Sunday, March 6, 2016

ALLAH ATEUA MTUME WA MAJINI NA MPINGA KRISTO

1. Allah ateua Mtume kwa Majini Quran 6: 130
2. Allah ateua Mtume wa Wanyama Surat An Naml 82
Ndugu zanguni,
Allah anasema katika Quran kuwa, ameteua Mtume kwa kila kiumbe mpaka Majini machafu. Hebu soma aya hapa chini
ALLAH ANASEMA KUWA MAJINI YANA MTUME WAO
Quran 6: 130. Enyi makundi ya majini na watu! Je, hawakukujieni Mitume kutokana na nyinyi wenyewe wakikubainishieni Aya zangu, na wakikuonyeni mkutano wa Siku yenu hii. Nao watasema: Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu. Na yaliwadanganya maisha ya dunia. Nao watajishuhudia wenyewe ya kwamba walikuwa makafiri.
Lakini nilipo soma Hadith nikagundua kuwa, Muhammad alikuwa anaongea na Majini na kuyafundisha Quran.
MTUME MUHAMMAD AKUTANA NA MAJINI USIKU
Allah S.W.T. ametuhakikishia wazi kuwa ujumbe aliopewa Mtume S.A.W. ulikuwa kwa Wanadamu na Majini na Mashetani pia. Na katika Qurani na Hadithi za Mtume S.A.W. kuna dalili zilizo wazi zinazoyakinisha kuwa Mtume S.A.W. alikuwa akikutana nao na kuwafundisha dini. Na hata wakati mwingine Majini walikuwa wakitoa majibu mazuri zaidi kuliko Binadamu kwenye masuala ya dini. Na mfano ni wakati waliposomewa Suratir Rahmaan. Hadithi iliyopokelewa na Jaabir bin Abdallah R.A.A. na iliyotolewa na Ttirmidhi kasema, “Wakati ambapo Mtume S.A.W. alipowasomea Majini Suratir Rahmaan, “
لَقَدْ قَرَأْتُهَا ‘‘يعني سُورَةَ الرَّحْمَنِ’’ عَلَى الْجِنِّ …، فَكَانُوا أَحْسَنَ مَرْدُودًا مِنْكُمْ ، كُنْتُ كُلَّمَا أَتَيْتُ عَلَى قَوْلِهِ ]فَبِأَيِّ آلاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ[ قَالُوا: لا بِشَيْءٍ مِنْ نِعَمِكَ رَبَّنَا نُكَذِّبُ ، فَلَكَ الحمد
Maana yake, “Hakika nimewasomea Majini (yaani Suratir Rahmaan)…wamejibu vizuri zaidi kuliko nyinyi. Kila nilipofikia kauli Yake (Mwenyezi Mungu S.W.T.) “Fabiayyi A-alaai Rabikumaa Tukadhibaan.) Maana yake, “Basi ipi katika neema za Mola wenu ambayo mnayoikanusha kuwa si kweli?” (Basi Majini) walijibu “Laa bishaay Min Niamika Rabbana Nukadhibu, Falakal Hamdu.” Maana yake, “Hakuna neema yoyote katika neema Zako Mola wetu tunayoikadhibisha, bali tunashukuru.” Na Mtume S.A.W. alipowasomea Wanadamu hawakujibu chochote, akawaambia, “Ndugu zenu wa Ki-Jini wamejibu jawabu nzuri waliposikia haya.” Na dalili nyingine kuwa Mtume S.AW. pia alikuwa ametumwa kwao ni kisa cha baadhi ya Majini ambao baada ya kuisikiliza Qurani waliiamini na wakarejea kwao na kuanza kuwaita wenzao kwenye dini ya Kiislamu.
ALLAH ANASEMA KUWA MAJINI YALITUMWA KWA MUHAMMAD ILI KUSIKILIZA QURAN
ALLAH HUYO HUYO ALISEMA KUWA KILA WATU/VIUMBE/WANYAMA WALIPEWA MTUME WAO. HAPO TEYARI KUNA SHAKA KWENYE QURAN YA MUHAMMAD AMBAYO SASA INAKABIDHIWA MAJINI MACHAFU.
Allah kasema katika Suratil Ahqaaf aya ya 29 mpaka 32, “
]وَإِذْ صَرَفْنَا إِلَيْكَ نَفَرًا مِنْ الْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ الْقُرْآنَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوا أَنْصِتُوا فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَى قَوْمِهِمْ مُنْذِرِينَ * قَالُوا يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنْزِلَ مِنْ بَعْدِ مُوسَى مُصَدِّقًا لِمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ وَإِلَى طَرِيقٍ مُسْتَقِيمٍ * يَا قَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِي اللَّهِ وَآمِنُوا بِهِ يَغْفِرْ لَكُمْ مِنْ ذُنُوبِكُمْ وَيُجِرْكُمْ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ * وَمَنْ لا يُجِبْ دَاعِي اللَّهِ فَلَيْسَ بِمُعْجِزٍ فِي الأرْضِ وَلَيْسَ لَهُ مِنْ دُونِهِ أَولِيَاءُ أُوْلَئِكَ فِي ضَلالٍ مُبِينٍ[
Maana yake, “Na (wakumbushe) wakati tulipowaleta kundi la Majini kuja kwako kusikiliza Qurani. Basi walipoihudhuria walisema (kuambiana): “Nyamazeni! (Msikilize maneno ya Mwenyezi Mungu)” Na ilipokwisha somwa walirudi kwa jamaa zao kwenda kuwaonya. Wakasema “Enyi watu wetu! Sisi tumesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya (Nabii) Musa, kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake na kinachoongoza kwenye haki na kwenye njia iliyonyooka. Enyi kaumu yetu! Muitikieni Mlingani, (Muitaji) wa Mwenyezi Mungu na muaminini, atakusameheni (Mwenyezi Mungu) dhambi zenu na atakukingeni na adhabu iumizayo. Na wasiomuitikia Muitaji wa Mwenyezi Mungu, basi hao hawatamshinda (asiwapate) hapa katika ardhi, wala hawatakuwa na walinzi mbele Yake. Hao wamo katika upotofu ulio dhahiri.”
Na kisa kingine ni cha Majini waliosikia Qurani kutoka kwa Mtume S.A.W wakati alipokuwa akiwasalisha Masahaba wake Sala ya Alfajiri. Na hii ilikuwa bila ya yeye kuwa na habari mpaka Mwenyezi Mungu S.W.T. alipomjulisha. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Suratil Jin aya ya 1 na ya 2, “
]قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِنْ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا * يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَنْ نُشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا[
Maana yake, “Sema: “Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la Majini lilisikiliza (Qurani) likasema: “Hakika sisi tumesikia Qurani ya ajabu. Inaongoza katika uwongofu; kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote tena na Mola wetu.”
Makala haya yametolewa katika kitabu changu kiitwacho, "Hakika ya Majini."
ALLAH SASA ATEUA MTUME KWA WANYAMA = 666. KUMBE BASI ALLAH NA MUHAMMAD NA DINI YAKE NDIO 666
Surat An Naml 82. Na itapo waangukia kauli juu yao, tutawatolea mnyama katika ardhi atakaye wasemeza, ya kuwa watu walikuwa hawana na yakini na Ishara zetu
Kifungu kuu katika Biblia ambacho kinataja "alama ya mnyama" ni Ufunuo 13:15-18. Marejeo mengine yanaweza kupatikana katika Ufunuo 14: 9, 11, 15:2, 16:2, 19:20, na 20:4. Alama hii hutumika kama muhuri kwa wafuasi wa Mpinga Kristo na nabii wa uongo (msemaji wa Mpinga Kristo). Nabii wa uongo (mnyama wa pili) ndiye ambaye husababisha watu kuchukua alama hii. Alama hasa huwekwa katika mkono au paji la uso na sio kadi mtu atabeba.
SIRI IMESHA FUNGUKA, SASA TUNAFAHAMU KUWA, ALLAH NDIE ATAKAYE LETA MPINGA KRISTO 666, NA ALLAH AMEKIRI KATIKA SURAT AN NAML KUWA YEYE AMESHA TEUA MTUME AMBAYE NI MNYAMA NA HUYO MTUME ANASOMA QURAN YA MUHAMMAD.
KAMA kweli Quran ni maneno ya Allah, na aliiteremsha, basi, leo tunafahamu kuwa Allah sio tu ataleta Mpinga Kristo, bali Allah na Muhammad ndio Mpinga Kristo.
Ndugu msomaji utakaesoma mpambano huu sitanukuu moja kwa moja maandiko lakini nitakachokiandika, mashahidi mtakuwa wenyewe kuona kama ni kweli au uongo ya kuwa vitabu hivi vinapambana kiasi hicho..nami sitaandika uongo kamwe.
Hebu tuanze:
BIBLIA: ‘Yesu Kristo alisulubiwa. QURAN: hapana hapana walimsulubisha mwandaazimu mwingine wakizani ndiye!!.
BIBLIA: Yesu ni Mwana wa Mungu. QURAN: ni uongo kwa kuwa Mungu hana mwana wala hazai!!.
BIBLIA: ’tunapata msamaha wa dhambi kupitia damu ya Yesu. QURAN: sivyo kabisa…Mnyaai Mungu ndiye akusameheni madhambi yenu pale mtakapoenda Makka japo mara moja kuhiji. (kiswali chandu cha uzushi..wale masikini je?..Ndiyo kusema pepo ni ya matajiri tu?!!).
BIBLIA: Majini wana asili ya mashetani, ni kundi au jeshi la yule muovu, msishirikiane nayo katika ibada wala kuwatolea sadaka.QURAN: ALLAH asema: nimekuumbeni na majini ili mpate kuniabudu!! (swali la uzushi:Shetani na majini yake yanaabudu na waisilamu ili yaende wapi wakati wao walisha laaniwa na wanachosubiri ni jehanam tu!!).
Huu ni Msiba Mwengine katika dini ya Allah ambayo sasa tumejifunza kuwa ni ya Mpinga Kristo.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 6, 2016

KUMBE ALLAH NI DHAIFU!


Katika somo letu la leo, ningependa tusoma mambo kadhaa ambayo Allah wa Uislam hana uwezo na mamlaka juu yake.
Waislam wanatuambia kuwa Uislam ni dini ya Allah ambaye hana uwezo wa kufanya yafuatayo:
Anasema hakuna wa kumsaidia katika udhaifu wake!
Q17:111 Na sema: Alhamdulillah,Himdi zote ni za Allah ambaye hana mwana,wala hana mshirika katika ufalme,wala hana rafiki wa kumsaidia KWA SABABU YA UDHAIFU WAKE. Na mtukuze kwa utukufu mkubwa.
MASWALI!
1. Udhaifu wake ni upi?
2. Kwanini Waislam wanampigania huyu Allah dhaifu?
Allah hana uwezo wa kuishi ndani ya binadamu. [Allah is not omnipresent]
Allah hana uwezo wa kuzungumza na kusikia lugha yeyote ile zaidi ya Kiarabu. Majlisi, Bihar al-Anwar, vol. 11, pg. 56; vol. 8, pg. 218 and 286 and vol. 10, pg. 81, al-Wafa Institute, Beirut, 1404 ah. and Tabarsi, Aminuddin, Tafsir Majma’ul-Bayan, vol. 2, pg. 206, Beyrut, Dar al-Ihya’ al-Torath al-Arabi.
Allah hasikii na hajibu maombi ambayo hayakuombwa Kiarabu See: Tawfiqi, Husein, Arabi, Nemune’i az Zabane Moqaddas, the Haft Aseman Periodical, no. 27. and Ibid, vol. 12, pg. 87.
Allah hawezi kusikia maombi ambayo yanaombwa bila ya kuangalia Makkah. Quran 2:148-149
Allah hana uwezo wa kumzuia Shetani kuishi ndani ya Pua yako wakati umelala. (Sahih Muslim, Book 002, Number 0462)
Allah hana uwezo wa kumkataza Shetani asikojoe kwenye masikio yako unapo pitiwa na usingizi. The Hadith (Bukari vol. 2 no. 245)
Allah hana uwezo wa kutetea vitabu vyake, ingawa alidai anaweza. S. 15:90-93 Shakir
Allah hawezi kusikia maombi yako kama kuna Mwanamke au Mbwa au Punda karibu na sehemu unayo fanyia maombi. Sahih Bukhari 1:9:490, Sahih Bukhari 1:9:493
Allah hawezi kutetea dini yake ya Kiislam na anahitaji msaada wa Waislam kuua na kutesa wale wote ambao wanaukataa Uislam. Allah sio Akbar kama anavyo dai. Quran Surah 9:29, Al Bukhari vol 4:196., Al Bukhari vol 1:35
Allah hapendi watu isipokuwa wale ambao ni Watumwa wake.al-Tirmidhi, 2396; classed as saheeh by al-Albaani.
Allah hana uwezo wa kutetea Mitume wake kutoka kwa Wanawake Wajane wa Kiyahudi. [Aal ‘Imraan 3:31], al-Tirmidhi,
Allah hana uwezo wa kuwatetea na kuwalinda Waislam kutoka kwa Mtume mwenye Nguvu kama Paulo ambaye Waislam wanadai kuwa, Ndie Mwanzilishi wa Imani ya Kikristo ambayo ni kubwa kuliko Uislamu. Qur'an 9:88, Sahih Bukhari, Book 52: Fighting for the Cause of Allah (Jihaad) Volume 4, Book 52, Number 41:
Allah hana uwezo wa kuwaokoa wanawake kutoka Jehannam, kwasababu eti wao ni viumbe dhaifu.Sura (37:22-23) Hadith: Bukhari (2:28) (Sahih Bukhari: 2:18:161; 7:62:125, ).
Allah hana uwezo wa kufanya miujiza kupitia waonyaji kama Muhammad ambaye alidai katumwa na Mwenyezi Mungu, jambo ambalo lingesaidia kutupa uhakikisho kuwa Muhammad alitumwa na Allah, kwasababu ya maovu mengi aliyo fanya ambayo ni kinyume na mambo yaliyo fanywa na Mitume walio kuja kabla yake.
Ndugu zanguni, listi ya mambo ambayo Allah hana uwezo wa kufanya ni mengi sana kiasi cha kujaza karatasi nyingi, leo nimeona niweke haya machahe kuhusu huyu Allah wa Uislam.
Allah hana uwezo wa kuwa na Mwana bila ya kuwa na Mke.
Sasa ngoja niulize?
Kuna sababu gani hapa duniani Mtu amwamini huyu Allah aliyejaa mapungufu na udhaifu, chuki, na kuacha kumwamimi Yahaweh aliyejaa upendo, hekima na mamlaka yote?
Mimi nitamfuata Yesu, Mungu Mtukufu YHWH, kwasabau katika Yesu hakuna lisilo wezekana (Luka 1:37)
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
March 6, 2016

Saturday, March 5, 2016

QURAN, ALLAH, MUHAMMAD, NA JIBRIL WANAKIRI KUWA YESU NI MUNGU KWASABABU "YESU NI NENO"

Ndugu msomaji,
Naanza kwa kunukuu Biblia:
Yohana 1:1 inasema “Neno alikuwa Mungu”. Yohana 1:14 inasema “Neno akafanyika mwili.” Hii inaonyesha wazi ya kwamba Yesu ni Mungu katika mwili. Matendo 20:28 inatuambia, “…Muwe wachungaji wa kanisa la Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe,” Ni nani aliyelinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe? Yesu kristo. Matendo 20:28 inasema ya kwamba Mungu alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe. Kwa hivyo Yesu ni Mungu!
SASA BASI, BIBLIA ILIYO KUJA KABLA YA QURAN INASEMA KUWA, YESU NI NENO, NA NENO NI MUNGU KAMA ILIVYO THIBITISHWA HAPO JUU.
JE KWEYE QURAN, ALLAH ANASEMA NINI KUHUSU ISA WA QURAN?
Qur-an Tukufu inasemaje!
Qur-anSurat al-Imran 3:45 aliposema malaika ewe Mariam Mwenyezi Mungu anakupa habari njema za “neno” litokalo kwake “jina lake” ni Masihi Isa Ibn Mariam, mwenye heshma katika Dunia na akhera ………….
Andiko hilo la Qur-an linaonyesha na kufunua kwa wazi juu ya kauli ya Malaika kwa Mariam iliyomtaka kujua juu ya mamlaka inayotakiwa kukaa ndani ya tumbo lake na hapa Qur-an huitaja mamlaka hiyo kuwa ni Mwana aitwaye Isa Ibn Mariam. Lakini Qur-an hutaja mwana huyo (Isa) kama “Neno” litokalo kwake (Mungu ).
Katika maneno ya Kiarabu ni:“Kalimatu minhu” - Neno litokalo kwake (Mungu)
Katika upana wa lugha neno “kalimatu” limetumika kama kisifa kinacho mwelezea “Mtu” maana imetumika kauli ya umoja, “Kalimatu” - Neno, kwa Waarabu huita “Mufrada” yaani umoja hivyo aya haikusudii “Maneno” ya kutamkika ila ni sifa na cheo cha mtu (Isa Ibn Mariam) kama Neno katika umoja na siyo wingi (Jami-u) hivyo Isa katika Qur-an hutambuliwa kuwa na cheo au sifa iitwayo Neno kabla ya zile za kibinadamu, katika Uislam manabii mbalimbali wamepewa vyeo na sifa mfano:-
Musa huitwa - Takalama llahu………aliyeongea na Mungu
Ibrahimu - Habiba llahu ……… kipenzi cha Mungu
Lakini nabii Isa huonekana kuwa na sifa mbili ya kwanza ni ile ya kuitwa
Kalimatu llahu - Neno la Mungu
Ruh” llahu - Roho itokayo kwa Mungu
Hivyo baada ya kufahamu hilo ni vyema sasa tukaangalia na kuchunguza kwa upana juu ya sifa hii ya “Neno” Je inatueleza nini juu ya asili na mamlaka haswaa ya (Isa) kabla ya kuja hapa duniani.
Surat Al Imran 45. Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu).
Quran inakiri kuwa Maryam alipata MWANA KWA KUPITIA NENO LITOKALO KWA MUNGU. Hivyo basi Isa asili yane ni NENO na sio binadamu. Rejea Surat Al Imran aya 45.
JE, BIBLIA INASEMA NINI?
Baada ya kuona wazo hilo la Qur-an hebu tuone Biblia nayo inasema nini juu ya hilo?
Yohana.1: 1-3 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
Katika sura na Aya hizo Biblia nayoinaeleza juu ya habari ya “Neno” (logos) pia inatupeleka mbele zaidi maana inasema kuwa huyo “Neno” (kalimatu) ni Mungu (rejea …….Yohana 1: 1-2 naye neno alikuwa Mungu) Je hii inamaana kuwa huyo Neno ni Yesu!
Na je inamaana Yesu ni Mungu kiasili?
Ndugu yangu mpendwa msomaji ukiwa ni Muislam au Mkristo yawezekana hilo likawa ndiyo swali lako. Ninakuomba kuwa makini zaidi tunapoingia sehemu hii ngumu na inayosumbua watu wengi.
Hebu kwanza tumfuatilie huyu Neno Je Biblia inasemaje juu ya Neno?
Zaburi 33:6 kwa “Neno” la Bwana Mbingu zilifanyika na Jeshi lake lote kwa Pumzi ya kinywa chake.
Biblia hapo inaonyesha kutaja tena habari ya “Neno” na huyu Neno hapo anaonekana kuwa na sifa ya kuumba, lakini ninayo imani kuwa Biblia inapotaja habari ya “Neno” bado ingali inazungumzia juu ya Mungu mmoja tu katika upana wa utendaji (Nafsi) hivyo Neno ndiye Mungu huyo.
Je Neno la Mungu ndiye Mungu huyo?
Ndiyo ni kweli ndugu msomaji wangu hebu nikupe mfano:-
Kwa kutumia kielelezo cha Neno lakawaida tunajifunza juu ya neno kama nafsi fikiri huenda ulimuudhi mtu Fulani naye kwa kughadhibika akaamua kukushitaki kwa kosa la kumtamkia “Neno” baya Swali! Je polisi watakapo kuja kukukamata watakamata “Neno” lako lililosema vibaya au utakamatwa wewe mwenyewe?
Jibu:- Niwazi kuwa utakamatwa wewe mwenyewe na hiyo ni kwasababu! Neno na mwenye Neno ni kitu kimoja.
Kielelezo hicho kinawiana fika na mamlaka ya Yesu kama Neno la Mungu huwezi kumtenganisha kiasili na mamlaka ya Uungu, yeye (Yesu) ni Neno kama nafsi (logos) ya utendaji wa Mungu, alikuwako kabla ya vyote.
Pamoja na hayo ninaamini bado unajiuliza maswali haya.
Je! Huyu Yesu ninani haswa na je vitabu vyote vya dini vina uwazi gani kuhusu Yesu kama ni Mungu, na je kweli zipo dalili na sifa za Uungu wake?
Maswali hayo ni mazuri ikiwa yapo katika fikra zako ndugu msomaji wangu mpendwa.
Kumbuka:
Mungu ufahamika kwa vigezo na sifa maalumu zinazomfanya aitwa Mungu vigezo na tabia hizo kamwe havipaswi kumhusu mwanadamu. Vinginevyo ikiwa yuko anayeonekana kuwa mwanadamu lakini vitabu halali vya Kidini yaani Qur-an na Biblia vikampa sifa za kimungu hiyo anapaswa kutazamwa upya na kwa umakini, asije akawa ni Mungu pamoja nasi (Emmanuel).
Kumbuka:
Mungu alijifunua kwenye kijiti na kusema na mtumishi wake nabii Musa (Qur-an 20:911)
Kulingana na ukuu na uweza wa Mungu huenda hilo lilikuwa ni jambo duni na lakushangaza ila Musa alipaswa tu kutambua kuwa alikutana na kuzungumza na Mungu na ndiyo sababu leo hii Musa huitwa katika Uislam.
Takalama llahu - aliyeongea na Mungu
Kubuka Musa alipoona ule moto alifikiri hata kuutumia kwa mambo binafsi lakini laajabu kumbe moto ule ulisitiri mamlaka ya Mungu aliye hitaji kuzungumza naye.
Katika kitabu cha ufunuo wa Yohana, Malaika alimwamuru mtume Yohana kumuabudu Mungu tu(ufunuo wa Yohana 19: 10). Mra nyingi Yesu katika maandiko aabudiwa (Mathayo 2;11; 14:33; 28:9,17; Luka 24:52; Yohana 9:38). Hakemei watu kwa kumuabudu. Kama Yesu hakuwa Mungu, angewaambia watu wasimuabudu, kama vile malaika alivyofanya. Kuna aya nyingi za maandiko zinazoshuhudia ya kwamba Yesu ni Mungu.
Allah anamwambia Muhammad katia Suratul Yunus aya 94 kuwa, kama Muhammad anashaka na ukweli kuwa Yesu ni Neno na Neno ni Mungu. Basi Muhammad atuulize Wakristo kuwa, Je, hayo madai ya Allah ni ya kweli? Hakika Biblia imekamilika na kusema bila ya shaka yeyote ile kuwa Yesu ni Neno na Neno alikuwa na Mungu kabla ya Mwanzo kuwepo. Allah na yeye amekiri hayo kuwa Yesu ni Neno ambalo lilikuwa na Mungu hata kabla ya Mwanzo kuwepo.
Leo nimejibu hoja ya Waislam kuwa, Yesu ni Mungu kwasababu "YESU NI NENO NA NENO NI MUNGU"
Katika huduma yake,
Max Shimba Ministries Org.
Copyright © Max Shimba Ministries 2016

YESU AKUBALI KUITWA MUNGU


Ndugu msomaji,
Kwenye somo letu la leo ninakuletea uthibitisho Saba (7) wa Yesu kuitwa Mungu.
Bila ya kupoteza muda tuanze kusoma aya za Biblia.

1. THOMASO ANAMWITA YESU MUNGU
Tomaso mwanafunzi wa Yesu alisema kuhusu Yesu, “Bwana na Mungu wangu” (Yohana 20:28). 28 Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! 29 Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki.
Baada ya Thomaso kumwita Yesu "Bwana na Mungu wangu", tunasoma kuwa Yesu anakubali na kumwabia, wewe Thomaso unameniona ndio unasadiki. Sasa Thomaso anasadiki nini? Kumbe Thomaso sasa anasadiki aliyo sema kuwa Yesu ni Bwana na Mungu.

2. YESU ANAITWA MUNGU MKUU NA WAFUASI WAKE
Tito 2:13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
KUMBE HATA WANAFUNZI NA WAFUASI WA YESU WALIMWITA YESU MUNGU tena MKUU. Tumesoma katika Tito Mlango wa 2 na aya ya 13 kuwa, Kristo Yesu ni Mungu Mkuu na Mwokozi wetu. Sasa wapi Yesu alikataa kuitwa Mungu Mkuu?
3. PETRO ANAKIRI KUWA YEYE NI MTUMWA WA YESU AMBAYE NI MUNGU WETU NA MWOKOZI WETU
2 Petro 1:1 Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo, kwa wale waliopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika hali ya Mungu wetu, na Mwokozi Yesu Kristo.
Petro anajitambulisha kuwa yeye ni mtumwa wa Yesu Kristo ambaye ni Mungu wetu na Mwokozi wetu.
Kumbuka Petro aliishi WAKATI WA YESU NA ALIKUWA MMOJA WA WANAFUNZI WAKE. Kama Petro aliye kuwa na Yesu anamwita Yesu Mungu, je, wewe ni nani kupinga ukweli huu?
4. MUNGU BABA ANAMWITA MWANA - YESU "MUNGU"
Waebrania 1:8-9 8 Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. 9 Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio.
Baba asema juu ya Yesu, “Lakini juu ya mwana asema haya, “Na Kiti chako cha enzi, MUNGU, Kitadumu milele, na haki itakuwa fimbo ya ufalme wako.” ==> Baba anasema kuwa kiti cha Enzi ni cha Yesu, na zaidi ya hapo anaongeza kwa kumwita "MUNGU"
KUMBE HATA Baba aliye Mbinguni anamwita Yesu ni Mungu. Hatusomi na wala hakuna aya ambayo Yesu anamwambia Baba yake asimwite Mungu.
AYA YA 9, Mungu Baba anamaliza kabisaa kwa kusema yafuatayo "KWAHIYO MUNGU, MUNGU WAKO". Hapo teyari Mungu Baba anasisitiza kuwa MWANA NI MUNGU NA YEYE BABA NI MUNGU.
5. MALAIKA WANAMWABUDU YESU: KUMBE YESU NI MUNGU
Katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana, Malaika alimwamuru Mtume Yohana kumuabudu Mungu tu (Ufunuo wa Yohana 19: 10). Mara nyingi Yesu katika maandiko aabudiwa (Mathayo 2;11; 14:33; 28:9,17; Luka 24:52; Yohana 9:38). Hakemei watu kwa kumuabudu. Kama Yesu hakuwa Mungu, angewaambia watu wasimuabudu, kama vile Malaika alivyofanya. Kuna aya nyingi za maandiko zinazoshuhudia ya kwamba Yesu ni Mungu.
6. VIONGOZI WA KIYAHUDI WASEMA YESU AMEKUFURU BAADA YA KUKUBALI KUWA YEYE NI MWANA WA MUNGU
Wakati wa kujaribiwa kwake mbele ya viongozi wa Kiyahudi, kuhani mkuu alimtaka Yesu, “Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu” (Mathayo 26:63). “Yesu akamwambia wewe umesema,’ Yesu akamwambia, wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni” (Mathayo 26:64) viongozi wa Kiyahudi walimdhania kwa kukufuru (Mathayo 26:65-66).
7. WAYAHUDU WANAZIDI KUSISITIZA KUWA YESU NI MWANA WA MUNGUBaadaye mbele ya Pilato, “Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu” Yohana 19:7) ni kwa nini makisio yake kuwa Mwana wa Mungu yachukuliwe kuwa kufuru na astahili hukumu ya kifo?
Wayahudi wilielewa vizuri sana chenye Yesu alimaanisha kwa maneno haya “Mwana wa Mungu” kuwa Mwana wa Mungu ni kuwa hali moja na Mungu. Mwana wa Mungu “wa Mungu” kusema uko katika hali sawa na Mungu-hakika kuwa Mungu- kulikuwa sawa na kukufuru kwa viongozi wa Kiyahudi; kwa hivyo walimtaka Yesu auwawe, kulingana na Mambo ya Nyakati 24:15. Waebrania 1:3 inadhihirisha haya wazi, “Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu.”
Tumesoma tena kwa ushahidi wa aya kadhaa kuwa Mungu Baba anamwita MWANA NI MUNGU, Wanafunzi wake wanamwita Yesu ni Mungu, Malaika wanasema tumwabudu Yesu ambaye ni Mungu, na Wayahudi wanasema Yesu alikufuru alipo kubali kuitwa Mwana wa Mungu na Pilato.
Kwakuwa inafahamika Yesu hakuwa na dhambi wala hakuwai tenda dhambi:
1. Je, kukubali kwake kuitwa Mungu kunamaanisha nini?
2. Kwanini Yesu hakumkatalia Thomaso pale alipomwitwa "Bwana na Mungu wangu?
3. Kwanini Petro anamwita Yesu ni Mungu wetu na Mwokozi wetu?
4. Kwanini Mungu Baba anamwita Mwana ambaye ni Yesu KUWA NI "MUNGU"
5. Kwanini Malaika wanasema tumwabudu Yesu, huku wakisisitiza kuwa anaye abudiwa ni Mungu pekee?
6. Kwanini Kuhani Mkuu alimtaka Yesu kukiri kuwa ni Mwana wa Mjungu? Je, jinu la yesu lilisababisha nini kwa Wayahudi?
7. Kwanini Wayahudi walimshataki Yesu mbele ya Pilato kuwa kajiita Mwana wa Mungu, na kufanya hivyo ni kukufuru?
Ni maombi yangu kuwa, hizi aya chache tulizo ziweka hapa zitakufungua macho na uelewe Uungu wa Yesu na kwanini Yesu hakukana kuitwa Mungu.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

Friday, March 4, 2016

QURAN, ALLAH, MUHAMMAD, NA JIBRIL WANAKIRI KUWA YESU NI MUNGU KWASABABU ANASAMEHE DHAMBI

Ndugu msomaji,
Tunaendelea kujifunza kuhusu Uungu wa Yesu. Quran, Allah, Muhammad na Jibril kwa mara nyingine tena wanakiri kuwa Yesu ni Mungu.
Hii ni sifa nyingine ya Mungu pekee na wala si ya mwanadamu.
Quran 40:2-3
Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mwenye kujua. Anaye samehe dhambi na anaye pokea toba, Mkali wa kuadhibu, Mwenye ukarimu, hakuna mungu ila Yeye; marejeo ni kwake.
Je, Bwana Yesu alikuwa na sifa hii? Katika tukio moja ambalo Yesu alionesha mamlaka yake ya Uungu kwa kusamehe dhambi na wakuu wa dini walioina hiyo kama kufuru kwani mwenye uwezo wa kusamehe dhambi ni Mungu pekee kwa vile hata wao hawakufahamu mamlaka ya Yesu ni Mungu
Marko.2:5-11
Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao, Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu? Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu? Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende? Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza), Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.
Hili ni mojawapo ya matendo ya Yesu kusamehe dhambi aliyotenda kuonesha Uungu wake na mamlaka yake.
Sura ya 4
Ubinadamu wa Yesu na sababu ya kuitwa Mwana wa Mungu toka mamlaka ya Uungu.
Ndugu mpendwa msomaji tutakubaliana kuwa hilo ni moja kati ya maswali nyeti yanayoulizwa na watu wengi wanao hoji na kutafiti mamlaka haswa ya Bwana Yesu.
“Ubinadamu wake”
Chanzo cha maswali yote yanayo ulizwa juu ya Bwana Yesu kinaanzia mara tu Yesu alipovaa mwili wa kibinadamu tendo hilo kwa fikra za haraka tu linaweza kudhaniwa kuwa ndilo linaloshusha mamlaka yake ya asili kama Mungu. Pamoja na hayo mimi binafsi nichoelewa ni kuwa tendo hilo kamwe halishushi mamlaka bali linafunika mamlaka aliyokuwa nayo kwa kadri ya sababu…………
Ifuatayo:-
Mungu aliwahi kujifunua wazi katika nyakati za nyuma na wanadamu wakaangamia
Fuatilia:- kutoka 19:20-21 Bwana akaushukia mlima, juu ya kilele cha mlima; Bwana akamwita Musa aende hata kilele cha mlima; Musa akapanda juu. Ndipo Bwana akamwambia Musa, Shuka chini, uwaonye watu wasije wakapasua njia waje kwa Bwana kutazama, kisha wengi miongoni mwao wakaangamia.
“swali la kujiuliza”
Je! Mungu aje katika hali gani ili mwanadamu aweze kuikabili?
“Jibu”
Ni lazima aje katika hali inayofunika uwazi wa mamlaka yake iliyo ya utisho kwa mwanadamu mdhambi.
Na anapokuwa katika hali ya ubinadamu ndipo anapoona njaa, kulia, kutembea, kusinzia na hali zote za ubinadamu anakuwa nazo na ndo maana Yesu ni Mungu 100% na mwanadamu 100%
Fuatilia kutoka 33:18,20 (Musa) Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako…. Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi
Sababu hiyo ya kimsingi ndiyo inayofanya Bwana Yesu kuchukua mwili wa kibinadamu kupitia Mariam kama tulivyo kwishaona. Hivyo mwili ya Bwana Yesu ulisitiri mamlaka kuu ya Uungu wake ambayo hainge kuwa busara kuufunua na kufanya binadamu kuangamia badala ya kuokolewa naye. Kwa kauli nyingine ni kuwa Mungu (Yesu) alitumia mwili huo ili kuwafikia waja wake kama tulivyoona hapo nyuma jinsi Mungu alivyojifunua hata kwa kichaka kwa kadri ya Qur-an tukufu. “Ubinadamu ni njia ya Mungu kusema na waja wake:”
Qur-an 42:51 ……….. Mungu husema na wajawake kwa njia ya:-
Ilhamu – sauti ya ndani ya moyo ya Mungu
Nyuma ya pazia – ishara ya kufunika mamlaka.
Kwa kadri ya Aya hiyo tunaona Qur-an ikitaja “Pazia” kama chombo cha mawasiliano ya Mungu kwa wanadamu, pazia hii umaanisha ni kitu kinachofunika ili kuzuia kuonekana kwa uhalisi wa jambo kwa lugha nyingine Mungu wakati Fulani huamua kufunika uhalisi wake kwa kujifunua nyuma ya “Pazia”.
“Pazia ni nini Kibiblia?”
Waebrania 10:20 ……….. ipitayo katika “Pazia” yaani mwili wake.
Katika Biblia Pazia huashiria mwili wa Bwana Yesu, hivyo hiyo ni njia ya kimawasiliano kati yake na binadamu inayofunika mamlaka yake ya Asili ya Uungu ili binadamu kumudu kukutana naye.
1Timotheo 3:16 Mungu alidhihirishwa katika mwili
Ebrania 10:5 Mwili uliniwekea tayari
Filipi 2:7 alijifanya hana utukufu …….. akawa na mfano wa mwanadamu.
Kwanini aitwe Mwana naye ni Mungu?
Tendo la Bwana Yesu kuitwa Mwana wa Mungu linaanzia kwenye chanzo cha kutwaa mwili.
Yohana 1:14 naye neno akafanyika mwili akakaa kwetu nasi tukaona utukufu wake utukufu
kama wa Mwana pekee atokae kwa baba …………..
Andiko hii linaonyesha hatua kuu mbili yaani:-
Kufanyika mwili
Kuitwa mwana atokae Mbinguni.
Sababu kuu
Tendo la Yesu kuamua kuchukua jukumu la kutuokoa lilimladhimu siyo kufunika Utukufu wake (Uungu ) tu kwa mwili bali pia kubadili kitambulisho chake cha mamlaka
“Fatilia mfano huu”
Maji yanaweza kugeuka katika hali mbalimbali katika kile ninachojua maji hayo mara yanapo badiri hali tu pia tendo hilo huambatana na kubadilli jina, yaani mfano maji yanapoganda hayaitwi tena maji bali huitwa barafu
Swali:- Je barafu si maji?
Jibu:- la barafu ni maji ila yamebadili asili kwa muda na baadae hurejea.
Sababu ya Bwana Yesu kuitwa mwana inatokana na kusudi lake tu la kuja Duniani Kutukomboa hivyo alifanyika barafu toka asili ya maji (alifaninyika mwana toka asili ya Uungu kama njia ya Ukombozi) lakini asili yake ya Uungu inabaki palepale.
Fuatilia ushauri mwingine juu ya Uungu wa bwana Yesu katika mafungu yafuatayo:-
Yohana 14:7-10……… aliyeniona mimi amemwona Baba
Tito 2:13 ……. Yesu Mungu mkuu na mwokozi wetu.
Yohana 20:28 Bwana wangu (Yesu) na Mungu wangu.
Ndugu mpendwa ninaamini hofu na mashaka ya moyo wako juu ya mada hii yamepingwa na uondolewa kupitia uchambuzi huu, fanya maamuzi yako leo kwa kujenga upya imani yako juu ya mamlaka ya Bwana Yesu kama tulivyo jifunza.
Hitimisho
Yesu ni Mungu na hivyo yeyote anayehitaji kwenda mbinguni, njia pekee na pekee tu ni Kristo Yesu-‘Matendo 4:12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

QURAN, ALLAH, MUHAMMAD, NA JIBRIL WANAKIRI KUWA YESU NI MUNGU KWASABABU ANAUMBA

ALLAH ANAULIZA KUWA, JE ALIYEUMBA NI KAMA ASIYE UMBA?
Surat An Nahl 17. Ati anaye umba ni kama asiye umba? Basi hebu, hamkumbuki?
Ndugu msomaji, hilo ni swali kutoka kwa Allah wa Waislam. Allah anataka ajibiwe, Je, aliye umba unaweza mlinganisha na asiye umba?
Ndugu zanguni, huu ni MSIBA MKUBWA sana kwa Waislam, maana Allah sasa anakiri kuwa, aliye umba hawezi kuwa sawa na asiye umba.
JE, ISA ALIWAI KUUMBA?
Ndugu msomaji wangu bilashaka umeanza kufunguka masikio kupitia Aya hiyo ya Quran katika Aya hiyo inaonekana orodha ya matendo makuu ambayo Bwana (Isa) anatangaza kuwa na uwezo wa kuyatenda bila shaka matendo hayo ikiwa umeyachunguza kwa makini, yanaonekana kuhusika na uwezo wa kiutendaji wa Mungu Mwenyezi, sasa hebu tufuatilie kwa makini.
Nukuu kwa muktasari Qur-an 3:49 Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia: Mimi nimekujieni na Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu, ya kwamba nakuundieni kwa udongo kama sura ya ndege. Kisha nampuliza anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ninakwambieni mnacho kila na mnacho weka akiba katika nyumba zenu. Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwi nyinyi ni wenye kuamini.
a) Nakuumbieni katika udongo kama sura ya ndege.
Bila shaka tendo hili hufanana fikiri na kile alichofanya Mungu pindi alipokuwa akimuumba Adamu maandiko yanaonyesha kuwa Mungu alifinyanga udongo na kumuumba Adamu vivyo hivyo Isa (Yesu) nae anafanya Uumbaji kwa kufinyanga udongo kwa sura ya ndege.
Ref: Mwanzo 2:7 Bwana Mungu akamuumba mwanadamu kutoka katika udongo wa ardhi
Qur-an 22:5…… tulikuumbeni kwa udongo mzee wenu Nabii Adamu ………
Hivyo Yesu anafanya tendo la Uumbaji kwa hatua zinazo fanana fika na kile alichofanya Mungu (kufinyanga udongo).
b) Kisha nampulizia mara anakuwa ndege.
Ndugu mpendwa yawezekana liletendo la kufinyanga udongo lisiwe na nguvu sana kwa wajenga hoja , lakini hapa ndipo panapo nishangaza zaidi Qur-an inapoonyesha wazi kuwa Isa aliweza kupulizia udongo nao ukapata uzima na kuwa kiumbe hai.
Wanasayansi huu ndio uumbaji na wanabaiolojia wamejitahidi kuumba na kutengeneza mtu lakini wamegonga mwamba inapofikia hatua ya kumfanya kuwa kiumbe hai, aweze Kutembea, Kunusa, kuona n.k
Lakini maandiko ya Qur-an ufunua siri hii ya ajabu, bilashaka tendo hili la kupuliza pumzi na kitu kikawa hai ndiyo uleta maana halisi ya Uumbaji na hili ndilo tendo linaloleta maana na uzito haswa unaofanya tendo hilo kuwa rasmi na kumhusu Mungu pekee.
Mafunuo ya Qur-an huonyesha kuwa tendo hilo haswa ndilo alilotenda Mungu alipokuwa akimuomba Adamu nalo ni tendo la kutoa uhai (Maisha) kwa kuomba.
Qur-an surat 15:28 Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.
Tunajua fika juu ya tabia ambazo Mungu umshirikisha mwanadamu na pamoja na ha yo zipo zile ambazo Mungu kamwe hawezi kumshirikisha mwanadamu, lakini katika andiko hilo tunaona Yesu akitenda kazi hiyo kuu yenye uhusiano kwa asilimia miamoja na uwezo wa Kiuungu bilashaka huyo Yesu anayo asili inayopita ubinadamu aliokuwa nao na siyo asili ya kawaida.
Je! Mbona Qur-an inasema aliumba kwa idhini ya Mungu?
Inawezekana ndugu msomaji wangu ukawa na swali la namna hiyo ndani ya moyo wako hebu niruhusu sasa niweze kuondoa mashaka uliyonayo.
Je! Neno kwa idhini humaanisha nini?
Katika tafsiri ya kawaida Neno “Idhini” humaanisha “ruhusa” au “Ukubali”
Hivyo Qur-an inapomnukuu Nabii Isa akisema kwa “idhini” inaleta maana tu ya ukubali, ruhusa toka kwa Mungu.
Swali:- je kwanini apewe ruhusa na hali yeye ni Mungu? Au Je kuna miungu wangapi?
Jibu:- katika mafunuo ya Biblia mara kadhaa Bwana Yesu ametumia kauli hiyo ya kuruhusiwa au kukubaliwa na Mungu (eg: Yohana 5:30) mara kadhaa Yesu alisema “ninenalo si neni yaliyoyangu nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo”
Kwanini aseme hivyo (kwa idhini)?
Kwa msingi ujio wa Yesu hapa Duniani ulimlazimu kufunika uwezo na mamlaka yake ya asili ya Kimungu, ilimpasa kumwelekeza mwanadamu kwa vielelezo hai vya kimwenendo, hali na mazingira hayo yalimfanya kujipa cheo cha chini mara kadhaa alipozumngumza na watu.
Rejea Qur-an 20:9-11 Mungu alijifunua kwa Musa kupitia kichaka cha moto bila shaka alichukua ufinyu huo ili kuwa Asili na mwanadamu.
Pamoja na hayo Bwana Yesu akuadhimu mara chache kufunua taratibu mamlaka aliyonayo kiasili, mfano ni pale aliposema.
Yohana 10:30 mimi na Baba tu umoja.
Kauli hiyo iliwafunulia mafarisayo juu ya mamlaka ya Yesu ya Kimungu, lakini haikuwa jambo rahisi kwao kukubaliana na hilo
na katika aya hiyo tunaona wakiadhimu kumpiga mawe kwa kujiita yeye ni Mungu.
Bilashaka Yesu alitambua saikolojia ya imani ya watu hao anaowajua hata mioyo, hivyo Yesu aliamua kushuka kwa kumtaja Mungu wanayemdhani kama Mungu aliye ng’ang’ana Mbinguni tu lakini kwa hakika hiyo ndiyo asili yake binafsi.
Ndiyo maana alisema kwa Idhini.
Katika wazo hilohilo ndiyo maana Yesu Utumia neno kwa “Idhini”alipenda watu watambue mamlaka yake katika utendaji wake zaidi kuliko katika maneno yake
Hata hivyo neno kwa “Idhini” halimaanishi kwa “uwezo” Idhini na uwezo ni mambo mawili yanayo tofautiana sana
Mfano:- wewe unaweza kupewa Idhini ya kuhubiri lakini usiweze (usiwe na uwezo ) wa kuhubiri hivyo idhini( ruhusa ) na uwezo nitofauti kulingana na maandiko tabia ya Yesu ihusuyo Uumbaji uonekana akiwa nayo katika asili (Yohana 1:1-3) hivyo ni tabia ya kiuwezo na mamlaka yake ya Kimbinguni kabla ya kujishusha na kuvaa ubinadamu (nitalieleza mbele kwaupana ) na kuja hapa duniani.
Neno idhini Isa (Yesu) analitumia anapo kuwa hapa Duniani kama sehemu ya hatua yake ya kujishusha na kutwaa ubinadamu kwaajili ya kuokoa, lakini bado tendo la uumbaji linarejea asili na mamlaka yake kama Muumbaji na si wa ndege tu bali Dunia kwa ujumla (Yohana 1:1-3)
Qur-an inampa cheo gani (Isa) kwa tendo la Kuumba?
Uandishi au kuchapaji mwandishi na mengineyo ya kimsingi.
Qur-an 16:17 …….Ati yeye aliyeumba (naye ni Mwenyezi Mungu) atakuwa sawa na wale wasio umba je hamkumbuki?
Andiko hilo la Qur-an linasema kuwa
– “Ati yeye aliyeumba (Mungu) atakuwa sawa na wasio umba”?
Jibu :- la” aliyeumba hawezi kuwa sawa wasioumba bali aliye umba anakuwa sawa na aliyeumba hivyo ikiwa Yesu aliumba je yeye ni nani?
Qur-an kamwe haimpi sifa au usawa kiumbe yeyote asiye na sifa inayohusika na Mungu, maana sifa inayomhusu Mungu haswa ile ya kuumba ndiyo humfanya Mungu kuitwa Mungu kamwe hawezi kupewa Mwanadamu.
Pamoja na hayo jambo la kushangaza ni pale Qur-an inapoo nekana kuweka wazi kuwa Nabii “Isa Ibn Mariam” naye alikuwa na sifa hiyo inayo mhusu Mungu maana naye aliweza kuumba
(rejea neno nakuumieni Qur-an 3:49)
Na kutokana na kile kichosemwa na aya tuliyoisoma punde Nabii Isa anaonekana kuwa sawa na Mungu au kwa lugha rahisi naya ufupi yeye ni Mungu Muumbaji aliye adhimu kuvaa ubinadamu, lakini ana mamlaka inapita huo ubinadamu (yeye ni neno, muumbaji).
Ndugu msomaji, leo tumejifunza kwa mara nyingine tena kuwa Yesu ni Mungu kwasababu aliumba Quran Sura 16 aya ya 17.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

Thursday, March 3, 2016

ALLAH ASEMA ISRAEL NI TAIFA BORA NA LA NEEMA KULIKO WALIMWENGU WOTE

1. Allah asema Israel ndio taifa la Mungu, Surat Al Baqara 47
2. Allah asema ardhi ya Israel ni ya Waisraeli, Soma Quran Surat Al Maida aya ya 21
3. Palestina yakatwa na haipo kwenye Quran
Ndugu wasomaji,
Huu ni Msiba kwa Waislam wanao pigia debe Wapalestina. Hivi kwanini Allah hakuitaja Palestina kwenye Quran yake? Lakini ameitaja Israel na Wairaeli?
Surat Al Jaathiya 16. Na hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu na hukumu na Unabii, na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote.
ALLAH ANASEMA KWA WAYAHUDI KUWA ARDHI YA ISRAEL IMETAKASWA NA IMEANDALIWA KWA AJILI YAO:
Allah (s.w.t.) amesema: Enyi watu wangu! Ingieni katika hiyo ardhi iliyotakaswa ambayo Allah amekuandikieni. Wala msirudi nyuma, msije mkawa wenye kukhasirika.(5:21)
Katika aya hapo juu, Allah anawaita Wayahudi kupitia Musa "WATU WANGU" zaidi ya hapo anawaambia kuwa Waende Israel kwenye ARDHI ILIYOTAKASWA, kumbe ata Allah anafahamu kuwa ardhi ya Israeli si ya Wapalestina. Ndugu msomaji, kwanini Allah anaiita ardhi ya Israel kuwa imetakaswa lakini hakuwai sema hivyo kwa Makka?
Ardhi hii imebarikiwa kiroho na kirutba. Ni jambo hili ndilo lililowafanya watu na staarabu tofauti kuigombania. Agano la Kale inatuhadithia ya kuwa ardhi hii ilibubujika asali na maziwa.(Hesabu, 13:27) Na katika kitabu cha Hesabu Sura ya 13 inatueleza kuwa WAISRAEL walipo kuwa wakitoka Misri walipata humo matunda ya makudhumani, tini na zaituni ambayo yalikuwa makubwa na kila tunda kubebwa na watu wawili.
Swali lamsingi: KWANINI ALLAH HAKUITAJA PALESTINA KWENYE QURAN YAKE?
Waislam, Allah kasema kwa Waisrel kuwa, WAINGIE KATIKA ARDHI ILIYOTAKASWA, sasa, kwanini nyie mnataka Wapalestina ambao hata Allah hawajui, wavamie ardhi ya Israeli?
Waislam wanawivu mkubwa sana kwa Israel kwasababu Allah amesema kuwa Israel ni ardhi iliyotakasika na hakusema kuwa Uarabuni kumetakasika. Huu ni MSIBA kwa Waislam.
ALLAH ANASEMA:
SURAT AL BAQARA 40. Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni neema yangu niliyo kuneemesheni, na timizeni ahadi yangu, na Mimi nitatimiza ahadi yenu, na niogopeni Mimi tu.
Allah anaendelea kusema kuwa Israel wana neema ya Mwenyezi Mungu, lakini hatusomi Palestina ikitajwa hata sekunde moja, wala hatusomi kuwa Waarabu wameneemika.
ALLAH ANASEMA KUWA ISRAEL NI ZAIDI YA WAARABU WOTE
Surat Al Baqara 47. Enyi Wana wa Israili! Kumbukeni zile neema zangu nilizo kuneemesheni, na nikakuteuweni kuliko wote wengineo.
ALLAH ANAKIRI KUWA AMEWATEUWA WAISRAELI KULIKO WATU WENGIENEO, IKIWEPO WAARABU, KUMBE NDIO MAANA WAARABU WANA CHUKI KUBWA KWA WAISRAELI KWASABABU WAO HAWAKUTEULIWA
Kama ulivyo soma hapo juu, Israel ina neema na ni zaidi ya wengine wote, pamoja na Palestina. Kumbe ndio maana Waarabu hawana ubavu kwa Israel.
Leo ningependa muelewe kuwa, Israel ni nchi iliyo barikiwa na hata Waarabu wafanye nini, hata Allah wao amekiri kuwa Waarabu wataendelea kufuata mkia kwa Israel mpaka Kiyama.
ALLAH KAWAPA ISRAEL KITABU, HUKUMU NA UNABII NA KUWAFADHILISHA KULIKO WALIMWENGU WOTE
Surat Al Jaathiya 16. Na hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu na hukumu na Unabii, na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote.
Kumbe Israel wamepewa Unabii, Kitabu na Hukumu. Hii ndio sababu Waraabu wanaendelea kusaliti amri kwa Israel.
Kwanini Allah hakuitaja Palestina kwenye Quran?
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

MUHAMMAD AKIRI KUPATA UTUME KWA KUCHEZEWA NAFSI YAKE NA SHETANI

Ndugu msomaji,
Kwanza ningependa tujifunze maana ya neno Nabii:
Nabii ni mtu gani?
Nabii ni mtu aliyeteuliwa rasmi kwa vigezo vya Kiungu ili kuleta ujumbe wa Mungu kwa wanadamu, kwa maneno mengine nabii ni msemaji wa siri za Mungu.
Mitume wote na manabii wote wa Biblia waliwai ongea na Mungu. Lakini, Mtume wa Allah "Muhammad" hakuwai ongea na Mungu HATA MARA MOJA. Je, utume wake tutauamini vipi maana hakuwai ongea na aliye mtuma?
Kama Muhammad alikuwa Mtume wa Mungu, kwanini hakuongea na Mungu aliye Mtuma? Maana ya neno Mtume kwa kifupi: Ni Mtu aliye tumwa.
HEBU TUANGALIE, HUYU MUHAMMAD ALIZALIWAJE NA KUUPATAJE UTUME WAKE?
1. MUHAMMAD ALIKUWA NA SHETANI TANGU KUZALIWA KWAKE,
Abu Huraira (r.a) amesimulia kuwa "Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa na shetani tangu alipozaliwa, (Fat'hul Baary Juzuu ya 6 Uk. 389).
Je, kuna ushahid wowote ule kuwa Muhammad alitolewa Shetani ALIYE KUWA NALO TANGU KUZALIWA KWAKE? Kama upo Basi Waislam, tuleteeni tuuone.
2. MUHAMMAD AKIRI KUPINGWA NA KUBANWA MBAVU ZAKE NA KIUMBE AKIWA PANGONI,
Katika kitabu kiitwacho: Maisha Ya Nabii Muhammad s.a.w uk 16-17 kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy, tunasoma kama ifuatavyo;-
Hata siku moja- katika mwezi wa Ramadhani mwezi 17, Jumatatu katika mwaka wa 40 ½ wa umri wake- mtume alimwona mtu kamsimamia mbele yake bila ya kumwona wapi katokea, akamwambia; “soma”. Mtume akamjibu; “Mimi sijui kusoma kwani sijapata kujifundisha kusoma.” Akaja akamkamata akambana, akamwambia tena; “soma,” Mtume akamjibu jawabu yake ileile. Hata mara ya tau akamwambia; “soma- Iqraa Bismi Rabbik.” Akamsomea sura hiyo ya 96 mpaka kati yake. Kisha mtume akaisoma kama alivyosomewa. Hii ndiyo sura ya kwanza kushuka katika Qur’an, ingawa haijawekwa mwanzo.
Mara, yule mtu (Malaika) akaondoka machoni mwake- asimwone kenda wapi. Na mtume naye akarejea kwake-khofu imemshika. Alipofika nyumbani, Bibi Kadhija alidhani ana homa, akamfunika maguo gubigubi na akakaa mbele yake akimsikiliza anavyoweweseka. Hata homa ilipomwachia alimweleza Bibi Kadhija yote yaliyomtokea; na Bibi Kadhija akamtuliza moyo wake, akamyakinishia ya kuwa hapana lolote baya litakalomzukia. Mara bibi huyu akaondoka akenda kwa jamaa yake – Bwana Waraqa bin Naufal- akampa habari yote iliyompata mumewe. Naye akamwamrisha amwite. Na mtume akenda akamweleza habari yake yote. Bwana Waraqa akamwambia; “ Huyo ndiye Jibril aliyemshukia Nabii Musa na Nabii Isa. Basi jibashirie kuwa wewe ni mtume wa umma huu, nami natamani kuwa hai nikuone unavyosimama kuwatengeneza jamaa zako; Inshaallah nitakuwa mkono wako wa kulia” Wakarejea kwao na khofu yote imemtoka”.
Alipokuwa pangoni alichezewa na Shetani: Katika kitabu kiitwacho “ Wakeze Mtume Wakubwa Na Wanawe” kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al Farsy uk.12 tunasoma maneno haya
3. MUHAMMAD AKIRI KUCHEZEWA NAFSI YAKE NA SHETANI
“Basi Mtume akafanya hofu akarejea kwa mkewe akamhadithia; na pale pale homa kubwa kabisa ikampanda akataka afunikwe maguo. Mara akawa anatetemeka kwa nderema na anaweweseka na kusema “Najikhofia nafsi yangu kuchezewa na Shetani na kuniharibu akili yangu na kunizuga”. Bibi Khadija palepale alimdakiza akamwambia; “ Wacha hayo; Siyo yatakayokuwa hayo. Wewe huwezi kuchezewa na mashetani. Shetani hawezi kumchezea mtu mwenye sifa zako. Wewe unatazama vyema jamaa zako, unachukuwa mizigo ya hata watu wasiokuwa wako, unawadhihirishia watu sifa zako nzuri ambazo hakuna mwenye nazo. Unafanya hivi na unafanya hivi. Furahi ndugu yangu. Tua moyo wako, Wallahi! Mimi naona umekwishakuwa mtume”.
Katika tukio hili lililompata Muhammad akiwa pangoni , ndipo Waislamu wote ulimwenguni wanapolieleza kuwa hapo ndipo Muhammad s.a.w alipoletewa wahyi (ufunuo) na kupewa unabii na utume. Lakini unapotafakari juu ya ujumbe huo utaona kuwa hata yeye mwenyewe hajui nini kilichokuwa kimemtokea kule pangoni. Ndiyo maana tunasoma kuwa alipofika nyumbani kwake mkewe Bi. Khadija alimfunika nguo mumewe akidhani ana homa. Muhammad alimweleza mkewe kilichomtokea kuwa ni “Shetani” hakumsema malaika yeyote kama Waislamu wanavyotaka kutuaminisha leo. Kwa sababu kama angekuwa ni malaika kama tunavyosoma ndani ya Biblia ,asingesita kujitambulisha kwa Muhammad kuwa yeye ni nani.
KUFUATANA KITABU CHA MAISHA YA NABII MUHAMMAD, tunajifunza kuwa Muhammad kwa mara ya kwanza kabisa alipata utume wake pangoni baada ya NAFSI YAKE KUCHEZEWA NA MASHETANI.
Wahyi (ufunuo) uliokuja kwa Muhammad alisikia makengele, uso kuwa mwekundu, jasho kumtoka. Katika Bukhar, Hadithi na 2, Juzuu na 1,Al-Lu’lu Kitabu cha 3.Uk. Na.874 Hadithi na 1505 “Hadithi ya Aisha r.a mama wa waumini amesema, kuwa Al Harith ibn Hisham r.a alimuuliza mtume wa Allah s.a.w ‘ Ewe mtume wa Allah hivi wahyi (ufunuo) hukujia vipi?’ Mtume wa Allah s.a.w akajibu, “ Wakati mwingine hunijia kama mlio wa kengele, na aina hiyo ndiyo ngumu zaidi kwangu, inaondolewa hali hiyo kwangu wakati tayari nimeshapata wahyi. Na nyakati nyengine malaika anakuja kwangu akiwa katika mfano wa mtu, kwa hiyo ananieleza na ninayazingatia aliyoyasema.” Aisha r.a alisema , Na hakika nilimwona unamshukia wahyi siku ya baridi kali na ilipomuondoka hali hiyo, paji lake la uso lilichuruzika jasho.”
Muhammad akiwa Medina aliulizwa na Wayahudi ikiwa ufunuo wake umetoka kwa Mungu wa Kweli kwa kumtaka atoe sifa za manabii. Akijibu swali hilo alisema:
Mkweli Mwaminifu Juzuu 3-4 Uk.63.Hadithi Na. 880. “Kasema Mtume (s.a.w):- (Mambo) mane ya sheria za mitume (Kuwa na) na haya,na kujipaka mafuta mazuri,na kuowa (wake),na kupiga mswaki.
Hizi si sifa za Ki-Mungu kwa nabii na mtume bali ni za kibinadamu tu.
4. QURAN INASEMA KUWA, NABII LAZIMA AFANYE MIUJIZA; MUHAMAMD AKIRI KUWA YEYE NI MTUME BANDIA NA HAKUFANYA MIUJIZA
Qur’an nayo inathibitisha kuwa manabii na mitume ni lazima wafanye miujiza.
Qurani 40:78 Suratul Al-Muumini [Waumini] inasomeka “Na kwa yakini tumewatuma mitume kabla yako wengime katika wao tumekusimulia (majina yao na habari zao) na wengine hatukukusimulia na haikuwa kwa mtume yoyote kuleta muujiza wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu”
Muhammad hakupewa kufanya muujiza wowote ili kuthibitisha madai ya unabii na utume wake.
Qur’an 29:50 Suratul Al-Ankabuut (Buibui). “Na walisema “Mbona hakuteremshiwa miujiza kutoka kwa Mola wake? Sema miujiza iko kwa Mwenyezi Mungu tu (akitaka atakuteremshieni na kama hataki basi),nami hakika ni mwonyaji mbainishaji (dhahiri tu).” (Taz. Qur,an 6:35-37 13:7,)
MASWALI:
(i). Kama Jibril ndie alitumwa na Allah, na huyo Allah ni Mungu, kwanini Muhammad alisema kuwa nafsi yake imechezewa na MASHETANI baada ya kukutana na Jibril?
(ii). Kama Jibril alitoka kwa Allah, kwanini Muhammad alipo toka pangoni alisema kuwa Jibril AMEMZUGA AKILI YAKE?
(iii) Je, wapi katika Injili au Taurat au Zaburi tunasoma kuwa Manabii na Mitume katika Biblia walipata kwa njia ya homa na kukiri kuchezewa na mashetani kama Muhammad wa kwenye Quran?
(iv) Kama Muhammad alikuwa Mtume wa Mungu, kwanini hakuongea na Mungu aliye Mtuma? Maana ya neno Mtume kwa kifupi: Ni Mtu aliye tumwa.
3. KUROGWA KWAKE MUHAMMAD
Zaidi ya hayo tunaona Muhammad alirogwa. Kurogwa ni hali ya mtu kuathirika na nguvu za giza yaani uchawi. Je nabii au mtume wa Mwenyezi Mungu wa Kweli anaweza kurogwa?
Amesema Mwanaisha Mkewe Mtume kuwa "Yahudi Mmoja aitwaye Labiid bin Al'answan alimroga Mtume Muhammad, ikawa Mtume baadhi ya Nyakati huchanganyikiwa na kuanza kuita Ovyo ovyo na kupiga makelele. (Sahih Muslim J. 4 uk. 38-39)
Hii ni uthibitisho mwingine mzito unaoonesha kuwa utume wa Muhammad una utata.
MASWALI:
(a) Hivi, kuna Mtume au Nabii yeyote yule ambaye alikiri kurogwa kama Muhammad?
(b) Hivi Allah alikuwa wapi wakati Muhammad anarogwa? [Ingawa Quran inakiri kuwa aliye teremsha uchawi/urogi ni Allah]
(c) Wapi tunasoma kuwa Muhammad aliombewa na kutoa huo uchawi/urogi aliofanyiwa na Labiid bin Al'answan?
YAANI INA MAANA MUNGU ALIKOSA MTU WA KUTUMA MPAKA ATUME MTU ALIYECHEWA NA MASHETANI KAMA HUYU?
Ndugu msomaji,
Muhammad hakuwa Mtume wa Mungu na wala hana sifa za KITUME.
1. Muhammad hakuwai ongea na Allah aliye mtuma.
2. Muhammad alikuwa na Shetani tokea kuzaliwa kwake.
3. Muhammad alikiri kuchezewa na Shetani wakati wa kusimikwa utume wake Pangoni.
4. Muhammad alikiri kuwa Shetani amechezea akili na nafsi yake.
5. Muhammad alikiri kuwa alirogwa na Labiid bin Al'answan.
SASA WAISLAM, NIONYESHENI, wapi kwenye Taurat, au Zaburi au Injili kama kuna Mtume aliye na sifa za ajabu kama za Muhammad.
Karibuni kwa Yesu ambaye ndie Njia Pekee ya Kwenda Mbinguni.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

Ancient Jewish Wedding Ceremony: “No man knows the day or hour, only the Father”

  The Ancient Jewish Marriage Rite: A Detailed Exposition of Betrothal, Preparation, and Consummation Dr. Maxwell Shimba Shimba Theological ...

TRENDING NOW