Tuesday, January 10, 2017

ALLAH KASEMA ADUI YAKE MKUBWA NI YESU KRISTO "MFALME WA WAFALME" WA KWENYE BIBLIA

Image may contain: people sitting and text
Ndugu msomaji,
Waislamu hudai kuwa Muhammad ametumwa na Mwenyezi Mungu wao, ambaye ni Mfalme wa Wafalme . Lakini tusomapo Biblia Takatifu katika kitabu cha Ufunuo 17:14 “ Hawa watafanya vita na Mwanakondoo, na Mwanakondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme; na hao walio pamoja naye ndiyo walioitwa na wateule, na waaminifu”

Katika Ufunuo 19:11-16 “ Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa Neno la Mungu. Na majeshi yaliyo mbinguni wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi. Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA “


Yesu Kristo ndiye Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana. Lakini tunaposoma Hadithi sahihi za Kiislamu zinaeleza kuwa adui mkubwa wa Allah (s.w) wanayemwabudu Waislamu, ni yule anayeitwa Mfalme wa Wafalme.

Sahih Al- Bukhari, Vol.8.Hadithi Na.225, Al-Lu’lu Wal-marjan,Juzuu ya 3, Hadithi Na.1385 “Hadithi ya Abu Huraira (r.a) amesema,Mtume wa Allah (s.a.w) amesema,” Majina yaliyo dhalili mno na mabaya mbele za Allah ni mtu kujiita,Malikil-Amlaak (Mfalme wa Wafalme).”

Hivyo, ufunuo aliopokea Muhammad, ambao anatutaka na sisi Wakristo tuuamini haujatoka kwa Mungu tunayemwamini sisi Wakristo, yaani, Yesu Kristo. Bali kama alivyonukuliwa katika vitabu vya Kiislamu, unatokana na kuchezewa na Shetani, na kwa sababu hiyo kwetu anakuwa nabii na mtume wa uongo’

Biblia Takatifu imetuonya kuwachunguza mitume na manabii. Katika kitabu cha Ufunuo 2:1-2 “ Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume, yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu. Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao siyo ukawaona kuwa waongo”

Kwa mujibu wa aya hizi Muhammad s.a.w hastahili kuitwa nabii na mtume wa Mungu wa Kweli, bali anaangukia katika kundi la manabii na mitume wa uongo. Hatufai.

Zaidi ya hapo, Allah ambaye ni adui mkubwa wa Yesu Kristo ambaye ni Mfalme wa Wafalme sio Mwenyezi Mungu.

Mungu awabariki sana


Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW