Friday, December 7, 2018

KWA NINI TUNASHEREKEA EID YA KRISMASI?

Image may contain: text
Shalom Wapendwa,
Krismasi maana yake nini?
“Krismasi,” kinasema kitabu cha Encyclopedia of Religion, inamaanisha “‘Misa ya Kristo,’ yaani, misa ya kusherehekea kuzaliwa kwa Kristo.”
Tunasherekea sikukuu (IDI) ya Kristmasi kwa kukumbuka kuzaliwa Mwokozi, Masihi wetu yaani Yesu Kristo wa Nazareti. Zaidi ya hapo, sikukuu ya kuzaliwa husherekewa mtu anapo kuwa hai, kumbe basi tunasherekea Yesu Kristo aliye hai milele yote.
Hivyo basi naweza kusema kuwa tunasherekea kukumbuka ujio wa Wokovu kwa Mwanadamu. Sote twafahamu kwamba mwanadamu alipotea baada ya lile anguko la dhambi ya Adamu na Hawa pale bustani ya Eden.
Mwanadamu alikuwa amehesabiwa kutokuwa na maisha ya raha ya umilele. Lakini kwa kuwa Mungu aliupenda ulimwengu, yaani Bwana Mungu alikupenda wewe na mimi ndipo akamtuma mwanaye wa pekee Yesu Kristo ili kila amuaminie awe na uzima wa milele, tele (Yohana 3:16). Kwa lugha nyepesi ni kwamba tunasherekea siku hii kukumbuka WOKOVU aliouleta Bwana Yesu Mungu Mkuu na Mwokozi wetu; Soma Tito 2:13, maana ndani yake ndimo kuna maisha halisi ya umilele.
Nabii isaya alitabili kuzaliwa kwa Yesu (takribani miaka 700 kabla ya kuzaliwa kwake Bwana Yesu Kristo) akisema;
"...bikira atachukua mimba,atazaa mtoto mwanamume,naye atamwita jina lake Imanueli." Isaya 7:14
Tabiri hii ya Nabii Isaya ni hakika na kweli. Zipo tabiri nyingi zilizowahi kutolewa, lakini tabiri ya Nabii Isaya imekamilika maana hakika Bwana amezaliwa. Kuzaliwa kwa Bwana Yesu ni muujiza ambao haukuwai kutokea wala haitegemewi kutokea, sababu kuzaliwa kwake kulitokana na uweza wa Roho Mtakatifu. Tena angali Bwana Yesu amezaliwa alikuwa tayari amekwisha vikwa uwezo, uweza na nguvu ndani yake.
Sasa waweza kufikiria kwamba ni mtoto gani anayezaliwa akiwa na utiisho wa ki-Mungu kama huo, kwa sababu Biblia inaanza kumuelezea kwamba alipozaliwa tu aliitwa mtoto MWANAMUME, yaani si mtoto wa kiume bali ni mwanamume ikionesha tayari alikuwa na nguvu za kipekee tena Yeye ni Imanueli Mungu pamoja nasi, soma Mathayo 1:23.
Biblia inasema;
"Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria, kusudi awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana." Wagalatia 4:4-5
Kumbe kabla ya ujio na kumpokea Bwana Yesu Kristo sisi tulikuwa chini ya sheria. Tukiitumikia miungu ya baba zetu, tulikuwa watu tusiokuwa na Mungu duniani. Hivyo basi hatukuweza kufanyika wana wa Mungu, bali ingawa tulikuwa ni watu wa Mungu tu.
Tunasherekea sikukuu hii kwa kukumbuka ujio wa injili duniani.
Yesu mwenyewe ndio injili.
Yeye alipozaliwa, Injili ndio ilizaliwa kwa mara ya kwanza chini ya jua.
Maana Yeye ni Neno, Injili ni habari njema ziletazo wokovu, hivyo ni neno la Mungu liletalo wokovu. Biblia imeeleza vizuri sana jambo hili, inasema;
" Malaika akawaambia, msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote;" Luka 2:10
Malaika wa Bwana anatambulisha kuwa ujio wa Yesu Kristo duniani ni ujio wa habari njema ya furaha. Yaani ni ujio wa injili, maana injili ina furaha ndani yake, hivyo siku ya leo tunaposherekea sikukuu hii, tunakumbuka ujio wa habari njema chini ya jua.
Kumbe basi, hakuna kosa lolote lile kusherekea na kukumbuka ujio wa WOKOVU NA HABARI NJEMA.
Je, upo tayari kusherekea na kufurai kuwa Wokovu na Habari njema umekuja kwa ajili yako?
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW