Ndugu msomaji,
Leo tutaangalia kwa undani sana MAKOSA MAKUBWA YA ALLAH kuhusu Yusufu mtoto wa Yakobo.
Allah anasema kuwa, Yusufu alipo kuwa Misri na kufuatwa na ndugu zake, eti, wazazi wake wote walienda Misri. Je, haya madai ya Allah ni ya kweli? Hebu kwanza tusome ushahid hapa chini:
TUANZE NA QURAN:
Surat Yusuf aya ya 99. Na walipo ingia kwa Yusuf aliwakumbatia wazazi wake na akasema: Ingieni Misri, Inshallah, mmo katika amani.
100. Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi. Na wote wakaporomoka kumsujudia. Na akasema: Ewe baba yangu! Hii ndiyo tafsiri ya ile ndoto yangu ya zamani. Na Mwenyezi Mungu ameijaalia iwe kweli. Na Mwenyezi Mungu amenifanyia wema kunitoa gerezani, na kukuleteni kutoka jangwani baada ya Shet'ani kuchochea baina yangu na ndugu zangu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mpole kwa alitakalo. Bila ya shaka Yeye ni Mjuzi Mwenye hikima.
ALLAH ANASEMA KUWA YUSUFU aliwakumbatia WAZAZI WAKE NA AKASEMA INGIENI MISRI kama alivyo shahidiwa kwenye Surat Yusufu aya ya 99 hapo juu, jee, hayo madai ya Allah ni ya kweli?
HEBU SASA TUANZE kupangua madai/hoja ya Allah moja baada ya nyngine kwa kutumia Taurat iliyo kuja kabla ya Quran.
BIBLIA INASEMA:
Mwanzo Mlango wa 35 :16 Wakasafiri kutoka Betheli, hata ukabaki mwendo wa kitambo tu kufika Efrathi, Raheli akashikwa na utungu wa kuzaa, na utungu wake ulikuwa mzito.
17 Ikawa alipokuwa anashikwa sana na utungu, mzalisha akamwambia, Usiogope, maana sasa utamzaa mwanamume mwingine.
18 Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.
19 Akafa Raheli, akazikwa katika njia ya Efrathi, ndio Bethlehemu.
20 Yakobo akasimamisha nguzo juu ya kaburi lake, ndiyo nguzo ya kaburi la Raheli hata leo.

BIBLIA IMETUTHIBITISHIA KUWA Raheli mama yake Yusufu alifariki wakati wa kuzaliwa kwa mdogo wake Benyamini na alizikwa njia ya Efrathi. Ushahidi huu ndio tumeusoma katika Mwanzo 35 aya ya 19.
Sasa maswali ya kujiuliza hapa, ni kwanini ALLAH ANASEMA KUWA YUSUFU ALIWAKARIBISHA wazazi wake na sio Mzazi wake, maana aliye kuwa hai ni Baba yake tu?
Wahadhiri wa Kiislam nilipo ongea nao wakadai kuwa eti, ni kweli mama yake mzazi wa kibaologia ambaye ni Raheli alifarikia lakini Benyamini alilelewa na Mama yake Mkubwa aitwaye Leah. Haya madai yapo vile vile katika (Abdullah Yusuf Ali, The Holy Qur'an, Saudi edition, fn. 1777). Je, tunaweza kuyakubali haya madai kama ni kamilifu na kuvunja hoja yangu ya UTATA wa Allah kuhusu WAZAZI WA YUSUFU walio ingia Misri?
Ngoja niongeze na hoja zaidi kutoka Waislam kabla ya mimi kujibu hayo madai yao ya Benyamini kutunzwa na LEAH hivyo basi Yusufu alipo sema kwa WAZAZI WAKE INGENI MISRI alikuwa sahihi.
Kufuatana na ushahidi wa Biblia [Mwanzo 35:16-20], inafahamika kuwa mama yake Yusufu alifariki wakati anamzaa Benyamini. Hivyo, ngoja tu hisi/KUBALI kuwa labda Quran na Allah walimaanisha ni LEAH ambaye aliitwa kama MZAZI WA Yusufu, kwasababu LEAH alikuwa mmoja ya wake wa Yakobo, na hivyo basi, Leah ndie aliye mlea Benyamini baada ya mama yake kufariki wakati akimzaa. Haya madai yanaweza kuwa sahihi kwa tamaduni za Kiarabu kuwa mzazi mwenza ana haki ya kutunza mtoto wa mumewe "mother" to a foster-mother. (Muhammad Asad, The Message of the Qur'an, p. 352, fn. 96; bold emphasis mine)
Ingawa tamaduni za Kiarabu kwenye hiki kisa hazina mshiko kwasababu Yakobo hakuwa Muarabu hata kama Leah alifanya hivyo na kumtunza Benyamini na Yusufu kumuita Leah Mama yake.
Zaidi ya hapo, hayo madai ya Waislam hayana nguvu tena kwasababu Biblia sio tu ilituambia kuhusu kifo cha Raheli, bali ilituambia vilevile kuhusu kifo cha Leah kabla ya Yakobo na familia yake kwenda Misri.
Mwanzo 46: 5 Yakobo akaondoka kutoka Beer-sheba; wana wa Israeli wakamchukua baba yao na watoto wao wadogo, na WAKE ZAO katika magari aliyoyapeleka Farao ili kumchukua.
6 Wakatwaa na wanyama wao, na mali zao walizokuwa wamezipata katika nchi ya Kanaani, wakaja Misri, Yakobo na uzao wake wote pamoja naye.
7 Wanawe, na wana wa wanawe, pamoja naye, binti zake na binti za wanawe, na uzao wake wote, aliwaleta pamoja naye mpaka Misri.

Unapo soma aya hapo juu, utagundua kuwa Biblia imesema kuhusu WAKE ZA WATOTO WA YAKOBO lakini haikusema kuhusu mke wake Yakobo aitwaye LEAH.
Ukiendelea kusoma aya zinazo fuatia utagundua kuwa Wote walio kwenda Misri wametajwa na hakuna jina la Raheli au Leah katika hizo aya. Lakini tunasoma majina ya wake za watoto wa Yakobo. Tafadhali soma Mwanzo 46 aya ya 8 mpaka 25.
SASA BASI, Yakobo alipo karibia kifo, aliwaambia wanawe wapi anataka azikwe Mwanzo Mlango wa 49: 29 Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti;
30 katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.
31 Humo walimzika Ibrahimu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea;
32 shamba na pango iliyomo lililonunuliwa kwa wazawa wa Hethi.

Katika aya ya 31 inathibitisha kuwa Yakobo alimzika Lea KANANI. Huu ni ushahidi zaidi kuwa Lea alizikwa KANANI na sio Misri, hivyo basi haiwezekani Lea kwenda Misri na apokewe na Yusufu kama amabvyo Quran inadai. Je, unwezaje kumwanini ALLAH AMBAYE ANAFANYA MAKOSA MAKUBWA NAMNA HII KUHUSU TUKIO LA MUHIMU KAMA HILI?
HITIMISHO:
1. Mama yake Yusufu alikufa muda mrefu hata kabla ya Yufuku kwenda Misri.
2. Lea vile vilealifariki muda mrefu hata kabla ya mumewe Yakobo kwenda Misri.
3. Hakukuwa na mke hata mmoja ambaye alikwenda na Yakobo Misri.
4. Allah alipo sema kuwa WAZAZI WA YUSUFU WALIENDA MISRI, hapo ni MAKOSA MAKUBWA SANA AMBAYO yanatufanya tuushuki uungu wa Allah.

Zaidi ya hapo, Quran huwa inasema kuwa baba na mama yako ni wazazi wako wa kibaologia na sio wa kambo, haya madai yalisemwa na Yusuf Ali .
Ndugu msomaji,
Kwa mara nyingine tena tunaona utata mkubwa sana katika Quran ambayo Waislam wanadai kuwa haina shaka ndani yake.
Je, baada ya kusoma hiki kisa na kuona shaka na utata ndani ya Quran, utaweza endelea kuiamini kuwa hicho kitabu ni thabiti na cha Mungu Mkuu?
Ndugu msomaji, mii sipo hapa kubishana bali kukuonyesha kuwa Quran sio kitabu cha Mungu na kimejaa shaka. Amua leo kumfuata Yesu aliye hai ambaye hana makosa wala utata ndani yake na ni MWOKOZI WA MAISHA YAKO.
MUNGU AKUBARIKI SANA NA KARIBU KWA YESU.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 21, 2016
March 21, 2016
No comments:
Post a Comment