Friday, June 9, 2017

ALLAH HAJUI HISABATI NA AU HESABU

No automatic alt text available.
Jambo ambalo linathibitisha kuwa Allah sio Mwenyezi Mungu, ni makosa makubwa ya kimahesabu katika Quran yake anayo dai kuiteremsha kwa Muhammad kwa usaidizi wa Jibril.
Sheria zake za mirathi zimegawanywa katika sura kadhaa kama Al Bagarah, Al Maidah, na Al Anfah. Lakina kwa undani zaidi zimewekwa katia Surat Al Nisaai.
Surat An Nisaai 11. Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu: Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili. Na ikiwa wanawake zaidi ya wawili, basi watapata thuluthi mbili za alicho kiacha maiti. Lakini akiwa mtoto mwanamke ni mmoja, basi fungu lake ni nusu. Na wazazi wake wawili, kila mmoja wao apate sudusi ya alicho kiacha, ikiwa anaye mtoto. Akiwa hana mtoto, na wazazi wake wawili wamekuwa ndio warithi wake, basi mama yake atapata thuluthi moja. Na akiwa anao ndugu, basi mama yake atapata sudusi. Haya ni baada ya kutolewa alicho usia au kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu, nyinyi hamjui ni nani baina yao aliye karibia zaidi kwenu kwa manufaa. Hiyo ni Sharia iliyo toka kwa Mwenyezi Mungu. Bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima.
Surat An Nisaai 12. Na fungu lenu ni nusu walicho acha wake zenu ikiwa hawana mtoto. Wakiwa na mtoto basi fungu lenu ni robo ya walicho acha, baada ya wasia waliyo usia au kulipa deni. Na wake zenu watapata robo mlicho kiacha, ikiwa hamna mtoto. Mkiwa mna mtoto basi sehemu yao ni thumni ya mlicho kiacha, baada ya wasia mlio usia au kulipa deni. Na ikiwa mwanamume au mwanamke anaye rithiwa hana mtoto wala wazazi, lakini anaye ndugu mume au ndugu mke, basi kila mmoja katika hawa atapata sudusi. Na wakiwa zaidi kuliko hivyo basi watashirikiana katika thuluthi, baada ya wasia ulio usiwa au kulipa deni, pasio kuleta dhara. Huu ndio wasia ulio toka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mpole.
Surat An Nisaai 176. Wanakuomba uhukumu, sema: Mwenyezi Mungu anakupeni hukumu juu ya mkiwa. Ikiwa mtu amekufa, naye hana mtoto, lakini anaye ndugu wa kike, basi huyo atapata nusu alicho acha maiti. Na mwanamume atamrithi ndugu wa kike ikiwa hana mwana. Na ikiwa wao ni ndugu wa kike wawili, basi watapata thuluthi mbili za alicho acha maiti. Na wakiwa ndugu wanaume na wanawake, basi mwanamume atapata sehemu iliyo sawa na ya wanawake wawili. Mwenyezi Mungu anakubainishieni ili msipotee; na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Ingawa Allah anasema kuwa, ameziweza hizo sheria kiuuwazi na bila ya shaka, lakini unapo zisoma hizo aya, zote zimejaa shaka na kuchakuana.
Quran 4:11 inasema kuwa akiwa mtoto mwanamke ni mmoja, basi fungu lake ni nusu. Lakini aya hiyo hiyo inadai kuwa Kaka mtu atapata mara mbili ya mwanake, kimahesabu, Kaka mtu atachukua kila kitu. Huu ni msiba wa kimahesabu kwa Allah.
Zaidi ya hapo, unapowahusisha Wazazi wa kike katika hiyo mirathi, Allah anawaacha solemba, maana mahesabu yanakuwa magumu kwake.
Ndio maana nauliza, hivi, ni nani alimfundisha hesabu na au hisabati Allah?
HUU NI MSIBA MKUBWA SANA KWA WAISLAM.

1 comment:

Unknown said...

Ukiandika bila kujua ndio utajipa mashaka, soma elewa ndio uandike. Usiandike tuu kwa sabab unachukia. Mf mdogo tu, akisema akiwa mtoto wa kike pekee atapata nusu imemaanishwa ikiwa mtoto ni mmoja tu wa kike ndio alieachwa na marehem bas atapata nusu. Calm down, understand ndio uandike

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW