Friday, March 30, 2018

KWA NINI YESU ALIKUJA?


Yesu alikuja duniani ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa Milele (Yn. 3:16) Yesu kwa hiari yake mwenywe alikufa ili awape Uzima wa milele kwa watu wake na ambao ni wa Mungu pia.

Kwa sababu ya dhambi hii wanadamu walitengwa na Mungu. Biblia inasema ya kwamba Kristo alikuwako Mbinguni kabla ya uumbaji wa nchi (Yohana 6:38; 8:23-58; Wafilipi 2:5-7, RSV)

Kwa hiyo tunapokuwa watu wazima ni lazima tutubu na kubatizwa ili tuweze kumpokea Yesu Kristo (Kuokoka) kwa kupitia Roho Mtakatifu ambaye ni Mungu.  Yesu alikuja kutupa Uzima kwa kufa kwake (Mauti yake pale Msalabani) ili tupate uzima wa Milele katika yeye na Baba.  Kwa Kifo chake wanadamu sasa wanaweza kutubu katika dhambi zao na tena kupata njia ya kwenda kwa Baba katika Jina la Yesu.

Wote tutakufa katika Kifo cha kawaida, lakini wote tutakuwa na nafasi ya kuishi tena.  Hatuwezi kuishi milele katika miili ya kibinadamu (Miili ya asili) maana hii ni miili  inayoishi kwa muda mfupi tu.  Wafu wote watafufuliwa kutoka Makaburini (Yohana 5:25-26).  Mungu anampango mkuu kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu  (1 Wakorintho 2:1-16). 

Kama ilivyojulikana tangu zamani kwamba Yesu atazaliwa, pia ilijulikana ya kwamba Yesu atakufa na kufufuka baada ya siku tatu mchana na usiku akiwa kaburini (Mathayo16:21).  Na baada ya kufufuka kwake atarudi tena mbinguni (Yohana 14:2,3).

Kifo (Mateso) na kufufuka kwake Yesu ni matukio muhimu sana katika historia ya mwanadamu. Lakini watu wengine wa dini hawaelewi Matukio haya vizuri. Moja ya mambo wanayofundisha kuhusu kifo cha Yesu ni kwamba alisulubiwa msalabani. Lakini neno la kigiriki stouros linamaanisha mti au nguzo iliyonyooka, iliyotumika kwa ajili ya kuwaadhibu wahalifu kwa kuwapigilia na misumari juu ya nguzo hizo au miti hiyo.  Kwa hiyo Yesu alikufa katika mti wa kuadhibia wahalifu na sio msalabani. 

Tunajua ya kwamba Yesu alifufuka kutoka katika wafu (Warumi 1:3-4). Kufufuka kwa Yesu kutoka katika wafu kwa uwezo na nguvu katika Roho Mtakatifu ni udhihirisho kuwa Yesu ni Mungu aliyeshinda mauti.

Kuna ushahidi zaidi wa ufufuo wa Kristo katika 1 Wakorintho 15:3-8 na Matendo 1:2-3 kuanzia Matendo 1:9-10 Tunaona ya kwamba Yesu alichukuliwa juu mbinguni. Alikuwa mzaliwa wa kwanza wa waliokufa na chimbuko la matunda ya mganda ambako kunafanyika siku ya Jumapili wakati wa Pasaka (Angalia Walawi 23:9-14).

Yohana 20:1 Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona jiwe limeondolewa kaburini.

Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13




No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW