Friday, March 3, 2017

YESU NI MUNGU PAMOJA NASI

Image may contain: ocean, text and water
YESU ALIPOKUWA DUNIANI ALIKUWA EMANUELI (MUNGU PAMOJA NA WANADAMU).
Mathayo 1:23-25 “Tazama; bikra atachukua mimba; naye atazaa mwana;nao watamwita jina lake Emanueli; yaani ,Mungu pamoja nasi”.Tabia ya Yesu inaonyesha kuwa kama mwanadamu,kuzaliwa kwake kwa uwezo wa Roho mtakatifu.Hapa tunaona jinsi alivyo na uwezo wa tofauti na wanadamu akiwa anafahamu mambo yote kabla akiwa duniani..Yeye pia ajua yote yaliyomo ndani ya moyo wa mwanadamu (Yohana 6:64,Yohana 13:1,Yohana 13:11,Yohana 18:4,Yohana 19:28).
Tena Yesu alitabiri kabla jambo kutokea,pia alijitabiria mwenyewe yatakayomtokea mbele (Marko 8:31,Luka 9:22, Luka 12:50, Luka 22:37, Luka 24:7-26, Yohana 3:14,Yohana 10:17-18,Yohana 7:33, Yohana 13:33, Yohana 14:28, Yohana 17:11, Yohana 16:5,10,16,18 ).
Yesu aliabudiwa na kusujudiwa akiwa hapa duniani,Sifa ya kuabudiwa na kusujudiwa ni ya Mungu pekee hivyo Yesu ni Mungu.(athayo 4:10).
Hata malaika wote wanamsujudia Yesu (Ufunuo 22:8-9, Waebrania 1;6).
Ndiyo maana Yesu alisujudiwa akiwa mtoto mchanga alipozaliwa (Mathayo 2:11, Mathayo 14:33< Luka 24;52).
Hata pepo wachafu walimsujudia Yesu (Marko 5:2,6).
YESU NI MUNGU.
Shalaom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW