Friday, March 16, 2018

WAISLAMU WAPIGWA MARUFUKU KUPIGA ADHANA CHUO KIKUU CHA DUKE NCHINI MAREKANI

Image result for WAISLAMU WAPIGWA MARUFUKU KUPIGA ADHANA CHUO KIKUU

Marekani imepiga marufuku adhana katika Chuo Kikuu cha Duke kilichoko Durham, North Carolina nchini humo. Chuo Kikuu cha Duke ambacho hivi karibuni kilikuwa kimetoa ruhusa kwa Waislamu wa chuo hicho kuadhini, kimepiga tena marufuku suala hilo. 


Wiki iliyopita, viongozi wa chuo hicho kilichopo katika jimbo la Carolina kaskazini walitoa taarifa rasmi iliyoruhusu adhana kupitia mnara wa kanisa shuleni hapo. 


Awali Michael Schoenfeld, Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Duke alinukuliwa akisema kuwa, wanafunzi wa Kiislamu wamekuwa na mchango mkubwa katika ustawi wa chuo na kwamba bodi ya shule inakubali watekeleze ibada zao shuleni hapo.


Hata hivyo ghafla viongozi wa chuo hicho wamepiga marufuku adhana bila kutolewa sababu maalumu. 


Baadhi wanamtaja Franklin Graham, kasisi wa Kimarekani kuwa chanzo cha marufuku hiyo, hasa kwa kuzingatia kuwa hivi karibuni alitishia kukata misaada yake kwa chuo hicho ikiwa Waislamu wataruhusiwa kuadhini chuoni hapo.


SHUKRANI KWA KUFUNGUA BLOGU YETU. TUPE MAONI YAKO KUHUSIANA NA HABARI ULIYOISOMA, ISAMBAZE BLOGU HII KWA WAISLAMU WENGI KADRI UWEZAVYO


No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW