Saturday, March 17, 2018

MPINGA MUNGU MAREHEMU STEPHEN HAWKING NA WENZAKE WANAAMINI NINI?

 Image result for stephen hawking
Walidai kwamba wangekuwa na akili, wakawa wajinga. (Warumi 1:22)

 
 Marehemu Stephen Hawking haamini katika Mungu lakini yeye anaamini kwamba "asili ya ulimwengu inaweza kuelezwa na fizikia, bila kipengele chochote cha miujiza au kuingilia Mungu."

Kwa miaka 50 mwanafalsafa muingereza, Anthony Flew, aliheshimiwa sana na Wanasayansi wenzake kuwa mtetezi mkuu wa fundisho kwamba hakuna Mungu. Kichapo chake "Theology and Falsification" yaani Theolojia na uwongo ambacho aliandika mwaka 1950, kilikuwa ndicho kichapo kilichochapishwa mara nyingi sana katika karne yote ya 20. Mnamo mwaka 1986, Flew aliitwa "Mchambuzi mkuu wa fundisho kwamba hakuna Mungu" Kwa hiyo watu wengi walishtuka sana Flew alipotangaza katika mwaka wa 2004 kwamba amebadili maoni yake. 
Kwanini Flew alibadili maoni yake?
Je Sheria za Asili zilitokea namna gani?
Ni kwa sababu ya Sayansi. Alikuja kuamini kwamba, Ulimwengu, Sheria zinazoongoza vitu vya Asili, na Uhai havingeweza kujitokeza vyenyewe. Je wewe unaonaje?

 
Mwanafizikia na Mwandishi Paul Davies anasema kwamba "Sayansi inaeleza vizuri sana matukio ya asili kama mvua. Lakini maswali yanapozuka kama vile, Kwa nini kuna Sheria za Asili? Sayansi haitoi jibu la wazi. Mambo ambayo Wanasayansi wamevumbua hayajajibu maswali kama hayo. Maswali mengi muhimu hayajajibiwa tangu zamani na bado yanatutatanisha leo "

Flew mwenyewe aliandika hivi Mnamo mwaka 2007 " Jambo muhimu si tu kwamba kuna Sheria za Asili, bali pia ni sahihi kabisa Kihisabati , ni za Kweli na zina Uwiano uliokamilika"

Mwanasayansi wa Fizikia, wa karne ya 20, Albert Einstein alisema kwamba" Zinathibitisha kwamba kuna mtu mwenye akili aliyezibuni "

Swali tunalopaswa kujiuliza ni, Sheria hizi za Asili zilitokea jinsi gani? Bila shaka swali hilo liliulizwa pia na Wanasayansi mashuhuri kama Isack Newton, Albert Einstein, na Heisenberg, na jibu lao lilikuwa zilitokezwa na Akili ya Mungu. 

Kwa kweli, wanasayansi wengi wenye kuheshimiwa sana hawaoni kwamba inapingana na sayansi kuamini kwamba kuna Muanzilishi mwenye Akili. Kwa upande mwingine, haipatani na Akili kusema kwamba, Ulimwengu, Sheria zinazouongoza, Uhai pamoja na Ubongo kwamba vilijitokeza tu ghafla vyenyewe. Sisi sote tunajua kwamba, vyombo vyote tunavyoviona, vitu kama, nyumba, magari, Meli au merikebu, ndege au helkopita, hata vifaa kama Komputa, TV au redio kwamba zimetengenezwa na mtu fulani tena mtaalamu zaidi na kwamba ni mtu mjinga tu angeokota Simu Porini, kisha aseme haijaangushwa hapo na mtu. Kwa kweli mtu mwenye utambuzi timamu atazungumza kama Mwandishi wa kitabu cha Waebrania kwamba "Maana kila nyumba imetengenezwa na mtu, lakini aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu" - Waebrania 3:4

Kwa kweli sote pamoja tunaguswa na Miundo tata ya Ulimwengu, na kwa kweli tunapotafakari Maajabu yake twajikuta tumevutwa kusema kama Mtunga Zaburi kwamba "Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu na anga laitangaza kazi ya mikono yake" - Zaburi 19 :1


No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW