Tuesday, January 10, 2017

UKRISTO SIO DINI


Ukristo ni imani maalum kulinganisha na nyinginezo, Kwa sababu inasimamia zaidi ushirika na Mungu kuliko matendo ya kidini. Kinyume na kushikilia orodha ya masharti ya fanya haya na usifanye yale, Lengo la Mkristo ni kutafuta ushirika wa karibu na Mungu Baba. Ushirika huo unawezeshwa na kazi aliyoifanya Yesu pamoja na huduma ndani ya maisha ya Mkristo ya Roho Mtakatifu.
Wakristo huamini ya kuwa Biblia ni Neno la Mungu na mafundisho yake ndiyo mamlaka ya mwisho (Timotheo wa pili 3:16, Petro wa pili 1: 20-21). Wakristo huamini juu ya Mungu mmoja akaaye katika utatu, Baba na Mwana (Yesu kristo), na Roho Mtakatifu.
NINI MAANA YA DINI:
Dini ni jaribio la mwanadamu mwenye dhambi kuwa na uhusiano na Mungu Mtakatifu. Imani ya kikristo ni uhusiano na Mungu kwa sababu yale ametufanyia kupitia kwa kusulubiwa kwa Yesu Kristo.
UKRISTO SIO DINI BALI NI IMANI MAALUM INAYO SIMAMIA ZAIDI NA KUSHIRIKIANA NA MUNGU KULIKO MATENDO YA KIDINI AMBAYO HAYATO KUFIKISHA MBINGUNI.
Kuna njia moja tu ya kushirikiana na Mungu .
YESU KRISTO NI NJIA YA PEKEE YA KUONDOA DHAMBI.
Alikufa kwa ajili yetu ili tujue upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yetu.
Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW