Wednesday, February 10, 2016

WASABATO WANASEMA KUWA YESU KRISTO NDIE MALAIKA MIKAELI


Kanisa na Imani au dini ya Wasabato inafundisha kuwa Yesu Kristo na Malaika Mkuu Mikaeli ni mtu mmoja. Hata hivyo, watu wengine kimakosa wanafikiria kuwa SDA wanafundisha kuwa, Yesu ni Malaika aliye umbwa, na kwahiyo hakuwa mtakatifu "divine" . Lakini, hivyo sio Wasabato wanavyo amini. Badala yake, wanasema katika Agano la Kale kuwa, udhihirisho wa Malaika Mkuu Mikaeli ulikuwa ni utambulisho wa Yesu Kristo kabla hajaja duniani na kwamba Malaika Mkuu Mikaeli hakuumbwa. KATIKA MADAI HAYA, wamekosea katika kulinganisha kwao, lakini katika kukubali kuwa hana na hakuumbwa, wanakubali kuwa Yesu ni Mungu.

Hebu tosome Biblia kwanza:
Yohana 8: 58 Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.

Hapa kuna matatizo makubwa kwa Wasabato, kwasababu neno la Kigiriki ego eimi linamaanisha " MIMI NIKO". Hili neno liliwafanya Wayahudi wachukie sana , pale Yesu alipo sema yeye ni NIKO "I AM" kiasi cha kutaka kumuua kwasababu alikua anatumia aya ya KUTOKA 3:14 pale Mungu alipo sema kuwa Jina lake ni NIKO" 14 Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; ["akasema,Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli;MIMI NIKO amenituma kwenu"]. Angalia vile vile katika Yohana 10: 30-33 kwa uhakikisho wa haya maneno.

Wasabato wanakubali kuwa Yesu ni Mungu, lakini kigeugeu chao kinawafanya wawe sawa na Mashahidi wa Jehovah na kupingana na aya za Biblia Takatifu na kualzimisha kuwa eti, Malaika Mkuu Mikaeli ni Yesu.


DAI LA KWANZA LA WASABATO KUWA YESU NI MALAIKA MIKAELI
1 Wasesalonike 4: 16 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.

Wasabato wanafurai sana hii aya, kwa kuweka ufafanuzi wa kithiolojia. Wasabato wanafundisha kuwa Yesu Kristo ni Malaika Mkuu Mikaeli, na hivyo kubadilisha maana halisi ya hii aya ili kusaidia theolojia ya imani yao kuwa Yesu ni Malaika Mkuu Mikaeli. Madai ya Wasabato ni makosa maana wanaizuia Biblia kuzungunza katika context/mazingira yake.

HOJA::::
Katika aya hapo ju, ipo wazi kuwa: Moja, Bwana atashuka, Pili, tunasoma kuhusu sauti ya Malaika Mkuu. Tatu, Tunajifunza kuwa kumbe Bwana wetu Yesu sio Malaika Mkuu, maana hiyo aya imewatenganisha hao wawili.


DAI LA PILI LA WASABATO KUWA YESU NI MALAIKA MIKAELI
Yuda 1: 9 Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.

Huu ni mfano mwingine wa thiolojia ya Wasabato inayo linda dai lao la Yesu ni Malaika Mikaeli. Ukizungumza kwa kutumia Biblia, YESU SIO MALAIKA MIKAELI. Hao ni wawili tofauti kabisa, na kuwaunganisha na kusema kuwa Yesu ni Mikaeli ni MAKOSA ambayo Wasabato wanafanya kwa kutengeneza hii aya ili isaidia thiolojia yao.

HOJA:::::
KATIKA AYA HAPO JUU, tunajifunza kuwa Malika Mkuu anasema kuwa NUKUU "Bwana akukemee" Sasa inafahamika kuwa Yesu ni Bwana. kivipi basi Mikaeli aseme Bwana akukemee kama yeye ndie huyo huyo Bwana Yesu? Kwanini hakusema NAKUKEMEA......



DAI LA TATU LA WASABATO KUWA YESU NI MALAIKA MIKAELI
Ufunuo 12:7 Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;

Ona tena hapa, jinsi Wasabato wanavyo itumia thiolojia kusaidia dai lao la Yesu ni Malaika Mikaeli. Hii haya haisemi hivyo wala saidia thiolojia ya Wasabato kuwa Yesu ni Mikaeli.

HOJA::::
Hiyo aya hapo juu inazungumzia Malaika Mikaeli akipigana na Joka, na ahakuna sehemu yeyote ile inamzungumzia Yesu.



BIBLIA INAKUJIBU KAMA IFUATAVYO
Waebrania 1: 5 Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?

Mungu Baba katika Waebrania 1: 5 anauliza, wapi kasema katika Biblia kwa Malaika yeyote yule kuwa wewe ni Mwanangu? Mungu anapinga dai la WASABATO KUWA Malaika Mkuu Mikaeli ni Yesu. Mungu anasema kuwa hajawai muita Mailaka yeyote yule kuwa yeye ni Mwanae.

MUNGU ANAENDELEA KUSEMA katika Waebrania 1 aya 13 Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote, Uketi mkono wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?

Hatusome sehemu yeyote ile kuwa Malaika Mkuu Mikaeli aliambiwa akae mkono wa Kuume wa Mungu Baba. Hivyo basi, dai la Wasabato kuwa Yesu ni Malaika Mikaleli limeshindwa kwa mara nyingine hapa.

MUNGU ANAWAAMURU MALAIKA WOTE WAMSUJUDU YESU
Waebrania 1: 6 Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu malaika wote wa Mungu.

Je, katika hiyo aya ya 6, ni nani huyo anaye sujudiwa? Hakika Biblia ipo wazi na inapinga thiolojia ya Wasabato kuwa Yesu ni Malaika Mkuu Mikaeli.

Max Shimba

For Max Shimba Ministries Org

JE, NI HAKI KWA MKRISTO KUSALI (KUOMBA) JUMAPILI?

(SEHEMU YA PILI)

Ndugu msomaji:

Katika ujumbe wa leo, nitawaletea ushahidi mbali mbali unao sema na au mruhumsu Mkristo kusali Jumapili kama ulivyo wekwa na shahidiwa katika Agano Jipya.

Ushahidi wa kubadilika kwa siku ya kusali unaweza kuuona mapema sana katika Agano Jipya. Agano Jipya lina ushahid mwingi sana ambao unasema kuwa SIKU YA SABATO haina nguvu tena na au si Sheria tena kusali Siku ya Saba ya Wiki.


SIKU ZOTE NI ZA BWANA MUNGU
Warumi 14: 5-6 inasema: 5 Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.
6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.

Ni vyema kuisoma Sura nzima ya Warumi 14, ingawa kuna ushahid mkubwa kuanzia aya ya 1 mpaka ya 12. Hata hivyo, maelekezo hapa ni kwa mtu binafsi kuamua katika akili yake ni siku ipi aitunze na au aitumie kusali na kumwabudu Bwana Mungu. Kwasabau hiyo, basi chaguo ni la Mtu na sio Mungu.


SABATO IMESEMWA NI KIVULI. YESU NDIE SABATO
Wakolosai 2: 16-17 inasema: 16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
17 mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.

Angalia kwa makini hapa jinsi siku zilivyo orodheshwa. Sikukuu huwa ni ya Kimwaka, Mwandamo wa Mwezi ni ya Kimwezi, Sabato ni ya Kiwiki. Hakuna mwenye ruhusa ya kuhukumu katika hili. Sabato imesemwa ni KIVULI. Ukweli kamili ni Yesu. Yesu ndie Sabato yetu.


WALIKUTANA SIKU YA KWANZA YA JUMA
Matendo ya Mitume 20 aya 7 Inasema: 7 Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.

Siku ya Kwanza ya Juma ni Jumapili, na hii ni siku ambayo watu walikusanyika na Kumwabudu Bwana Mungu. Hivyo basi, hii aya inaweza kuonyesha kuwa Kanisa lilikutana/kusanyika siku ya Jumapili.

Katika mkusanyiko huu, kuna mambo Mawili Muhimu sana yalifanyika:
1. Walimeka Mkate -Kula Meza ya Bwana. [Communion]
2. Walisoma Neno.

Zaidi ya hapo, Luka hakutumia njia ya Kiyahudi katika kuhesabu siku, yaani kutua kwa jua mpaka kutua kwa jua. Luka alitumia njia ya Kirumi ambayo siku inaanza Saa Sita ya Usiku. [midnight to midnight.] Huu ni ushahidi tosha kuwa Luka hakutumia na au hesabu siku kwa kutumia Njia ya Kiyahudi ya kuhesabu Sabato.


PAULO ANALIAMBIA KANISA LIKUTANE SIKU YA KWANZA YA JUMA
1 Wakorintho 16: 1-2 inasema: 1 Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo.
2 Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;

Ona hapa Mtume Paulo analiambia Kanisa likutane siku ya kwanza ya Juma ambayo ni Jumapili na aliwataka waweke akiba katika siku hiyo ya kwanza ya Juma.

Hivyo basi, siku ambayo Kanisa liliambiwa likutane ni Jumapili. Je, hii ni siku ya kisheria ya Mkristo kukutana? Jibu ni lako na uchaguzi ni wako.


YOHANA ALIKUWA KATIKA ROHO SIKU YA BWANA
Ufunuo 1 :10-11 inasema: 10 Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
11 ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.

Katika Kamusi ya Biblia kuhsu "SIKU YA BWANA" katika Ufunuo 1:10. hii ni tukui la kwanza katika maandishi ya Kikristo kuwa watu wakuna siku ya kwanza τῇ κυριακῇ ἡμέρᾳ, "ta kuriaka hamera." Hii ni uthibitisho kuwa, ilikuwa ni desturi ya Wakristo kukutana katika siku hio. Vile vile, ushahid huu uliweza kuoneka katika Karne ya Pili, Soma (Ignatius, Epistle to the Magnesians, 1. 67).


Katika Makanisa mengi sana ya leo" SIKU YA BWANA" inafahamika kuwa ni Jumapili kama ilivyo kuwa tokea Karne ya Pili

Nategemea huu ushahid unatosha kukuambia kuwa Biblia hamlazimishi mtu kusali siku ya Jumamosi. Kma unashida ya aya angalau moja basi Warumi 14 aya ya 1-12 imetupa haki ya kuchagua siku ya kumwabudu Bwana Mungu ambayo inaweza kuwa Jumatau, Jumanne, Tuma Tano, Alahamisi, Ijumaa, Jumamosi au JUMAPILI. Zote hizo ni siku za Bwana.

Na hakuna mwenye haki ya kukuhukumu unapo amua kusali Jumatatu au siku yoyote ile. Soma Warumi 6 aya 14. KUMBUKA TUPO HURU KATIKA KRISTO.

Hivyo basi, leo nimewapa ushahid kadhaa kuhusu siku halali ya kuwambudu Bwana Mungu. SIKU ZOTE NI ZA BWANA.

Mungu awabariki sana,

Max Shimba

For Max Shimba Ministries Org

MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED

Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

Tuesday, February 9, 2016

UTAFITI: BIBLIA NDIO KITABU BORA NA KINACHO SOMWA SANA KULIKO VYOTE DUNIANI


Mtafiti James Chapman ameweka kumi bora ya vitabu vinavyo somwa sana duniani. Kwa taarifa yako, Biblia ndio kitabu kinacho ongoza kusomwa kuliko vitabu vyote hapa duniani. Quran HAIPO hata kwenye 20 bora.

Zaidi ya hapo, Biblia ndio kitabu kilicho chapishwa sana katika kipindi cha miaka 50 iliyo pita.

Biblia inaongoza kwa kuwa na nakala zaidi ya Bilioni 4 zilizo chapishwa katika kipindi cha miaka 50.

Ikifuatiwa na kitabu cha "Works of Mao Tse-tung" chenye nakala Milioni 820. Kitabu cha Harry Potter nakala millioni 400, The lord of the Rings trilogy nakala milioni 103 na kitabu cha Paulo Coelho's the Alchemist chenye nakala millioni 65.

Sunday, February 7, 2016

JE, MUHAMMAD AU JIBRIL NI ROHO YA KWELI/ROHO MTAKATIFU?

Leo nitawajibu Waislam wote duniani kwa kutumia Biblia Takatifu kuwa Muhammad hakuwa Roho ya Kweli kama alivyo ahidiwa na Yesu Kristo ambaye ni Bwana na Mwokozi wetu.

Mara nyingi Waislam wanauliza, "Roho ya Kweli ni nani ambaye Yesu alimuhadi katika Yohana 16 aya ya 12 mpaka 14.
Nimekuwa nikiwauliza Waislam, hivi wao wanafikiri huyu Roho wa Kweli ni nani? Na wakanijibu kuwa huyo Roho wa Kweli ni Malaika Jibril.

Yohana 16:13 inasema: Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

Zaidi ya hapo, Waislam wengi wanadai kuwa, Yesu alikuwa anamtabiri Muhammad, na wakati huo huo, wengine wanasema kuwa alikuwa anatabiriwa Jibril. KINYUME CHAKE, kama ilivyo shahidiwa katika Yohana 16 aya 13, Yesu alikuwa anamzungumzia Roho Mtakatifu. Tunafahamu hili kwasababu Yesu anamzungunzia Roho ambaye atawaongoza Wanafunzi wake kuanzia wakati huo na sio miaka mamia baadae.

Ukiisoma Biblia kwa makini kuanzia Yohana 16 aya ya 5 mpaka 15 utagundua hapo hapo kuwa Waislam wote pamoja na Allah wao ni waongo.

Lakini, kuna njia nyingi tunaweza kuzitumia kufahamu kama Waislam wako sahihi katika ufafanuzi wao kwa kuangalia na au soma kila wakati Yesu alipo sema "ROHO" katika Injili hiyo hiyo ya Yohana na tuone kama kweli alikuwa anamtabiri Muhammad wa Waislam katika aya mojawapo.

UTHIBITISHO WA KWANZA:
Yohana 1 aya ya 32 inasema: Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake "YESU".

Wote tunafahamu kuwa Muhammad hakuwa Mtakatifu na vile vile hakuwa anapaa kama ndege na alikuja miaka 600 baada ya Kristo, hivyo basi, ni dhahiri kuwa Roho Mtakatifu sio Muhammad ambaye alikuja miaka 600 baadae. Yohana hakuwai mwona Muhammad.

UTHIBITISHO WA PILI:
Yohana 1:33, [ Yohana Mbatizaji anaendelea kusema] "Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu."

Yohana anaweka kiuwazi zaidi aya hiyo hapo juu kuwa Yesu ndie atakaye kuwa anabatiza kwa Roho Mtakatifu.

Kwa kifupi Yesu atamtuma ROHO ambaye ni Mwenye Nguvu ya Mungu na ni Mungu.

Je, Muhammad ni huyo Roho? HAPANA KABISA, kwasababu Yesu aliwabatiza Wanafunzi wake na zaidi ya hapo, wafuasi wake walibatizwa kwa Roho Mtakatifu katika siku ya Pentekoste. Mda mchache baada ya Yesu kupaa kwenda kwa Baba yake Mbinguni, hivyo basi, na narudia tena, hii ilifanyika Miaka mia sita 600 kabla ya Muhammad kuzaliwa. Wanafunzi wa Yesu hawakubatizwa kwa kupitia Muhammad wala Waislam hawabatizi au batizwa.

UTHIBITISHO WA TATU:
Yohana 3 aya ya 5 inasema: Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

Nauhakika hakuna Muislam duniani pote anayeweza kusema kuwa Muhammad anazaa, maana katika ya hapo juu Yesu anasema Mtu lazima azaliwe kwa Roho, JE, MUHAMMAD ALIZAA/ANAZAA?

UTHIBITISHO WA NNE:
Yohona 3 aya ya 6 inasema: Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.

Hapa Muhammad anatupwa nje mara moja kwasababu ya haya maneno ambayo Yesu ameyasema, kwasababu #1 Muhammad alikuwa binadamu, mbaya zaidi hivi sasa amekufa -marehemu. na #2 KwasaMbabu tena, Roho inazaa kwa kutumia Nguvu ya Mungu, ambaye ni Roho Mtakatifu. Huku kuzaliwa kwa Roho kulianza miaka 600 kabla ya Muhammad kuzaliwa.

UTHIBITISHO WA TANO:
Yohana 3 aya ya 8 inasema: Upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.

HAKUNA HATA MMOJA WETU ALIYE ZALIWA KUPITIA MUHAMMAD. Hivyo basi Muhammad anashindwa tena kuwa Roho ya Kweli.

UTHIBITISHO WA SITA:
Yohana 3 aya ya 34 inasema: Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.

Je, Muhamamd alikuwa hana kipimo? Hapo tena Muhammad kashindwa maana alikuwa amepimiwa maneno tu na Allah wake. Muhammad alikiri kuwa yeye hajui Mungu atamfanya nini baada ya kifo, pale alipo ulizwa na watu, je, nini kitatokea baada ya kifo. Muhammad hakuwa "omniscient".


UTHIBITISHO WA SABA:
Yohana 4 aya ya 24 inasema: Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

Mungu sio Muhammad, asante Mungu, kwa kuweka huu ukweli kuwa Roho Mtakatifu ni Mungu. Kumbe hata Jibril sio Roho Mtakatifu.

UTHIBITISHO WA NANE:
Yohana 6 aya ya 63 inasema: Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.

Muhammad hawezi kutoa uzima wa milele, ni kitu ambacho Mungu peke yake anaweza kukupa. Ndio maana tunajua kuwa Yesu ni Mungu, kwasababu, Yesu anatoa uzima wa Milele kwa wale wote wamwaminio.

UTHIBITISHO WA TISA:
Yohana 7 aya ya 39 inasema: Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.

Je, Muhammad atapewa kwa kila mtu ambaye anamwamini Yesu? HAPANA KABISA, Quran inasema kuwa Ukimwanini Mwamad/Allah basi umemwamini Allah. Hivyo Muhammad hawezi kuwa Roho ya Kweli, maana tunao Mwamini Yesu tumepewa Roho Mtakatifu na sio Muhammad ambaye amesha kufa.

UTHIBITISHO WA KUMI:
Yohana 14 aya ya 16,17, na 18 inasema: 16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.

Hizi aya zinapendwa sana na Waislam na wanapenda kuzitumia kama ushahidi wao. Je, Muhammad aliishi na Mitume wa Yesu katika karne/Century ya kwanza? HAPANA KABISA TENA KABISA. Muhammad hakuwepo wakati wa karne/Century ya kwanza pale Wafuasi wa Yesu walipo pewa huyo Roho Mtakatifu. Yesu alisema kwa Wanafunzi wake kuwa hata waacha YATIMA, Je, iweje Muhammad aliye kuja miaka 600 baadae awe na Wanafunzi wa Yesu katika karne/Century ya Kwanza?

UTHIBITISHO WA KUMI NA MOJA:
Yohana 14 aya ya 26. Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Hii aya Waislam hawaipendi kabisaa, kwasababu Yesu anasema KIUWAZI KABISA KUWA, ni nani huyu WAKILI wetu, NI WATATU KATIKA MUUNGANO MTAKATIFU. Huyu Roho Mtakatifu ana adhama zote za Baba na Mwana, HIVYO BASI, Muhammad tena ameshindwa vibaya sana hapa. Muhammad alikuwa Mtenda dhambi, huku Yesu hakuwai tenda dhambi hata moja.

UTHIBITISHO WA KUMI NA MBILI:
Yohana 15 aya ya 26 inasema: Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia.

Kwa mara nyingine tena, hii ndio raha ya kufundisha katika context yake. Tumesoma katika aya hapo juu kuwa Yesu alisema nani ni Msaidizi wetu, na kwa undani zaidi, HAPA KWENYE HII AYA YA 26 Yesu anasema kuwa huyo Msaidizi ni Roho Mtakatifu.
Je, Muhammad aliishi wakati wa Mitume wa Yesu na kuwa msaidizi wao, HAPANA KABISA, inafahamika kuwa Muhammad alikuja miaka 600 baadae.

UTHIBITISHO WA KUMI NA TATU:
Yohana 16 aya ya 13 inasema: Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

Muhammad tena ameshindwa hapa, maana hakunena na wala hakuwai sikia kutoka kwa Mungu, Yehova, bali kwa Jibril ambaye anadai kuwa alitumwa na Allah. Zaidi ya hapo, Muhammad hakutoa utabiri wa mambo yatakayo kuja. MUHAMMAD AMESHINDWA TENA KWA MARA YA KUMI NA TATU.

UTHIBITISHO WA KUMI NA NNE:
Yohana 16 aya ya 15 inasema: Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.

Yesu anasema kuwa yote ya Baba ni yangu, je, binadamu wa kawaida anaweza kudai kuwa kila kitu cha Mungu Baba ni chake? Hakika Yesu ni Mungu. ZAIDI YA HAPO, Yesu anasema kuwa huyo Roho Mtakatifu atatufundisha kuhusu YEYE/Yesu, wakati inafahamika kuwa Muhammad hakuwai fundisha kuhusu Yesu na wala Muhammad hakuwai sema kuwa Yesu ana Baba. Kumbe basi Roho Mtakatifu hawezi kuwa Jibril au Muislam bali ni Mungu mwenye adhama zote za Baba na Mwana.

UTHIBITISHO WA KUMI NA TANO:
YESU ANAWAPA ROHO MTAKATIFU WANAFUNZI WAKE
Yohana 20 aya ya 21 na 22 inasema: 21 Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. 22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.

AYA HAPO JUU IPO WAZI kabisa kuwa YESU ALIWAPA ROHO MTAKATIFU WANAFUNZI WAKE NA HAKUWAPA MUHAMMAD AMBAYE alikuwa bado HAJAZALIWA.

Hivyo basi, leo nimetoa USHAHIDI ZAIDI YA KUMI NA TAKO KUTOKA INJILI YOAHANA kuwa Muhammad hakuwa Roho ya Kweli, zaidi ya hapo, Jibril hakuwa Roho ya kweli.

LEO NIMEJIBU KUHUSU ROHO WA KWELI AMBAYE YESU ALIKUWA ANAMSEMA kwa kutumia Aya hizo hizo ambazo Yesu alizitumia kumzungumzia huyo Roho wa Kweli.

Katika huduma yake,

Max Shimba,

Max Shimba Ministries 2013
December 26, 2013
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

Saturday, February 6, 2016

ALLAH WA WAISLAM AKIRI KUWA YEYE SIO BABA BALI NI BWANA MWENYE WATWANA

1. Uislam ni dini ya yatima na Watwana.
2. Ukristo ni imani pekee yenye Mungu Baba na Wakristo ni watoto wa Mungu.


MUHAMMAD ANASEMA KUWA ALLAH SIO BABA
Surat Al Maida 18. Na Mayahudi na Wakristo wanasema: Sisi ni wana wa Mwenyezi Mungu na vipenzi vyake. Sema: Basi kwa nini anakuadhibuni kwa ajili ya dhambi zenu? Bali nyinyi ni watu tu kama wale wengine alio waumba. Humsamehe amtakaye na humuadhibu amtakaye. Na ni wa Mwenyezi Mungu tu ufalme wa mbingu na ardhi. Na marejeo ni kwake Yeye.

Kama aya inavyo sema hapo juu, Muhamma na Allah wanakana kuwa Wakristo na Wayahudi sio watoto wa Mungu, eti kwasababu ya Allah kuto kuwa na mwana bila ya Mke. Hii aya inapingana na Biblia ambayo inasema kuwa sisi ni watoto wa Mungu.


WAKRISTO NI WATOTO WA MUNGU
Waebrania 12: 7 Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? 8 Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. 9 Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? 10 Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake.

Yeremia 31:
18 Hakika nimemsikia Efraimu, akijililia hivi, Umeniadhibu, nami nikaadhibika, kama ndama asiyeizoelea nira; unigeuze, nami nitageuzwa; kwa maana wewe u Bwana, Mungu wangu.
19 Hakika baada ya kugeuzwa kwangu, nalitubu; na baada ya kufundishwa kwangu, nalijipiga pajani; nalitahayarika, naam, nalifadhaika, kwa sababu naliichukua aibu ya ujana wangu.


Muhammad alikuwa bila ya matunzo na malezi ya Baba na mama yake. Baba yake alikufa kabla ya muhammad kuzaliwa, na Mama yake alikufa alipo kuwa na miaka sita [6] . Huyu Muhammad kwanza aliishi na babu yake na kwa muda mwingi aliishi na wajomba zake. MUHAMMAD ALIKOSA MALEZI BORA YA WAZAZI WAKE NDIO MAANA ANACHUKIA SANA WAKRISTO PALE WANAPO SEMA KUWA MUNGU NI BABA YETU. Hii chuki ilimuingia kwasababu yeye alikuwa hana baba na kuanza chuki kubwa kubwa kwa Mungu.


LAKINI KATIKA BIBLIA TUNASOMA KUWA MUNGU NI BABA YETU:
Kumbukumbu la Torati 32: 6........Je! Yeye siye Baba yako aliyekununua? Amekufanya, na kukuweka imara.

Zaburi 2: 7 Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.

Isaya 63: 16 Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Ibrahimu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, Bwana, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako.

Mathayo 6: 9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,

Yohana 20: 17 Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.

UISLAM HAUNA BABA, BALI UNA BWANA MWENYE WATWANA. Ngoja nitumbue jipu, Allah ambaye ni mungu wa Waislam SIO YEHOVA ambaye ni Mungu wa Wakristo. Allah yeye ni dhaifu, duni, na yupo chini ya YEHOVAH ambaye ni Mungu Mkuu.

Allah sio baba bali ni roho dhaifu ambayo ipo chini na duni kwa YEHOVAH, ndio maana Allah anapenda WATWANA na kuwafanya Wiaslam wote kuwa ni WATUMWA WAKE - Muslims are SLAVES OF ALLAH.

SASABU inayo mfanya Allah kushindwa kuwapenda binadamu ni jibu tosha kuwa Allah hakuumba binadamu na ndio maana amejaa chuki kubwa kubwa kwa bianadamu. ZAIDI YA HAPO, Allah yeye ni BWANA MWENYE WATWANA.


WAISLAM NI WATUMWA WA ALLAH - SLAVES OF ALLAH
Surat Azzumar 10. Sema: Enyi waja wangu mlio amini! Mcheni Mola wenu Mlezi. Wale wafanyao wema katika dunia hii watapata wema. Na ardhi ya Mwenyezi Mungu ni kunjufu. Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu.

Surat Azzumar 36. Je! Mwenyezi Mungu si wa kumtosheleza mja wake? Na ati wanakutishia kwa hao wenginewe wasio kuwa Yeye! Na aliye hukumiwa na Mwenyezi Mungu kupotea hana wa kumwongoa.

Aya hapo juu zinakiri kuwa Allah yeye anawatumwa na ni tofauti na Yehovah wa kwenye Biblia ambaye yeye anatuita sisi ni watoto wake.

Hii roho mbaya iliyomtisha na kumbana mbavu Muhammad, ipo kwa ajili ya kufanyiwa kazi, ndio maana Waislam wao wanapigana kwa ajili ya Allah. Allah hana upendo zaidi ya chuki.

ALLAH YEYE ANAPENDA WATU WANAO PIGANA KWA AJILI YAKE TU.
Surat Assaf 4. Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao pigana katika Njia yake kwa safu kama jengo lilio kamatana. Maelezo

Surat An Nisaai 74. Basi nawapigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu wale ambao wanao uza uhai wa dunia kwa Akhera. Na anaye pigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu kisha akauliwa au akashinda basi tutakuja mpa ujira mkubwa.
75. Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako. Maelezo
76. Walio amini wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio kufuru wanapiana katika njia ya upotofu. Basi piganeni na marafiki wa Shet'ani. Hakika hila za Shet'ani ni dhaifu

Hivi Mungu gani huyu anaye penda kuwachinganisha watu? Hakika Allah ahakuumba ndio maana yeye hapendi watu na amewaitwa WATWANA huku yeye akiwa ni BWANA wao. HUU NI MSIBA MKUBWA SANA.


SOMA BIBLIA YENYE UPENDO:

MWENYEZI MUNGU ANAKUPENDA, NAYE ANATAKA KUKUPANGIA MPANGO WA AJABU KWA MAISHA YAKO.
UPENDO WA MUNGU
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Yohana 3:16

MPANGO WA MUNGU KWAKO
Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Yohana 10:10

Warumi 5:8 Bali Mungu aonyesha pendo Lake Yeye Mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.

Kulingana na Warumi 5:8, Mungu alionyesha pendo Lake kwetu sisi kwa njia ya mauti ya Mwanawe. Kwa nini ilimpasa Kristo kutufia? Kwa sababu Andiko la tangaza watu wote kuwa wafanya dhambi. Kufanya "dhambi" kuna maanisha kukosa alama. Biblia inatangaza "wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu (utakatifu mkamilifu) wa Mungu" (Rum. 3:23). Katika maneno mengine, dhambi zetu zatufarikisha sisi na Mungu wetu aliye utakatifu mkamilifu (haki na kweli) na kwa hivyo sharti Mungu awahukumu watenda dhambi.

Ndugu msomaji,

Nakukaribishga sana kwa Mungu wa Wakristo ambaye anakupenda sana. Njoo huku kwa Yesu ili upate uzima wa milele. Njoo kwa Yesu ili upate upendo wa Mungu. Ndugu uansubiri nini?

Mungu awabariki sana na Yesu anakupenda,

Max Shimba Ministries Org

MATOLEO 20 TOFAUTI YA QURAN ::::::::20 VERSIONS OF QURAN::::::::::

Je, Kati ya haya Matolea 20 (Ishirini) ya Quran, toleo lipi ni la kweli?
Je, Nabii wa Allah ajulikanaye kwa jina la Muhammad, alisoma toleo lipi?

Ndugu msomaji,
Leo nitaweka ukweli kuhusu Quran ambayo ina Matoleo 20 na kati ya hayo Ishirini (20) Matoleo 7 (Saba) yametajwa katika Hadith Mwaminifu za Muhammad.
Hapa chini ni Wasomaji Saba (7) ambao wote wana Matoleo Mawili mawili. Hawa Wasomaji saba wanapatikana hapa:
Nafi (from Medina; d.169/785)
Ibn Kathir (from Mecca; d.119/737)
Abu `Amr al-'Ala' (from Damascus; d.53/770)
Ibn `Amir (from Basra; d.118/736)
Hamzah (from Kufah; d.156/772)
al-Qisa'i (from Kufah; d.189/804)
Abu Bakr `Asim (from Kufah; d.158/778)
WASOMAJI SABA NA MATOLEO YAO YA QURAN
1. Msomaji : Nafi`
MATOLEO YAKE
Warsh
Qalun
2. Msomaji: Ibn Kathir
MATOLEO YAKE
al-Bazzi
Qunbul
3. Msomaji: Abu `Amr al-'Ala'
MATOLEO YAKE
Al-Duri
al-Suri
4. Msomaji: Ibn `Amir
MATOLEO YAKE
Hisham
Ibn Dhakwan
5. Msomaji: Hamzah
MATOLEO YAKE
Khalaf
Khallad
6. Msomaji: al-Qisa'i
MATOLEO YAKE
al-Duri
Abu'l-Harith
7. Msomaji: Abu Bakr `Asim
MATOLEO YAKE
Hafs
Ibn `Ayyash
HAWA NI WASOMAJI WENGI WATATU NA MATOLEA YAO MAWILI KILA MMOJA
"The Three" readers
1. Msomaji: Abu Ja`far
MATOLEO YAKE
Ibn Wardan
Ibn Jamaz
2. Msomaji: Ya`qub al-Hashimi
MATOLEO YAKE
Ruways
Rawh
3. Msomaji: Khalaf al-Bazzar
MATOLEO YAKE
Ishaq
Idris al-Haddad
Wadhalimu wa dini ya Kiislamu wanakiri kuwa kuna WASOMAJI wengi zaidi, lakini wanasema kuwa hawa walio tajwa hapo juu ndio thabit na sahihi. Kumbe basi kuna VERSIONS ISHIRINI ZA QURAN !!!!!!
SASA MASWALI YAKUJIULIZA NI HAYA:
1. Kati ya hao wasomaji wakurani, ni yupi yupo sahihi?
2. Kama Allah ndie aliteremsha Quran kwa Muhammad, kivipi awe na wasomaji wengine na kumsahahu Muhammad mtume wake kipenzi?
3. Kama Quran ni moja na ipo kwa Kiarabu tu, kivipi isomeke kitofauti kwa mara ISHIRINI [20] katika lugha hiyo hiyo ya Allah?
4. Je, Kati ya haya Matolea 20 (Ishirini) ya Quran, toleo lipi ni la kweli?
5. Je, Nabii wa Allah ajulikanaye kwa jina la Muhammad, alisoma toleo lipi?
Ndugu msomaji, leo tumejifunza kuwa katika Uislam kuna siri nyingi sana ambazo zimefichwa na wanaona aibu kusema ukweli kuwa QURAN INA MATOLEO/VERSIONS 20. HUU NI MSIBA KWA ALLAH NA MTUME WAKE MUHAMMAD.
Mungu awabariki sana na kuendelea kuwafungua macho.
Katika huduma yake
Max Shimba Ministries Org.

Ancient Jewish Wedding Ceremony: “No man knows the day or hour, only the Father”

  The Ancient Jewish Marriage Rite: A Detailed Exposition of Betrothal, Preparation, and Consummation Dr. Maxwell Shimba Shimba Theological ...

TRENDING NOW