Friday, December 7, 2018

KANISA SIO JENGO
KANISA SIO JENGO
Watu wengi siku hizi wanaelewa Kanisa kumaanisha jengo. Huku si kuelewa kibibilia maana ya Kanisa. Neno “Kanisa” maana ya asili yatoka kwa neno la Kiyunani ekklesia lililo na maana ya “kusanyiko” au “walioitwa.” Maana ya asili ya “Kanisa” sio ile ya jengo, bali ni watu. Unapowauliza watu ni kanisa gani wanashiriki, mara nyingi huwa wanajihushisha na jengo. Warumi 6:5, yasema, “…salimia kanisa linalokutana kwa nyumba.” Paulo anaashiria kanisa lilo katika nyumba yao- si jengo la Kanisa bali mwili wa washiriki.
KANISA NI MWILI WA KRISTO
Kanisa ni Mwili wa Kristo, ambapo Yesu ndie kichwa. Waefeso 1:22-23 yasema, “Akivitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.” Mwili wa Kristo umejengwa na wanaoamini katika Yesu Kristo toka siku ya Pentekosti (Matendo Ya Mitume 2) hadi Kristo arudi. Mwili wa Kristo uko na sehemu mbili:
1) Kanisa lote kwa ujumula ambalo ni wale wote wako na uhusiano na Kristo. “Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni Upendo” (1 Wakorintho 12:13). Aya hii inasema yeyote atakaye amini in sehemu ya mwili wa Kristo na ameupokea Roho wa Kristo ni ushaidi. Kanisa la jumla la Mungu ni wale wote ambao wamepokea wokovu kwa imani katika Yesu
2) Lile Kanisa ya nyumbani vile imeelezwa katika Wagalatia 1:1-2: “Paulo, mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu), na ndugu wote walio pamoja name, kwa makanisa ya Galatia.” Hapa tunaona kwamba katika mkoa (mji) wa Galatia kulikuwa na makanisa mengi chenye tunaita makanisa ya nyumbani. Kanisa la Kibaptisiti, Kilutheri, Katholiki na mengine, si kanisa, vile iilvyo katika kanisa la ujumla, bali haya ni makanisa ya nyumbani (Mshambani/Mjini), ule mwili wa nyumbania wa waumini. Kanisa la jumla linajumlisha wale wote ni wa Kristo na wamemwamini kwa wokovu. Washirika wa kanisa la jumla lazima watafute kuwa na ushirika na kujengana wakiwa katika lile kanisa la nyumbani.
Kwa ufupi, Kanisa si jengo ama dini. Kulingana na Bibilia, kanisa ni mwili wa Krsito-wale wote wameweka imani yao kwa Yesu Kristo kwa wokovu (Yohana 3:16; 1 Wakorintho 12:13). Kanisa la nyumbani ni kusanyiko la Wakristo wa kanisa la jumla. Kanisa la nyumbani ni mahali ambapo washirika wa kanisa la jumla wanaweza kutumia nguzo ya “mwili” ya 1 Wakorintho 12: himizana, funzaneni, na kujengana ninyi kwa ninyi katika hekima na neema ya Bwana Yesu Kristo.
Barikiwa sana na Yesu, Mungu Mkuu

No comments:

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW