kila wakati. Ni kwa sababu ya kufahamu kila kitu ndiyo hukumu yake ni ya haki (Zaburi 139:1-5; Methali 5:21).
Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine na yeye pekee anaweza kuhudumia mahitaji ya mioyo yetu sote. Yeye pekee ndiye anayepaswa kuabudiwa (Kumbukumbu la torati 6:4). Mungu ni mwenye haki. Hafanyi makosa yoyote. Ni kwa sababu ya kuwa mwenye haki ndiyo iligharimu Yesu kupitia hukumu kwa ajili ya dhambi zetu zipate kuondolewa (Kutoka 9:27; Mathayo 27: 45-46; Warumi 3: 21-26).
Mungu yu juu ya yote. Ni mkuu wa uumbaji wake wote wala hawezi kubadilika katika mipango yake mwenyewe (Zaburi 93:1; 95:3; Yeremia 23:20). Mungu ni roho. Haonekani na macho ya kawaida (Yohana 1:18; 4:24). Mungu ni wa utatu. Yeye ni sehemu tatu ndani ya mmoja, zenye nguvu sawa na utukufu. Jina lake hutajwa kwa umoja hata japoelezwa katika utatu –“ Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu’ (Mathayo 28:19; Marko 1: 9-11). Mungu ni kweli. Anakubaliana na hali hiyo tu ya ukweli, si mfisadi wala mwongo (Zaburi 117:2; Samueli wa kwanza 15:29).
Mungu ni mtakatifu. Amejitenganisha na kila hali ya unajisi na hataki unajisi wa kila aina karibu naye. Mungu huona uovu wote na humkera. Moto kila mara hutajwa pamoja na utakatifu. Mungu hutajwa kama Moto ulao (Isaya 6:3; Habakkuk 1: 13; Kutoka 3;2, 4.5; Waebrania 12:29). Mungu ni wa neema. Ni mwema mwenye rehema, mkarimu, na mwenye upendo. Kama haingekuwa neema ya Mungu hali zake zote nyengine zingetuacha mbali naye. Mungu anahitaji kutujua kila mmoja wetu kibinafsi (Kutoka 34:6; Zaburi 31:19; Petero wa kwanza 1;3; Yohana 3:16; Yohana 17:3).
Hii ilikuwa ni mojawapo ya jinsi ya kujibu swali linalopaswa kujibiwa na Mungu mwenyewe. Hata hivyo endelea kuwa na ujasiri wa kumtafuta Yeye (Yeremia 29:13).
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW