Thursday, August 16, 2018

UTATU WATHIBITISHWA KWA AYA NA HISABATI

Image may contain: text
1 Yohana 5:7 Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. 

Biblia imekamilika na haina shaka ndani yake. Wapinga UTATU huwa wanasema. 1 + 1 + 1 = 3. Je hii ni kweli au si kweli.

Tuanze kuichambua hoja ya 1 + 1 + 1 = 3:

Aya inasema: KWA MAANA WAKO WATATU (3) WASHUHUDIAO MBINGUNI "BABA, NA NENO NA ROHO MTAKATIFU". Umeiona namba tatu hapo. Hivyo 1 + 1 + 1 = 3 inabeba sehemu ya kwanza ya aya kama nilivyo inukuu hapa. Zaidi ya hapo, kuna kiunganishi "NA" alipo tajwa Baba, "NA" Mwana "NA" Roho Mtakatifu. "NA" kimahesabu ni JUMLISHA.

ENDELEA KUSOMA AYA:
... Aya inasema: NA WATATU HAWA NI UMOJA.

Ikimaanisha hawa sasa wapo pamoja Kifra, Roho, na Kiutendaji. Ili uelewe UTATU, tunahitaji kutambua kwamba Mungu Baba na Yesu “Mwana” na Roho Mtakatifu wana uhusiano wa milele kabla ya kuwepo kwa kitu chechote kile.

1 x 1 x 1 = 1

Baba, Mwana na Roho ni watu watatu walio na ushirikiano sawa wakiwepo kama Mungu. Hawa watatu walikuwa, na wataendelea kuwa na uhusiano wa milele (MILELE KIMAHESABU NI INFINITY ∞ + ∞ + ∞ = ∞) . Hawa watatu walikuwepo kabla ya mwanzo kuwepo na wataendelea kuwepo milele na milele yote.

1 + 1 + 1 = 3
1 X 1 X 1 = 1
∞ + ∞ + ∞ = ∞

1 Yohana 5:7 Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.

1 + 1 + 1 = 3
1 X 1 X 1 = 1
∞ + ∞ + ∞ = ∞

Soma kijarida http://www.maxshimbaministries.com/2016/04/utatu-unathibitishwa-kwa-kutumia.html

Shalom,

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW