Sunday, October 9, 2016

BIBLIA INAKATAZA USHOGA


Je, Biblia inasema nini juu ya Ushoga?
Je, Ushoga ni dhambi?
Ndugu msomaji,
Leo, watu wengi kupitia viongozi fulani wa dini hawashutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja. Hata hivyo, Biblia iko wazi kuhusu jambo hilo. Inatuambia Mungu aliumba mwanamume na mwanamke na kwamba alikusudia ngono ifanywe kati ya mume na mke tu. (Mwanzo 1:27, 28; 2:24) Hivyo, haishangazi kwamba Biblia inashutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja.—Waroma 1:26, 27.
Waislam mara nyingi wamekuwa wakisema na kuwashutumu Wakristo, eti, Ukristo unaruhusu ushoga, huku ikifahamika kuwa, hakuna aya hata moja inayo ruhusu huu uchafu.
Walawi 18:22-23 "Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko".
Neno la Mungu kama lisemavyo kwenye Biblia linasisitiza kila mara kwamba ushoga na usagaji ni dhambi (Mwanzo 19:1-13; Mambo ya Walawi 18: 22; Warumi 1:26-27; Wakorintho wa kwanza 6:9). Warumi 1:26-27 inatufundisha ya kwamba ushoga ni njia mojawapo ya kumkana na kutomtii Mungu. Mtu anapodumu katika dhambi na kutokuamini biblia inatuambia ya kwamba “Mungu huwaachilia” kutenda maovu zaidi ili wapate kujua ubatili wa maisha bila Uwepo wa Mungu. Wakorintho wa kwanza 6:9 inasema kuwa mashoga hawataurithi ufalme wa Mungu.
Wanadamu wanajinenea kuwa wenye hekima na kupumbazika. Mtume Paulo ameeleza vizuri katika Waroma1:21-27.
Mungu amewaacha wafuate akili zao. Kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao ,Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.Waroma1:28
Watu wengine wanasema kwamba ushoga upo kwenye chembe za urithi. Wengine wanasema kwamba mtu hujifunza zoea hilo. Si kusudi la makala hii kujadili ikiwa zoea hilo ni la kurithiwa au ni la kujifunza. Kwa wazi, kusema kwamba ushoga unasababishwa na jambo fulani hususa haingekuwa kweli. Inaonekana kwamba kama ilivyo kwa mazoea mengine, ni vigumu kufahamu chanzo cha zoea hilo.
Hata chanzo kiwe nini, jambo muhimu ni kutambua kwamba Biblia inashutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja.

Mungu hakuumba mwanadamu mwenye tamaa ya ushoga. Biblia inatuambia mtu huwa shoga kwa sababu ya dhambi. (Warumi 1:24-27), na pia kwa sababu ya uamuzi wake mwenyewe. Mtu anaweza kuzaliwa na msukumo juu ya ushoga kama vile watu pia huzaliwa na msukumo juu ya fujo na dhambi nyinginezo. Hili halihalalishi dhambi yoyote inayofanywa na wanadamu. Je, mtu akizaliwa na msukumo wa hasira mbaya, ni halali aendeleze hasira zake mbaya? La, hasha. Hata kwa ushoga pia si halali.
Hata hivyo Biblia haiitaji dhambi ya ushoga kuwa ndiyo kubwa zaidi. Kila dhambi ni chukizo kwa Mungu. Ushoga ni mojawapo ya mambo yaliyoorodheshwa katika wakorintho wa kwanza 6:9-10 yatakayozuia mtu asiingie katika ufalme wa Mungu. Kulingana na Biblia msamaha wa Mungu juu ya shoga upo sawa na wa mzinzi, muabudu sanamu, muuaji, mwizi na kadhalika. Mungu tena aahidi uwezo juu ya kushinda dhambi, pamoja na ushoga, kwa wale wote watakao mwaminiYesu kristo kwa wokovu wao (wakorintho wa kwanza 6:11; wakorintho wa pili 5:17).
JE, UNAWEZA KUISHINDA TAMAA HII YA USHOGA?
Unaweza kuepukaje kujihusisha na ngono ya watu wa jinsia moja?
 Kwanza Mtupie Mungu mahangaiko yako yote kupitia sala, ukiwa na uhakika kwamba ‘anakujali wewe.’ (1 Petro 5:7; Zaburi 55:22) Mungu anaweza kukuimarisha kwa kukupa amani “yenye ubora unaozidi fikira zote.” Amani hiyo ‘itaulinda moyo wako na nguvu zako za akili’ na kukupa “nguvu zinazopita zile za kawaida” ili usitende kulingana na tamaa zisizofaa. (Wafilipi 4:7; 2 Wakorintho 4:7) Sarah, ambaye alihofia kwamba anavutiwa na watu wa jinsia zote mbili, anasema: “Kila wakati ninapopatwa na hisia hizo, mimi husali; na Yehova hunitegemeza. Nisingeweza kukabiliana na tatizo hilo bila msaada wake. Sala ndiyo msaada wangu mkubwa!”—Zaburi 94:18, 19; Waefeso 3:20.
 Pili Jaza akili yako mambo ya kiroho yenye kujenga. (Wafilipi 4:8) Soma Biblia kila siku. Usidharau uwezo wake wa kuongoza akili na moyo wako daima. (Waebrania 4:12) Kijana mmoja anayeitwa Jason anasema: “Biblia—kutia ndani maandiko kama vile 1 Wakorintho 6:9, 10; na Waefeso 5:3—imenisaidia sana. Mimi husoma maandiko haya kila wakati tamaa mbaya zinaponijia.”
 Tatu Epuka ponografia, yaani picha au habari za kingono na propaganda za ngono kati ya watu wa jinsia moja ambazo zinaweza kuchochea mawazo yasiyofaa.* (Zaburi 119:37; Wakolosai 3:5, 6) Sinema na vipindi fulani vya televisheni pia huendeleza wazo la kwamba ngono kati ya watu wa jinsia moja ni mtindo mwingine tu wa maisha. “Maoni yaliyopotoka ya ulimwengu yaliathiri sana akili yangu, na kufanya nichanganyikiwe kuhusu hisia za kuvutiwa na watu wa jinsia yangu,” anasema Anna. “Sasa mimi huepuka kabisa kitu chochote au mtu yeyote ambaye anaunga mkono ngono kati ya watu wa jinsia moja.”—Methali 13:20.
 Nne Zungumza na mtu unayemwamini kuhusu hisia zako. (Methali 23:26; 31:26; 2 Timotheo 1:1, 2; 3:10)
MAMBO YA KUFIKIRIA
 Kwa nini Mungu hushutumu ngono kati ya watu wa jinsia moja?
 Utafanya nini ikiwa unakabiliana na hisia za kuvutiwa kingono na mtu wa jinsia yako?
 Unaweza kuongea na nani ikiwa unahangaishwa na hisia za kufanya ngono na mtu wa jinsia yako?
Walawi 18:22-23 "Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko".
Ushoga ni dhambi na umekatazwa kwenye Biblia.
Mungu awabariki sana.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
For Max Shimba Ministries Org.

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW