Wednesday, March 21, 2018

KWANINI YESU ALITHIBITISHA KUWA MAANDIKO "BIBLIA" HAINA SHAKA?

Kwenye injili, je Yesu aliamini kuwa Maandiko hayana makosa (kwenye maandishi yake ya awali)?

jibu hili lilitolewa kwenye tovuti ambayo haipo tena www. wam.umd.edu /~cbernard/Theology/inerrancy.html.

Yesu amekuwa akiyachukua masimulizi ya kijistoria ya Agano la Kale kama rekodi za ukweli halisi. Anataja:

Abeli (Luka 11:51)

Nuhu (Mathayo 24:37-39; Luka 17:26, 27)

Abrahamu (Yohana 8:56)

Tohara (Yohana 7:22; linganisha na Mwanzo 17:10-12; WaLawi 12:3)

Sodoma na Gomora (Mathayo 10:15; 11:23,24; Luka 10:12)

Lutu (Luka 17:28-32)

Isaka na Yakobo (Mathayo 8:11; Luka 13:28)

Mana jangwani (Yohana 6:31, 49, 58)

Nyoka jangwani (Yohana 3:14)

Yesu kama Bwana wa Daudi (Mathayo 22:43; Marko 12:36; Luka 20:42)

Daudi akila mikate ya wonyesho (Mathayo 12:1-8; Marko 2:23-28; Luka 6:1-5)

Sulemani (Mathayo 6:29; 12:42; Luka 11:31; 12:27)

Elisha (Luka 4:27)

Yona (Mathayo 12:39-41; Luka 11:29, 30, 32)

Zakaria (Luka 11:51)

Kifungu cha mwisho kinaleta dhana ya Yesu ya umoja wa historia kutokea "kuumbwa kwa dunia" hadi "kizazi hiki."

Amemwongelea Musa mara kwa mara kama mtoaji sheria (Mathayo 8:4; 19:8; Marko 1:44; 7:10; 10:5; 12:26; Luka 5:14; 20:37; Yohana 5:46; 7:19). Hutaja mara kwa mara mateso ya manabii wa kweli (Mat 5:12; 13:57; 21:34-36; 23:29-37; Mak 6:4 [linganisha na Luka 4:24; Yohana 4:44]; 12:2-5; Luka 6:23; 11:47-51; 13:34; 20:10-12) na anatoa maoni kuhusu umaarufu wa manabii wa uongo (Luk 6:26). Anathibitisha vifungu muhimu kama Mwanzo 1 na 2 (Mat 19:4,5; Mak 10:6-8).

Kuna watu wanaoweza kupinga kuhusiana na jambo hili na kusema kuwa Yesu alikuwa akitumia mambo ya kubuniwa na hadithi za kimila kuelezea mambo aliyokuwa akifundisha. Wazo hili linawezekana kuwa sahihi katika vifungu vingine lakini halielekei kuwa hivyo hapa. Kwanza, jambo ambalo mtu analipata tokana na kusoma habari za kwenye injili ni kuwa Yesu anachukulia masimulizi ya Agano la Kale kuwa historia halisi. Lengo la kunukuu Maandiko linaonyesha kuwa Yesu aliamini masimulizi haya kuwa yanawasilisha matukio halisi kihistoria. Pili, haionekani kuwa ni maana mojawapo ya kweli kudai kuwa Yesu alikuwa anatumia tu mambo ya kubuniwa yaliyopo kwenye jamii yake kuelezea mafundisho yake kwenye vifungu kama Mathayo 12:41; 24:37; 11:23,24; 5:12; 4:4.

Tatu, anachukulia kuvuviwa kwa Biblia kuwa ni jambo la kweli. Anatumia misemo "Andiko linasema . . .", na "Mungu anasema . . ." kwa kubadilishana na kwa kufanya hivyo anaonyesha kuwa maandishi ya Agano la Kale ni Neno la Mungu. Akinukuu Mwa 2:24, Yesu alisema, "Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sabaabu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye . . ." Tazama kuwa Mwa 2:24 si nukuu ya moja kwa moja ya maneno ya Mungu kwenye maandishi bali ni ufafanuzi wa mwandishi au msimulizi wa maandishi haya. Yesu anayachukulia maneno ya kifungu hiki cha Maandiko kuwa maneno ya Muumba mwenyewe. Kuvuviwa kwa nakala za awali (autographa) kunaonyesha kuwa Maandiko yalichukuliwa kutokuwa na makosa. Kama Yesu alikuwa sahihi kulichukua Agano la Kale kuwa ni maneno halisi ya Muumba, kulichukulia Agano la Kale kuwa lina makosa ni sawa na kumchukulia Mungu kuwa ana makosa.

Nne, aliamini kidhahiri kabisa mamlaka ya Biblia. Katika malumbano haya na Mafarisayo na Masadukayo, Yesu anayatumia Maandiko kama mamlaka yake ya kutatua malumbano haya. Anayaona Maandiko kuwa neno maneno yenye nguvu zaidi (Yohana 5:39-47; Mathayo 22:29, 31; Mak 12:24-26, Luk 20:37). Maandko yanaposema, Mungu anasema na suala lenye kuleta malumbano linasuluhishwa.

Shalom

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW