Tuesday, August 1, 2017

YESU ALIJIITA MUNGU MBELE YA WAYAHUDI

Image may contain: one or more people and text


YESU alijita-mbulisha kwao kuwa ni MUNGU lakini hawakuelewa
Yohana 10:30-33 “Yesu akawajibu, kazi njema nyingi niwewaonyesha zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe? Wayahudi wakamjibu, kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwasababu wewe uliye.mwanadamu wajifanya kuwa Mungu.
Wayahudi walisema anakufuru kwa kusema kuwa yeye ni Mungu.
Kimsingi Yesu ndiye Baba mwenyewe ndio maana anasema huwezi kumtenganisha na Baba; ukimwona yeye umemuona Baba.
Yohana 14:7-9 Katika mstari 8 na 9 Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba yatutosha. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote,wewe usinijue, Filipo?
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

God

  Theology 101 When we attempt to conceive what God is like, we are immediately confronted with the limitation of human imagination, for ou...

TRENDING NOW