Wednesday, August 2, 2017

UTHIBITISHO KWAMBA MUNGU YUPO (SEHEMU YA SABA)

Image may contain: 1 person, meme and text
Kufahamika kwa maadili hutangaza Mtunzi wake:
Yapo maadili-msingi yanayotambuliwa na watu wa kila zama na kila mahali. Japo wanaishi mbele ya utisho wa kutoweka na kila huyo akipambana abakie, watu wote wanajua nafsini mwao kutunza uhai wa wengine ni muhimu kuliko kuupoteza, kuonesha huruma ni bora kuliko ukatili, urafiki kuliko usaliti. Wanaafiki heshima yafaa kuliko dharau, ushujaa kuliko woga, bidii kuliko uvivu, ukweli kuliko uongo, kutakiana heri kuliko kuoneana wivu, na kuridhika kuliko kutamani. Kufahamika kwa maadili yanayofanana ulimwengu kote ni uthibitisho wa uwepo wa mtunzi wake mmoja. Baba wa mema yote amewaachia wanadamu kanuni 10 za namna ya kuishi na akaziandika kwa wino usiofutika (Kutoka 20; Warumi 2:14,15). Maadili ya Bwana Mungu hutia mjinga hekima na kumpatia raha moyoni. Sheria yake ni kweli na haki. Tena ni tamu kuliko asali na hutamanika kuliko dhahabu safi (Zaburi 19:7-14). Kwa nini kizuri kisijitangaze?
UNABII KUHUSU ISRAELI
Huu ndio uliojaa kuliko wote, kimaelezo ya utabiri wake, na pia katika wingi wa thibitisho zihusuzo ukweli wake kimatukio kihistoria. Tutazingatia tu mambo halisi mepesi yahusuyo hatima ya ajabu ya Waisraeli.
Agano la Kale limeandika kwa ajili yetu jinsi Mungu alivyofanya ahadi madhubuti kwa Ibrahim (Kama 1800 K.K), iliyokuwa imemaanisha kati ya mengi kwamba, uzao wake ungekuwa taifa (Israeli), ambalo lingeimiliki nchi ya Kanaani, iliyoitwa baadaye Palestina. Kama 1400 K.K. Waisraeli walitolewa Misri wakati wa 'Kutoka' chini ya Mussa, na miaka 40 baadaye walianza kurithishwa nchi waliyoahidiwa. Lakini kabla ya hapo, kabla hawajaingia hiyo nchi, walionywa sana na Mungu kupitia kwa Mussa mkosi ambao ungewapata kama wakimwacha Mungu wao na kuabudu sanamu, na kuiga mambo ya Wapagani wa Kikanaani.
Katika mlango wa 28 wa Kumbukumbu la Torati, kuna unabii wa ajabu sana - na ulikuwa onyo kali - juu ya balaa ambalo lingewafika Waisraeli kama hawakuwa watiifu. Msomaji anashauriwa kujisomea kifungu chote mwenyewe. Hapa tuna nafasi ndogo tu ya kuonyesha yaliyo msingi kimtazamo.
"Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote... BWANA atakupeleka wewe, na mfalme wako utakayemweka juu yako kwa taifa usilolijua wewe wala baba zako... Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza BWANA... BWANA atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya
dunia...wala katika mataifa hayo hutapata raha iwayo yote.." Kumb. 28:15,36-37,64-65.
Hapa napo unabii ulikuwa unaeleweka: Waisraeli wangetawanywa katika mataifa, kuishi huko katika mazingira ya taabu, wakibezwa na kudharauliwa. Ni ajabu iliyoje kuona maisha yao yalivyothibitisha uhakika wa maneno hayo! Mtawanyo wa Wayahudi dunia nzima ulianza katika enzi za Waashuru katika karne ya 8, K.K. Jambo hili liliendelea wakati wa Wababeli kwenye karne ya sita. Baada ya sehemu yao kurudi kutoka Babeli siku za Wafalme wa Kiajemi, jumuia ya Waisraeli iliishi katika ardhi yao kama 500 K.K mpaka siku za Kristo, chini ya tawala za kiajemi, Kiyunani na waliowafuata, na mwishowe Warumi. Katika mwaka 70 B.K, miaka 40 baada ya Kristo kusulubiwa msalabani, palitokea patashika mbaya kuliko zote. Jiji la Yerusalemu lilishambuliwa na kuporwa na majeshi ya Kirumi kwa sababu ya uasi; hekalu likateketezwa kwa moto na Wayahudi kutawanywa mateka dunia yote (ya Kirumi) - tazama kielelezo kwenye jalada. Wamekuwa huko tangu wakati huo, kama ilivyotokea; ncha moja wa dunia hata ncha nyingine!
Na wamekosa, kama ilivyoandikwa mpaka hivi karibuni 'utulivu',
wakipata mateso na mara nyingine maangamizi. Wapogrom wa Urusi katika karne ya 19 na mpango wa Hitler wa uhilikishaji katika karne ya 20 ni mifano michache tu ya karibuni. Wayahudi wamekuwa kila mahali wakikabiliwa na chuki na kukataliwa, kiasi kwamba uwepo wao kama jamii ya watu, ni mojawapo wa maajabu ya kihistoria. Tunaona vile vile ya kwamba Unabii huu juu ya hatima ya Waisraeli umeendelea kuwa kweli kwa zaidi ya miaka 2500 sasa. Nani angeweza kuliona hilo, tukizingatia mtawanyo ulivyokuwa na mateso, kwamba Wayahudi wangeendele kwa karne nyingi kuwa jamii kamili ya watu inayoendelea kutambulika hadi sasa!
Lakini ni zaidi ya hayo... Lakini jambo la ajabu zaidi juu ya unabii kuhusu Israeli halijasemewa, kwani manabii walitabiri pia wazi wazi badiliko lisilotegemewa la mafanikio kwa Waisraeli. Fikiria, kwa mfano, utabiri wa nabii Yeremia, uliotolewa karibu miaka 600 K.K.
"Kwa maana, tazama, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapowarejeza watu wangu wa Israeli na Yuda waliofungwa... nani nitawarudisha hata nchi niliyowapa baba zao, nao wataimiliki (30:3)
"Basi sasa, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi...Tazama,
nitawakusanya, na kuwatoa katika nchi zote nilikowafukuza, katika hasira yangu... nami nitawaleta tena hata mahali hapa, nami nitawakalisha salama salimini; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao..." (32:36-38)
"Nami nitawarudisha wafungwa wa Yuda, na wafungwa wa Israeli, na kuwajenga kama kwanza. Nami nitawasafisha na uovu wao wote..." (33:7)
Na hapa pia hakuna utata juu ya lile alilokuwa akisema nabii: Kitendo kile cha kutawanywa na mateso kwa Waisraeli kitageuzwa. Wayahudi watarudi tena katika nchi ile ile ambayo kutoka kwao walifukuzwa zaidi ya miaka 1990 iliyopita, na kuishi hapo kwa amani zaidi. Madondoo hayo mafupi kutoka kwa Yeremia, yanaweza kuzidishwa mara nyingi kwa matamko kama hayo kutoka Isaya na Ezekieli.
Hatuhitaji hasa kuzama sana ili kuonyesha jinsi utabiri huo wa kurudishwa upya Israeli ulivyotimizwa kikamilifu. Ushirika wa kisayuni ulikuwa na nguvu kati ya Wayahudi waliotawanywa katika nchi nyingi mwishoni mwa karne ya 19. Uanzishwaji wa Palestina kuwa makao ya kitaifa ya Wayahudi mwaka 1917 ulisababisha idadi yao kukua haraka katika nchi hiyo. Hili lilipozua chuki kali kwa Waarabu, Wayahudi walipambana na jaribio lao la kuwakandamiza mwaka 1948, na kuanzisha taifa lao la Kiyahudi. Nalo lilipanuliwa mwaka 1967 katika jaribio la pili kwenye vita vya siku sita, ambapo Israeli ilijichukulia upya sehemu kubwa ya ardhi yake ya kale, na Yerusalemu kuwa makao makuu ya taifa lao chini ya utawala wao wenyewe, kwa mara ya kwanza katika miaka 2500. Kwa kifupi, kuibuka kwa taifa huru la Wayahudi Mashariki ya Kati imekuwa ni kitu kisichotegemewa kabisa. Chini ya miaka 100 iliyopita hakuna mchunguzi wa kisiasa aliyedhani inawezekana.
Hatujihusishi hapa na 'siasa' za jambo hilo. Tunachoangalia hasa ni unabii wa Biblia. Kuna mengi mengine Biblia inayosema juu ya Wayahudi. Manabii wanasema, kwa mfano, kwamba kutakuwa na matatizo makubwa Mashariki ya Kati, na kwamba Israeli itafikishwa kwenye toba mbele ya Mungu wake. Hapo ndipo unabii wa mwisho wa kurudishwa upya na amani utakapotimia. Hapa tungependa kusisitiza tu kwamba manabii walitabiria kurudi kwa Waisraeli kwenye ardhi yao wenyewe, na sisi katika karne hii tumeona kwa macho yetu utabiri huu ukianza kutimizwa.
====USIKOSE SEHEMU YA NANE ==== UNABII AINA TATU - HATIMA TATU
Baada ya kufika hapa, ni kitu cha manufaa kufanya muhtasari wa yale tuliyoona.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW