Friday, February 5, 2016

MAOMBI YA KUSAMBARATISHA UCHAWI NA NGUVU ZA GIZA

Baba katika Jina la Yesu.
Laana zote nilizo tupiwa na wabaya wangu zimeshindwa kwa jina la Yesu na nazivunja na kuzisambaratisha kwa Damu ya Yesu.
Mshindwe wote mnao tuma laana kwangu katika Jina la La Yesu.
Nawavunja na kuwaharibu na kuwakatakata Wachawi wote kwa damu ya Yesu.
Nasambaratisha kila neno la uovu lililosemwa juu yangu na famila yangu katika jina la Yesu.
Naharibu na kuisambaratisha madhabahu yenu mliyo fanyia kafara kwa damu ya Yesu.
Navunjavunja na kubomoa kila uovu na uchawi mnaonifanyia katika jina la Yesu.
Nairudisha misukule yote na majini yote yawarudie nyie na kuwalipa dhambi zote mnazo fanya katika jina la Yesu.
Naharibu kila uchawi, kila urogi, kila ndumba kila aina ya uovu ambao mnaufanya ili uniumize mimi na familia yangu katika jina la Yesu.
Nawateketeza kupitia damu ya Yesu Wachawi wote walio tumiwa kunitumia uchawi katika jina la Yesu.
Nawateketeza na kuwaharibu majini yote yaliyo tumwa kuja kufanya kazi hiyo waliyo tumwa na Wachawi katika jina la Yesu.
Nawateketeza na kuwauwa Makuhani wote ambao walienda kunishitaki kwa Wachawi ili waniharibie maisha, nawateketeza kupitia damu ya Yesu. Nawachoma kwa Moto wa Roho Mtakatifu katika Jina la Yesu.
Nateketeza aina zote za vyombo vya kichawi vilivyo tumiwa kuja kunichunguza katika jina la Yesu.
Naharibu fikra zao zote ambazo wanazitumia kufanya kazi zao za kichawi katika jina la Yesu.
Nafuta kumbukumbu zoote zangu ambazo wamewapa Mashetani, Majini, Roho chafu, nafuta hizo kumbukumbu kwa kutumia damu ya Yesu, katika jina la Yesu aliye hai.
Nawateketeza waweka kumbukumbu wa kimashetani kupitia damu ya Yesu aliye hai. Naharaibu na kuchoma kupitia moto wa Roho Mtakatifu makabrasha yote yenye kumbukumbu zangu katika jina la Yesu.
Kila uchawi ulio fanywa ili uje kuharibu maisha yangu na ubomoa kupitia damu ya Yesu.
Kila uchawi ulio fanywa ili uje kuniua nauvunja na kuuteketeza kupitia damu ya Yesu.
Kila uchawi ulio fanywa ili kuja kuiba mali zangu, nauvunja na kuubomoa na kuuharibu kupitia damu ya Yesu.
Kila uchawi ulio fanya kuja kuniharibia familia yangu, nausambaratisha na kuuvunja na kuubomoa katika jina la Yesu.
Kila neno la kichawi lililo tumwa ili kuja kuniharibia, kunidhihaki, kunitendea mabaya nalirudisha kwa aliye lituma katika jina la Yesu.
Kila uovu, uchawi, wanga, ndumba, ramli, yaliyo tumwa kuja kwangu navunja yote hayo kupitia damu ya Yesu na katika Jina la Yesu.
Nyota yangu ambayo wanaita nairudisha kupitia damu ya Yesu. Nyota yangu ya baraka nailinda na kuzungushia na kuizingira na damu ya Mwana Kondoo katika jina la Yesu.
Namteketeza yule mtu aliye kuja kuiba nyota yangu katika jina la Yesu.
Nateketeza mbinu zote wanazo tumia ili kuja kuiba nyota yangu katika jina la Yesu.
Nateketeza wivu wao, chuki yao, laana zao, maovu yao na kila aina ya uchafu ambao wanao kwa ajili yangu katika jina la Yesu.
Naizungushia na kuizingira nyumba yangu na damu ya Yesu.
Naishungushia na kuizingira familia yangu na damu ya Yesu.
Nashungushia na kuzingira maisha yangu yote na damu ya Yesu.
Navunja laana zote zilizo semwa na mabau zangu katika jina la Yesu.
Navunja laana zato ambazo zilisemwa bila ya mimi kufahamu, nazivunja na kuziharibu kupitia damu ya Yesu na katika jina la Yesu.
Narudisha kila mali walizo ziiba kutoka kwangu katika jina la Yesu.
Narudisha kila baraka walizo ziiba kwangu katika jina la Yesu.
Narudisha amani na upendo katika familia yangu.
Damu ya Yesu ipo juu ya Maisha yangu na inasafisha kila uovu, kila uchawi unaaribiwa na damu ya Yesu katika jina la Yesu.
Leo hii mtaiona Nguvu iliyopo katika damu ya Yesu.
Katika Jina la Yesu aliye hai ninaomba.
Amen
Max Shimba Ministries
03/01/2014

Kwanini Mkristo anauhakika wa kwenda Paradiso zaidi ya Muislamu?

1. Je, Kurani inatoa uhakika kwa Waislamu?
Kurani inatengeneza tu mazingira ya mashaka kuhusiana na kuingia Paradiso au hapana. Muislamu hanauhakika wa kuiepuka jehanamu ya moto:
“Hao wanao waomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi - hata miongoni mwao walio karibu mno - na wanataraji rehema zake na wanaikhofu adhabu yake. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaa kutahadhari nayo” (Kurani 17:57).
Waislamu hufikiria kwamba hawawezi kuwa na uhakika kuhusiana na kwenda Paradiso, kwa sababu Kurani inasema Mola huamua na mwanadamu hawezi kujua kwamba ameokoka:
"Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza. Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya! Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo? Ni Moto mkali!" (Kurani 101:6-11).
Muislamu hana uhakika ni upande gani anaohusika nao. Mola alimuumba mwanadamu kufanya wema au uovu:
"Hujui ya kwamba Mwenyezi Mungu anao ufalme wa mbingu na ardhi? Humuadhibu amtakaye, na humsamehe amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu." (Kurani 5:40).
Muislamu hajui ni nani atakuwa pamoja na Mola Paradiso. Kwa hiyo Kurani haiwezi kutoa uhakika kwa Muislamu kuhusiana na kwenda Paradiso.
2. Je, Muhammad anatoa uhakika kwa Waislamu?Kurani iko wazi kwamba Muhammad hawezi kumsaidia Muislamu kuingia Paradiso:
"Wala nasaha yangu haikufaini kitu nikitaka kukunasihini, ikiwa Mwenyezi Mungu anataka kukuachieni mpotee. Yeye ndiye Mola wenu Mlezi; na kwake mtarejeshwa" (Kurani 11:34).
"Hata ukiwa na pupa ya kutaka kuwaongoa, lakini Mwenyezi Mungu hamwongoi yule anaye shikilia kupotea. Wala hawatapata wa kuwanusuru" (Kurani 16:37).
"Sema: Uombezi wote uko kwa Mwenyezi Mungu. Ni wake Yeye tu ufalme wa mbingu na ardhi. Kisha mtarejeshwa kwake." (Kurani 39:44).
Kwa hiyo Kurani inakataa kwamba Muhammad aweza kuwa muwezeshaji kwa Muislamu kuingia Paradiso. Angalia pia Kurani 7:188, 4:123 na 9:80. Hivyo ni nini faida yake, ikiwa kila mwanadamu atateseka jehanamu, kabla ya wenye haki kuchaguliwa kutoka hao waendao jehanamu?
Je ni nini basi kwa habari ya Muhammad kuwa mfano kwa Waislamu kuingia Paradiso? Pia hili nalo halina mbadala kwa Muislamu, kwa sababu Muhammad aliona shaka kuhusu kuingia Paradiso:
“Sema: Mimi si kiroja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyo fanywa wala nyinyi. Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi." (Kurani 46:9).
Pia nyaraka zingine katika uislamu zinasema kwamba Muhammad hakuwa na uhakika wa kwenda Paradiso [1].
3. Are Christians sure about going to Paradise?Wakati Waislamu wanajaribu kutii sheria za Mola, wanabaki kutokuwa na uhakika wa wokovu, Mkristo anauhakika wa kwenda Paradiso. Mkristo atamjibu Muislamu juu ya swali “Bwana zangu, nifanye nini ili nipate kuokoka?” kwa [2]:
“Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka” (Matendo ya Mitume 16:31).
Ni lazima Muislamu afahamu kuokoka kwa upendo na neema ya Mungu. Uislamu hauna Mwokozi. Mwamini ndani ya Mwokozi Mkuu Yesu Kristo wakati wote anakuwa na uhakika wa kwenda Paradiso. Wokovu wa pekee kwa mwanadamu umetolewa kupitia Yesu Kristo, Neno la Mungu. Kwa sadaka ya mwenye haki Yesu Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi, mwamini ana uhakika wa kuingia Paradiso. Kuna mistari kadhaa kwenye Maandiko Matakatifu yanayothibitisha kuingia Paradiso kwa waaminikwenye utukufu wa Yesu Kristo:
“Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye Mimi hata akifa atakuwa anaishi” (Yohana 11:25).
"Nyumbani mwa Baba yangu kuna makao mengi. Kama sivyo, ningeliwaambia. Nakwenda kuwaandalia makao. Nami nikienda na kuwaandalia makao, nitarudi tena na kuwachukua mkae pamoja nami, ili mahali nilipo, nanyi mpate kuwepo. Ninyi mnajua njia ya kufika ninakokwenda.Thomasi akamwambia, “Bwana, sisi hatujui unakokwenda, tutaijuaje njia?" Yesu akawaambia, “Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kwa kupitia Kwangu" (Yohana 14:2-6).
4. HitimishoMkristo ana uhakika wa kwenda Paradiso. Muislamu huishi na kufa, hana uhakika wa wokovu. Mkristo, kwa upande mwingine, amemkubali Yesu Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi zake na ana uhakika. Hii ni habari njema kuhusu upendo na neema ya Mungu ni kitu ambacho Mkristo anataka kuwashirikisha rafiki zake wailslamu.
Rejea:
1. Sahih al-Bukhari, Volume 4, Book 51 and Volume 5, Book 58, Number 266.
2. E.M. Hicham, How Shall They Hear? Sharing your Christian faith with Muslims, Ambassador Publications, Belfast, 2009, 88.

SIFA SABA ZA ROHO MTAKATIFU

Yohana 14: 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele. 17Huyo ndiye Roho wa kweli ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi naye anakaa ndani yenu.

Yesu Kristo ametupa zawadi ya ajabu sana: Zawadi ya Roho Mtakatifu. Katika baadhi ya maeneo, zawadi hiyo inajulikana kama Roho Mtakatifu, na sehemu nyingine ametajwa kama Msaidizi (Msaidizi na Roho Mtakatifu). Roho Mtakatifu ni sehemu ya tatu ya Uungu, sehemu ya tatu ya Utatu wa Mungu Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Yeye ni Msaidizi katumwa na Yesu, baada ya Msaidizi wetu kuja ambaye ni Roho Mtakatifu, Yesu alipaa tena mbinguni. Roho Mtakatifu hutolewa kwa wote ambao wamempokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wao

Kuna mambo saba ambayo tunahitaji kuelewa kuhusu Roho Mtakatifu. Tunajua kwamba, katika Biblia, saba ni namba ya kukamilika/ kukamilisha, au ukamilifu, na sifa saba zote tofauti za Roho Mtakatifu ni kweli kamili na kamilifu. Tunaweza kuzitegemea sifa hizi za ajabu za Roho Mtakatifu, wakati wote, katika kila hali na katika maisha yetu yote.

1. Roho Mtakatifu ni Msaidizi Mwenye Upendo. Tunapokabiliana na mateso katika maisha, mwongozo wa Roho Mtakatifu ni muhimu zaidi na ni faraja katika mioyo yetu: Roho Mtakatifu ni mtu ambaye ana upendo kwetu na anajua kila kitu kuhusu maisha yetu. Roho Mtakatifu alitupenda tangu kabla ya kuumbwa ulimwengu. Yeye alivyotupenda vizuri. Yeye anatupenda milele na anaendelea kutupenda milele yote. Roho Mtakatifu tu ndie mwenye uwezo wa kweli wa kutufariji mioyo yetu, kwa sababu hakuna mtu anaye tupenda sisi kama anavyotupenda Yeye Roho Mtakatifu.
Warumi 5: 5 wala tumaini halitukatishi tamaa, kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo Lake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ametupatia.

2. Yeye (Roho Mtakatifu) ni Msaidizi Mwaminifu. 

ROHO MTAKATIFU NI MUNGU

Ndugu msomaji,
Watu wengi hawafahamu kuhusu Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu Ni Nani?
Baadhi ya watu wanadhani Roho Mtakatifu ni aina fulani ya nishati, uweza au radi. Lakini wanakosea.
Roho Mtakatifu Ni Mtu-Person, "SIO BINADAMU", nikimmanisha kuwa sio Mtu kwa maantiki ya Binadamu.
Na kwa kweli ni ‘mtu’ muhimu sana; ni Nafsi ya Tatu katika Utatu wa Mungu (Mt 28:19) (2Kor 13:13). Yeye ni mtu roho, kama vile wewe ulivyo ila Yeye hafungwi na mwili. Twaweza kumwomba kila siku tukisema, ‘Roho Mtakatifu, nijaze kwa uweza wako, niongoze, nipe hekima na ujasiri’ kwa sababu ni mtu kweli tunayeweza kuzungumza naye na kujihusisha naye.
Wengine wanasema kuwa ni Nguvu Fulani ya Mungu. Wengine wanasema ni Malaika Jibril. Lakini, Biblia inatumabia nini kuhusu Roho Mtakatifu?
Hebu ungana nami moja kwa moja na tujifunze kwa pamoja kwa kutumia aya za Biblia kuhusu Roho Mtakatifu. Kwa kifupi, ROHO MTAKATIFU ni Mungu.
Swala la kuwa Roho mtakatifu ni Mungu limo ndani ya aya nyingi za biblia kama vile Matendo 5:3-4. Katika ayah ii Petro anapambana na anania aliyemdanganya Roho mtakatifu na nasisitiza yakuwa “hukumdanya mtu bali Mungu.” Hili ni tangazo la wazi kwamba kumdanganya Roho mtakatifu ni kumdanganya Mungu. Tunaweza pia kujua Roho mtakatifu ni Mungu kwa kuwa ana tajwa na hali sawa na za Mungu. Roho mtakatifu yuko kila mahali katika Zaburi 139:7-8, “nitaenda wapi nijifiche na Roho? ama nitakimbilia wapi mbali na uwepo wako? Nikipanda juu mbinguni, huko uko; nikifanya malazi yangu kuzimu, tazama uko huko,” tena katika wakorintho wa Kwanza 2:10 tunaona hali yakuwepo kila mahali kwa Roho mtakatifu “Lakini Mungu ameyajulisha kwetu kupitia Roho wake mtakatifu. Kwa kuwa Roho huyachunguza mambo yote, naam, mambo ya siri ya Mungu. Kwa maana ni nani ayajuaye ya mwanadamu isipokuwa roho ya mwanadamu inayokaa ndani yake? Vivyo hivyo, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.”
Tunaweza kujua kweli kwamba Roho mtakatifu ni Mungu kwa kuwa ana akili, hisia na mapenzi yake. Roho mtakatifu hufikiri na hujua (Wakorintho wa kwanza 2:10). Roho mtakatifu anaweza kuugua (Waefeso 4:30). Roho hutuombea (Warumi 8:26-27). Roho mtakatifu hufanya maamuzi kutokana na mapenzi yake mwenyewe (Wakorintho wa kwanza 12:7-11). Roho mtakatifu ni Mungu, sehemu ya tatu ya utatu wa Mungu. Kama Mungu, Roho mtakatifu anaweza kufanya kazi ya msaidizi na mshauri kama vile Yesu kristo aliyevyoahidi kuwa atakuja kufanya (Yohana 14:16,26; 15:26).
Je, Roho Mtakatifu Ni Nafsi Halisi?
Madaktari husema kwamba nafsi halisi ni sharti iwe na akili, hiari, na hisia. Na Roho Mtakatifu tunampima kwa vigezo hivyohivyo vitatu.
Je, Roho Mtakatifu Ana Akili?
Akili ni uwezo wa kujifunza, kuelewa na kufikiri. Ndiyo, ana akili sana! (Rum 8:27) (1Kor 2:10-13).
Je, Roho Mtakatifu Ana Hiari?
Hiari inahusiana na kusudio, uchaguzi, takwa na azimio. Ndiyo, Roho Mtakatifu ana hiari yake mwenyewe na anakubaliana na Baba na Mwana (1Kor 12:11).
Je, Roho Mtakatifu Ana Hisia?
Je, ana hisia na hisia kali? Anapenda na hiyo ndiyo hisia yenye nguvu sana aliyonayo, na kuna hisia kali katika kuugua kwake awapo kwenye maombezi (Rum 15:30; 8:26,27).
Mungu awabariki sana,
Katika Huduma Yake,
Max Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

JE BIBLIA IMETIWA MIKONO (CHAKACHULIWA)?

Neno Biblia ni neno lenye asili ya Lugha ya kiyunani nao huita “Biblos” neno hili linapotamkwa humaanisha “Maktaba” au Mjumuiko, Mkusanyiko wa vitabu”.

Biblia ni kitabu kilicho andikwa na waandishi wasio pungua “arobaini”ambao walikuwa sehemu na mahala tofauti lakini kwa uongozi wa Roho Mtakatifu waliweza kuandika maneno yaliyowiana.

Matendo 11;19wanafunzi wa Yesu walitawanyika baada ya ile dhiki

1Petro 1:20 walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Isaya 34:16 tafuteni katika kitabu cha Bwana mkasome.

Pamoja na hayo siku hizi za karibuni kumeibuka vikundi mbalimbali vinavyoendesha mikutano,inayojulikana kwa jina la “mihadhara” vikundi hivyo vimeibua mafundisho yasiyo sahihi kwa kudai kuwa Biblia imetiwa mkono na si kitabu cha kweli, hivyo kupitia uchambuzi huu tutaangalia mada mbalimbali kwa kuanza na mada hii tete juu ya ukweli wa Biblia, ambapo vitabu vyote yaani Biblia na Qur an vitasaidia kutoa ufumbuzi.


VIGEZO VYAO VYA KUDAI KUWA BIBLIA SI YA KWELI
Yeremia 8:8-9 inasema kuwa “kalamu ya waandishi imeifanya kuwa uongo.”

Jibu kwa kifupi

Katika kujibu swali hili, ni muhimu kuanza kwa kuangalia makosa ya kiusomaji yaliyofanywa na wajenga hoja wa mada hii. Kwa kutolichunguza kwa makini andiko hilo ili kuelewa muktadha wake, hebu tuchunguze….!

Yeremia 8:8
Mwasemaje sisi tuna akili na torati ya Bwana tunayo pamoja nasi? Lakini tazama kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.

JIBU LA KWANZA
Katika aya hiyo, yako mambo ya kimsingi ambayo kamwe wajenga hoja hawayazingatii jambo la kwanza. Nabii Yeremia anasema “Torati ya Bwana tunayo pamoja nasi” hivyo kabla ya kujenga swali lolote ingepaswa kujulikana kwamba Torati haikuwa kwingine bali ilikuwa mikononi mwa manabii, hivyo ilikuwa salama.

JIBU LA PILI
Sehemu ya pili, ni pale andiko linaposema “lakini tazama” kauli hii uhashiria kuwepo kwa upande wa pili wa watu au kundi lililo anzisha jitihada nyingine pinzani mbali, pindi Torati ikiwa imehifadhiwa na manabii ambapo jitihada hizo zililenga kuikosoa Torati ambayo ilihifadhiwa na kutunzwa na manabii.

JIBU LA TATU
Na sehemu ya mwisho ni ile kauli inayosema kalamu ya uongo ya waandishi “imeifanya kuwa uongo” kauli hii kamwe hailengi kuonyesha kuwa kulifanyika tendo la kuivuruga au kuibadilisha torati yenyewe la hasha” hapo limetumika neno “imeifanya” kuwa uongo, hii inamaana kuwa torati yenyewe ni ya kweli lakini wao walianzisha jitihada zao za kuikosoa …….

MIFANO HAI
Chukulia mfano mtu akikwambia “wewe unanifanya mimi kuwa mjinga? Je- tayari umekuwa mjinga? Jibu – hapana”. Isipokuwa yeye anafanya mambo Fulani ili kufanya uonekane hivyo na hali sivyo ulivyo.

Je waandishi waliifanyaje Torati kuwa uongo na kwa namna gani?

Kwa kadri ya msingi wa maandiko ya Biblia tendo la kuifanya torati kuwa uongo huhashiria “kutamka” au “kuandika maneno yanayo pingana na torati ya Bwana”.

Biblia inaonyesha kuwa kulikuwa na watu waliojaribu kutunga na kuweka sheria zao zilionekana zikipingana na zile halali za Mungu Yehova, hivyo huko ndiko kuifanya torati au sheria halali ya Mungu kuwa uongo na si badala yake kuiharibu sheria yenyewe ya Mungu kwenye kitabu husika, fuatilia ushahidi ufuatao:-

Isaya 10:1 Ole wao wawekao amri zisizo haki na waandishi waandikaoManeno ya ushupavu ili kumpotosha mhitaji asipate haki yake………

Yohana 19:5 Wayahudi wakajibu sisi tunayo sheria na kwa sheria hiyo amestahili kufa kwakuwa alijifanya mwana wa Mungu.
Maandiko hayo yanonyesha vile ambavyo wanadamu nao walivyokuwa na jitihada za upande wao wa kuasisi sheria na taratibu zao ambazo kwa kadri ya maandiko zinaonekana kupingana na zile za halali za Mungu,hivyo hizo ndizo sheria “torati” za uongo.

Pia kama nilivyokwisha eleza kuwa kwa upande mwingine tendo hilo la Kalamu ya uongo ya waandishi kuifanya Torati kuwa uongo humaanisha kutamka au kufundisha yaliyo kinyume na Torati hiyo ya Bwana, lakini huenda hoja ikawa ni kuwepo kwa neno kalamu ya uongo ambalo hufanya kuwepo na maana moja tu ya kuandika, katika hili Biblia inaweka wazi kuwa hata mdomo huweza kuwa kalamu pia ”waswahili wanasema maneno uumba” unapoongea uongo ni sawa na kuandika uongo huo kwenye bongo za wengine. Hivyo maneno ni kalamu.


Tukio linganifu katika mafunuo ya Qur-an
Katika mafunuo ya Qur-an maelezo na picha hiyo ya kibiblia tuliokwishaiona huonekana pia, tatizo la kuibuka kwa makundi ya watu waliojaribu kugeuza au kuyafanya maneno ya Mungu au vitabu vilivyoaminiwa na jamii fulani kuwa uongo linaonekana kutawala katika pande zote za kidini. Hebu tupitie aya kadhaa za Qur an:-


KUMBE QURAN NI MKUSANYIKO WA UONGO
Qur –an 15:91 “Ambao wameifanya Qur an kuwa mkusanyiko wa uongo alioukusanya nabii Muhammad akadai kuwa ni maneno ya
Mwenyezi Mungu.”


KUMBE WATU WANAPINDA NDIMI KWENYE QURAN
Qur an 3:78 “ Kuna watu wanaopinda ndimi zao kwa kusoma vitabu ili tufikiri

kuwa maneno yao hayo ni ya kitabu cha Mwenyezi Mungu hali
hayakutoka kwa Mwenyezi Mungu nao wanamsingizia
Mwenyezi Mungu uongo mkubwa……”

Kwa ushahidi huo wa maandiko ya Qur an tunaweza kupata picha ya jumla juu ya hoja hii nyeti, maandiko hayo ya Qur an hususani ile aya ya kwanza yanaonyesha tukio linganifu na lile la Kibiblia, hapo pia inaonekana kuwepo kwa makundi ya watu fulani waliokosoa na kuibeza Qur an kuwa ni mkusanyiko wa uongo tendo linalolingana sawia na lile la Torati ya Bwana.
Qur an inasema kuwa watu hao waliifanya Qur an kuwa ni mkusanyiko wa uongo.


Hoja ya msingi:
Je’nisahihi kutumia ushahidi wa andiko kuthibitisha mapungufu ya Qur an?

Endapo jibu si sahihi vivyo hivyo hakuna usahihi wowote wa madai ya kupotoshwa kwa Biblia kwa kutumia maneno hayo ya Yeremia kuwa kalamu ya waandishi ‘imeifanya kuwa uongo’ maneno ambayo ndiyo yanayotumiwa na Qur an pia katika muktaza uleule, kimsingi maneno hayo yanaonyesha tu upidhani uliolikabili neno hilo la kweli toka wa waandishi na watunzi wa maneno na vitabu vya uongo na siyo kupotoshwa kwa neno lenyewe.


MASWALI:
Maswali ya kujibu Kwa wanaodai kupotoshwa Kwa Biblia
Nani alifanya upotoshaji huo?

Wapi na ni lini upotoshaji huo ulifanywa?

Yako wapi magombo ya asili ambayo hayakupotoshwa ili kusaidia kujua maeneo ya vifungu vilivyopotoshwa?

Kulikuwa na sababu zipi zilizofanya Mungu anyamaze na kutolinda mafunuo yake ya wokovu kwa wanadamu wake?

Je nini ukweli na maana ya Mungu kutoa maelekezo yanayoonyesha uhakika na kutokuwepo uwezekano wa
kubadilishwa kwa mafunuo yake matakatifu?


Fuatilia Aya zifuatazo kuona uhakika wa Biblia:-
Mathayo 5:18 “yodi wala nukta ya torati haitaondoka…………..
Zaburi 15:4 “ameapa hayabadili maneno yake……………..
Qur-an Surat Ban Israel17:77 Ndiyo desturi ya wale tuliowatuma (tuliowapa utume) kabla yako katika mitume wetu. Wala hutapata mabadiliko katika desturi yetu.

Qur-an Surat Fatir 35 : 43 Wala hutapata mahadiliko katika kawaida(desturi) ya Mungu (allyoiweka)wala hutakuta mageuko katika kawaida ya Mwenyezi Mungu.

Ushahidi huo wa maandiko ya vitabu vyote viwili unaonyesha na kuthibitisha vile ambavyo hoja zinazo tolewa kwa kudai kuwa Biblia imeharibiwa si hoja za kimsingi na zaidi ya yote ni hoja zinazoonekana kushusha nguvu na uwezo wa Mungu wa kulinda na kusimamia mambo yake,lakini zaidi ya yote ni kutaka kumfanya mwongo pale alipoahidi kulinda maneno yake na kutokubali mageuzi katika mafunuo yake.


“Kamwe Biblia haijapotoshwa na haiwezi kupotoshwa”.
Qur- an Sura ya 87:18

“Hakika hayo mnayoambiwa humu (ndani ya Qur- ran) yamo katika vitabu vilivyotangulia. Vitabu vya Ibrahim, Musa, Isa na manabii wengine………………..”


Maneno hayo ya Qur-an yanatupatia Mwangaza unaotupa msingi wa kuichunguza vyema mada hii ya muhimu, maelezo ya Qur-an katika Aya hiyo yanaonyesha kuwa msingi wa mafunuo hayo ya Qur-an unategemea sana na kujengwa juu ya yale yaliyokwisha funuliwa awali katika vitabu vilivyo katika mkusanyiko wa “Biblia takatifu” hata hivyoMaandiko ya Qur-an kwa uwazi huyataja na kuyathibitisha mafunuo hayo ya kibiblia kwa kadri ya Aya zifuatazo:-


1. Torati - Musa
Qur-an 2:53 Natulimpa Musa kitabu (Torati) cha kupambanua na kuongoa ………
Qur-an 28:48 “Mnayakataa alopewa Musa”


2. Zaburi – Daud
Qur-an 4:163 Na Dawdi tukampa “Zaburi”
Qur-an 17:55 Dawd tukampa “Zaburi”


3. Injili-Bwana Yesu
Qur-an 5:47 watu wa “Injili” wahukumu kwa yale aliyotelemsha Mwenyezi Mungu ndani yake.


Mafungu hayo ya Qur-an kwa uwazi mkubwa yanaonyesha uzito na ukweli wa vitabu hivyo vya kale, kwa maana nyingine ndiyo maana Qur-an inaweka wazi kuwa mafunuo hayo (ya Qur-an) yanatokana na msingi wa Biblia (87:18).


BIBLIA NI ZAIDI YA QURAN
Biblia Mhimili wa Qur-an
Pamoja na mafunuo hayo mapya ya Qur-an bado mtume Muhammad aliendelea kuonyesha umuhimu na nafasi ya “Biblia” katika imani yake hiyo ya uislam.


Mafungu na Aya kadhaa tutakazozipitia zitatusaidia kuoana ukweli huu utakao tupa mwelekeo wa kuelewa vile Biblia ilivyo tegemeo (Mhimili) mkuu wa Qur-an. Kwa kadri ya Aya kadhaa za Qur-an inaonyesha dhahili kuwa Qur-an si kitabu kinachojitegemea chenyewe, badala yake kinapaswa kupimwa na kusaidiwa na mafunuo ya Biblia takatifu


Fuatilia nukuu zifuatazo za Qur-an ili kupanua ufahamu wa hoja hii ya msingi:-

Qur-an 10:94… “Ukiwa na shaka katika haya tuliyo kutelemshia nenda ukawaulize
watu wasomao vitabu kabla yako…………….”


Hoja za msingi
Ikiwa Qur-an ni kitabu chenye kujitosheleza chenyewe kuna haja gani ya kuwauliza waliyosoma vitabu vya kabla ya Qur-an?
Qur an 16:43 … Nendeni mkawaulize wenye kumbukumbu za vitabu vya


Mwenyezi Mungu vya kale ikiwa ninyi hamjui


Jifunze kupitia mfano
Katika dunia yetu Hospitali mbalimbali zinazotibu magonjwa ya kila aina humo wapo Madaktari bingwa, kwa kawaida ili kumtambua Daktari bingwa (Mhimili) ni pale tu unapopata ugonjwa na kwenda katika hospitali unayo iamini lakini hatimaye mwisho wa yote una taarifiwa kuhamishwa na kupelekwa katika hospitali nyingine kwa uchunguzi zaidi, “bila shaka huko ndiko kwa daktari bingwa”.


Ni wazi kama utakuwa msomaji mwaminifu katika sehemu hii tutakubaliana na kupata jibu kuwa “Biblia takatifu ni Mhimili wa Qur-an” na kwamba hakuna usahihi wa mafundisho yanayosikika kudai kuwa kitabu hiki kitakatifu kimetiwa maneno ya uongo au kuharibiwa kwa namna yeyote ile.

“Bwana akubariki kwa uelewa huu, na unapochukua hatua kuelimisha wengine.”

For Max Shimba Ministries

By permission

Monday, February 1, 2016

MKE WA MUHAMMAD AISHA ANASEMA KUWA MUHAMMAD ALIKUWA AMEROGWA

Muhammad Aliwahi Kulogwa (Kwa Apizo, ‘Under a Spell’)

" ‘Aisha anasimulia: Nabii alifanyiwa uchawi hata akaanza kudhani kuwa anafanya kitu fulani wakati hakuwa anafanya. Siku moja alimwomba (Allah) kwa muda mrefu sana kisha akasema, ‘Naona kuwa Allah amenipa mwongozo wa namna ya kujitibu mwenyewe.’..." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 (Mwanzo wa Uumbaji) sura ya 10 na.490 uk.317.

Tazama pia juzuu ya 4 kitabu cha 53 (Wajibu wa Khumus) sura ya 34 na.400 uk.267, juzuu ya 8 kitabu cha 73 (Mienendo Myema) sura ya 56 na.89 uk.56-57, juzuu ya 8 kitabu cha 75 (Kitabu cha Maombi ‘Book of Invocations’) sura ya 59 na.400 uk.266-267. Juzuu ya 7 na.658-660 uk.441-443.

Pia tazama Muislam Sahihi juzuu ya 2 kitabu cha 4 (Kitabu cha Sala) sura ya 309 na.1888 uk.411

Muhammad alilogwa. Alisimulia ‘Aisha: Nabii aliendelea kwa kipindi fulani akidhania kuwa anafanya tendo la ndoa na mke wake, lakini haikuwa hivyo. Siku moja alisema kwangu, "O ‘Aisha! Mungu ameniagiza kuhusiana na suala nililomuuliza. Watu wawili walikuja, mmoja alikaa karibu na miguu yangu na mwingine karibu na kichwa changu. Yule aliyekuwa karibu na miguu yangu alimuuliza yule wa karibu na kichwa changu (akininyooshea kidole), ‘Mtu huyu ana shida gani? Yule mwingine akamjibu, ‘Ameathirika na uchawi. Yule wa kwanza akauliza, ‘Ni nani aliyemfanyia uchawi?’ Yule mwingine akajibu, ‘Lubaid bin A’sam." Yule wa kwanza akauliza, ‘(Alitumia) nyenzo gani?.’ Yule mwingine alijibu ‘Ngozi ya chavua ya mtende wa kiume na chanio lililowekwa nywele, na kuwekwa chini ya jiwe kwenye bwawa la Dharwan.’" Kisha Nabii alikwenda kwenye bwawa lile na kusema, "Hili ndilo bwawa lilelile nililoonyeshwa kwenye ndoto. Ncha za mitende yake inaonekana kama vichwa vya mashetani, na maji yake yanaonekana kama mchanganyiko wa hina."… ‘Aisha aliongeza, "(Mchawi) Lubaid bin A’sam alikuwa anatokea Bani Zuraiq, mshirika wa Wayahudi." Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 (Mienendo Myema) sura ya 56 na.89 uk.57. Tazama pia Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 75 (Kitabu cha Maombi ‘Book of Invocations’) sura ya 59 na.400 uk.266

1. Kwanini tumfuate Mtume aliye rogwa?
2. Hivi kuna Mtume au Nabii yeyote yule kwenye Biblia na yeye alirogwa?
3. Kwanini Allah alishindwa kumlinda Mtume wake kutoka nguvu za kurogwa?
4. Hivi wapi tunasoma kuwa Muhammad alifanyiwa maombi na urogi ukamtoka?

Hakuna ushahid wowote ule ambao unasema kuwa Muhammad aliombewa na kutokwa huo uchawi. Huu ni msiba kwa Nabii wa Allah kufa huku akiwa amefanyiwa urogi.

Ndugu msomaji,

Mtu yeyote yule akifa kwa kurogwa na huku akiwa amejaa Mashetani, basi huyo mtu yeye ataishia kwenye Jehannam ya moto.


Karibuni kwa Yesu aliye hai.

Max Shimba Ministries

Ancient Jewish Wedding Ceremony: “No man knows the day or hour, only the Father”

  The Ancient Jewish Marriage Rite: A Detailed Exposition of Betrothal, Preparation, and Consummation Dr. Maxwell Shimba Shimba Theological ...

TRENDING NOW