Friday, February 26, 2016

MASHAHIDI WA YEHOVA WANAFUNDISHA KUWA HAKUNA JEHANNAM

(i) Wanafundisha kuwa, kifo ndio mwisho wa maisha yako
(ii) Wanafundisha kuwa, hakuna Jehannam.
Ndugu msomaji,
Mashahidi wandai kwamba hakuna Jehannam. Wanasema mwovu anapokufa, basi anapotea moja kwa moja tu! Wanadondoa Mhubiri 3:20-21; 12:7.
Je, haya madai ya Mashahid wa Yehova ni ya kweli?
Je, ni kweli kuwa hakuna maisha baada ya kifo, yaani wewe ukifa ndio unapotea moja kwa moja?
Biblia Yasema Nini kuhusu jambo hili?
1. Ni kweli mwili wa mtu hurudi mavumbini anapokufa, Mwanzo 3:19. Lakini mwanadamu si mtu tu -MWILI NA NYAMA PEKEE!
Mwanadamu ni nafsi ya roho pia, maana tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, (Mwanzo 1:26) naye Mungu hana mwili bali ni roho (Yohana 4:24; Luka 24:39). Miili ya wanadamu wote itarudi mavumbini hata wakiwa wema au waovu. Lakini roho za mwanadamu ndizo zitakazoishi milele ama pamoja na Mungu ama katika Jehannam.
WEWE NI MFANO WA MUNGU
Mwanzo 1: 26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
MUNGU NI ROHO, KUMBE BASI WEWE NI ROHO!
Yohana 4: 24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Kumbebasi wewe ni roho na sio mwili na nyama.
2. Kifo Cha Roho-Kifo maana yake ni utengano. Ukitenga roho na mwili basi mwili umekufa, Yakobo 2:26. INASEMA: Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.
Vivyo hivyo, ukitenga roho na Mungu aliye uhai wetu, basi roho nayo imekufa. (Mungu hakumwambia Adamu uongo aliposema “Siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika” Mwanzo 2:17. Adamu hakufa kimwili siku ile bali alikufa kiroho maana alitengwa na Mungu, na kufukuzwa katika bustani.
Kifo cha roho hakina maana kwamba roho haitakuwapo tena. Roho ni ya milele. Roho ya mwovu inapotengwa na Mungu, basi tunaweza kusema imekufa hata ingawa ili roho bado ipo, 1 Timotheo 5:6 6 Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai.
Waefeso 2:5; Warumi 8:10. Walakini, mtu akifa katika dhambi zake, basi roho ya mwovu yule itakuwa katika hali ya mateso daima mbali na Mungu, 2 Thesalonike1:7-9; Mathayo 25:41-46. Hii ndiyo inayoitwa MAUTI YA PILI na ndiyo kifo cha kiroho, Ufunuo 21:8; 20:14-15.
3. Ikiwa hakuna mahali pa mateso panapoitwa Jehannam, mbona Yesu hakujua? Maana Yesu ametuonya mara nyingi kuhusu Jehannam, Mathayo 10:28; Luka 12:5; Mathayo 5: 22, 29-30; 23:33.
Yohana 10: 28 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.
4. Mhubiri 3:20-21; 12:7 haisema kwamba hakuna Jehanum. Mistari hii inaonyesha kwamba mwili unarudi mavumbini mtu anapokufa. Lakini, miili yetu haitakaa mavumbini daima. La! bali Yesu atakapokuja, wafu wote watafufuliwa, Yohana 5:28-29; Ufunuo 20:12-15. Si vigumu kwa Mungu kufufua miili yetu kutoka
mavumbini, Ezekiel 37:1-13. Isitoshe, mara tutakapofufuliwa miili yetu itabadilishwa kama apendavyo Mungu maana nyama na damu haviwezi kuurithi ufalme wa Mungu, 1 Wakorintho. 15:50-54.
5. Mashahidi wanasema kwamba hakuna adhabu ya milele, Soma Daniel 12:2; Mt. 25:46; Yonana 5:28-29; Ufunuo 20:10.
JEHANNAM:
Jehanamu, kama vile mbinguni, si mahali patajwapo kwa utisho tu bali ni mahali dhahiri. Hapa ni mahali ambapo wasiohaki watakutana na ghadhabu isiyokoma ya Mungu. Watavumilia mateso ya kihisia, kiakili, na kimwili wakiwa katika akili zao timamu huku wakijihisi kuaibika na kujuta kwa matendo yao maovu.
Jehanamu inaelezewa kama shimo la giza (Luka 8:31, Ufunuo wa Yohana 9:1), na Ziwa la Moto, liwakalo na kiberiti ambapo watakao kuwemo watateswa usiku na mchana milele na milele (Ufunuo 20:10). Huko kutakuwa na kulia na kusaga meno, ikiashiria machungu makali na hasira (Mathayo 13:42). Hapa ni mahali ambapo mdudu hatakufa wala makaa kuzimika (Marko 9:48). Mungu hafurahishwi na kufa kwa mtu muovu, lakini hutaka wazighairi njia zao mbaya ili waishi (Ezekiel 33:11). Lakini hatatulazimisha kumkubali; tukiamua kumkataa yeye. Hana budi kutupatia tulilolichagua – kuishi mbali naye.
Je unaamini kuwa kunayo maisha baada ya kifo?
Ni nini hufanyika baada ya kufa?
Je, unaamini kuwa hakuna Jehannam kama Mashahid wa Yehova?
Je, unaamini kuwa ukisha kufa wewe ndio umeishia hapo/unapotea moja kwa moja kama ambavyo Mashahid wa Yehova wanavyo kiri?
Mungu awabariki sana,
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wake.
Max Shimba Ministries Org
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW