Tuesday, December 25, 2018

KWANINI WAKRISTO TUNATUMIA MTI WA KRISMAS?

Image may contain: sky, christmas tree and outdoor
JE, NI SAHIHI KIBIBLIA KUTUMIA MTI WA KRISMASI?
SEHEMU YA KWANZA
SOMO:-UKWELI KUHUSU MTI WA KRISMAS
(CHRISTMAS TREE)
NA
MAJIBU YA UFAFANUZI KWA WAPINGA CHRISTMAS
Ili iwe vyepesi kwetu kulielewa vizuri somo hili Tutajifunza somo hili kwa kuligawa katika vipengele vinne ambavyo ni:-
1? HISTORIA YA MTI WA KRISMAS NA UCHAMBUZI WAKE.
2? KWANINI WAKRISTO TUNATUMIA MTI WA KRISMAS?
3? VITU VIWI VYA KUEPUKWA KATIKA SHEREHE YA KRISMAS.
4? MAJIBU YA UFAFANUZI KWA WAPINGA KRISMAS.
Mstari muhimu wa kukumbuka:-
ISAYA 60:13:-" Utukufu wa Lebanoni utakujia wewe, (miti ya) mberoshi na mtidhari na mteashuri pamoja; ILI KUPAPAMBA MAHALI PANGU PATAKATIFU, Nami nitapatukuza mahali pa miguu yangu.".
UTANGULIZI
Katika kipindi kama hichi cha kusherekea sikukuu ya Krismasi. Moja vitu muhimu sana vinavyotumika katika kuipamba na kuitambulisha sherehe hii ni hichi kinachoitwa "Mti wa Krismas" (Christmas tree). Ambao mti huu ni maarufu sana duniani kote katika kuitambulisha Krismas yenyewe. Kila inapofikia majira kama haya ya sikukuu hii, mti huu huwekwa kama pambo muhimu la Krismasi katika makanisa au majumbani mwetu.
Mti huu wa Krismas una historia yake hata kabla ya kuingizwa kwa sherehe yenyewe ya Krismas hapo kabla.
Wako watu wengine kwa mafundisho yao potofu ya kutokuiekewa ile KWELI HALISI YA BIBLIA na kutokuwa na ufahamu mzuri wa kupambanua kujua kipi ni kipi kilicho sahihi na ambacho siyo sahihi kukifuata. Watu hao wapotoshaji wa sikukuu hii, wanapoona wakristo hasa tuliookoka kwenye makanisa ya kipendekoste tunautumia huo mti wa Krismas. Kumekuwa na kelele zao nyingi za kutukashifu imani yetu eti kwa kuutumia huo mti wa Krismas eti tunaabudu miungu ya kipagani ~Tamuz na kufuata desturi za kipagani.
HIII SIYO KWELI HALISI. Bali ni hila za shetani tu za kupindisha pindisha mambo kihistoria ili kututoa katika msingi wa imani yetu ya kweli. HATUNABUDI KUWA NA UFAHAMU MZURI KATIKA KUIELEWA HISTORIA NA KUIPAMBANUA VYEMA kulingana na kipimo cha kweli ya Neno la Mungu (Biblia ).
WAKOLOSAI 2:4-8:-"Nasema neno hili, MTU ASIJE AKAWADANGANYA KWA MANENO YA KUSHAWISHI. Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo. Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; wenye shina na wenye kujengwa katika yeye; mmefanywa imara kwa imani, kama mlivyofundishwa; mkizidi kutoa shukrani. ANGALIENI MTU ASIWAFANYE MATEKA KWA ELIMU YAKE YA BURE NA MADANGANYO MATUPU, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo."
WAEFESO 4:14-15:-" ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. LAKINI TUISHIKE KWELI katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo.".
Kumekuwa na kelele nyingi za mafundisho ya upotoshwaji kwa kigezo kupitia dondoo za kihistoria kuhusu sherehe hii ya Krismasi. Neno la Mungu limetuonya hapo TUSIDANGANYIKE BALI TUIFAHAMU ILIYO KWELI NA KUISHIKA.
N. B:- Wakristo katika imani yetu ya wokovu hatuongozwi na historia kama dira ya imani yetu. BIBLIA NDIO DIRA YETU NA KIPIMO CHETU. Na historia yoyote ile usahihi wake tutaufuata baada ya kuupima kwa misingi ya Neno la Mungu (Biblia ) inasema nini au inatufundisha nini kuhusu jambo husika! ". Sio lazima jambo hilo litajwe moja kwa moja kama lilivyo, bali Biblia imetupa kanuni zilizoko kwenye maandiko za kupima kila jambo kama ni vyema au sio vema kwa Mungu.
[ 2 PETRO 1:19; ZABURI 119:105; 2TIMOTHEO 3:15-17].
Ndiomaana tuko hapa leo ili kujifunza neno la Mungu kwa usahihi. Ili Kupitia katika somo hili tupate ufafanuzi na kuelewa kilicho sahihi kwetu wakristo tuliookoka kukifuata.
Endelea kufuatilia somo hili mpaka mwisho.
1? KIPENGELE CHA KWANZA.
HISTORIA YA MTI WA KRISMAS NA UCHAMBUZI WAKE
?? ORIGIN OF THE MODERN CHRISTMAS TREE
(Christmas tree - Wikipedia)
Modern Christmas trees originated during the�Renaissance�of�early modern Germany. Its 16th-century origins are sometimes associated with Protestant Christian reformer�Martin Luther, who is said to have first added lighted candles to an�evergreen�tree.
The first recorded Christmas tree can be found on the keystone sculpture of a private home in�Turckheim, Alsace (then part of Germany, today France), dating 1576.
While today the Christmas tree is a recognized symbol for the holidays, it was once a pagan tradition unassociated with Christmas traditions.
Other sources have offered a connection between the symbolism of the first documented Christmas trees in Alsace around 1600 and the trees of pre-Christian traditions. For example, according to the�Encyclop�dia Britannica, "The use of�evergreen trees, wreaths, and garlands to symbolize eternal life was a custom of the ancient Egyptians,�Chinese, and�Hebrews. Tree worship was common among the pagan Europeans and survived their conversion to Christianity in the Scandinavian customs of decorating the house and barn with evergreens at the New Year to scare away the devil and of setting up a tree for the birds during Christmas time."
During the Roman mid-winter festival of Saturnalia, houses were decorated withwreaths�of evergreen plants, along with other antecedent customs now associated with Christmas.
The�Vikings�and�Saxons worshiped trees.
In�Poland�there was an old�pagancustom of suspending a branch of fir, spruce or pine called�Pod?a?niczka�from the ceiling. An alternative to this wasmistletoe. The branches were decorated with apples, nuts, cookies, colored paper, stars made of straw, ribbons and colored wafers. Some people believed that the tree had magical powers that were linked with harvesting and success in the next year.
In the late 18th and early 19th century, these traditions were almost completely replaced by the German custom of decorating the Christmas tree.
?? (Christmas tree - Wikipedia)
?? UCHAMBUZI WAKE IKO HIVI.
Kama ulivyosoma hapo juu . Miongoni mwa wapagani wa ulaya kabla ya kuwa wakristo na suala hili la Krismas kuanza. Hapo mwanzoni kabla, wapagani hao walikuwa na desturi ya Ibada ya kuabudu mimea/miti ya kijani na kuipamba, wakaingiza majumbani mwao. Kwa sababu waliamini kwamba miti hiyo ilikuwa na nguvu za kimiujiza za kuweza kuwalinda na roho ovu , katika kuwapa mavuno na kuwafanikisha katika mwaka ujao. Miti hiyo pia ilishirikishwa na masuala ya sikukuu ya miungu (sarturnalia-mungu wa kilimo). Na hata baada ya wapagani hao kuwa wakristo waliendelea kuwa na imani hiyo juu ya miti.
Kwa sababu miti hiyo ilitumiwa na wapagani. Sasa JE WAKRISTO KUTUMIA TU MITI HIYO NI KOSA?
Jibu ni hapana! Kwa sababu gani? Ni muhimu kuelewa vizuri Biblia neno la Mungu inaiita miti hiyo kuwa ni "MITI YA BWANA" yeye ndiye aliyeiumba na kuifanya kuwako mimea yote. Biblia inasema katika ISAYA 41:19-20:-"Nitapanda katika jangwa mwerezi, mshita, mhadasi, na mbono; nitatia katika nyika mberoshi, mtidhari, na mteashuri pamoja; ili waone, na kujua, wakafikiri, na kufahamu pamoja, ya kuwa mkono wa BWANA ndio uliofanya jambo hilo. Mtakatifu wa Israeli ndiye aliyeliumba."
ZABURI 104:16:-" Miti ya BWANA nayo imeshiba, Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda".
Unaweza kuona! Kumbe hiyo miti siyo ya wapagani, ni ya Mungu. Kwahiyo kama miti ni ya Mungu. Sio kosa sisi wakristo kuitumia. INATEGEMEA TU NI MATUMIZI GANI YA HIYO MITI JINSI TUNAVYOITUMIA ! Kuitumia miti yoyote au mimea yoyote kama kifaa kwa ajili ya matumizi ya kumpa yeye Mungu utukufu sio kosa. Ni halali kabisa!
Kwa mfano juu ya hilo Biblia inasema :- " Msifuni, jua na mwezi; msifuni, nyota zote zenye mwanga. Msifuni, enyi mbingu za mbingu, na maji mlioko juu ya mbingu........Msifuni BWANA kutoka nchi, Enyi nyangumi na vilindi vyote......Milima na vilima vyote, MITI YENYE MATUNDA na mierezi yote. Na vilisifu jina la BWANA, kwa maana aliamuru vikaumbwa..... " [ZABURI 148:1-13]. "Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo, Maana VITU VYOTE ni watumishi wako" [ZABURI 119:91].
Unaweza kuona! Kumbe MITI nayo ni miongoni mwa vitu vinavyopaswa kutumiwa kumwadhimisha yeye BWANA katika kumtumikia na kumsifu (kumpamba).
Sasa ni muhimu kuelewa vizuri walichokosea wapagani sio kutumia hiyo miti, bali ni MATUMIZI MABAYA ya hiyo miti. Wao kwa ujinga wao kosa kubwa walilolifanya ni "kuiabudu hiyo miti na kuitumaini kama kinga yao badala ya Mungu aliye hai. Waliiweka imani yao kwenye mti badala ya kwa Mungu aliye juu". Ndiyo kosa!
Neno la Mungu linatuonya tusiwe na miungu mingine ila BWANA na tena hatupaswi kukitumainia chochote kile badala ya kumtumainia Mungu wetu aliye juu.
HABAKUKI 2:18-20:-" Sanamu ya kuchora yafaa nini, hata yeye aliyeifanya ameichora? Sanamu ya kuyeyuka, nayo ni mwalimu wa uongo, yafaa nini, HATA YEYE ALIYEIFANYA AIWEKEE TUMAINI LAKE, na kufanya sanamu zisizoweza kusema? OLE WAKE YEYE AUAMBIAYE MTI, Amka; aliambiaye jiwe lisiloweza kusema, Ondoka! Je! Kitu hicho kitafundisha? Tazama, kimefunikwa kwa dhahabu na fedha, wala hamna pumzi ndani yake kabisa. Lakini BWANA yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake."
KUMBUKUMBU 16:21-22:" Usipande MTI UWAO WOWOTE KUWA ASHERA(mungu) kwako kando ya madhabahu utakayofanya ya BWANA, Mungu wako. Wala usisimamishe nguzo; ambayo BWANA, Mungu wako, aichukia."
Soma pia [KUTOKA 20:3; ISAYA 44:14-19; ZABURI 52:7-8].
Ifahamike vizuri kuwa sisi wakristo tuliookoka tunapoitumia miti hiyo ya Krismasi hatuitumii kwa malengo yale kama walivyoitumia wao wapagani . Maana yetu ya kuitumia miti hiyo iko tofauti kabisa na jinsi ilivyokuwa ikitumika kwa wapagani. Sisi hatuitukuzi wala kuiabudu miti hiyo, wala tumaini la imani yetu haiko juu ya mti bali kwa BWANA.
2? KIPENGELE CHA PILI
KWANINI WAKRISTO TUNATUMIA MTI WA KRISMAS?
Ni kwa mambo makuu mawili:-
(1) Sisi tunautumia mti huu KAMA PAMBO TU la sherehe. Na hata ukiingia makanisani wakati wa majira haya ya Christmas, miti hii hupamba kwenye madhabahu, malangoni n.k. nyumbani mwa Mungu wetu.
Na jambo hili la KUPAMBA KWA MITI liko ki-biblia pia . Tazama neno la Mungu linavyosema:-
ISAYA 60:13:-" Utukufu wa Lebanoni utakujia wewe, (miti ya) mberoshi na mtidhari na mteashuri pamoja; ILI KUPAPAMBA MAHALI PANGU PATAKATIFU, Nami nitapatukuza mahali pa miguu yangu.".
Ndani pia ya hekalu la sulemani alilomjengea Mungu kulikuwamo na miti fulani ya mapambo katika kupapendezesha mahali patakatifu
[2NYAKATI 3:5-6; 1WAFALME 6:14-18].
Na si hilo tu. Kuhusu hoja ya kuitumia miti nyakati za sikukuu. Bado hata hapo ni jambo linaloungwa mkono ki-biblia. Sio kosa wala sio upagani. Tazama neno la Mungu linachosema kwa mfano katika
MAMBO YA WALAWI 23:39-41:-" Lakini siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, hapo mtakapokuwa mmekwisha kuyachuma mavuno ya nchi, mtaweka sikukuu ya BWANA muda wa siku saba; siku ya kwanza kutakuwa na kustarehe kabisa, na siku ya nane kutakuwa na kustarehe kabisa. Nanyi siku ya kwanza mtajipatia matunda ya MITI MIZURI, na MAKUTI YA MITENDE, na MATAWI YA MITI MINENE, na mierebi ya vijitoni; nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, muda wa siku saba. Nanyi mtaishika kuwa sikukuu kwa BWANA muda wa siku saba katika mwaka; ni amri ya milele katika vizazi vyenu; mtaishika katika mwezi wa saba."
Kwahiyo watu wanaotaka kujua uhalali wetu ki-biblia wa kutumia miti nyakati hizi za sikukuu, andiko hilo hapo. Kama watatuita sisi wakristo kwa kutumia miti hiyo eti ni upagani. Hao ni wapumbafu wa kawaida! Hawaijui Biblia kwamba Mungu ndio mwanzilishi wa elekezo la kutumia mti wakati wa sikukuu kwa msingi huo huo pia.
(2) NI ISHARA YA MTI WA UZIMA KUPITIA KWA YESU KRISTO MWOKOZI
Kwanini mti wa Christmas unahusishwa na tendo la kuzaliwa kwa Yesu? Hili ni tendo hasa la ufunuo wa rohoni zaidi. Lakini mtu ukiwa mwilini huwezi elewa lolote.
Iko hivi! Baada ya mwanadamu kuanguka dhambini katika bustani ya Edeni . Alihukumiwa adhabu ya kifo. Na baada ya hapo Mungu alimfukuza kutoka katika bustani ya Edeni. Na hakuweza kuruhusiwa tena kula matunda ya mti wa uzima, Mungu alisema wakila hawa wataishi milele. Biblia inasema Mungu akailinda NJIA YA MTI WA UZIMA, ili mwanadamu asije akausogelea [ MWANZO 3:22-24].
Dhambi ndiyo iliyotutenganisha na mti wa uzima na kufanya tufe milele. Tulipotea kutoka kwenye njia ya mti wa uzima.
Sasa ni muhimu kuelewa Yesu Kristo alizaliwa ulimwenguni ili awaokoe wenye dhambi. Tena Alikuja kutufuta na kuokoa kile kilichopotea njia [MATHAYO 1:21; LUKA 19:9-10].
Sasa Yesu Kristo alipozaliwa ulimwenguni, yeye ndiye aliyekuwa ni njia ya huo mti wa uzima [ YOHANA 14:6; MITHALI 3:18].
Ndiomaana Mti wa Krismas mara nyingi utakuta umepambwa kwa namna fulani ya mfano wa matunda na nyota/taa zenye mwanga. Nyota/taa juu ya mti huo vinamwakilisha Yesu Kristo mwenyewe [MATHAYO 2:1-11; UFUNUO 22:16; YOHANA 8:12]. Kumbuka Yesu Kristo yeye ndiye njia. Sasa mti huo kupambwa kwa nyota/taa, maana yake inamainisha kuwa Yesu Kristo yeye ndiye njia ya huo mti wa uzima.
Sasa kwa ujumla wake MTI HUO WA KRISMAS unatufundisha mambo makuu mawili kwamba:-
(i) Yesu Kristo amekuja kuturudisha kwenye mti wa uzima
(ii) Na sisi tulio ndani ya Yesu yaani tuliookoka, ndio wenye kibali cha kuishi milele kwa kula matunda ya mti ule wa uzima. Haleluya!
UFUNUO 22:1-5, 14:-".........Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake"
UFUNUO 2:7:-" Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, NITAMPA KULA MATUNDA YA MTI WA UZIMA, ulio katika bustani ya Mungu ". Haleluya!
Ndiyo maana mti wa krismas umekuwa ni alama/nembo muhimu kote duniani katika kuitambulisha Krismas. Hii ndiyo maana ya mti huu na makusudi ya sisi wakristo kuuendelea kuutumia mti huo katika makanisa yetu, majumbani mwetu nakadhalika katika majira haya ya sikukuu.
MUNGU AKUBARIKI.
Sehemu ya pili itaendeleaa...........!
????????????????????
Ukipenda kuwasiliana nami kwa ushauri , maombezi na mafundisho zaidi ya masomo ya neno la Mungu. Karibu :-
Mtumishi wa Mungu aliye hai.
MWL, REV:-ODRICK BRYSON
SIMU:- 0759 386 988; 0717 591 466
Email:- Odrick16@gmail.com.
Whatsapp group.
"KWELI YOTE YA NENO LA MUNGU ISIYOGOSHIWA"
[ 2 WAKORINTO 2:17 ]

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW