YESU ALIPO INGIA TU DUNIANI, ANAANZA KWA KUSUJUDIWA, SWALI MWENYE HAKI YA KUSUJUDIWA NI NANI?
Mathayo 2:10-11 “Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno. Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane.
Kulingana na Biblia, watu hao wanaoitwa mamajusi walitoka “sehemu za mashariki,” nao walipata habari za kuzaliwa kwa Yesu wakiwa huko. (Mathayo 2:1, 2, 9) Bila shaka iliwachukua muda mrefu kusafiri kutoka huko hadi Yudea. Hatimaye walipompata Yesu, walianguka na kumsujudia. —Mathayo 2:11.
Mathayo 2: 1 Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, 2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.
Mwenye haki ya kuabudiwa na kusujudiwa ni Mungu peke yake. Sasa iweje hawa wataalamu wa Nyota na wajuzi kutoka Mashariki ya Mbali wamwabudu na kumsujudia Yesu?
Kwanini mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye?
Ndio utafahamu kuwa YESU NI MUNGU.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13
No comments:
Post a Comment