Friday, March 23, 2018

Unyegereshano (Kutiana Ashiki) katika Uislam

Related image
Halliyatul-Muttaqiin, Uk. 110
Imesimuliwa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Usijishughulishe katika kujamiiana na mkeo kama kuku; bali kwanza kabisa jishughulisha katika kutiana ashiki kwa unyegereshano pamoja na mke wako na kuchezeana naye halafu ufanye mapenzi naye.”14

Wasa’ilush-Shi’a, Juz. 20, Uk.118, namba 25186
Imesimuliwa pia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Starehe na michezo yote haina maana isipokuwa kwa mitatu tu: Upanda farasi, kurusha mishale na unyegereshano na mke wako, na hii mitatu ni sahihi.”15

Halliyatul-Muttaqiin, Uk. 115
Imesimuliwa kutoka kwa Imam Ali (a.s.): “Yeyote anayetaka kuwa karibu na mke wake lazima asiwe na papara, kwa sababu wanawake kabla ya kuji- ingiza kwenye tendo la kufanya mapenzi lazima wajiingize kwenye unyegereshano ili kwamba wawe tayari kwa ajili ya kufanyiwa mapenzi.16

Ibid., Juz. 20, uk. 188, namba 25185
Imesimuliwa kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s.): “Malaika wa Mwenyezi Mungu na wale ambao ni mashahidi juu ya matendo yote ya wanadamu wanawaangalia katika kila hali isipokuwa wakati wa mashindano ya kupanda farasi na ule wakati ambapo mwanaume anajiingiza katika kujishughulisha na unyegereshano na mke wake kabla hawajajihusisha katika kujamiiana.” 17

Taratibu Za Kunyegereshana

Kuna vikwazo vichache sana kwenye taratibu zinazotumika katika unyegereshano; kupigana mabusu, kukumbatiana na kadhalika yote haya yanaruhusiwa. Hapa chini ni baadhi ya mbinu zinazofaa kwenye taratibu maalum:

A) Upapasaji Kwenye Matiti

 Mustadrak al-Wasaa’il, Juz. 2. Uk.545
Imesimuliwa kutoka kwa Imam ar-Ridhaa (a.s): “Usijiingize kwenye kujamiiana isipokuwa kwanza ujishughulishe katika unyegereshano, na ucheze naye mkeo sana na kumpapasa matiti yake, na kama ukifanya hivi atazidiwa na ashiki (na kusisimka kwa upeo kamilifu) na maji yake yat jikusanya. Hii ni ili ule utoaji wa majimaji uchomoze kutoka kwenye mati- ti na hisia zinakuwa dhahiri usoni mwake na kwenye macho yake na kwamba anakuhitaji kwa namna ileile kama wewe unavyomhitaji yeye.” 18

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW