Saturday, August 4, 2018

UNAJUA UCHAWI UNAO PUKUTISHA PESA ZAKO?




“KUPATA hekima ni bora kama nini kuliko dhahabu! Na kupata uelewaji kunapasa kuchaguliwa kuliko fedha,” inasema Methali 16: 16. Kwa nini hekima ni yenye thamani sana? Kwa sababu “hekima ni ulinzi, kama vile pesa ni ulinzi; lakini faida ya ujuzi ni kwamba hekima huwahifadhi hai waliyo nayo.” (Mhubiri 7:12)
Wengi wamejaribu kwenda kwa waganga kutafuta chanzo na pengine huko waliambiwa kuwa wanarogwa, wakagangwa kwa zindiko, lakini hali yao haijabadilika! Sasa kwa sababu saikolojia ni zaidi ya uchawi, leo nimeona ni bora nikafundisha kuhusu uchawi wa kweli unaopokonya watu pesa zao na kuwaacha wakilalamika kuwa kipato ni kidogo.
Katika hali ya kawaida mchawi hasa wa pesa za wanadamu wengi ni ELIMU DUNI YA JINSI YA KUTUMIA PESA. Watu wengi wanafundishwa shuleni masomo mbalimbali na wanahitimu vyema, lakini wanapokuja katika uwanja wa maisha wanajikuta wanafeli vibaya kutokana na kutojua nidhamu ya pesa. Haishangazi kwamba “mtu mwenye hekima moyoni” anaitwa “mwenye akili” au “mwenye utambuzi”! (Methali 16:21)
Wako madaktari, mainjinia na walimu wengi ambao wanapata pesa, lakini maisha yao ni duni kiasi kwamba wanazidiwa hata na watu ambao ni wauza dengu sokoni. Hii ina maana kuwa elimu ya darasani ni mbali na ile ya matumizi ya pesa binafsi. “Kuna njia ambayo imenyooka mbele ya mwanadamu,” anasema Sulemani, “lakini njia za kifo ndizo mwisho wake baadaye.” (Methali 16:25) Hilo ni onyo juu ya kujidanganya na kufuata njia inayopingana na sheria ya Mungu. Nafsi ya mfanyakazi mwenye bidii imemfanyia kazi kwa bidii,” anaendelea kusema mfalme mwenye hekima, “kwa sababu kinywa chake kimemkaza sana.” (Methali 16:26)
Wataalam wa masuala ya pesa wanasema, ili mtu apate ziada katika pesa yake lazima awe na nidhamu ya matumizi. Sababu hii inatupa mbali dhana kwamba maendeleo yanataka wingi wa pesa. Dondoo zifuatazo zikizingatiwa hata mwenye kipato kidogo atapata ziada!
Tumia pesa taslimuKuna watu wengi sana wanaishi kwa kukopa kopa vitu madukani na kwa watu. Mtindo huu ni mbaya sana kwa ukadiriaji wa matumizi, kwani haumtii uchungu mkopaji hadi pale atakapokuwa analipa. Mara nyingi ukopaji huongeza gharama, hivyo inashauriwa ukiwa na 500 itumie hiyo, bila kutafuta ziada kwenye deni. “Anayetembea na watu wenye hekima atakuwa na hekima, lakini anayeshirikiana na wajinga atapatwa na mabaya.” (Methali 13:20) Hekima ya kimungu inatoa ulinzi mkubwa kama nini!
Panga mafungu madogo madogo ya bajeti:
Katika maisha pendelea kupanga bajeti yako kwa mafungu madogo madogo hasa ya wiki. Usivuke mipango hiyo kwa kutumia bajeti ya wiki inayofuata. “Watu hutupa kura ndani ya mkunjo wa nguo,” anasema mfalme wa Israeli, “lakini kila uamuzi unaofanywa kupitia kura hiyo hutoka kwa Mungu.” (Methali 16:33)
Pendelea kukaa nyumbaniWatu wengi wanapenda kutembea tembea mitaani huku wakiwa na pesa nyingi mifukoni. Fahamu kuwa kutembea na pesa usizozipangia bajeti utajikuta unashawishika kuzitumia.
Hivyo unashauriwa kutulia nyumbani na kama utatoka siku za weekend ni vema mtoko huo uwe na bajeti, si kukurupuka tu na mapesa yako na kujikuta uko baa au kwenye majumba ya starehe!
Nunua vitu kwa jumla:
Kama unataka kupata ziada katika kipato chako pendelea sana kununua vitu kwa jumla ambavyo utavitumia kwa mwezi mzima. Epuka kununua vipimo vidogo vidogo kwani vinaumiza na kuvuruga bajeti.
Pika chakula nyumbani kwakoWatu wengi hasa vijana wanapenda sana kula kwenye migahawa na hotelini. Ulaji huu ni ghali, hivyo inashauriwa kila mtu ajipikie chakula chake nyumbani. Hii itamsaidia kutumia pesa kidogo katika suala la chakula.
Ifundishe familia kubana matumizi Kuna watu hawawafundishi watoto na wake zao nidhamu ya matumizi ya pesa. Mume/mke asinunue vitu ambavyo familia haikuvitengea bajeti na asiwepo mtumia hovyo vitu vilivyonunuliwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Mazoezi ni muhimu:
Familia nyingi hazitilii mkazo suala la kufanya mazoezi, lakini wataalam wanasema ufanyaji wa mazoezi unajenga afya na hivyo kupunguza gharama za matibabu. Hii inakwenda sambamba na ulaji wa milo bora.
Akiba na mipango: 
Familia lazima ijiwekee akiba benki. Utunzaji wa pesa nyumbani au mfukoni umebainika kuwa ni mgumu na mara nyingi hushawishi matumizi. Lakini sambamba na hilo la akiba lazima pesa zinazotunzwa zipangiwe malengo ya matumizi na malengo hayo yatimizwe kidogo kidogo si mpaka yasubiri pesa ziwe nyingi.
Upunguzaji wa familiaIngawa ni hali halisi ya maisha ya kiafrika kwa familia moja kuwa na watu wengi lakini inashauriwa kwamba, ili kupata ziada ya kipato lazima familia iwe ndogo, vinginevyo mshahara wote unaweza kutumika kwa chakula tu. Laa kama familia itakuwa ni kubwa basi kila mmoja afanye kazi ili uwepo usaidianaji wa kuendesha familia.
Yako mengi ya kujifunza katika somo hili asanteni.
Mhubiri 7:11 Hekima ni njema, mfano wa urithi; Naam, nayo ni bora kwao walionao jua. 12 Kwa maana hekima ni ulinzi, kama vile fedha ilivyo ulinzi; na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.


No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW