Wednesday, October 26, 2016

ALLAH AMECHAKACHUWA KUHUSU SAYANSI NA UUMBAJI?


1. Kurani iliitarajia sayansi ya kisasa: Jua na mwezi ziko kwenye mkondo na huzunguka kwenye mhimili wao (Sura 21:33; 36:27-40). Kurani pia inafundusha nadharia ya mlipuko mkubwa uliosababisha kuumbwa kwa dunia (Sura 21:30; Sura 51:47,48). Neno la Kiarabu falak linamaanisha "mkondo." Wanajimu wanatuambia kuwa jua huzunguka kwenye kitovu cha kundi la nyota kila baada ya miaka karibu milioni 250. Neno la Kiarabu yasbahuna (linatokana na sabaha)linamaanisha kuzunguka mkondo wake.
1 Itikio: Jambo hili ni ndoto za mchana kwa sababu mbili.
1) Maneno hayako bayana: falak ni neno la Kiarabu lenye kumaanisha njia, kuendelea kwenye mkondo, na yasbahuna inaweza kumaanisha kuharakisha, ingawa maana yake ya moja kwa moja zaidi ni kuogelea.
2) Muhammad alituambia wazi kabisa maana yake, na inamaanisha kuwa jua na mwezi vinasafiri juu ya dunia, vikiwa vimepanda kibandawazi kwenye anga la dunia.
Tena, kuna vyanzo viwili vya maneno aliyosema Muhammad.
"Mungu aliumba bahari iliyo fasrakh tatu (kilomita 18) toka mbingni. Mawingu yamethibitiwa, inasimama angani kwa amri ya Mungu. Hakuna tone lake lolote linalomwagika. Bahari zote hazitembei, lakini bahari hutembea kwa mwendokasi wa mshale. Inao uhuru wa kutembea angani kwa uwiano sawa, kana kwamba ni kamba iliyovutwa kwenye eneo kati ya mashariki na magharibi. Jua, mwezi, na nyota zinazorudi nyuma [sayari 5] zinakimbia kwenye kilindi cha tumbo lake. Hivi ndivyo neno la Mungu (linavyomaanisha): ‘KIla kimojawapo huogelea angani.’ ‘Anga’ ni mzunguko wa magari yanayokokotwa na farasi kwenye kilindi cha tumbo la hiyo bahari." al-Tabari juzuu ya 1, uk.235.
Abu Dhar alisimulia: Nabii aliniuliza jioni moja, ‘Unajua mahali jua linakokwenda (wakati linapozama)?" Nilimjibu, "Allah na Mtume wake wanafahamu hilo vizuri zaidi." Aliniambia, "Linakwenda (yaani linasafiri) hadi linasujudu chini ya kiti cha enzi, na linapata ruhusa ya kuchomoza tena, na linaruhusiwa na kisha (muda utakuja wakati ambapo) litakuwa linataka kusujudu lakini kusujudu kwake hakutakubaliwa…" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 4 na.441, uk.283. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 1 sura ya 73 na.297-300, uk.95-96 pia lina maelezo ya kina ya maongezi ya Muhammad na Abu Dharr.
2. Kurani inauelezea mhimili wa jua karibu na kitovu cha kundi letu la nyota
2 Itikio: Jua halina mhimili wake peke yake kwenye kundi letu la nyota. Kama Kurani ilikuwa inajaribu kufundisha sayansi ya kisasa, ingepaswa kusema kuwa jua, mwezi, dunia, na nyota zinazorudi nyuma (sayari) zinazunguka pamoja kwenye mhimili mmoja.

Tena, tunafahamu kabisa kitu ambacho Muhammad alikimaanisha, kwa sababu alituambia, kama Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 4 na.441, uk.283 na al-Tabari juzuu ya 1, uk.235 ilivyorekodi.
3. Sehemu ya kupumzikia jua inamaanisha kuwa linaangaza kwenye upande mwingine wa dunia
Tena, tunafahamu kabisa kitu ambacho Muhammad alimaanisha, kwa sababu alituambia kama Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 4 na.441, uk.283 na al-Tabari juzuu ya 1, uk.235 ilivyorekodi.
4. Sehemu ya jua kupumzikia inamaanisha uharibifu mkamilifu wa jua
4 Itiko: Mtu wa kawaida anayesoma hili, kwenye lugha yoyote ile, anaweza kufikiri kuwa inaongelea mzunguko wa vipindi, sio uharibifu mkamilifu.
5. Lugha ya ufananisho: Jua, mwezi, na sayari huweka alama ya njia angani. Aya hizi hazikuwa na lengo la kuunga mkono au kupinga sayansi ya kisasa, bali zilikuwa ni maelezo ya kishairi zikisema tu kwamba Allah alihusika na vitu ambavyo watu walikuwa wakiviona.
5 Itikio: Mtazamo huu ungeweza kuwa sahihi isingekuwa maneno ambayo Bukhari na al-Tabari wameandika kuwa Muhammad aliyasema. Kama Bukhari na al-Tabari walikosea kuhusiana na hili, basi kuna kigezo gani cha kusema kuwa walikuwa sahihi kwa jambo lolote.
Ndio maana nasema kuwa Allah sio Yehova Mwenyezi Mungu aliye umba kila kitu.
Allah kachakachuwa kuhusu uumbaji.
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW