Monday, October 3, 2016

ALLAH SIO YEHOVA "YAHUH" ( يهوه ) MWENYEZI MUNGU (SEHEMU YA NANE)



JE MALAIKA MKUU WA YEHOVA NDIO YULE YULE WA ALLAH?
Ikiwa Allah ndiye Yehova, basi ni wazi kuwa malaika mkuu atakuwa mmoja pia. Ikiwa si mmoja hata malaika mkuu watakuwa tofauti.
Tuanze kuangalia Allah anavyosimulia katika Qurani naye anasema hivi
Je, Malaika Mkuu wa Allah ni nani?
Quran 81 au surat At-Takwyr 19-21 (Kukunja/jua litakapokunjwa)
Kwa hakika hii (Qurani) ni kauli (aliyokuja nayo) mjumbe mtukufu (Jibrili) Mwenye nguvu, mwenye cheo cha hishima kwa mwenyenzi Mungu. Anayetiiwa huko (mbinguni na malaika wenziwe) kisha muaminifu.
Ufafanuzi wa aya hizi. ulio ndani ya Qurani unaelezea aya hizi 19-21, unafundisha hivi…….
Mjumbe mtukufu na mwenye kutiiwa huko mbinguni ni Jibrili, ambaye ndiye mkubwa wa malaika wote.
Katika Surat At Takwyr tumejifunza kuwa Malaika Mkuu wa Allah ni Jibril.
Je, Malaika Mkuu wa Yehova ni nani?
Malaika mkuu wa Mungu Yehova ni huyu;
Yuda 1:9, Lakini MIKAELI Malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthumbutu kumshitaki kwa kumlaumu bali alisema Bwana na akukemee
Hapa tunaona aya zinatufundisha waziwazi kuwa malaika mkubwa wa Allah anaitwa Jibril na Malaika mkuu wa Menyezi Mungu wetu Yehova anaitwa Mikaeli.
Swali; Kwa kuwa Malaika hao ni tofauti, je, Allah ndiye Yehova? Kwa kujua zaidi tofauti ya malaika, jipatie nakala ya somo la: Malaika Jibrili na Gabrieli, je ni Malaika mmoja. Somo hilo tunalo, jipatiehttp://www.maxshimbaministries.org/…/malaika-gabriel-wa-bib… .
Mwanzo1:26-27
Mungu akasema “Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale samaki wa baharini, ndege wa angani na wanyama, na nchi yote, pia na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba mwanamume na mwanamke aliwaumba. Hapa tunaona Mungu wetu Yehova ameumba mtu kwa mfano wake, lakini Allah anasema hana anayefanana naye hata mmoja……
Swali kwako mfuatiliaji:
Je, Allah ndiye Yehova?
Tafadhali usome aya hizi ili kujua zaidi (Mwanzo 5:1-2, 9:6, 1Korintho 11:7, Kolosai 1:15, 3:10, Matendo 17:28-29,Yakobo 3:9). Pengine waweza kusema Je, Mungu amefanana na mimi kivipi? Jua kwamba Mungu ni Roho (Yohana 4:24) Naye alitupa pumzi (yaani roho ya uhai (Mwanzo 2:7) isitoshe Mungu ndiye Baba wa roho zetu (Waebrania 12:9) Mungu anasema Roho zetu ni mali yake (Ezekieli 18:4, Hesabu 16:22)
Nawakaribisha Waislamu wote kwa Mungu wa Kweli anaye itwa YEHOVA.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW