Friday, February 12, 2016

QURAN INASEMA NINI KUHUSU YESU?



A. YAKIRI KUWA YESU NI MUNGU
B. YAKIRI KUWA YESU HANA DHAMBI
C. YAKIRI KUWA YESU ATAHUKUMU ULIMWENGU
D. YAKIRI KUWA YESU NI NENO LA MUNGU
Yafuatayo ni maswali amabyo Waislam wengi wamekuwa wakijiuliza, hivi Yesu ni nani kwenye Quran yao?
1. Yesu ni binadamu pekee aliye zaliwa kupitia Bikira na bila ya Baba wa kidunia. Hii ni sifa ya kipee ambayo hakuna Mtume au Nabii aliye nayo. 21. (Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa. 22. Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali.
2. Masia Yesu ni tofauti na binadamu wote kwasababu yeye anaitwa “Kalimatullah” (NENO LA ALLAH)
Masia, Isa mtoto wa Maryam, Nabii wa Allah na Neno lake” (Sura The Women 171; Sura al Imran 40).
3. Isa alizaliwa kutokana na Roho ya Allah; kwa sababu hii, hakuhitaji Baba wa kidunia.
Masia, Isa Mwana wa Maryam, Nabii wa Allah na Neno Lake ni Roho kutoka kwa Mungu..
(Sura The Women 169).
4. Isa ni motto pekee aliye weza kusema akiwa mchanga Only Isa spoke while in the cradle
30. (Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii.
(Sura Miriam 19:30)
Zaidi ya hapo, Isa hakuitaji mtu yeyote yule kumfudisha kusoma wala kuandika.
13Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya BWANA, au kumfundisha kama mshauri wake? 14Ni nani ambaye BWANA ametaka shauri kwake ili kumwelimisha, naye ni nani aliyemfundisha njia iliyo sawa? Ni nani aliyemfundisha maarifa au kumwonyesha mapito ya ufahamu?
(Isaiah 40:1,13-14)
5. Isa alikuwa ni Nabii thabiti na hakuwa na dhambi au kosa lolote lile. Mitume wote walitenda dhambi, na dhambi zao zimesemwa kwenye Quran na Taurat. Isa hakuwa na dhambi.
45. Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu). (Sura al Imran 45)
Vivle vile Al-Bukhari amefundisha kuwa Isa bin Maryam alikuwa ni mtu dhabiti na asiye an dhambi:
Shetani aligusa kila kiumbe wakati wa kuzaliwa kwake, ISIPOKUWA Yesu, Mtoto wa Maryam; Shetani alipo jaribu kumgusa alishindwa (Hadith of Sahih Bukhari Vol 4, Book 54)
6. Yesu hakuwa kama watu wengine, kwasababu Yesu aliweza kuumba Uhai kama Allah
49. Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia: Mimi nimekujieni na Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu, ya kwamba nakuundieni kwa udongo kama sura ya ndege. Kisha nampuliza anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ninakwambieni mnacho kila na mnacho weka akiba katika nyumba zenu. Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwi nyinyi ni wenye kuamini.
(Sura al Imran 49)
7. Isa ni nabii pekee aliye weza kujua siri iliyo ndani ya nyoyo za watu.
49. Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia: Mimi nimekujieni na Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu, ya kwamba nakuundieni kwa udongo kama sura ya ndege. Kisha nampuliza anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ninakwambieni mnacho kila na mnacho weka akiba katika nyumba zenu. Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwi nyinyi ni wenye kuamini.
. (Sura Al Imran 48)
8. Isa alifanya miujiza mikubwa mikubwa zaidi ya binadamu wote
Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma …
(Sura Al Imran 48)
9. Isa alifufua watu kwa kutumia NENO
na ninawafufua maiti …
(Sura al Imran 48 & Sura The Table 110)
10. Isa ndie binadamu pekee aliye itwa Masiha “the Masih”
Masia, Isa Mwana wa Maryam, alikuwa Nabii wa Allah na Neno Litokalo kwake …
(Sura The Women 169)
Katika Taurat tunajifunza kuhusu asili hasili ya Masia:
5BWANA asema, “siku zinakuja, nitakapomwinulia Daudi Tawi lenye haki, Mfalme atakayetawala kwa hekima na kutenda lililo haki na sawa katika nchi. 6Katika siku zake, Yuda ataokolewa na Israeli ataishi salama. Hili ndilo jina atakaloitwa kwalo: BWANA Haki Yetu..
(Jeremiah 23:5-6)
11. Isa aligawana Mamlaka na Mungu
117. Sikuwaambia lolote ila uliyo niamrisha, nayo ni: Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Na mimi nilikuwa shahidi juu yao nilipo kuwa nao. Na ulipo nifisha ukawa Wewe ndiye Muangalizi juu yao. Na Wewe ni shahidi juu ya kila kitu
(Sura The Table 117)
12. Isa alikuwa ni Ishara ya Baraka kutoka kwa Allah
(Sura Miriam 20)
13. Isa alitoka ahadi ya maisha wakati wa siku ya ufufuo.
55. Pale Mwenyezi Mungu alipo sema: Ewe Isa! Mimi nitakufisha, na nitakunyanyua kwangu, na nitakutakasa na wale walio kufuru, na nitawaweka wale walio kufuata juu ya wale walio kufuru, mpaka Siku ya Kiyama. Kisha marejeo yenu yatakuwa kwangu, nikuhukumuni katika yale mliyo kuwa mkikhitalifiana
(Sura al Imran 55)
14. Isa atatoa hukumu kwa viumbe vyote;
El-Bukhari anasema kuwa:
Katika saa ya Mwisho, Isa Mwana wa Maryam atarudi na kuhukumu ulimwengu.
Leo nimekuonyesha kwa ushahid wa Quran na vitabu vya kiislam kuwa, hata Isa wao alifanya miujiza zaidi ya Allah na Mtume wake Muhammad.
Max Shimba Minsitries.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW