Monday, March 19, 2018

VINASABA (DNA) NDANI YA BIBLIA

Image result for DNA NI NINI?
VINASABA (DNA) NI NINI?
DNA Ni kifupi cha neno (Deoxyribonucleic Acid). Hizi ni chembechembe asili za urithi au viini tete ambavyo hupatikana katika kila kiumbe hai.

Nasaba hupatikana katika kiini cha seli hai na huwa na taarifa za urithi kutoka kwa mzazi kwenda kwa mtoto. Taarifa za nasaba ndizo pekee zenye kutoa ukweli usiopingika kuhusu uzao wa mtoto.

Msingi wa Uchunguzi wa DNA (Vinasaba) Kila Binadamu ana mpangilio wa chembechembe asili za urithi aliyorithi kutoka kwa wazazi wote wawili (Baba na Mama). Mpangilio wa chembechembe asili za urithi hurithiwa nusu kutoka kwa baba na nusu kutoka kwa mama. Hivyo basi ili kutambua uhalali wa mzazi kwa mtoto ni lazima mtoto awe na chembechembe asili za urithi nusu zinazooana na za baba na nusu nyingine zinazooana na za mama.

ZIMEANDIKWA KWA NJIA AMBAYO TUNAWEZA KUELEWA


Bila shaka! Ikiwa Mungu ndiye aliyeumba uhai, basi Mungu ndiye anayestahili kusifiwa wala si mageuzi. (Ufunuo 4:11) Pia, ikiwa sisi tumeumbwa na Muumba mwenye hekima, basi tupo hapa kwa kusudi fulani. Hali isingekuwa hivyo ikiwa uhai ulijitokeza wenyewe.
Habari yoyote iwe ni picha, sauti, au maandishi, inaweza kuhifadhiwa na kushughulikiwa kwa njia nyingi. Kwa mfano, kompyuta hufanya hivyo kielektroniki. Kwa kutumia DNA, chembe hai huhifadhi na kushughulikia habari kwa njia ya kikemikali. DNA hupitishwa wakati chembe zinapogawanyika na viumbe vinapozaliana—uwezo unaoaminika kwamba ndiyo unaofafanua maana ya uhai.
Chembe hutumia habari jinsi gani? Hebu wazia kwamba DNA ni kama kitabu cha mapishi chenye maelekezo na hatua mbalimbali, na kila hatua imeandikwa kwa umakini na utaratibu maalumu. Hata hivyo, badala 
Habari zilizo kwenye chembe ya urithi huhifadhiwa mpaka zitakapohitajiwa, labda ili kubadili chembe zilizochakaa au zilizo na ugonjwa kwa kutokeza chembe mpya au kupitisha tabia kwa mtoto.
Kufafanua habari zilizo katika DNA kama “lugha ya molekuli ya chembe za urithi hakutoshi,” anasema Küppers. Anaendelea kusema hivi: “Kama tu ilivyo katika lugha za wanadamu, lugha ya molekuli ya chembe za urithi ina utaratibu maalumu.” Kwa ufupi, DNA ina “sarufi,” au kanuni, zinazoongoza kikamili jinsi maagizo yanavyotolewa na kutekelezwa.
“Maneno” na “sentensi” katika DNA huunda “maagizo” mbalimbali ambayo huongoza kutokezwa kwa protini na viini vingine vinavyojenga chembe mbalimbali zinazounda mwili. Kwa mfano, “maagizo” hayo yanaweza kuongoza kufanyizwa kwa chembe za mifupa, misuli, neva, au chembe za ngozi. Mwanabiolojia wa mageuzi, Matt Ridley aliandika hivi: “Uzi wa DNA una habari au ujumbe ulioandikwa kikemikali, na kila herufi moja inawakilisha kemikali moja.” Akaongezea hivi: “Ni jambo la kushangaza kwamba alama hizo au utaratibu huo hubadilika na kuwa maandishi tunayoweza kuelewa.”
Mwandikaji wa Biblia Daudi alisali kwa Mungu hivi: “Macho yako yalikiona kiini-tete changu, na katika kitabu chako sehemu zake zote zilikuwa zimeandikwa.” Zaburi 139:16) Daudi alitumia lugha ya kishairi. Hata hivyo, kulingana na kanuni, alikuwa sahihi kabisa akiwa mwandishi wa Biblia. Hakuna mwandishi yeyote wa Biblia aliyeathiriwa hata kidogo na hekaya au mapokeo ya watu wa kale.—2 Samuel 23:1,2; 2 Timotheo 3:16.
Wanasayansi wengi husema nini? 
Wanabiolojia wengi na wanasayansi fulani hufikiri kwamba DNA pamoja na maagizo yake yaliyopangwa vilitokana na matukio yaliyojitokeza yenyewe ambayo yalifanyika kwa kipindi cha mamilioni ya miaka. Wanasema kwamba hakuna uthibitisho wa ubuni katika maumbile ya molekuli hiyo wala katika habari inayobeba na kuituma wala jinsi inavyofanya kazi.
Biblia inasema nini? 
Biblia inasema kwamba kufanyizwa kwa sehemu mbalimbali za mwili wetu—hata wakati zitakapofanyizwa—kunahusisha kitabu cha mfano ambacho chanzo chake ni Mungu. Ona jinsi Mfalme Daudi alivyoongozwa na roho kueleza mambo, akisema hivi kumhusu Mungu: “Macho yako yalikiona kiini-tete changu, na katika kitabu chako sehemu zake zote zilikuwa zimeandikwa, kuhusiana na siku ambazo zilifanyizwa na hakukuwako hata moja kati ya hizo.”—Zaburi 139:16. 
Uthibitisho unafunua nini?
Ikiwa fundisho la mageuzi ni la kweli, basi inapaswa angalau kuonekana kwamba huenda DNA ilijitokeza yenyewe kupitia mfuatano wa matukio. Ikiwa Biblia inasema kweli, basi DNA inapaswa kutoa uthibitisho wenye kusadikisha kwamba inatokana na Muumba mwenye utaratibu na akili.
Shalom
Max Shimba Ministries 

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW