Friday, July 8, 2016

JE, BIBLIA INARUHUSU KULA NYAMA YA NGURUWE?Ndugu msomaji,
Katika hili somo, tutajifunza kuhusu ulaji wa Nyama ya Nguruwe na kwanini Wakristo wanakula Nyama ya Nguruwe.
Tuanze moja kwa moja kwa kusoma aya za Biblia:
Biblia inasema kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna kiumbe cha kukataliwa, kama kitapokelewa kwa shukrani, kwa kuwa kimetakaswa kwa Neno la Mungu na kwa kuomba { 1 Timotheo 4:4-5}
Kama hakuna kiumbe cha kukataliwa maana viumbe wote ni vizuri sasa ubaya wa nguruwe ni nini? Kama hacheuwi hii ndio sababu ndio Mungu ametaka awe hivyo!
SASA TUANZE NA KITABU CHA MWANZO. JE NGURUWE ALIRUHUSIWA KULA?
Bwana Mungu akambariki Nuhu na wanawe ,akawambia Zaeni ,mkaongezeke ,mkaijaze nchi, kila mnyama wa katika nchi watawaogopa ninyi na kuwahofu ,na kila ndege wa angani pamoja na viti vyote vilivyojaa katika ardhi,na samaki wote wa baharini vimetiwa mikononi mwenu ,kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu ,kama nilivyowapa mboga za majani ,kadhalika hivi vyote ,balo nyama pamoja na uhai ,yaani damu yake msile" {Mwanzo 9:1-4}
Ndugu msomaji wangu maandiko yamefunua wazi kwamba Mungu alitoa Wanyama wote kuliwa baada ya mboga za majani walakini hatuoni Mungu akitoa sheria ama akiwabagulia Wanyama wa kuliwa yaani walio safi na wasio safi, bali maandiko yametuonyesha kuwa Mungu alitoa wanyama wote kuwa chakula kwa Wanadamu.
Je sheria inayohusiana na Wanyama safi na wasio safi ilitolewa wapi?
Ndugu msomaji kama ambavyo nilivyokwisha kutangulia kusema kuwa sheria hii inayohusiana na vyakula haikutolewa tangu mwanzo kwa ushaidi wa andiko ambalo nimekupa limeonyesha hivyo,swali la lini sheria hii ambayo ilihusiana na vyakula ilitolewa maandiko yapo wazi kabisa eneo ilo ni baada ya wana Israel kutolewa utumwani Misri ndipo tunaona katika Biblia sheria inayohusiana na Wanyama walio safi na wasio safi kwaiyo kabla ya hapo wanyama wote walikuwa chakula { Mambo ya Walawi 11 :1-7} kupitia fungu ili la Biblia tunaona kuwa Mungu anatoa sheria inayohusiana na wanyama wanaopaswa kuliwa na wasiopaswa kuliwa ?
Ni kweli kabisa Mungu alitoa hiyo kuwa ni sheria kwao wana wa Israel walakini tusiishie tu hapo katika kuangalia sheria kuwa ni sheria tusafiri pamoja kifikra, utakumbuka kuwa watu ambao kiasili sio wayahudi walikuwa hawana desturi za usomaji wa Torati? Je hii sheria iliyohusiana na Wanyama safi na wasio safi ilifahamika kwao? Bila shaka jibu ni hapana labda utajiuliza kwanini? Napenda tujifunze ili jambo na kutokuacha historia ya vizazi pia na chanzo cha kusambaa kwa wanadamu duniani kote..
Theolojia inatueleza kwamba vizazi vya ulimwengu huu vimetokana na wana watatu wa Nuhu ambao ni Shemu, Hamu, na Yafethi sasa katika historia ya chanzo cha mataifa mbalimbali kama inavyoelezwa kwamba wanadamu yaani mataifa yote yaliotokana na watoto wa Nuhu walikuwa wakiishi pamoja na walikuwa na lugha moja na usemi mmoja na waliishi pamoja, wanadamu hawa ikumbukwe kwamba hawakupewa sheria yoyote inayohusiana na wanyama wapasao kuliwa na wasiopaswa hawakupewa na hapa tunaelezwa ndio chanzo cha mataifa mbalimbali maana baada ya Mungu kuwachafulia lugha walisambaa kila mmoja mahali pake ( Mwanzo 11:1-9} Sasa swali la kujiuliza je wanadamu hawa waliondoka na ufahamu upi kuhusiana na vyakula, kwamba nguruwe haramu ama? Maana ifahamike kuwa kwao walipewa wanyama wote kuwa chakula kwa sababu hawakuwa na sheria inayohusiana na vyakula safi na visivyo safi kwao wanyama wote ni safi tu waliondoka na imani hiyo kama walivyopokea huu ndio ukawa mwanzo wa mpishano wa vyakula baina ya watu walioitwa wa mataifa na wayahudi baada ya wao kupewa sheria iliyohusiana na wanyama walio safi na waschakula.
Wayahudi walipata tabu sana kushiriki katika kalamu za watu ambao kiasili hawakuwa wasomaji wa torati na kuishi katika nchi zao, kwa sababu walipishana katika desturi za vyakula ,wayahudi hata wale ambao walikuja kuwa wafuasi wa Kristo walipata ugumu mno katika eneo ilo, sababu wao wayahudi walipewa sheria kuhusiana na wanyama safi na wasio safi ila mataifa kwao wanyama wote walikuwa safi sasa mtume Paulo hali akiwa na ufunuo wa Kimungu aliwaeleza wale wayahudi waliokuwa wakristo zama zile na walikuwa wakiambatana na mitume katika uinjilisti alisema maneno haya.
"Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni,bila ya kuuliza uliza kwa ajiri ya dhamiri, maana ,dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo, mtu asiyeamini akiwaalika ninyi mnataka kwenda ,kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila ya kuuliza -uliza kwa ajili ya dhamiri" { 1 Wakorintho 10:25-28}.
Kwanini mtume Paulo awaagize wale kila kitu ikiwa wapo wanyama waliozuiliwa je alikuwa anapingana na Mungu? Lah hasha! hakuwa akipingana na Mungu ,bali Mtume Paulo alifahamu kesi kuhusiana na vyakula Yesu aliye kielelezo cha imani yetu aliitatua kupitia Marko 7 :15-19 pale alivyovitakasa vyakula vyote, akamaliza utata huo, hivyo baada ya hapo kila chakula kilikuwa halali kuliwa rejea tena kusoma Mwanzo 9:1-4
Biblia inasema viumbe vyote ni safi unganisha na Mwanzo 9:1-4 upate maana halisi, hivyo kula nguruwe sio dhambi ni halali kabisa
Sio vyakula ambavyo vinatuudhurisha mbele za Mungu tunakula kwa ajili ya miili yetu sio kwa ajili ya Mungu (Warumi 15:17 na Marko 7:15-19)
Hakuna kosa kula Nguruwe kwa mujibu wa Agano Jipya asanteni mbarikiwe nyote.
Mungu awabariki sana.
By permission and sources: Pastor Samuel J. M, Christ Nations Org, Max Shimba Ministries Org, NKJV, Gideon Bible 1960, Green Island Tabernacle, Word of Faith Mission.
Ni mimi Dr. Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo, Mungu Mkuu 
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW