Tuesday, March 20, 2018

KWANINI KUNA INJILI NNE KWENYE BIBLIA TAKATIFU?

Image result for four gospels

Injili nne zina malengo tofauti na kwa kiasi fulani watu tofauti walioandikiwa.

Mathayo:
Iliandikwa kwa mara ya kwanza kwenye lugha za Kiebrania (Kiaramu?) kwa mujibu wa Papias. Injili hii inatilia mkazo ufalme wa Mungu, tofauti na Injili ya Yohana inayotilia mkazo jinsi ya kuupata wokovu. Injili ya Mathayo inanukuu nabii nyini za Agano la Kale, na inaonyehsa jinsi ambavyo maisha ya Yesu yanavyofanana na maisha ya Israel kwenye Agano la Kale. Watu wanaichukulia Injili ya Mathayo kuwa kama "simba" kwani inamsistiza Kristo kuwa Mfalme. Irenaeus (mwaka 182-188 BK) kwenye kipande cha 28 cha kazi yake anasema kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa kwa Wayahudi, ikisistizia kuwa Kristo ni wa ukoo wa Daudi.
Marko:
Inasistizia matendo ya Kristo. Watu wengi wanaichukulia Injili ya Marko kuwa kama "maksai", yenye kumsistiza Kristo kuwa mtumishi.
Luka:
Injili ndefu zaidi, iliandikwa na daktari na mshiriki wa safari za kimisheni za Mtume Paulo. Luka anaonekana kuwa mwanahistoria mkubwa zaidi wa ulimwengu wa kale. Watu wengi wanaichukulia Injili ya Luka kuwa kama "binadamu", ikisistizia uanadamu wa Kristo.

Yohana:
Hii inaweza kuwa Injili ya maana zaidi, kwani inasistizia maisha ya Kristo kwa kiasi kidogo lakini maneno na mafundisho yake kwa kiasi kikubwa. Watu wengi wanaichukulia Injili ya Yohana kuwa kama "tai", ikisistizia uungu wa Kristo.

Kwenye Agano la Kale, Masihi anaitwa ". . . Chipukizi . . . mfalme" wa nyumba ya Daudi (Yer 23:5, 6), "mtumishi wangu, aitwaye Chipukizi" (Zek 3:8), "huyu ndiye . . . Chipukizi" (Zek 6:12), na "chipukizi la Bwana" (Isa 4:2).

Hapakuwa na injili zaidi ambazo Wakristo walizikubali kwa ujumla. Irenaeus, aliyeandika karibu mwaka 182-188 BK, alisema palikuwa na Injili nne (Irenaeus Against Heresies kitabu cha 3 sura ya 11.8, uk.428).

Shalom

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW