Thursday, March 22, 2018

KWANINI YESU ALIOMBA KWA BABA YAKE AOKOLEWE NA MAUTI?



Ufahamu kuhusu maombi ya Yesu kwa Baba aokolewe na mauti.

Baadhi ya Waislamu na hasa wa madhebu ya ahmadia huwa wanatumia baadhi ya mistari kama vile (Mathayo 26;39.Marko 14;35;Luka 22;42) kuhoji kuwa kama yalikuwa ni mapenzi ya Mungu afe msalabani kwanini aliomba “ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke” na wanatumia aya zifuatazo kujithibitishia kuwa Mungu alimsikia (Yohana 26;39 11;11-42 na Ebrania 5;7). Kabla ya kushughulikia mengineyo hebu tushughulikie hoja hii ya kusikiwa kwa maombi ya Yesu.

Waislamu wengi hawamjui Yesu kama jinsi ambavyo hawamjui Mungu, wale wakristo wanaomfahamu Kristo vizuri wanafahamu lile fundisho maarufu la unyenyekevu wa Yesu (The Doctrine of Kenosis), Fundisho hili lafundisha jinsi ambavyo kitu Fulani cha ulimwengu wa kiroho kinavyoweza kuvaa mwili wa kibinadamu (Incarnation) na kufanya shughuli za kibinadamu; (Kwa waislamu majini hufanya hivyo). Kristo kwa asili maisha yake hayakuanzia katika tumbo la Mariam yeye alikuwako tangu mwanzo. (Yohana 1;1-5,14).

Quran inasema “Yesu ni Roho” Hivyo alipotungwa mimba tumboni mwa Mariam alikuwa anachukua mwili wa kibinadamu (Filipi 2;5-8) na kwa tendo hili tunapata Mungu mwanadamu yaani Immanuel Mungu pamoja nasi (Mathayo 1;23) hata hivyo kwa unyenyekevu wake Yesu hakutumia uwezo wake wa Kiungu, bali aliishi kama mtu wa kawaida, angeweza kubadili mawe kuwa mkate lakini hakufanya hivyo na angeweza kuagiza majeshi kumi na mawili ya malaika lakini hakufanyahayo. Yesu mwenye asili ya kiungu wakati huohuo akiwa mwanadamu anayeishi bila kuutumia uwezo wa Kiungu kama mwanadamu alihisi njaa, alichoka, alikula na zaidi ya yoote aliogopa kifo na mauti kama binadamu yoyote.Yesu aliomba ikiwezekana kikombe hiki kimuepuke

Lakini si kwa mapenzi yake bali ya Baba yake hivyo kwa kuwa ilikuwa ni mpango wa Mungu Yesu kufa kwa ajili ya ulimwengu alitumwa malaika kumtia nguvu kukabiliana na kifo cha msalaba hivyo hatimaye alisulubiwa, alikufa na kufufuka kama majibu ya kuokolewa na mauti unaona!,Hii ni tofauti na mauti iliyomkuta Muhamadi ambaye alihaha na kuogopa kufa sana badala ya kumtumainia mungu,Muhamad alisema “Enyi watu! Hakika kukata roho kuna machungu makubwa” (Maisha ya nabii Muhamad uk 80 kifungu cha tatu)Hivyo Yesu asife bali kuokolewa na mauti baada ya kifo.

· Kwa mujibu wa IVP Bible background commentary (New Testament) inasema “Wayahudi wanaamini kuwa Mungu alisikia maombi ya Yesu na Mungu aliyajibu kwa kumfufua na sio kwa kuikwepa mauti yenyewe bali kwa kufufuka kutoka mautini”

· The applied New testament commentary by Thomas Hale inasema hivi “Yesu aliomba aokolewe na mauti ya msalaba (Marko 14;35-36) lakini Mungu hakuchukuliana na Maombi hayo,Mungu angeweza kumuokoa kutoka mautini lakini hakuchagua hivyo,ingawaje siku ya tatu alimfufua toka kwa wafu”Matendo 2;22-28.

Kwa kufundisha kinyume na ukweli huu Waislamu wanataka kutuambia kuwa Yesu ni Muongo, huku Quran inathibitisha kuwa hakuwa na dhambi. Yesu mwenyewe alisema anautoa uhai wake (Yohana 10;14-18) Yesu mwenyewe anawachanganya wislamu kwa kuwa yeye mwenyewe ni njia kweli na uzima hivyo aliutoa uhai wake yeye mwenyewe na kuutwaa tena.

Shalom,

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW