Wednesday, March 28, 2018

JE, INJILI YA MAFANIKIO NI YA KIBIBLIA?

Image result for prosperity gospel


Biblia inataja maskini zaidi ya mara 245 na hii inaonesha jinsi Mungu alivyo na mengi ya kusema kuhusu umaskini. Suala hili lipo karibu na moyo wake na kamwe hautaji umaskani kama baraka, wala utukufu, au jambo la kufurahiwa, kinyume chake Biblia inasema ni laana.

Mimi Ninaamini Katika INJILI YA MAFANIKIO Maana BIBLIA imesema wazi ya kwamba INJILI YA YESU inatuingiza kwenye FAMILIA YA MUNGU ALIYEFANIKIWA, na Yesu alikuwa maskini kwa ajili yangu ili nami nipate kuwa tajiri kwa umaskini wake.

Hakuna mwanadamu hapa chini ya jua asiyetaka mafanikio ya kimwili! Hakuna mwanadamu asiyetamani kumiliki majumba, magari, fedha na kila aina ya mali ambayo Mungu aweza kumjalia. 

Kristo Yesu alikuwa masikini ili sisi tuwe matajiri 2 Wakorintho 8:9 "Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake"

Neno Ijili likiwa na maana ya HABARI NJEMA, linathibitisha moja kwa moja kuwa, INJILI YA MAFANIKIO ni ya Kibilia maana habari NJEMA KWA MASKINI NI KUTOA UMASKINI WAKE, kama ilivyo habari njema kwa mgonjwa ni kupona.

Sasa mpendwa, kwanini unapinga HABARI NJEMA huku kila siku unaenda kazini kufanya kazi au unafanya biashara ili upate mafanikio? Hata huyo Mchungaji wako anaye pinga hii INJILI iweje aombe fedha ambazo anadai ni za laana, tena analazimisha mtoe KIKUMI NA SADAKA? 

Kama INJILI YA MAFANIKIO ni mbaya na inaendana kinyume na Biblia, kwanini Mungu huyohuyo anawataka wafuasi wake watoe KIKUMI NA SADAKA kutoka fedha unazo ziita wewe za LAANA? Nabii Hosea anakwambia "Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa."(Hosea 4:6)

UTHIBITISHO:

Wafilipi 4:19 "Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu".

Waumini ambao huwapa maskini kwa hiari watabarikiwa na Mungu, lakini utawezaje kumsaidia maskini wakati unapinga vikali INJILI YA MAFANIKIO? "Amhurumiaye masikini humkopesha Bwana,/naye atamlipa kwa tendo lake jema" (Methali 19:17). Baraka hizi za kimungu zinaweza kuwa za kiroho badala ya vifaa, lakini malipo ni ya uhakika-kutoa kwa maskini ni uwekezaji wa milele.

“Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.” MITHALI 22:7

Mtu aliyeokoka anatakiwa we ana mali huku anamcha Bwana, mtazamo wa dunia ni kwamba wenye mali hao hawajaokoka nawasiona mali ndio wameokoka.

“Naye Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu.” MWANZO 13:2

“Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu. Kisha walizaliwa kwake wana saba, na binti watatu. Mali yake nayo yalikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng’ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watu wa nyumbani wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.” AYUBU 1:1-

Zamani kwenye agano la kale watu wa Mungu walitambulika kwa utajiri wao. Shetani hatishwi na masikini sababu anajua hana madhara na kazi zake na mfumo wa dunia umetengeneza mfumo watu wenye dhambi wazidi kuwa matajiri halafu sisi tulio wa Mungu tuendelee kuwa masikini.

“Nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.” Isaya 45:3

Unatakiwa ufute kwenye akili yako kwamba kuwa na mali ni mpaka uwe hujaokoka. 

Shalom

Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Tito 2:13





No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW